KAZI inaanza
tena! Supastaa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’
anapanda katika kizimba cha Mahakama Kuu ya Tanzania kwa yale madai ya
kumuua bila kukusudia, aliyekuwa nyota wa muvi nchini, marehemu Steven
Charles Kanumba ‘The Great’, Risasi Jumamosi limeambiwa.
Supastaa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Akizungumza
na gazeti hili juzi jijini Dar es Salaam, mtoa habari ambaye aliomba
hifadhi ya jina alisema kuwa, Februari 17, mwaka huu, staa huyo
atatakiwa mahakamani hapo kwa ajili ya kesi yake kuanza huku akisema,
kuna mabadiliko kidogo katika kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’.
ITAKUWAJE?
Kwa
mujibu wa mtoa habari huyo, Lulu mwenye umri wa miaka 18, atasomewa
upya mashitaka dhidi yake ambapo atatakiwa kujibu tena kama anakubali
aliua bila kukusudia au la!
“Elizabeth (Lulu) atasomewa upya mashitaka ya kumuua Kanumba bila kukusudia.
“Ataulizwa
ni kweli au si kweli? Atatakiwa kujibu swali moja kati ya hayo mawili,
kama ni kweli atasema kweli kama si kweli atasema si kweli,” kilisema
chanzo hicho huku kikisisitiza jina lake lisichorwe gazetini.
MUDA WA KESI SIKU 730
Habari zaidi zikadondokea Dawati la Risasi Jumamosi na
kusema kwamba, kesi hiyo itaendeshwa kwa siku mia saba na thelathini
(730), kwa maana ya miaka miwili hadi hukumu itakapotolewa.
NI NDANI YA SHERIA MPYA
Katika
Siku ya Sheria Duniani iliyoadhimishwa jijini Dar es Salaam, Februari
3, mwaka huu, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman alisema
kuanzia sasa kesi zote za jinai zitatakiwa kumalizika katika kipindi cha
miaka miwili.
Kesi ya Lulu nayo ni ya jinai na kwa sababu hiyo, hadi Februari ya mwaka 2016 itatakiwa iwe imemalizika.
Wakili wa Lulu, Peter Kibatala.
WAKILI WAKE
Chanzo
hicho kililithibitishia gazeti hili kwamba, Lulu atatetewa na yuleyule
wakili wake mwenye ‘ngekewa’ ya kuwatetea watu maarufu nchini, Peter
Kibatala.
Kibatala
ameshawahi kuwa wakili wa Mbongo Fleva, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’
katika kesi ya madai ya kuiba ‘power window’ za gari la msanii mwingine
wa Bongo Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
Pia
aliwahi kumwakilisha wakili mwezake, Mabere Nyaucho Marando kwenye kesi
ya Mbongo Fleva, Judith Wambura ‘Jide’ alipoburuzwa kortini na uongozi
wa Clouds Media Group baada ya Marando kuwa na udhuru.
Ilibaki
kidogo awe wakili wa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu katika kesi
ya kumpiga makofi meneja wa hoteli moja (jina tunalo) iliyopo Kawe
Beach, Godluck Kuyumbu lakini akakosa sifa baada ya shauri hilo
kusiklizwa Mahakama ya Mwanzo Kawe, Dar.
HAWA HUENDA WAKAITWA
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, katika kesi hiyo huenda wakaitwa watu ambao watasaidia kutoa ushahidi.
Watu
hao ni wale waliokuwa na ukaribu na marehemu, hasa siku ya tukio au
kushirikishwa kwa namna moja au nyingine kwa jinsi ambavyo waendesha
mashitaka wataona.
DOKTA KIDUME
Aliyekuwa
akimtibu Kanumba, Dokta Kidume anaweza kufika mahakamani hapo kwa
sababu ndiye aliyekuwa mtu wa pili kufika kwenye chumba cha marehemu
mara baada ya kuanguka.
Mdogo’ wa marehemu Kanumba, Seth Bosco.
SETH BOSCO
Huyu
ni ‘mdogo’ wa marehemu Kanumba, yeye siku ya tukio alikuwa nyumba moja
na marehemu, ila vyumba tofauti. Ndiye aliyemwona Kanumba akiwa katika
hali mbaya baada ya kutoelewana na Lulu na kukimbia kumwita Dokta
Kidume.
Hawa
wote walishahojiwa na Jeshi la Polisi Tanzania katika Kituo cha
Oysterbay, Dar, mara baada ya kifo hicho. Seth alihojiwa mara tano.
TUJIKUMBUSHE
Kanumba
alifariki dunia Aprili 7, 2012 nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es
Salaam. Kifo chake kilidaiwa kilitokana na kuangukia sehemu ya nyuma ya
kichwa na hivyo kuufanya ubongo kutikisika (brain concussion).
Hata
hivyo, baadaye ilifahamika kuwa, sehemu ya maini na majimaji ya machoni
vilipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kulikuwa na
sumu au kitu kingine katika mwili wa Kanumba. Majibu hayajatoka hadi
leo.
WAKILI KIBATALA
Risasi
Jumamosi lilimsaka Wakili Kibatala kwa njia ya simu ili kumsikia
alichonacho kufuatia kesi ya mteja wake kuanza kusikilizwa ambapo
alisema:
“Tutakutana mahakamani jamani, kwa sasa niko bize sana.”
LULU
Juzi,
simu ya Lulu ilipigwa kwa muda mrefu lakini haikupokelewa huku baadhi
ya watu wake wa karibu wakisema kuwa, staa huyo ameasisi tabia mpya ya
kutopokea simu zenye namba ngeni machoni mwake.
-GPL