Home » , » ALIYEOKOTA FLASH YA SHILOLE AMKATA MOOD, AMEVUJISHA NGOMA MOJA KUTOKA KWENYE FLASH HIYO...

ALIYEOKOTA FLASH YA SHILOLE AMKATA MOOD, AMEVUJISHA NGOMA MOJA KUTOKA KWENYE FLASH HIYO...

Audio: Aliyeokota flash ya Shilole amkata Mood, amevujisha ngoma moja kutoka kwenye flash hiyo

Shilole aka ‘ShiShi Baby’ amejikuta akiwa na ngoma mpya hewani bila kupenda, huku akipokea simu za watangazaji kadhaa wakitaka auelezee wimbo huo hali ambayo imemkata mood kiasi flani.

Shilole amesema kuwa hakufahamu chochote kuhusu kutoka kwa wimbo wake na kwamba chanzo cha kuvuja wimbo huo flash yake iliyopotea.
“Ndo nashangaa, nishipigiwa simu nashangaa sielewe mimi lakini hiyo sio ngoma niliyokuwa nimepanga kuachia. Imevuja hiyo ngoma bila shaka, kwa sababu mimi sijategemea kabisa, ila nimepoteza flash na ilikuwa na ngoma zangu.” Amesema Shilole.
Hata hivyo Shilole ameipa baraka ngoma hiyo iendelee kupigwa tu redioni. Lakini kwa kuwa flash imepotea na ngoma kadhaa, huenda aliyeikota akaamua kuwa anaachia moja moja! Ni wazo tu, aliyeiokota amtafute ShiShi arudishe mood yake kiroho safi

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger