Showing posts with label Dini. Show all posts
Showing posts with label Dini. Show all posts

MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMBAYE WATU WENGI HUDHANI KWAMBA NI YESU MWENYEWE...

 
Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi. 

Ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.

Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS''
  Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji. 

 
Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.

Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.


Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.


watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu.

Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.

 
Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi

Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.


watumishi wa Mungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya Yesu katika uinjilisti huko Kongo.
 Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu.

Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa takwimu za mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.

Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu.

kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia ya iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.

MTOTO AMVAMIA PAPA FRANCIS NA KUMHAG NA KUCHEZA MBELE YA MAELFU HUKO VATICAN CITY..



Today in viral photos: over the weekend, a brave little boy walked up to Pope Francis while he was giving a speech and hugged him. The youngster was part of a group of children who were invited to sit near the Pontiff as he addressed an audience of families in St. Peter’s Square during the plenary assembly of the Pontifical Council for the Family at the Vatican on Oct. 26. The youngster wouldn’t leave the Pope’s side, even though cardinals tried to guide him off stage. But the Pope was cool about it and even let him sit in his big white chair at one point.

MAMA RWAKATARE ATENGWA NA MAKANISA KWASABABU YA ILE NDOA ALIYOFUNGISHA YA MBUNGE WA CCM ALIYEOLEWA NA KIJANA MDOGO...

 

MBUNGE wa Viti Maalumu, Mchungaji Getrude Rwakatare (CCM) wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, ametengwa katika Ushirikiano wa Makanisa baada ya kanisa lake kulalamikiwa kufungisha ndoa inayodaiwa kukiuka taratibu za kikanisa, kisheria na kimaadili, Tanzania Daima Jumatano limejulishwa.Ndoa inayolalamikiwa kufungishwa na kanisa hilo ni ile iliyoibuliwa na gazeti hili wiki iliyopita ambayo inamhusisha Mbunge  wa Viti Maalumu, Rosweeter Kasikila (CCM) mwenye umri wa miaka 60 na kijana Michael Christian wa miaka  26.


Ndoa hiyo ambayo ilifungwa katika kanisa hilo Septemba Mosi mwaka 2011, imebaki kuwa gumzo na kuwaacha hoi baadhi ya mawaziri, wabunge pamoja na majirani wanaoishi jirani na mbunge huyo mjini Bagamoyo, Pwani.
 
Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Haki za Jamii ya makanisa hayo, Mchungaji William Mwamalanga, alisema uamuzi wa kulitenga kanisa la Mama Rwakatare umetokana na kikao cha Kamati ya Maadili iliyokutana jana jijiji Dar es Salaam.
Alisema Kanisa la Mchungaji Rwakatare halifai kuendelea kuwa katika ushirika huo kutokana na kubariki ndoa hiyo aliyodai kuwa ni batili.
 
Mchungaji Mwamalanga alisema utaratibu wa ndoa katika makanisa unafahamika, ikiwa ni pamoja na wafungaji wa ndoa kutakiwa kutangaza ndoa hiyo hadharani kwa kipindi cha wiki tatu.
“Ndoa hii haikutangazwa hadharani, kibaya zaidi inasemekana imefungwa ndani ya ofisi na sio kanisani. Hiyo haiwezi kuitwaa ndoa maana haijakidhi vigezo na taratibu za kikanisa, ni lazima Mchungaji Rwakatare awajibike,” alisema.
 
Alisema lazima nyumba za ibada zikubali kutogeuzwa kichaka cha kusaidia uovu kama ilivyofanywa na kanisa hilo la Mikocheni B kwa kukubali kufanikisha ndoa hiyo kinyume cha taratibu.
“Tunalaani ndoa hiyo kuanzia mawio hadi machweo kwa kuwa hata maandiko ya kitabu kitakatifu cha Biblia kinawathamini yatima kama alivyo huyo kijana Michael anayeonekana kutoafiki ndoa hiyo kwa matakwa yake,” alisema mchungaji huyo.
 
Alisisitiza kuwa wanamtenga Mchungaji Rwakatare na kanisa lake kwani amewachafua  na kuyatia aibu makanisa mengine yote nchini.
 
Mchungaji huyo pia alimtaka Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete kuwaengua kwenye chama hicho Mchungaji Rwakatare na Kasikila kuhusiana na ndoa hiyo.
“Rwakatare ni mtunga sheria, anajua wazi kuwa ndoa inatakiwa pia kubandikwa katika ubao wa matangazo. Ni wazi kuwa wameamua kuvunja sheria na kutenda kosa la jinai,” alidai.
 
Mwamalanga alisema kuwa kwa hatua hiyo ndoa hiyo ni batili na haramu kwa kuwa ni aibu pia kwa mtoto kumuoa mwanamke mwenye umri wa mama yake.
 
Katika hatua nyingine, mchungaji huyo alisema umoja wao unafanya kila iwezalo kuhakikisha kijana Michael anarudishiwa vyeti vyake ambavyo kwa sasa vimezuiliwa na Mbunge Kasikila.
Pia aliitaka Kamati ya Maadili ya Bunge kuwaita na kuwahoji wabunge hao kwa kitendo chao cha kuhalalisha ndoa hiyo kwani kimeutia doa muhimili huo.
 
Alisema Bunge ni sehemu tukufu, hivyo Rwakatare na Kasikila hawana hadhi ya kukaa huko, hivyo alishauri waenguliwe.
 
Alipopigiwa simu kueleza msimamo wake juu ya uamuzi wa umoja wa makanisa hayo kumtenga kwa kuhalalisha ndoa hiyo, Mchungaji Rwakatare aling’aka na kukata simu.
Alipopigiwa tena simu yake ilizimwa na hakuweza kupatikana tena hadi tunaenda mitamboni.
  

- Tanzania Daima

KUMBE ASKOFU GWAJIMA NI TAJIRI NO.1 MIONGONI MWA MAASKOFU....!!AWANUNULIA WACHUNGAJI WAKE 30 KILA MMOJA GARI,MABASI 20 KWA AJILI YA WAUMINI,ANAINGIIZA MILIONI 3 KWA SIKU...


UCHUNGUZI  wa kina uliofanywa na Gazeti la Uwazi kwa muda wa siku 30 umebaini kuwa Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar, Josephat Gwajima ndiye anayeongoza kwa utajiri wa viongozi wa imani ya Kikristo, hususan wa njia ya kilokole.
Gari la kifahari aina ya Hummer 2 analomiliki Mchungaji Gwajima.
Utafiti huo umefanywa kwa kutembelea makanisa makubwa ya kiroho ya jijini Dar es Salaam na kuomba kuzungumza na viongozi wake ambapo Gwajima alitoa ushirikiano kwa asilimia mia moja kuliko wengine.
MAKANISA YALIYOTEMBELEWA
Makanisa yaliyotembelewa na majina ya viongozi wake kwenye mabano ni pamoja na Full Gospel Bible Fellowship (Askofu Zachary Kakobe), Living Water Center ‘Makuti Kawe’ (Mtume Onesmo Ndegi), Kanisa la Maombezi ‘GRC’ (Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’), Mikocheni B Assemblies of God (Mama Rwakatare) na Kanisa la Efatha (Nabii na Mtume Josephat Mwingira).

Mabasi aliyonunua Gwajima kwa ajili ya waumini wake.
KWA NINI GWAJIMA NI NAMBA MOJA?
Anakuwa namba moja kwa sababu alianika mali zake na kipato chake kingine bila kushikwa na kigugumizi. Gwajima alisema anamiliki gari la kifahari aina ya Hummer 2 ambalo gharama ya manunuzi mpaka kufika Tanzania ni wastani wa shilingi milioni 250.

AWANUNULIA WACHUNGAJI MAGARI
Akizungumza na Uwazi hivi karibuni kwenye ofisi za kanisa lake, Kawe, Dar, Mchungaji Gwajima alisema hivi karibuni aliwanunulia wachungaji wake 30 magari ya kutembelea. Alisema fedha hizo alizitoa mfukoni mwake.





Baadhi ya magari aliyonunua Mchungaji Gwajima kwa ajili ya wachungaji wake.
Baadhi ya magari aliyoyakumbuka ni Subaru Forester (sokoni linauzwa shilingi milioni 17), Mitsubishi Pajero (shilingi milioni 16), Toyota Spacio new model (milioni 20) na Toyota Harrier Lexus (milioni 35).

ANAMILIKI JUMBA LA GHOROFA NNE
Mchungaji huyo alikwenda mbele zaidi kwa kuanika maisha yake ambapo alisema awali alikuwa akiishi kwenye  nyumba ya kupanga iliyopo Mbezi Beach, Dar lakini kwa sasa amehamia katika nyumba yake mpya ya ghorofa nne, mbili zikiwa hazijakamilika. Nyumba hiyo ipo Mbezi Beach.


ANA MABASI 20 KWA AJILI YA KUSAFIRISHIA WAUMINI WAKE
Gwajima: “Pia nimeweza kwa neema ya Mungu kununua mabasi ishirini. Haya ni kwa ajili ya kusafirishia waumini wa kanisa langu wakati wa kuja kwenye ibada na kurudi makwao.”

Alisema mabasi hayo ambayo hakuyataja majina na wala yenyewe hayajaandikwa majina mbele akidai ni ‘oda’ maalum, kila moja alilinunua kwa shilingi milioni 120.

SAFARI YA ULAYA NA MAREKANI KILA MWAKA HUMWINGIZIA SHILINGI MILIONI 192
Akizungumzia kipato, Gwajima alisema mbali na sadaka ambazo huendeleza kanisa, yeye mwenyewe kila mwaka huwa na safari ya Marekani kwenda kufundisha Injili  kama mwalimu.

“Pia nimekuwa nikijipatia fedha kutokana na kazi ya ualimu ambapo kila mwaka mara moja huwa nakwenda nchi za Ulaya na Marekani kufundisha kwa siku 60. Katika siku hizo huwa nalipwa dola za Marekani 2,000 kwa siku,” (kama shilingi milioni 3.2).
Kwa hesabu hiyo, kwa siku sitini Mchungaji Gwajima hukamata shilingi milioni 192 na kurudi nazo Tanzania.


ATAMBA KUWA NA WAUMINI WENGI KULIKO WENZAKE
Gwajima alisema kwa sasa kanisa lake limepanuka ambapo alitamba kuwapa Neno waumini wapatao 70,000 kwa siku hivyo yu mbioni kuanzisha makanisa  mengine  mikoa yote ya Tanzania.

Kiongozi huyo alifafanua kuwa amefanikiwa kuwa na waumini wengi kuliko makanisa mengine kutokana na huduma nzuri anayotoa kwa waumini na jamii kwa jumla.
“Nimefanikiwa kuwa na waumini wengi kuliko wengine kwa sababu nahubiri Neno tu, sirushiani maneno na makanisa mengine.
“Sisi (yeye na wachungaji wake) hatuna utamaduni wa kuwashambulia wachungaji wenzetu. Wao hata wakitusema vipi, sisi tunakaa kimya kwani kujibishana kunaleta mgawanyiko,” alisema Gwajima.


MZEE WA UPAKO
Uwazi lilifika kwa Mzee wa Upako, Ubungo Kibangu, Dar lakini ilikuwa ngumu kumuona, wasaidizi wake wakisema ana huduma ya kiroho.

Hata hivyo, kwa kutumia kumbukumbu za nyuma ambapo mtumishi huyo wa Mungu aliwahi kuhubiria waumini wake (ikaandikwa kwenye Uwazi) akitaja utajiri alionao na mahubiri hayo kurushwa na Channel Ten, alisema:
“Mimi ndiye Mzee wa Upako, nikitoka nje nakuta magari yangu sita, nachagua leo niendeshe hili au lile. Najiambia hapana hili nililiendesha jana, nachukua lingine.”

ATAJA MAGARI ALIYONAYO
Katika mahubiri hayo, Mzee wa Upako aliyataja magari hayo kuwa ni Mercedes Benz, Land Rover Discovery, Range Rover Sport, BMW X5, Ford Escape na Range Rover Vogue.

Aidha, mtumishi huyo wa Mungu aliendelea kutamba kuwa nyumbani mwake kuna viyoyozi  (AC) na kubainisha kwamba huwa akitoka kwenye gari lenye kiyoyozi anaingia katika nyumba yenye kiyoyozi.
Kiongozi huyo ana kanisa kubwa la ghorofa Ubungo Kibangu na mabasi makubwa matano ambayo hutumika kuwasafirishia waumini wake kutoka Barabara ya Mandela hadi kanisani kwake.

KWA WACHUNGAJI WENGINE, UWAZI LAAMBULIA PATUPU
Kwa wachungaji wengine wa kiroho, mwandishi wetu alipigwa danadana za nenda rudi, nenda rudi lakini kwa muda wote huo hakuweza kuonana na viongozi wake ili na wao wafungukie utajiri wao licha ya kwamba baadhi yao unajulikana.

Uwazi lilipenda kusikia kutoka kwenye vinywa vyao na si kwa kuambiwa na watu wengine au kuhisi.
Kwa Askofu Kakobe, nako hali ilikuwa hivyohivyo ingawa siku za nyuma aliwahi kunukuliwa akisema kwamba yeye siyo tajiri.
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger