Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

POLISI WATOA UFAFANUZI JUU YA MILIPUKO YA MABOMU ILIYOTOKEA ZANZIBAR..

JESHI la Polisi Zanzibar, jana limetoa ufafanuzi wa matukio ya milipuko iliyotokea katika maeneo manne tofauti.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Polisi Hamdani Omari Makame, alisema tukio la kwanza lilitokea Februari 23 mwaka huu, saa saba mchana eneo la Pangawe.

Alisema mlipuko huo ulitokea baada ya waumini wa dhehebu la Evengilistic kumaliza ibada na haukuleta madhara yoyote.

Aliongeza kuwa, wakati polisi wakishughulikia tukio hilo, saa 6:36 mchana ikatokea milipuko mingine mitatu katika maeneo mawili tofauti.

"Mlipuko wa kwanza ulitokea eneo la Malindi mjini Zanzibar kwenye Mkahawa wa Mercury unaomilikiwa na Bw. Simai Mohammed Saidi (45) lakini haukuwa na madhara.

"Ilipofika saa 8:35 na 8:40 kwenye mtaro mmoja uliopo karibu na Mkunazini, eneo la Mji Mkongwe, Mjini Zanzibar ilitokea milipuko miwili iliyopishana kwa muda wa dakika chache," alisema.

Alisema milipuko hiyo pia haikuleta madhara kwa binadamu isipokuwa gari moja lenye namba Z.355 ET Harrier mali ya Bw. Mohammed Ibrahim Ali, lililoegeshwa karibu ya mtaro lilipata madhara kidogo kwa kutoboka bati upande wa nyuma kulia.

Kamishna Makame alisema milipuko yote ilitengenezwa kienyeji na Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wamechukua mabaki ya milipuko hiyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kitaalamu.

Aliongeza kuwa, polisi wameimarisha doria katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Zanzibar ili kuhakikisha matukio kama hayo hayatokei tena na kuweza kuwakamata wahalifu hao.

"Tayari timu ya Makachero wakiwemo Wataalamu wa Uchunguzi wa Kisayansi kutoka Makao Makuu ya Upelelezi, Dar es Salaam, wamewasili mjini Zanzibar kuungana na Makachero wenzao wa Zanzibar kuendelea na uchunguzi huu," alisema.



Alisema katika hali isiyo ya kawaida, Mkoa wa Kusini Unguja, juzi saa nane mchana katika Kijiji cha Unguja Ukuu, eneo la Kae Pwani, kulikuwa na wavuvi wakivua vyuma ili kwenda kutengeneza nanga ya boti lao, lakini wakati wakiendelea na kazi hiyo chuma walichokuwa wakikitengeneza kililipuka na kujeruhi watuwanne.

Waliojeruhiwa na kukimbizwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ni Juma Abdallah Juma (32), Shabani Khamisi Ibarahim (32) Haji Khamisi(35) na Sumai Hussein Hassan (38).


Wakati majeruhi hao wakiendelea na matibabu, majeruhi mmoja Juma Abdallah Juma (32) alifariki dunia saa 11 jioni na mmoja kati yao Sumai Hussein Hassani (38) alitibiwa na kuruhusiwa ambapo wengine wawili wanaendelea na matibabu.

HUYU NDIYE MZUNGU ALIYEKAMATWA NA KILO 5 ZA MADAWA YA KULEVYA UWANJA WA NDEGE DAR-ES-SALAAM

Raia wa Henellic, Alexamdrios Atanasios, amekamatwa maafisa wa usalama wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jumapili usiku Februari 24, 2014, akiwa na kilo tano za madawa ya kulevya.

Habari zinasema mzungu huyo alikamatwa wakati wa upekuzi, akijiandaa kupanda ndege ya Swiss air kueleke jijini  Zurich, Uswisi.
Madawa hayo yalikutwa yakiwa yamefichwa kwenye “sakafu” ya begi lake baada ya mitambo ya kisasasa yaupekuzi, kugundua kuwa kulikuwa na ‘mzigo’.
Habari zinasema, kwa sasa mtuhumiwa anashikiliwa kwenye kituo cha polisi cha uwanjani hapo  akisubiri taratibu za kisheria ili afungukliwe mashtaka.

Binti wa kitanzania abakwa na kuafriki dunia....Alikuwa nchini China AKIJIUZA , Wanaume watano wa kinigeria wadaiwa kuhusika


Kumeibuka mchezo mchafu, kuna Watanzania wanawachukua warembo nchini na kuwapeleka China kwa ahadi kwamba wanakwenda kufanya kazi saluni, wakifika kule wanawanyang’anya paspoti na kuwauza kwa wanaume (ukahaba), sasa yamemkuta Mbongo aitwaye Sabrina au Habiba....

Habari za uhakika kutoka kwa chanzo chetu nchini humo zilisema kuwa, Sabrina (24), alifariki dunia Alhamisi iliyopita kufuatia kubakwa na wanaume watano, raia wa Nigeria ambao wamo nchini humo kibiashara.
 
Tukio hilo lilijiri kwenye hoteli moja iliyopo kwenye Mji wa Guangzhou ambao umejaa wageni wengi, wakiwemo Watanzania.
 
SIKU YA TUKIO
Rafiki wa karibu wa Sabrina, Saada alisema siku ya tukio, marehemu akiwa katika harakati zake za kutafuta wateja alikutana na Mnigeria mmoja ambaye walipatana kulala wote kwa usiku mzima.

“Kumbe yule Mnaigeria alikuwa na wenzake wanne. Usiku walimwingilia wote kwa nguvu kwa kumbaka mpaka akapoteza maisha palepale. Ni ukatili mkubwa.
 
“Wale watu walipogundua Sabrina amekufa waliuchukua mwili wake na kuutupa chini kutoka ghorofa ya tano,” alisema rafiki huyo.
 
MAITI YAKUTWA HAINA FIGO, MOYO
Habari zaidi zilidai kuwa mpaka juzi (Jumamosi) madaktari waliokuwa wakiuchunguza mwili wa Sabrina waligundua hauna figo na moyo, jambo linalozidi kuzua hofu juu ya muaji yake.
 
NI BIASHARA ILIYOIBUKA CHINA?
Ilidaiwa kuwa nchini China imeibuka biashara ya viungo mbalimbali vya binadamu ambapo ili vipatikane ni lazima mwenye viungo hivyo auawe kwa njia yoyote.
 
SABRINA AFA, MGANDA APOTEA
Mtoa habari wetu alisema wakati Wabongo wakiwa kwenye maombolezo ya kifo cha Mtanzania huyo, mrembo mwingine raia wa Uganda, nchi ambayo imo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki amepotea katika mazingira ya kutatanisha nchini humo.
 
Baadhi ya watu wana wasiwasi kuwa kupotea kwa msichana huyo kunahusiana na kushamiri kwa biashara ya viungo vya binadamu.
 
SABRINA ALIKWENDAJE CHINA?
Mwezi Julai, mwaka jana, Sabrina alikwenda nchini humo akidanganywa na mwanamke mmoja kwamba atapata kazi kwenye saluni ya wanawake lakini baada ya kufika alijikuta akiingizwa kwenye biashara ya ukahaba bila ridhaa yake mpaka alipokutwa na mkasa huo uliopoteza maisha yake.
 
TAHADHARI KWA WAREMBO WANAOKWENDA CHINA KUFANYA KAZI SALUNI
Imebainika kuwa, kumeibuka wimbi la Wabongo wanaofanya ‘uwakala’ wa kuwachukua wasichana wa Kitanzania kwa kuwadanganya kwamba wanakwenda kufanya kazi za saluni nchini humo.
 
Mara baada ya kufika, wasichana hao hunyang’anywa paspoti ili washindwe kuondoka nchini humo na kushinikizwa kujiuza (ukahaba) huku waliowapeleka wakipokea fedha kutoka kwa wateja.
 
KUIKOMBOA PASPOTI
Habari zilisema kuwa mhusika hurejeshewa paspoti yake baada ya malipo yake kwa ‘wakala’ kufikia dola za Marekani 8,000 (kama shilingi milioni 12), ndipo huachiwa ‘huru’ kuendelea na maisha yake.
 
Wengi wakishaachiwa hushindwa kurejea Bongo na kujikuta wakiendelea kuuza miili katika mahoteli na klabu huku wakikutana na majanga mbalimbali.
 
MASOGANGE, KAJALA NA DIDA
Watanzania waishio nchini humo wamewatahadharisha mastaa wa Bongo, wakiwemo Mtangazaji wa Radio TimesFM, Khadija Shaibu ‘Dida’, msanii wa filamu Kajala Masanja na Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’ ambao hupenda kwenda nchini humo kwa shughuli zao, kutokubali kuwa karibu na mawakala wa kuchukua wasichana Bongo kwa kuwadanganyia kazi ya saluni kwani wanaweza kujikuta pabaya siku moja.
 
DIDA
Ijumaa Wikienda lilimsaka Dida siku ya Jumamosi iliyopita na kumuuliza kuhusu kuwepo kwa mawakala hao ambapo alikiri kusikia huku akisema warembo wenyewe wanapaswa kuwa macho na udanganyifu huo.
 
“Najua wapo Wabongo wanaofanya shughuli hiyo, si China tu hata India, unapelekwa kwa ahadi ya kazi ya saluni, ukifika hamna cha saluni wala nini? Warembo wawe makini jamani, nenda China kama una uwezo wako mwenyewe kufanya ‘shoping’ lakini si kupelekwa,” alisema Dida.
 
BALOZI WA TANZANIA-CHINA
Juzi, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Balozi wa Tanzania nchini China, Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo ili azungumze lolote kuhusu tukio la Sabrina, lakini simu yake ilionekana kutokuwa hewani kwa muda mrefu.

**
Source:  Gazeti  la   Ijumaa Wikienda/GPL

Milipuko miwili ya mabomu yautikisa mji wa Zanzibar...



Milipuko  miwili  inayosadikiwa  kuwa  ni ya  mabomu imetokea  katika  maeneo  mawili  tofauti  mjini  Zanzibar  na  kusababisha  hofu  kubwa  kwa  wananchi....

Mlipuko  wa  kwanza  umetokea  katika  hoteli  ya  Mercury  iliyopo  Forodhani  na  wa  pili  umetokea  kanisa  la  Anglikana  eneo  la  Mkunazini...

Habari  zaidi  zitakuijia  hivi  punde.

Madai ya Wajumbe wa Bunge la Katiba kutaka nyongeza ya posho yagonga MWAMBA .....



Madai ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutaka nyongeza ya posho ya vikao vya Bunge hilo yamegonga mwamba.  
 
Habari kutoka ndani ya kamati iliyoundwa na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho ili kufuatilia madai hayo, zimedai kuwa baada ya uchunguzi wa kina, wajumbe wa kamati hiyo hawakuona sababu ya kupendekeza posho hizo kupandishwa.
 
Taarifa hizo zilidai kuwa wajumbe hao wamefikia uamuzi huo baada ya kupitia viwango vya posho vinavyolipwa na  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali na Mashirika ya Umma.
 
Pia kamati hiyo ilichambua viwango vya posho walivyolipwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na viwango vya posho ya kujikimu vya Sh80, 000 kwa siku wanavyolipwa watumishi wa Serikali.
 
 “Hili jambo linahitaji busara sana na kutazama mazingira ya nchi pia, kwa hiyo wajumbe wale baada ya kuoanisha viwango vya posho vya taasisi mbalimbali wameona Sh300,000 zinatosha,” alisema mmoja wa wajumbe ambaye hakutaka jina lake kutajwa.
 
Mjumbe mwingine, ambaye pia hakutaka kutajwa, alisema kuwa watakaa leo kukamilisha taarifa ya utafiti wao, kabla ya kuikabidhi kwa Mwenyekiti Kificho.
 
Alisema pamoja na umuhimu wa kazi za mbunge, lakini isingekuwa rahisi kuongeza posho katika mazingira ya sasa, ambapo wananchi wanalia hali ngumu ya maisha.
 
Wajumbe hao walioteuliwa na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalumu, Pandu Ameir Kificho ni William Lukuvi, Mohamed Abood Mohamed, Freeman Mbowe,  Paul Kimiti, Jenister Mhagama na Asha Bakari.
 
Awali, taarifa kutoka ndani ya Bunge zilidokeza kuwa wajumbe hao walikuwa wakutane jana saa 9:00 alasiri ili kuandaa ripoti itakayopelekwa kwa Kificho ikiwa imebeba ushauri kuwa kiwango cha sasa cha posho kinatosha. 
 
Sh300,000 wanazolipwa wajumbe wa Bunge Maalamu la Katiba zinajumuisha Sh80,000 kwa siku ambayo ni posho ya kujikimu na Sh220,000 kwa siku kama posho maalumu ya kuhudhuria kikao.
 
Posho maalumu ya Sh220,000 inajumuisha posho ya dereva inayopaswa iwe kati ya Sh40,000 na Sh45,000 kwa siku, usafiri wa ndani (mafuta ama teksi), mawasiliano na matumizi mengine binafsi.
 
Ofisi ya Bunge Maalumu
Alipoulizwa kuhusu jambo hilo mmoja wa makatibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad alisema suala la posho linashughulikiwa na Serikali.
 
“Ninachokifahamu ni kuwa suala la posho limetoka mikononi mwa Kificho na sasa lipo serikalini. Kamati iliyoundwa bado inalishughulikia suala hilo. Hicho ndiyo ninachokifahamu,” alisema Hamad ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wawakilishi.
 
Kwa nyakati tofauti gazeti hili lilimtafuta Kificho, Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya kuzungumzia suala hilo, lakini simu zao za mkononi zilikuwa zikiita bila majibu. 
 
Hoja ya kutaka nyongeza ya posho iliibuliwa na wajumbe wawili ambao ni wabunge wa CCM waliodai kuwa kiwango cha Sh300,000 wanacholipwa, hakitoshi kwa kile walichodai kuwa ni kuishi Dodoma ni gharama kubwa. 
 
Hata hivyo uchunguzi wa kina umebaini kuwa baadhi ya wajumbe wanaishi katika hoteli za kati ya Sh20,000 na Sh40,000 kwa siku huku baadhi yao wakiishi katika hosteli kwa Sh8,000 kwa siku.
 
Mmoja wa wajumbe, Augustino Mrema alidai kuwa baadhi ya wajumbe wanataka kuligeuza Bunge hilo ‘shamba la bibi’ kwa kudai posho zaidi kwa kisingizio cha kupanda gharama za maisha.
 
Mrema alisema kiasi cha Sh300,000 wanacholipwa wajumbe kinatosha kwani zipo hoteli nzuri za kati ya Sh15,000 hadi Sh40,000 ambazo zina hadhi na sifa ya kuishi wajumbe wa Bunge la Katiba. 
 
“Mjumbe ameamua kwenda kuishi chumba cha Sh200,000 wakati akijua atalipwa posho ya Sh300,000 halafu analalamika kupanda kwa gharama za maisha, hizi gharama zimetengenezwa,” alisema Mrema. 
 
Alisema gharama za teksi kutoka bungeni hadi maeneo ya Area C na D haizidi Sh12,000 wakati chakula kinaanzia Sh6,000 hadi Sh20,000 na kuhoji iweje Sh300,000 zionekane hazitoshi.
 
Hoja ya baadhi ya wajumbe kudai posho zaidi imepigiwa kelele nchi nzima huku wananchi wakimtaka Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge hilo, kama wataendelea kung’ang’ania kupanda kwa posho. 
 
Mjumbe mwingine wa Bunge hilo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro ameahidi kuanzia leo kukusanya saini za wajumbe wanaopinga suala hili ili ampelekee Rais Kikwete kama ushahidi.

>>Mwananchi

Picha kutoka bungeni: Waziri mkuu akiwa na wajumbe wa bunge maalumu la katiba mjini Dodoma leo


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba na Mbunge wa Zamani wa Morogoro, Shamim Khan, nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Februari 24, 2014. Kulia ni mbunge wa Sumve Richard Ndassa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba na Mbunge wa Zamani wa Morogoro, Shamim Khan, nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Februari 24, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Singida Magharibi Mohamed Bissanga na Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa ,wote wakiwa ni wabunge wa Bunge Maalum la Katiba, nje ya ukumbi wa Bunge Mjiji Dodoama Februari 24, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo, Pinda akizungumza na Katibu wa Bunge, Thomas Kashilillah, nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Februari 24, 2014. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)

AFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KOSA LA KUMNAJISI MTOTO...!!

MKAZI wa mtaa wa Nsemulwa, Athuman Mussa (54) amehukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumnajisi mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne mdomoni.


Hukumu.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Chiganga Ntegwa baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka uliongozwa na Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Ally Mbwijo.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Juni 26 mwaka jana saa 12:00 jioni nyumbani kwake katika mtaa wa Nsemulwa katika Mji wa Mpanda.

Kumnajisi Mtoto

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Ntengwa alieleza kuwa siku hiyo ya tukio mshitakiwa alimkuta mtoto huyo ambaye wazazi wake ni jirani zake akiwa anacheza na watoto wenzake karibu na nyumba yake akamwita na kuingia naye ndani akiahidi kumpatia zawadi ya pipi aina ya jojo.
Baada ya mtoto huyo kuingia ndani ya nyumba, Athumani alimvuta kwenye kochi sebuleni na kisha alimwingizia uume wake kwenye mdomo wa mtoto huyo hadi hapo alipomaliza haja yake kisha akamwamuru aondoke nyumbani kwake ndipo mtoto huyo alipotoka mbio na kurejea kwao akilia.

 Kumnajisi
Aliiambia mahakama baada ya mtoto huyo kufika nyumbani kwao mama yake alimuuliza kilichomfanya alie ndipo alitema mbegu za kiume ambazo zilikuwa mdomoni mwake na kisha alimwelezea mama yake kila kitu alichotendewa na mshitakiwa.
Baada ya mama kuelezwa unyama huo wa Kumnajisi mtoto wake, naye alianza kulia kwa nguvu na kusababisha majirani kufika nyumbani hapo ambapo walielezwa alichofanyiwa mtoto huyo ndipo majirani walikwenda nyumbani kwa mshitakiwa wakamkamata na kumfikisha kwenye kituo cha polisi Wilaya ya Mpanda Jijini DAR.
Source: Habari L

UPDATE: MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YATANGAZWA RASMI LEO...!! YATAZAME HAPA..


Baraza la Mitihani la Tanzania limetangaza matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 na kiwango cha ufaulu Kimeongezeka kwa asilimia kati ya 0.61 na 16.72 ukilinganisha na mwaka 2012. 

Jumla ya watahiniwa laki 235,227 sawa na asilimia 58.25 ya waliofanya mtihani wamefaulu.  

Wanafunzi 74,324 sawa na asilimia 21.09 wamefaulu katika madaraja ya I -III.

Wavulanawaliopata daraja la kwanza (division one) ni 5,030 na wasichana ni 2,549 
 
Waliopata daraja la pili (Division 2) Wavulana ni 14,167 na wasichana ni 7,561

Waliopata daraja la pili (Division 2) Wavulana ni 14,167 na wasichana ni 7,561.  Wavulana waliopata daraja la tatu (Division 3) ni 27,904 na wasichana ni 17,113.

Jumla ya wanafunzi waliopata daraja la 4 (division 4) ni laki 126,828, wasichana wakiwa 62,841 na wavulana 63,987. 
 
Jumla ya wanafunzi laki 151,187 wamepata '0' (division ziro) . Wasichana ni 72,237 na wavulana ni 78,950.



 Bofya  hapo  juu  kuyatazama

SIMANZI...!! MFUNGWA AOMBA kuahirishwa adhabu ya kunyongwa KWAKE ILI AMPATIE MAMA YAKE FIGO ,AMBAYE NI MGONJWA..

Ronaldo Phillips mfungwa anayetarajiwa kunyongwa Marekani
Hukumu ya kunyongwa kwa Ronald Philllips aliyepatikana na hatia ya kumuua mtoto wa miaka mitatu katika jimbo la Ohio nchini Marekan imeahirishwa kutokana na mshitakiwa huyo kuomba kuchangia baadhi ya viungo vyake vya mwili zikiwemo figo ili kunusuru uhai wa mama anayeumwa.

Ronald Phillips alitarajiwa kunyongwa Alhamis kwa njia ya sindano ya sumu baada ya kupatiakana na hatia ya kumuua mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu mwaka 1993
 Gavana wa jimbo la Ohio John Kasich amesema kama ombi hilo la mshitakiwa litasaidia kuokoa uhai wa mtu mwingine basi na likubalike, lakini litakuwa jambo geni kuahirishwa kwa adhabu iliyokwisha kupitishwa japo kuwa madaktari wanapaswa kuthibitisha.
Phillips mwenye umri wa miaka 40 alihukumiwa kifo kutokana na makosa ya ubakaji na mauaji ya binti wa rafiki yake wa kike Sheila Marie Evans.

Dawa ya sumu iliyotarajiwa kutumika kumuua Phillips ni aina ya midazolam na hydromorphone, mchanganyiko wa dawa ambayo ingetumika kwa mara ya kwanza nchini Marekani kunyonga watu
Jimbo la Ohio liliamua kutumia mchanganyiko wa dawa hii kwa sababu haikuwa na kiasi cha kutosha cha dawa ya kawaida inayotumika kunyongea watu ijulikanayo kama pentobarbital.

Mama mzazi wa Phillips amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya figo na dada yake Phillips pia anasumbuliwa na maradhi ya moyo ambapo anasema anahitaji kutoa viungo vyake haraka iwezekanavyo

Rais Kikwete awasili nchini akitokea London ambapo alihudhuria Mkutano uliojadili mbinu za kupambana na Ujangili duniani



Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadik akimpokea Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere akitokea London Uingereza ambapo alihudhuria Mkutano uliojadili mbinu za kupambana na Ujangili duniani.Mkutano huo uliandaliwa na mwana mfalme wa Uingereza Prince Charles.(picha na Freddy Maro)

"Siyo vibaya kwa wanaotaka kuwania urais kutangaza nia mapema, kwa sababu inawapa nafasi wananchi kuwapima"....Hii ni kauli ya January Makamba baada ya kuhojiwa na kamati ya maadili jana



Kamati ndogo ya Maadili ya CCM imeendelea kuwahoji wanachama wake walioonyesha nia ya kuwania urais, jana ilikuwa zamu ya mawaziri watatu. 
 
Waliotarajiwa  kuhojiwa jana ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba.

 Makamba alikuwa wa kwanza kufika mbele ya kamati hiyo jana asubuhi, huku Wassira akifuatia. Hata hivyo, Membe hakuonekana.
 
Hata hivyo, kanuni za uongozi wa maadili za CCM kifungu cha 7 (i) kinaeleza kuwa wanachama wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi katika muhula unaofuata, yaani ubunge, uwakilishi, udiwani na nafasi nyingine katika chama wanaweza kutangaza nia zao, lakini hawaruhusiwi kufanya kampeni kabla ya muda uliowekwa rasmi, muda wa kampeni unaanza baada ya majina ya wagombea kuteuliwa na kikao kinachohusika.
 
Makamba
Baada ya kuhojiwa Makamba, alisema siyo vibaya kwa wanaotaka kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kutangaza nia mapema, kwa sababu inawapa nafasi wananchi kuwapima.
 
Mbali na hilo Makamba alisema siyo dhambi kwa mtu kuonyesha nia, bali ni dhambi kwa mtu kutoa fedha kwa nia ya kutaka uongozi na kuvitaka vyombo vya dola kuchukua hatua za kisheria kwa watu wa aina hiyo.
 
Kikao hicho kinachoongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara, Philip Mangula, juzi kiliwahoji mawaziri wakuu wa zamani Edward Lowassa na Fredrick Sumaye pamoja na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini.
 
“Ipo faida ya kuwajua mapema wanaotaka uongozi kuliko kuwajua mwishoni, kwa sababu mnapata faida ya kuwachambua na kuwauliza maswali, mbaya ni mtu kutoa pesa ama kutumia pesa.
 
“Hata katika maoni yangu na ushauri (ndani ya kikao hicho cha maadili), nimesema kwamba hilo ndilo kubwa na la msingi, kwa sababu linawaweka pembeni watu wenye vipaji vya uongozi kama huna fedha basi huwezi kuwa kiongozi,” alisema Makamba.
 
Alisisitiza matumizi ya fedha katika kutafuta uongozi yanakatazwa kwa mujibu wa kanuni za chama chao na sheria za nchi na kwamba ushahidi unapopatikana chama kifanye kazi yake na Serikali ichukue hatua dhidi yao.
 
Makamba alisema ipo sheria ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ambazo zote zinakataza matumizi ya fedha.
 
“Kwa hiyo hawa wanaotajwa wanatumia fedha vilevile vyombo vya dola viwachukulie hatua, siyo tu kwenye chama,” alisema Makamba.

Makamba alisema kuwa mazungumzo yao ndani ya kikao hicho yalikwenda vizuri, akidai yeye hakuitwa kwa ajili ya kugawa fedha kwa wananchi na wala hakukuwa na shitaka lolote, isipokuwa ilikuwa ni kutoa ushauri na kukumbushana kuhusiana na misingi muhimu ya chama chao ya namna ya kupata uongozi.
 
“Kwa hiyo nilipata fursa nzuri ya mimi kutoa ushauri wangu kuhusiana na namna ambavyo tunaweza kuyafanya mambo haya vizuri zaidi, na namna ambayo tunaweza kutafuta uongozi kwa namna nzuri zaidi badala ya kukigawa,”alisema.
 
Makamba alisema kuwa mazungumzo yao yalikuwa mazuri sana na kwamba hakukuwa na jambo baya, wala hakuwa ameshitakiwa bali walikuwa katika majadiliano ya kawaida ya ndani ya chama na kuwa aliitwa kutokana na kutajwatajwa na wanachama.
 
Wassira
Kwa upande wake Wassira alisema hana mpango wa kutangaza kugombea urais leo wala kesho, lakini muda ukifika ataamua.
 
Alisema: “Kutamani nafasi ya urais siyo dhambi.”
Wassira alisema yeye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hawezi kutoboa mtumbwi ndani ya chama, halafu waangamie wote.
 
Alisema hajafanya vurugu zozote ndania ya chama na kwamba katika kikao cha jana aliitwa kwa ajili ya kujitathimini na kuangalia mustakbali wa chama katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
 
Ripoti ya kamati hiyo ya maadili ya chama huenda ikawasilishwa kwenye mkutano Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), unaotarajiwa kufanyika leo mjini Dodoma.
 
Akizungumzia suala hilo mwishoni mwa wiki iliyopita, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Philip Mangula alisema mwanachama yeyote wa chama hicho hatakiwi kutoa michango, misaada, zawadi kwa mtu au katika shughuli yoyote bila kupata ridhaa ya uongozi.
 
“Kufanya jambo hilo ni kwenda kinyume na kanuni za chama. Ndani ya chama kila ngazi ina Kamati ya Maadili, wote ambao wameanza kwenda kinyume na kanuni za chama watahojiwa katika kamati hizo,” alisema Mangula na kuongeza:
 
“Hairuhusiwi kuwasafirisha wajumbe, kuwapa malazi, chakula, vinywaji na ukifanya hivyo utakuwa unakwenda kinyume na utaratibu uliowekwa na Kamati ya Sheria, Katiba na Kampeni.”

Akihutubia kilele cha maadhimisho ya miaka 37 tangu kuzaliwa kwa chama hicho, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete aliziagiza Kamati za Maadili na Usalama, kuwachukulia hatua stahiki viongozi na wanachama wake wanaomwaga fedha ili kupata uongozi.
 
Kadhalika, Rais Kikwete alipozungumza na wajumbe wa Halmashauri ya CCM ya Mkoa wa Mbeya, alisema kuanza kwa kampeni kabla ya wakati wake ni moja ya mambo yanayosikitisha na kwamba suala hilo limekabidhiwa kwa Mangula kwa hatua zaidi za kinidhamu.

>>Gazeti  la Mwananchi.

Skendo ya Rose Mhando: Mapya yaibuka, katibu wa chama cha injili apasua jipu



Siku chache baada ya staa wa Injili Bongo, Rose Muhando kudaiwa kutiwa mbaroni kwa utapeli wa shilingi milioni 6, nyuma ya skendo hiyo, mapya yameibuka.

Kwa mujibu wa Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Stella Joel, mara kadhaa Rose alishaingia kwenye skendo nyingi kutokana na jamaa aliyetajwa kwa jina la Nathan Wami.
 
Alisema katika albamu ya Rose ya kwanza kabisa iitwayo, Jipange Sawasawa alijikuta akiingia kwenye balaa la kubambikiwa msala wa kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya ambapo katika mazingira yeye utata, staa huyo alijikuta akiziachia shilingi milioni 30 bila kujijua kwa baadhi ya polisi wa Dodoma. Hiyo inadaiwa ilikuwa ‘karibisha mgeni’.

Stela alifafanua kuwa, hata msala ambao ulimfikisha Rose korokoroni katika Kituo cha Polisi  cha Msimbazi Dar hivi karibuni siyo wa shilingi milioni 6 kama ilivyoelezwa awali bali ni sh. milioni 2 ambazo si yeye aliyezipokea bali ni mwanaume huyo.
 
Alieleza kuwa katika msala huo wa  milioni 2 alizodaiwa kuchukua na kushindwa kwenda kufanya shoo Mombasa, Kenya, staa mwenzake wa Injili, Jennifer Mgendi alidaiwa kujua kila kitu alikataa kwenda Msimbazi kumtoa Rose akidai kuwa hajui chochote.
 
Stella alifunguka: “Tofauti na watu wanavyojua, Nathan hakuwahi kuwa meneja wa Rose bali alikuwa ni msaidizi wake tu. Kwa hiyo si kweli kusema eti Nathan aliamua kumwacha mwimbaji huyo kwa kisingizio cha kukosa mwelekeo.
 
“Msada pekee wa Nathan kwa Rose ni kumlipia gharama za studio alipokwenda kurekodi kwa mara ya kwanza wakati Rose akiwa anasali Kanisa la Saint Mary, Chimuli, Dodoma. Ila kama mlivyiosema kwenye gaeri la Ijumaa (Wikienda) kuna mengi yapo nyuma ya pazia.
 
“’Ukichaa’ wa Rose ni pale alipokosea akaenda na Nathan, Cosota (chama cha hatimiliki) na kuingia makubaliano kwa maandishi kwamba huyo Nathan ndiyo awe analipwa mrabaha (sehemu ya mapato) ya kazi zote za Rose. Ni juzijuzi tu ndiyo Rose akaniagiza mimi nikamtengulie huo mkataba,” alisema katibu huyo ambaye pia ni mwimba Injili.
 
Aliendelea kufafanua kuwa mikataba yote ya kazi za Rose alikuwa akisaini Nathan hadi mwimbaji huyo alipochukuliwa na lebo kubwa ya Sony inayosimamia kazi zake kwa sasa.
 
Akaongeza: “Kama pesa yote ingekuwa inaingia mikononi mwa Rose asingekuwa hivi alivyop leo. Fikiria mpaka sasa Rose ana gari moja tu (Toyota Prado), viwanja 3 na shamba la eka 100 pale Dumila, basi (Morogoro).”
 
Kwa upande wake, Rose alisema kuwa Nathan alimfanya mashine ya kutoa na kuweka fedha benki (ATM).

Nathan alipoulizwa juu ya madai yote hayo alijibu kwa sauti yenye uhakika: “Hayo madai si ya kweli. Mimi nimeishi na Rose kwa zaidi ya miaka 12. Mimi ndiye niliyemsaidia yeye. Asingekuwa alivyo sasa kama si mimi.” 

>>Risasi Jumamosi/ GPL

Rais Atangaza majina ya wajumbe wa bunge la katiba ....Bofya hapa kuyaona



UTANGULIZI
1. Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.

2. Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:
(i) Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(iii) Wajumbe 201 kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.

3. Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-

(i) Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)
(ii) Taasisi za Kidini (20)
(iii) Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);
(iv) Taasisi za Elimu (20);
(v) Watu wenye Ulemavu (20);
(vi) Vyama vya Wafanyakazi (19);
(vii) Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii) Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);
(ix) Vyama vya Wakulima (20); na
(x) Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).

4. Mchakato wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13 Desemba, 2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha, Tangazo hilo la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe 02/01/2014.
 
5. Mapendekezo hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

6. Kufuatia mwaliko huo, taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao. Mapendekezo hayo yalijumuisha majina 2,762 kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar mapendekezo hayo yalihusisha watu 874. Hivyo basi, taasisi na makundi mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina 3,636. Lakini, na kinyume na Sheria, watu 118 walijipendekeza wenyewe na kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.

7. Mchanganuo wa idadi ya watu walipendekezwa katika makundi mbalimbali ni kama ifuatavyo:

***Orodha  ni  ndefu  sana. << BOFYA  HAPA  KUONA  MAJINA  HAYO >>


Bofya  hapo  juu

DUDE NAE ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE 2015

WIMBI la wasanii kuingia kwenye siasa limeendelea kushika kasi ambapo awamu hii msanii wa maigizo na filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ametangaza kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

‘Akistorisha’ na paparazi wetu, Dude alisema kutokana na sanaa kutotoa masilahi ipasavyo, ameamua kuingia kwenye ulingo
DUDE
WIMBI la wasanii kuingia kwenye siasa limeendelea kushika kasi ambapo awamu hii msanii wa maigizo na filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ametangaza kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

‘Akistorisha’ na paparazi wetu, Dude alisema kutokana na sanaa kutotoa masilahi ipasavyo, ameamua kuingia kwenye ulingo wa siasa ambapo anatarajia ‘kunyakua’ Jimbo la Tabora Mjini ambalo kwa sasa linaongozwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage.
“Natarajia kugombea ubunge nyumbani kwetu Tabora mjini, niko tayari kuchuana na Rage na kwa sasa  nipo katika maandalizi ikiwemo kuwa karibu na wananchi kwani  wananikubali sana, hivyo natarajia ushindi tu,” alisema Dude.

Mvua kubwa yenye upepo yaharibu nyumba zaidi ya 10 Ilolo jijini mbeya






Bibi Enea mwenye umri zaidi ya miaka 80 mkazi wa Ilolo akituonyesha jinsi maji yalivyoharibu vitu vyake


 
 





Kanisa la Moravian Ilolo likiwa limejaa maji ndani



Hakika inasikitisha watoto hawa wametoka shule wanakuta nyumba yao imebomoka na mvua kubwa ilionyesha jijini Mbeya  wazahi wa watoto hao hawakuwepo nyumbani




 
 

 
 


>> mbeya yetu
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger