Showing posts with label JOKATE. Show all posts
Showing posts with label JOKATE. Show all posts

LICHA YA KUWA NA SKENDO YA KUIBIANA MWANAUME (DIAMOND), JOKATE AJITOKEZA NA KUMFARIJI WEMA KWENYE MSIBA WA BABA YAKE MZAZI...

 
LICHA ya kuwa waliwahi kupokonyana bwana (Nasibu Abdul ‘Diamond’), mwigizaji Wema Sepetu na  mtangazaji Jokate Mwegelo wamekutana katika msibani na kupiga stori.

 Kwa mujibu wa meneja wa Wema, Martin Kadinda, Jokate aliibuka Jumanne iliyopita usiku kwenye msiba wa baba Wema uliochukua nafasi nyumbani kwao Sinza-Mori jijini Dar na kumfariji hadi usiku mnene.
“Fani ya urembo na ubunifu ni fani za watu makini sana ambao chuki kwao ni mwiko, nimefurahishwa na kitendo cha Jokate kuja msibani kwani anaonyesha dhahiri kuwa ni mtu mwenye huruma na imani,” alisema Kadinda.


"Sijawahi kumvulia nguo na kufanya mapenzi na mwanaume yeyote tangu niachane na Diamond"...Jokate Mwegelo



Mtangazaji  wa Channel O mwenye mvuto wa aina yake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amefunguka kuwa tangu amwagane na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ hajawahi kungonoka  na mwanaume mwingine. 
 
Penzi la Jokate na Diamond lilichanua kwa takriban miezi miwili mwaka jana wakati Kidoti alipomwagana na aliyekuwa mpenzi wake, mcheza kikapu wa Ligi ya NBA ya Marekani, Hasheem Thabit.
 
Alipoulizwa anamudu vipi hisia za matamanio ya  kufanya  mapenzi, Jokate alisisitiza kuwa kazi pekee ndiyo silaha kubwa ya kumuepusha na vishawishi ingawa anatambua upo umuhimu wa kuwa na mpenzi.
 
“Akitokea mkweli, nipo tayari ingawa hadi sasa hata sijajua nani anaweza kuwa kama alivyokuwa Hasheem, nilimpenda sana,” alisema

JOKATE:MH! DIAMOND ANAPENDA KUZAA,SIO KWANGU TU WANAWAKE WAKE WOTE HUWA NASIKIA ANATAKA KUZAA NAO...

MTANGAZAJI maarufu Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amefunguka kuwa aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ alitaka wazae kipindi walipokuwa wapenzi.
Jokate alifunguka hayo juzikati alipokuwa akifanya mahojiano maalum na mapaparazi wa Global Publishers, pamoja na kufunguka mengi, alibainisha kuwa Diamond huwa anapenda watoto kwenye uhusiano.
“Mh! Diamond anapenda kuzaa, tena siyo kwangu tu wanawake wake wote huwa nasikia anataka kuzaa nao,” alisema Jokate.

"KWA ZAIDI YA MWAKA MMOJA SIJAFANYA MAPENZI...." JOKATE


Jokate 123

Hii  ni  mara  ya  kwanza  kwa  Jokate  Mwegelo  kuongelea  mambo  ya  chumban...


Maongezi  hayo  yalifanyika  kati  yake  na   Millard  Ayo   ambaye  ni  mtangazaji   wa  Clouds  FM.Katika  maongezi  hayo, Jokate  naye ameeleza  jinsi  anavyosumbuliwa  kutongozwa  na  mamia  ya  wanaume  kwa  siku  


 Yafuatayo ni maongezi  yao: 

 Millard Ayo: Nini kimekufanya ufunguke na hizi info ambazo hujawahi kuzizungumzia na mara nyingi umekua ukigoma kuziongelea kwenye media?

 Jokate: Nahisi kwa sababu watu wanazidi kuizungumzia na wanaizungumzia sivyo, hawazungumzii kiuhalisia na kiukweli inanisumbua ndio maana nimeamua kusema kitu kidogo alafu niufunge huu ukurasa.
  
 Millard Ayo: Imekua ikikusumbua kwa mda gani?
 Jokate: Kwa muda mrefu, toka mwaka jana… kwenye facebook watu wanatoa comment na najua kabisa watu hawajaelewa hili swala na mimi sipendi mashabiki wangu kutokunielewa.

 Millard Ayo:  umewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond pamoja na Hasheem?
Jokate: Hahahahahhaha !!!! Yeah..
  
 Millard Ayo: Uhusiano wa nani kati ya hawa wawili ulidumu kwa muda mrefu?
 Jokate: Wa Hasheem.. karibia miaka miwili mitatu
  
Millard Ayo: Na wa Diamond?
 Jokate: Oooh kipindi kifupi sanaaa, sijui mwezi sijui miezi miwili… kidogo alinipa tabu, ila kiukweli nilitaka tu kwa sababu kuna watu wengi walikua wanasema Jokate yani vurugu, unajua sio kila kitu unachokisikia ndio chenyewe na media saa nyingine inapenda kuandika vitu ambavyo sio vya ukweli au wanaviwasilisha sivyo.
  
 Millard Ayo: Sasa hivi uko single?
 Jokate: Yeahkwa muda mrefu tu niko mwenyewe alafu saa nyingine wananisumbua sana  tena  wengi  tu, lakini nafurahia kwa sababu naweza kufocus kwenye kazi zangu mfano wiki ijayo nakwenda kushoot movie na JB, muziki na biashara zangu kwa hiyo inanipa fursa nzuri kufanya vitu vyangu, yani mwenyewe kujiamulia asubuhi nakwenda kufanya vitu vyangu hivyo bila kusumbuliwa si unajua Wanaume wanaweza kusema wanataka attention nini… sio kitu kibaya atleast kwa sasa hivi.
  
 Millard Ayo: Umekaa single kwa muda gani sasa hivi? zaidi ya mwaka?
 Jokate: Yeah, kwa zaidi ya mwaka mmoja sijafanya  mapenzi… sijawahi na mtu ambae nimeweza kumuita like oohh this is my boyfriend… najua ni ngumu lakini nabusubusu watu wengi…. hahah a hah natania hapo, basi tu imetokea hivyo pengine bado sijapata mtu ambae nimeona ataweza kuwa kama wale..
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger