Showing posts with label SOKA. Show all posts
Showing posts with label SOKA. Show all posts

RONALDO NDIYE MFALME WA SOKA DUNIANI KWASASA ,AWABWAGA MESSI NA RIBERY

MRENO Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka wa FIFA kwa mara ya pili katika historia yake, akimuangusha mshindani wake mkuu, Lionel Messi.
Nyota huyo babu kubwa wa Real Madrid alikuwa anakabiliwa na ushindani wa mbali kidogo kwa nyota wa Barcelona, Messi na wa Bayern Munich, Franck Ribery katika kinyang'anyiro cha Ballon d’Or. 
Akiwa mwenye hisia kali, Ronaldo aliyekwenda jukwaani kuchukua tuzo yake akiwa ameambatana na mtoto wake wa kiume, Cristiano alishindwa kujizuia na kumwaga machozi wakati anapokea taji hilo.
Namba 1: Cristiano Ronaldo ameshinda Ballon d'Or na kutajwa ndiye mwanasoka babu kubwa duniani
Family time: A tearful Ronaldo was on stage with his son Cristiano to collect the award
All smiles: Ronaldo couldn't help but grin broadly when he posed with the trophy
Hisia: Ronaldo alishindwa kujizuia na akamwaga machozi jukwaani wakati anapokea tuzo ya Ballon d'Or
Winner: Pele holds up Ronaldo's son Cristiano as the Portuguese star picks up his award
Mshindi: Pele akiwa amemshika mtoto wa Ronaldo, Cristiano wakati Mreno huyo anapokea tuzo yake

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amepewa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 66 katika mechi 56 za klabu na nchi yake, Ureno mwaka 2013 hatimaye kuirejesha tuzo yake aliyoitwaa awali mwaka 2008.
Pamoja na kwamba Ronaldo hakutwaa taji kubwa mwaka 2013, alifunga mabao yote manne Ureno ikiitoa Sweden katika kinyang'anyiro cha tiketi ya kombe la Dunia baadaye mwaka huu.
"Hakuna maneno ya kusema wakati huu," Ronaldo alisema, huku akifuta machozi. "Nataka kuwashukuru wenzangu wote na washirika pale Real Madrid, katika timu ya Ureno na familia yangu, ambako wako nami,".
"Wale ambao wananifahamu mimi, wanafahamu kwamba  watu wengi wananisaidia: kocha wangu, rais wetu, na sitaki  kusahau kumtaja Eusebio. Mpenzi wangu na mwanangu pia. Nasonga zaidi,". 
Glamorous: Ronaldo with his girlfriend Irina Shark during the awards ceremony
Ronaldo na mpenzi wake Irina Shark katika sherehe za tuzo
Nominees: The trio of Ronaldo, Lionel Messi and Franck Ribery before the ceremony
Washindani: Ronaldo, Lionel Messi na Franck Ribery kabla ya sherehe
Incomparable: Legendary striker Pele won an honourary prize at the Gala in Zurich
Gwiji Pele alipea tuzo katia usiku huo mjini Zurich
Emotional: The Brazilian couldn't keep back the tears
Emotional: The Brazilian couldn't keep back the tears
Mfalme wa soka: Gwiji wa Brazil, Pele alishindwa kujizuia kutoa machozi alipokuwa jukwaani
Out at the top: Retied Jupp Heynckes was named Coach of the Year after winning the Champions League
Retied Jupp Heynckes ameshinda tuzo kocha bora wa mwaka wa dunia baada ya kuiwezesha Bayern Muich kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya
Stunner: Zlatan Ibrahimovic won the Puskas prize for the best goal of the year for his goal against England
Mkali: Zlatan Ibrahimovic ameshinda tuzo ya Bao Bora la mwaka, maarufu kama Puskas 
Unreal: His overhead kick was during Sweden's 4-2 friendly win over England in November 2012
Bao lake tik tak Sweden ikiifunga 4-2 England Novemba mwaka 2012 ndilo bao bora la mwaka
Recognised: German keeper Nadine Angerer won the women's Player of the Year award
Kipa wa Ujerumani, Nadine Angerer ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa kike wa mwaka wa Dunia
Duo: Ronaldo and Angerer pose side-by-side after being named the best players in the world
Wawili: Ronaldo na Angerer baada ya kutajwa wanasoka bora wa dunia 
Shot stopper: Angerer in goal for the German national team during a friendly against Japan
Prize: She was part of the Germany team that won the women's European Championships last year
Taji: Angerer alikuwemo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichoshinda Kombe la ubingwa wa Ulaya kwa wanawake

YANGA,AZAM SASA WAKO MBIONI KUMSAJILI OKWI ..

YANGA na Azam kama zinamtaka straika wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ni fedha yao tu, lakini kuna sharti lazima walifanye.

Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) limetoa masharti na muongozo wa klabu zinazomtamani mchezaji huyo aliyesitisha mkataba na Etoile du Sahel ya Tunisia.

Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba aliiambia Mwanaspoti kuwa: “Hakuna kinachoizuia klabu kutaka kumsajili Okwi, cha muhimu wanatakiwa kuongea na Etoile du Sahel ya Tunisia, wakimalizana nao basi watamchukua, hivyo ni ruksa cha muhimu ni kufuata sheria na haki.”

Okwi ameidhinishwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuichezea SC Villa ya Uganda kwa muda wa miezi sita huku sakata lake la Etoile likifanyiwa ufumbuzi.

Mchezaji huyo anaidai Etoile malimbikizo ya mishahara pamoja na dau lake la usajili huku Simba iliyomuuza kwa Waarabu hao nayo ikidai dau lake Sh 480 milioni.

Suala hilo lipo Fifa na Kawemba amewahakikishia Simba kwamba wasiwe na wasiwasi watapata haki yao.

MAJANGA TENA KWA MAN UNITED! WELBECK ASUBIRIA UPASUAJI ....!!

KLABU ya Manchester United lazima iamue kumpeleka Danny Welbeck kufanyiwa upasuaji wa goti ambao utamuweka nje mshambuliaji huyo wa England kwa wiki nyingine tano.
United tayari inamkosa kiungo Michael Carrick, ambaye atakuwa nje hadi Krisimasi kwa majeruhi.
Majeruhi: Danny Welbeck atalazimika kufanyiwa upasuaji wa goti ambao utamuweka nje kwa wiki nyingine tano
Blow for United: Michael Carrick is sidelined until Christmas with an achilles injury
Pigo United: Michael Carrick atakuwa nje hadi Krisimasi kwa majeruhi

Matatizo yanayomsumbua Welbeck tayari yamemfanya amekosa mechi sita zilizopita za United. 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anapatiwa matibabu yanayompa matumaini anaweza kuepuika upasuaji, lakini United inahofia italazimika kumpeleka kwenye upasuaji ikiwa hali yake haitaimarika.
Welbeck amekwishafanyiwa upasuaji wa goti mara mbili. Marouane Fellaini pia anaweza kuwa nje kwa wiki hadi 10 atakapofayiwa upasuaji wa mguu wake wa kulia.
Stroll: Carrick walked all 18 holes at the DP World Tour Championship in Dubai
Carrick alikwenda kwenye ziara ya mashindano ya dunia ya DP Dubai
Michael Carrick
Michael Carrick
Carrick aliungana na Caroline Wozniacki kumtazama Rory McIlroy akicheza
Crunch time: David Moyes will be without Carrick and possibly Welbeck for games with Spurs and Everton
David Moyes atawakosa Carrick na Welbeck katika mechi na Spurs na Everton


RONALDO APIGA HAT TRICK YA 19 LA LIGA REAL IKIUA 5-1...SASA NDIYE KINARA WA MABAO HISPANIA,BAYERN MUNICH WAWEKA REKODI MPYA BUNDESLIGA

RAIS wa FIFA, Sepp Blatter alizomewa ile mbaya jana Uwanja wa Santiago Bernabeu wakati Cristiano Ronaldo anafunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Real Sociadad kwenye Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.
Mashabiki wa Real Madrid walikuwa wakimzomea Blatter aliyemkandia Ronaldo hivi karibuni na kumfagilia Lionel Messi wa Barcelona.
Na wakawa wanamuimba Ronaldo Ballon d' Or, maana yake anastahli kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia.  Ronaldo alifunga dakika ya 12, 26 kwa penalti na 76, wakati mabao mengine ya Real yalifungwa na Benzema dakika ya 18 na Khedira dakika ya 36. Bao la kufutia chozi la wapinzani wao lilifungwa na Griezmann dakika ya 61.
Ronaldo sasa amefunga mabao tisa katika mechi nne zilizopita na anaongoza kwa mabao La Liga. Amefunga mabao 62 mwaka huu na sasa amefikisha hat-tricks 19 katika Ligi ya Hispania.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: López, Carvajal, Arbeloa, Alonso/Illarramendi dk70, Varane, Pepe, Khedira/Isco dk77, Modric, Benzema/Morata dk83, Bale na Ronaldo.
Real Sociedad: Bravo, Martínez/Ansotegi dk59, José Ángel, Elustondo/Zurutuza dk45, González,  Iñigo Martínez, Vela, Bergara, Seferovic/De la Bella dk45, Xabi Prieto na Griezmann.
Kiwango tofauti: Cristiano Ronaldo amefunga hat-trick ya 19 La Liga jana akiiongoza Real Madrid kuirarua 5-1 Real Sociedad
Different level: Cristiano Ronaldo scored a hat-trick as Real Madrid comfortable saw off Real Sociedad
Celebration: Gareth Bale congratulates the No 7, though he perhaps should have got on the scoresheet himself
Celebration: Gareth Bale congratulates the No 7, though he perhaps should have got on the scoresheet himself
Celebration: Gareth Bale congratulates the No 7, though he perhaps should have got on the scoresheet himselfPANDE ZA MUNICH

KLABU ya Bayern Munich imepaa kileleni mwa Bundesliga kwa pointi nne zaidi na sasa imeweka rekodi mpya ya kucheza mechi 37 bila kufungwa, kufuatia ushindi wa 3-0 dhidi ya Augsburg jana.
Jerome Boateng, Franck Ribery na Thomas Muller ndio walifunga mabao hayo.
Ushindi huo unaifanya Bayern - ambayo mara ya mwisho ilifungwa katika ligi Oktoba 2012 - iipiku rekodi ya Hamburg kucheza mechi 36 bila kufungwa kati ya Januari 1982 na Januari 1983.
37 games unbeaten: Thomas Mueller blows a kiss to his fans after coring a penalty
Unstoppable: Bayern Munich players celebrate after securing victory
Unstoppable: Bayern Munich players celebrate after securing victory

Borussia Dortmund ilifungwa 2-1 na Wolfsburg. Dortmund walitangulia kupata bao dakika za majeruhi kipindi cha kwanza kupitia kwa Marco Reus, lakini Ricardo Rodriguez akasawazisha dakika ya 56 na Ivica Olic akafunga la ushindi dakika ya 69.
Rare goal from defence: Jerome Boateng got Bayern off to the perfect start
Rare goal from defence: Jerome Boateng got Bayern off to the perfect start
Surprise: Wolfsburg's Ivan Olicscored as his side beat Borussia Dortmund 2-1
Surprise: Wolfsburg's Ivan Olicscored as his side beat Borussia Dortmund 2-1

HATIMAYE KASEJA AMWAGA WINO JANGWANI KWA ADA YA Ths Milioni 40....!!

Golikipa hodari nchini, Juma Kaseja jana(Novemba 08,2013) amesaini Mkataba wa miaka miwili na klabu ya Yanga SC  kwa Shilingi Milioni 40.

Kaseja amesainshwa na vigogo wa Usajili wa Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb na Seif Ahmed ‘Magari’ mbele ya Meneja wake, Abdulfatah Salim Saleh Ilala mjini Dar es Salaam.

Kaseja sasa anakwenda kuungana na makipa wawili aliowahi kufanya nao kazi Simba SC, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’.

Hii inakuwa mara ya pili Kaseja kusajiliwa Yanga, baada ya awali kusajiliwa mwaka 2009 akitokea Simba SC ambako baada ya msimu mmoja wa Mkataba wake kumalizika akaachwa na kurejea Msimbazi.

Kaseja aliachwa Simba SC mwishoni mwa msimu kwa madai kiwango chake kimeshuka na amelazimika kuukosa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara, ingawa sasa baada ya kumwaga wino Yanga anarudi kazini Januari.

Kikubwa kilichoisukuma Yanga SC kumsajili kipa huyo ni uzoefu wake katika michezo ya kimataifa na inataka inufaike naye katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.

Juma Kaseja aliibukia sekondari ya Makongo, Dar es Salaam ambako aliitwa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2001 chini ya kocha Mnigeria, Ernest Mokake aliyekuwa akisaidiwa na mzalendo, Juma Matokeyo, wote sasa marehemu.

Mwaka huo huo alisajiliwa na Moro United aliyoichezea hadi mwaka 2003 alipohamia Simba alipopiga kazi hadi 2009 akaenda Yanga na kurejea mwaka mmoja baadaye ambako alifanya kazi hadi mwishoni mwa msimu uliopita alipotupiwa virago.

TAZAMA OZIL ANAVYODATISHWA NA MREMBO HUYU ...!

Capristo akipozi kupigwa picha na Ozil ambaye alionekana kufurahia kufanya barabarani Jijni London.
KIUNGO Mesut Ozil amekuwa akiteka vichwa vya habari tangu atue Arsenal kwa dau la Pauni Milioni 42.5 kutoka Real Madrid, lakini anaonekana kuekwa akili mno na mpenzi wake, mlimbwende Mandy Capristo. Nyota huyo wa Ujerumani aliyeisaidia Arsenal kurejesha makali yake katika Ligi Kuu England tangu atue Emirates msimu huu, Capristo mwenye umri wa miaka 23, ni bonge la supa staa nchini kwao Ujerumani na kwa sasa ni msanii wa kujitegemea baada ya kujitoa katika bendi ya wasichana wenzake, Monrose, lakini Ozil hawezi kuimba mbele ya watu.
 
...Capristo akipozi kupigwa picha na Ozil.
 
 ...Ozil na Capristo wakirejea ndani baada ya kumaliza kupigana picha.
 Arsenal inamenyana na Liverpool Jumamosi ya leo ikiwa na kikosi chake kamili wakiwemo wapachika mabao hatari, Daniel Sturridge na Luis Suarez wamewasili Emirates.

HATIMAYE MAHAKAMA YAWATUPA JELA MIEZI 12 MASHABIKI WA MBEYA CITY WALIOLETA VURUGU SIKU YA MECHI DHIDI YA PRISONS..!!


MAHAKAMA ya mwanzo, mjini Mbeya, leo imewahukumu kifungo cha miezi 12 kwenda jela au kulipa faini ya sh.300,000 kila mmoja, watu watano kati ya sita walioshitakiwa kwa kosa la kuharibu mali katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons.  Habari kamili inakuja...

Tazama video ya magoli ya Simba vs Kagera sugar na fujo zilizotokea uwanjani..



1October 31 2013 kulikua na mechi ya Simba vs Kagera Sugar kwenye uwanja wa taifa ambapo timu hizo zilitoka 1-1 huku goli lililoleta malalamiko likiwa ni la Kagera Sugar ambalo lilifungwa kwa njia ya penat.
Kocha wa Kagera Sugar amesifia maamuzi ya refa na kusema ‘nafurahi timu imesawazisha kwenye dakika za mwisho na refa amefanya kazi yake kwa sababu ni siku nyingi sana marefa hawagawi penat kama hizo, timu nzuri inacheza mpaka goli’
Kocha Kibaden wa Simba kasema ‘nashukuru tumemaliza mpira salama na vijana wametoka salama, sijafurahishwa na jinsi mpira ulivyochezeshwa, sitaki kusema hayo kwa sababu watu wana macho na wanaweza kukosoa lakini uamuzi haukuwa sawasawa, kama tutaendelea na mpira wa aina hii nafikiri tutaondoka kwenye mwelekeo… naomba TFF mpya iliyokuja ijaribu kutazama watu wapumbavu wa aina hii wanaokuja pale kuwaudhi watu, sijafurahishwa na mpira ulivyochezeshwa mwanzo hadi mwisho na nilijua kitatokea nini’

WENGER NI KIBONDE WA MILELE WA JOSE MOURINHO, HAKUNA UBISHI

USIJALI sana Arsene – bila shaka itakuwa bahati ya mara ya 10 wakati Jose Mourinho na timu yake, Chelsea watakapokwenda Uwanja wa Emirates Jumatatu ya Desemba 23, mwaka huu.
Kipigo cha Arsenal cha mabao 2-0 katika Kombe la Ligi maarufu kama Capital One kutoka kwa Chelsea usiku wa jana ilikuwa ni mara ya tisa Wenger anakutana na Mourinho na kutoka kichwa chini.
Rekodi yake dhidi ya Mreno huyo inamaanisha yeye ni mnyonge: amefungwa mara tano na kutoa sare nne. Anapotokea Mourinho, Wenger ni kibonde sana.
Ubabe pale pale: Ushindi wa Chelsea kwa Arsenal unamfanya Jose Mourinho aendeleze rekodi ya kutofungwa na Arsenal Wenger (chini)

Arsenal manager Arsene Wenger watches the League Cup fourth round match against Chelsea
Old foes: Mourinho and Wenger greet each other before the Capital One Cup clash
Mourinho na Wenger walisalimiana kabla ya mechi ya Kombe la Ligi jana
Spacial Juan: Juan Mata celebrates helping his Chelsea boss extend his unbeaten record over Wenger
Spacial Juan: Juan Mata akishangilia kumuwezesha kocha Chelsea kuendeleza ubabe wake kwa Wenger

Once again: Didier Drogba heads past Phillippe Senderos in the 2007 League Cup final in another Mourinho win
Mara nyingine tena: Didier Drogba akipiga kichwa pembeni ya Phillippe Senderos katika Fainali ya Kombe la Ligi mwakia 2007 katika mechi nyingine Mourinho anamfunga Wenger

MOURINHO v WENGER


Des 12 2004Arsenal 2 Chelsea 2Ligi Kuu
Apr 20 2005Chelsea 0 Arsenal 0Ligi Kuu
Ago 7 2005Chelsea 2 Arsenal 1 Ngao ya Jamii
Ago 21 2005Chelsea 1 Arsenal 0Ligi Kuu
Des 18 2005Arsenal 0 Chelsea 2Ligi Kuu
Des 12 2006Chelsea 1 Arsenal 1Ligi Kuu
Feb 25 2007Chelsea 2 Arsenal 1Fainali Kombe la Ligi
Mei 6 2007Arsenal 1 Chelsea 1Ligi Kuu
Okt 29 2013Arsenal 0 Chelsea 2Kombe la Ligi
Katika mechi hiyo ya Kombe la Ligi, ambayo Arsenal ilibadilisha wachezaji nane wa kikosi cha kwanza na Chelsea 10 na bado Wenger alichapwa.
Pat down: But Mourinho has fared poorly against Pep Guardiola over the years
Ametulia chini: Lakini Mourinho naye ni kibonde wa Pep Guardiola

TAZAMA PICHA ZA FUJO ZILIZOFANYWA NA MASHABIKI WA MBEYA CITY MARA BAADA KUPATA USHINDI WA 2-0 DHIDI YA PRISONS HAPO JANA..!


Taarifa kutoka 87.8 Mbeya zinaamplfy kwamba mashabiki wa Mbeya City wamelishambulia gari la wachezaji wa Prisons na kumuumiza mchezaji mmoja ambapo pia walivunja vioo vya  gari aina Toyota Coaster na magari mengine yaliyokuwa kwenye msafara wa timu hiyo ikitoka uwanjani baada ya kufungwa na Mbeya City kwa mabao 2-0.

mbeyayetu.blogspot.com wameripoti kwamba Mashabiki hao walilishambulia magari hayo na kuyavunja vioo na baada ya hapo wakakimbilia kusikojulikana.

Mmoja wa maofisa wa Prisons alisema ana uhakika kuwa waliofanya hivyo ni mashabiki wa Mbeya City kwa kuwa walikuwa wamevaa jezi za rangi ya zambarau ambayo huvaliwa na timu hiyo.






Hapa chini ni baadhi ya fans Mbeya City wakiwa wamebeba jenela la timu ya Prisons, chini ya hii picha ni baadhi ya picha wakishangilia magoli uwanjani

GOOD NEWS: Jamal Malinzi ashinda urais wa TFF...


Habari tulizozipata  ni kwamba Jamal  emil Malinzi amefanikiwa kushinda uchaguzi wa TFF kwa nafasi ya urais aliyokuwa anagombea dhidi ya Makamu wa zamani wa Rais wa TFF Athumani Nyamlani.

Uchaguzi huo, uliotawaliwa na kashkashi za hapa na pale, ulifanyika katika ukumbi wa NSSF WATER FRONT, Dar es salaam 
  
Jamal Malinzi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha soka cha mkoa wa Kagera ameshinda uchaguzi huo ikiwa ni mara yake ya pili kugombea baada ya kushindwa na Rais wa zamani wa TFF Leodgar Chillah tenga mwaka 2008
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger