Showing posts with label UKATILI. Show all posts
Showing posts with label UKATILI. Show all posts

UKATILI...!! MUME AMPIGA MTALAKA WAKE NA KUMNYOFOA MDOMO HUKO MKOANI RUVUMA...

  

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linafanya uchunguzi kuhusu tukio la mume na mke kumshambulia mtalaka wake Faustina Komba (35) mkazi wa jiji la Mbeya kwa kumpiga ngumi, makofi na kumng'ata mdomo wake wa chini na kuuondoa wote. 
 
Habari zilizopatikana mjini hapa na kuthibitishwa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Deusdebit Nsimeki zimewataja watuhumiwa hao kuwa ni Hamidu Mapunda na Regina Mpangala  wakazi wa Mshangano, nje kidogo ya Halmashauri  ya manispaa Songea.

Imedaiwa Desemba 7, jioni huko Faustina alishambuliwa kwa kupigwa ngumi, makofi na kung'atwa mdomo wake wa nchini ambao uliondolewa kabisa na Regina ambaye alishirikiana na mume wake Mapunda.

Inadaiwa chanzo cha ugomvi wao Faustina na Mapunda ambaye alikuwa mume wake wa zamani ni kugombea mtoto wao Mussa Mapunda (5).

Imeelezwa kuwa wakati wakigombana mke wake wa sasa (Regina) aliingilia kati akiwa na lengo la kumsaidia mume wake Mapunda.

Kamanda Nsimeki alifafanua zaidi kuwa wakati ugomvi unatokea mke wa sasa wa Mapunda alikuwepo na alishuhudia Mapunda akipigwa kipande cha tofali kichwani ambacho kilisababisha atokwe na damu nyingi, ndipo alipoingilia kati na kuanza kumsaidia mume wake lakini Faustina inadaiwa alimkamata Regina na kumng'ata sehemu ndogo ya mdomo wake wa chini ndipo naye Regina aliamua kumng'ata sehemu ya mdomo wake wa chini na kuundoa wote.


Kamanda Nsimeki alisema kuwa Faustina na Regina wamelazwa katika hospitali ya mkoa Songea kwa matibabu na shauri hilo linasubiri wao wapate nafuu.

UKATILI...!! MKE AMUUA MUMEWE KWA KUMPIGA NA KIKOMBE KICHWANI HUKO MBURAHATI DAR..

SHETANI anazidi kuuatamia ulimwengu! Mama mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Farida mkazi wa Mburahati jijini Dar, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kudaiwa kumuua mumewe aliyetajwa kwa jina la Amosi Joseph kwa kumpiga kwa kukombe kichwani, Ijumaa linaidondosha kama ilivyo. 

Akisimulia  mkasa mzima, mtoa habari hii aliyetajwa kuwa dada wa marehemu anayejulikana kwa jina la Khadija, alisema siku ya tukio kaka yake aliamka asubuhi na kumuaga kuwa anakwenda bondeni kwa mkewe (Farida) kwa kuwa walikuwa nyumba tofauti.

 

Aliongeza kuwa, muda mfupi baada ya kaka yake kuondoka nyumbani hapo, wifi yake (Farida) alifika nyumbani hapo na kumwambia kuwa kaka yake ameumia sana aende akamuone.
 
“Mimi nilimshauri ampeleke hospitali tu nikidhani ameumia kidogo, kwa sababu wamekuwa na kawaida ya kupigana mara kwa mara na tulishawaonya. Wifi aliondoka na mimi nikaendelea na shughuli zangu.
 
Muda mfupi, uliingia ujumbe kwenye simu yangu ya mkononi ukisomeka kuwa kaka yangu alikuwa amefariki dunia huku ujumbe huo ukinionya kutolia ili nisimshitue mama,” alisema Khadija.
 
Dada mwingine wa marehemu aliyejulikana kwa jila la Christina, alisema yeye aliwahi kufika nyumbani kwa Farida na kumkuta kaka yake akiwa amelala chali huku damu zikimvuja, muda mfupi polisi waliwasili na kufanya taratibu zote muhimu.
 
Marehemu Amoni alizikwa siku chache baada ya kufariki dunia kwenye makaburi ya Mburahati City jijini Dar huku Farida akiwa mikononi mwa polisi kwa upelelezi zaidi.

-Gpl

Ukatili...!! Mwanamke amuua mpenzi wake kwa kumvuta KORODANI huko mkoani Simiyu...




JESHI la Polisi mkoani Simiyu linamshikilia mwanamke na mkazi wa Kijiji cha Usiulize wilayani Meatu kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake kwa kumvuta korodani, kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo alisema tukio hilo lilitokea juzi saa tisa usiku katika Kitongoji cha Mlimani Kijiji cha Usiulize Kata ya Mwamalole.
Alisema katika tukio hilo, wapenzi wawili Jumanne Gunda (39), mkazi wa Kijiji cha Kinyambuli wilayani Mkalamo, akiwa amelala na mchumba wake, Mariamu Khamis (49) mkazi wa Kijiji cha Ibaga Wilaya ya Mkalamo mkoani Singida, kulitokea kutoelewana kati yao na kusababisha wagombane.
Katika ugomvi huo, ambao chanzo chake ni wivu wa kimapenzi, Mariamu anatuhumiwa kuzivuta korodani za mpenzi wake na kusababisha mishipa muhimu kukatika na kusababisha kifo cha Jumanne papo hapo.
Kufuatia kifo hicho, Mariamu aliburuza mwili wa mpenzi wake mpaka chooni kwa lengo la kuutumbukiza katika shimo la choo. Hata hivyo kutokana na udogo wa tundu la choo, alishindwa kutumbukiza mwili huo chooni na hivyo kuamua kuutelekeza humo.
Asubuhi kulipopambazuka, majirani wa nyumba waligundua mwili wa marehemu ukiwa umetelekezwa chooni na kutoa taarifa Kituo cha Polisi, ambao walifika katika eneo la tukio na kumtafuta mtuhumiwa, Mariamu.

Baada ya Mariamu kukamatwa, anatuhumiwa kukiri kumuua mpenzi wake katika ugomvi kati yao, uliotokea usiku walipokuwa wamelala wote wawili. Anatuhumiwa kukiri kumvuta korodani zake na kusababisha kifo chake.

PICHA: UKATILI! MWANAMKE AKATWA MGUU NA MUMEWE....!!



 



Hali ya wanawake inazidi kuwa mbaya ndani ya nchi yao TANZANIA inayosifiwa kuwa ni Kisiwa cha Amani (Amani kwa wanaume) Tukio hili lilitokea mapema mwezi wa nane mwaka huu Kijiji cha Nyantira Tarime Mara. Katika mazungumzo yake huyu binti alisema kwamba anatamani sana kurudi nyumbani kwa wazazi wake, tatizo ni kwamba kwa kuwa alilipiwa MAHARI na mume wake (aliyemkata panga mguu na kuutoa) hawezi kurudi kwao , wala mama yake hawezi kumkubalia arudi kwao ni mpaka baba yake aje atoe ruhusa ya yeye kurudi nyumbani au abaki kwa mume muuaji avumilie-MFUMO DUME UMEKAMATA MIZIZI (mbayaaaaa, sanaaaa. anajisemeaga Mch Rwakatare)




Samahani kwa picha mbaya, lakini hatuna budi kuonyesha unyama uliopita kipimo ambao wanawake wanaupitia. Na huu ni mfano halisi kwa mwanamke huyu wa Tarime Musoma. picha ya juu ni kipande cha mguu wa huyo binti ambao mume alipitisha panga mithili anakata muwa, picha inaonyesha mguu uliobaki na mguu wa kushoto pia ulikatwa lakini haukutoka, pamoja na mkono wake wa kushoto ulikatwa lakini haukutoka. ( Kumbuka tupo kwenye maandalizi mazito ya kuandimisha siku 16 za kupinga ukatili dhili ya Wanawake)



Mama mzazi wa binti aliyekatwa mguu na mkwe wake akilia kwa uchungu mkubwa alipokuwa anaelezea kisa kilichomkumba binti yake. Ni huzuni kubwa sana ukivaa viatu vya familia hii. Mama anasema kwa utamaduni wao baba wa mtoto aliyekatwa yaani mume wake ndiye mwenye dhamana ya kuamua mtoto arudi nyumbani au aendelee kubaki kwa mume fedhuli aliyemgeuza mwenzake ni pingili la muwa au kitoweo Bucher.


Juu ni mama na chini ni binti akiwa na mawazo juu ya kupoteza mguu wake kwa sababu tu mume kaamua kuukata. Huyu binti ameathirika sana kisaikolojia kutokana na tatizo hilo la kukatwa mguu wake na mume wake. hivyo anaomba asaidiwe arudi nyumbani kwa wazazi wake, au popote pa kuishi ilimradi aondolewe kwenye mazingira yale aliyopatia mkasa huo. Mbaya zaidi baba mkwe wake anamwambia "wewe unaona raha kulala kitandani wakati mtoto wangu analala chini jela) kwa kauli hiyo huyu binti yupo hatarini zaidi. wanaweza kumuua wapoteze ushaidi. hata hivyo binti aligusia sababu ya kufanyiwa unyama huo ni mwanaume kuwa na mwanamke mwingine na kwamba alishahamishia mapenzi huko, na kumuona yeye kama dudu mtu. (Wakati tunaendelea na maadhalizi ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya Wanawake, bado hali ni tete)

Hawa ndio Washika dau wetu wakubwa serikalini. wanasimamia Wizara ya Jinsia Maendeleo ya Jamii na Watoto. jamani waheshimiwa sana mko wapi? huku wanawake twafaaa, mnatusaidia vipi? viti vya bunge vinakalika vipi kwa hali hii? ni lini wanawake tutapaza sauti zetu ili dunia ijue unyama huu unaoendelea dhidi ya wanawake wa Tanzania? Wanawake Hatuna AMANI kabisa ndani ya nchi yetu. Wizara na Taasis mbalimbali, Wadau wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake, kuna jinsi ya kumsaidia huyu mama kwa kumuondoa pale kwenye ile nyumba alimofanyiwa UNYAMA huu na akapewa makao salama? Usikose kufuatilia Joyce Kiria Wanawakelive EATV na hapa kwenye ukurasa wetu, ili upate mkasa huu wakati tunajipanga kuendelea na mapambano ya Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake. 
-credit wanawake live tv

UKATILI...!! KIJANA ACHINJWA NA WAUAJI WATOWEKA NA KICHWA CHAKE HUKO SUMBAWANGA ... !

MATUKIO ya mauaji ya kikatili yameendelea kushamiri mkoani Rukwa, baada ya watu wasiojulikana kumuua kikatili mtu mmoja kwa kumchinja  na kutokomea kusikojulikana na kichwa cha mtu huyo.

Baadhi ya askari polisi wakitelemsha maiti ya mtu ambaye ameuawa  kwa kukatwa kichwa na watu kutoweka na kichwa chake usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya kuhifadhi katika hchumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya mkoa iliyopo mjini Sumbawanga.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa watu hao baada ya kufanya mauaji hayo walikwenda kumtupa kwenye eneo hilo ambapo asubuhi ya kuamkia leo ndio kiwiliwili chake kilibainika kuwepo hapo lakini hakina kichwa kwani waliondoka nacho.

Kwa upande wake, Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema kuwa polisi inaendelea kuwasaka watu waliohusika na tukio hilo hili hatua ziweze kuchukuliwa

UKATILI! HAUSIGELI ABAKWA NA KULAWITIWA NA BABA MWENYE NYUMBA HUKO ARUSHA...


VITENDO vya ukatili kwa watoto wenye umri mdogo vimeendelea kushamiri katika jamii, ambapo msichana wa kazi aliyetambulika kwa jina la Anna (13) mkazi wa ngaramtoni wilayani arumeru mkoaani arusha, ameharibika vibaya sehemu zake za siri kutokana na kitendo cha kunajisiwa na kulawitiwa na baba mwenye nyumba wake aliyejulikana kwa jina la Godifrey John(33). 

Akizungumza na mwandishi wetu  baada ya kuokolewa na shirika la shaloom center for street children, linalojihusisha na utetezi wa haki za mtoto, mtoto huyo anaeleza kuwa, alianza kufanyiwa vitendo vya ukatili tangu April mwaka huu baada ya kutoka kijijini kwao masumbwe kilichopo wilayani kahama, mkoa wa shinyanga. 

Alisema kitendo hicho kilikuwa kikimuumiza sana, lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga alilazimika kuzoea maumivu makali  aliyokuwa akiyapata kwani mwajiri wake alikuwa akishamaliza kumwingilia alikuwa akimtishia kumuua iwapo angethubutu kutoboa siri hiyo kwa mtu yeyote. 

Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano, anaeleza kuwa, bosi wake huyo ambaye pia ni mfanyabiashara wa mazao, alikuwa akimnajisi na kumlawiti kwa kumziba mdomo ili asitoe sauti baada ya kumfungia mke wake chumbani majira ya usiku na mchana hasa kipindi ambacho mkewe alikuwa kwenye hali ya kujifungua. 

Alisema bosi wake huyo alikuwa akimwacha mkewe kitandani na kumfuata sebuleni alikokuwa amelala na kuanza kumwingilia kinyume na maumbile huku akiwa amemziba mdomo ili asitoe kelele wakati akifanyiwa ukatili huo. 
 
''Alikuwa akiniingilia mara kwa mara, sikumbuki ni mara ngapi, na akianza kunifanyia mchezo mbaya alikuwa akiniziba mdomo na mkewe alikuwa akimfungia chumbani kwa komeo na kuna kipindi alikuwa mkali akinikaripia'' alisema. 
 
Alisema kuwa, alifika mkoani arusha, mwezi februari mwaka huu, baada ya kuchukuliwa na mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la zawadi samuel ambaye ni rafiki yake na mtuhumiwa, ambaye alikuwa akihitaji msichana wa kazi kutokana na mkewe kuwa mjamzito.
 
"Huyo zawadi tulikutana nae kwenye basi nikitoka masumbwe kwenda kahama mjini, akaniambia kuwa anipeleke arusha akanitafutie kazi, nilikubali tukaondoka kesho yake, ila hadi sasa sina mawasiliano na wazazi wangu na sina ndugu yeyote hapa arusha,'' alisema anna. 

Aliongeza kuwa katika kipindi cha miezi 8 alichofanya kazi kwa mtuhumiwa huyo, hakuwahi kulipwa mshahara ambao walikubaliana shilingi 20,000 kwa mwezi, ila aliwahi kumpa shilingi 10,000 na kumnunulia sketi mbili tu. 

Alieleza kuwa mbali na kumfanyia unyama, alikuwa akimtesa kwa kumfanyisha kazi nyingi ikiwemo kumlazimisha kusomba maji umbali mrefu bila kupumzika, huku akishindwa kumsomesha kama alivyoahidi kufanya hivyo hapo awali.
 
 Kwa upande wa mwakilishi wa shirika la shaloom center, Enezael Joseph alisema kuwa wamefanikiwa kumwokoa mtoto huyo katika mazingira magumu baada ya kupata taarifa kuwa amekuwa akifanyiwa vitendo vya unyanyasaji kinyume cha sheria. 

Alisema kuwa shirika hilo lilipata taarifa kutoka kwa majirani wa mtuhumiwa ambao walichoshwa na vitendo vya manyanyaso anavyovipata mtoto huyo na kuamua kumfuata mtoto huyo na kuzungumza naye ndipo alieleza mambo mazito ya kulawitiwa na kunajisiwa naa mtuhumiwa kila kukicha.
 
 Joseph anasema kuwa baada ya taarifa hizo walitoa taarifa kituo cha polisi ngaramtoni na kupewa hati ya matibabu (PF3)  ambapo msichana huyo baada ya kupimwa katika hospitali ya seliani ya jijini arusha, aligundulika kuharibiwa vibaya sehemu zake zote za siri.
 
Alisema baada ya kupata majibu ya dakitari walirejea na kuwakabidhi polisi ambapo walifungua hati ya mashtaka ya kulawiti yenye kumbukumbu namba NGT/RB/1113/2013 ambapo mtuhumiwa alikamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaaendelea.
 
Hata hivyo mtuhumiwa wakati akitiwa mbaroni alisikika akidai kwamba anachofahamu kwa msichana huyo ni kwamba anamdai fedha zake za mshahara ila hayo madai mengine si kweli kwani amepandikizwa ili kumdhalilisha.

UKATILI...! MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AUAWA KINYAMA NA KUTOBOLEWA JICHO MOJA HUKO TARIME..!!


MWALIMU wa shule ya msingi Nyarero katika tarafa ya Inchage wilayani Tarime mkoani Mara, Joshua Makuri (34), amekutwa amekufa na mwili wake kutelekezwa katika maeneo ya uwanja wa shule ya msingi Turwa Tarime.
Katibu tarafa ya Inchage, Jonathan Machango, alisema jana kuwa mwili wa marehemu uligundulika mwishoni mwa wiki iliyopita na watu waliokuwa wakipita karibu na maeneo ya viwanja vya shule ya msingi Turwa.
Mwili huo kwa mujibu wa Machango, ulikutwa na majeraha ambapo jicho moja lilikuwa limetobolewa.
Machango alisema watu hao walipoona mwili huo, walitoa taarifa Polisi ambapo askari walifika na kuuchukua na baada ya muda ndugu za marehemu walijitokeza kuutambua katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Wilaya Tarime.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa maalumu wa Tarime Rorya ACP, Sweetbelt Njewike, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea kubaini waliohusika na tukio hilo.
Mwalimu Makuri alikuwa akifundisha katika Shule ya Msingi Nyarero na mwili wake ulichukuliwa na ndugu zake kwa maziko yaliyotarajiwa kufanyika katika kijijini cha Nyarero.

---HABARI LEO

UKATILI..!MWIZI WA KUKU AVULIWA NGUO NA KUFINGIWA NDANI YA TENGA ILI ACHOMWE MOTO BAADA YA KUKAMATWA NA WANANCHI..

Huyu  ni  mkenya   aliyekuwa  ameiba  kuku.Wananchi  walipomnasa walimpa  kichapo  kikali  na  kisha  kumfungia  ndani  ya  tenga  la  kuku  kwa  ajili  ya  kumchoma  moto….
Wangali  katika  maandalizi  ya  kutafuta  petrol, polisi  waliwasili  eneo  la  tukio  na  kumuokoa  kwa  kumpeleka  kituoni.
Bofya hapo chini ili kuiona picha hiyo...

UNYAMA...!! MUME ATEKETEZA NYUMBA KWA PETROLI HUKU WATOTO WAKE WAKIWA NDANI...KISA UGOMVI KATI YAKE NA MKEWE..

 Mtoto aliyefariki

Mtoto Matrida Michael mwenye umri wa miaka 9, mkazi wa Mtoni kwa Azizi Ally, wilayani Temeke jijini  Dar es Salaam, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Oktoba 23, mwaka huu kufuatia majeraha ya moto aliyoyapata. 
Marehemu Matrida na watoto wenzake wawili, Tatu Mapunda (9) na Flora Mapunda (7), waliungua moto Oktoba 16, mwaka huu saa tano usiku wakiwa wamelala baada ya chumba chao kulipuliwa kwa petroli na mtu anayedaiwa kwa ni Brighton Mnamwa.
Inadaiwa kwamba chanzo cha Mnamwa kuamua kulipua watoto hao ni ugomvi baina yake na mkewe Janeth Lwena, waliyekuwa katika mzozo wa kumgombea mtoto wao wa miaka mitatu aitwaye Tulizo.


Watoto ambao wako hoi

Mama mdogo wa marehemu Mary Ivo ambaye alikuwepo msibani hapo, alisema kwamba dada yake yupo Muhimbili anawauguza majeruhi wawili waliobakia na kwamba wakati wa ugomvi wao, mke alimzidia nguvu mumewe.
Aidha aliendelea kueleza kwamba baada ya mke kumzidi nguvu, mume alizusha ugomvi mkubwa huku akitishia kumuua kwa panga, hata hivyo mke alimdhibiti.
‘Baadaye mume huyo inadaiwa kwa aliondoka hapo nyumbani na haikujulikana alikoenda, ndipo mke alienda chumba cha jirani na kumuomba Matrida abakie na watoto pale chumbani akatoe taarifa polisi lakini mtoto aliyekua akigombewa alienda naye kituoni,’ alisema mama mdogo.
Habari zinasema kwamba yule mume alienda kituo cha mafuta kununua petroli ili aweze kuwatekezeza wote, lakini hakujua kama mkewe pamoja na mtoto aliyekua akigombewa hawakuwepo.
Taarifa zaidi zinaeleza kwamba baada ya mume huyo kurudi, alimimina mafuta hayo katika chumba hicho kisha kukilipua wakati watoto hao watatu wakiwa katika usingizi na wananchi walipojitokeza walikuta chumba kikiteketea huku sauti ya watoto ikisikika wakiomba msaada.

Wananchi waliokuwepo kwenye eneo la tukio walisema kwamba walipatwa na uchungu hivyo walijitosa kuuzima moto ule na kuwaokoa watoto hao watatu huku wakiwa wameungua vibaya, waliwakimbiza Hospitali ya Temeke na kutokana na hali yao kuwa mbaya walipelekwa Muhimbili ambapo Matrida alifariki dunia.
Naye Michael Melkiori Kess, baba wa marehemu alisema kwamba amesikitishwa na kitendo hicho na amedai ni cha kinyama hivyo ameiomba dola kumsaka mtu huyo hatari kwani huko aliko kwa sasa bado anaweza kusababisha majanga megine.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mtoni Sabasaba, Mwita Mang’ana alisema kwa kitendo hicho ni cha kinyama kwani amesababisha kujeruhi watoto wasiokua na hatia na amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha kuwa mtuhumiwa anapatikana .

Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba msako wa kumtafuta mtuhumiwa unaendelea sambamba na uchunguzi wa tukio

WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KILA MMOJA KWA KOSA LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA....

Askari wa polisi mjini Singida akiwaelekeza washitakiwa wanne wa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha kuingia kwenye gari tayari kwenda kuanza kutumikia adhabu zao kila mmoja miaka 30 jela baada ya kutiwa hatia kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.Washitakiwa hao walitiwa hatiani kwa kosa la kuteka gari la chuo kikuu cha SUA SU 37012 na kisha kuwapora abiria shilingi 8.7 milioni.Pia walibomoa na kusachi jeneza lililokuwa limehifadhiwa mwili wa marehemu mwanafunzi wa SUA,Munchari Lyoba uliokuwa ukipelekwa mkoa wa Mara kwa mazishi. 
Mshitakiwa aliyetiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha na kupora abiria wa gari la SUA shilingi 8.7 milioni Hamisi Issah (wa kwanza kulia) akipanda gari tayari kwenda kuanza kutumikia adhabu yake jela miaka 30.Pia mwenye kofia ya bakharasia,Abubakari Jumanne naye katiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi.
Washitakiwa wanne waliotiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha wakiwa kwenye gari la polisi tayari kwenda kuanza adahabu zao za kila moja miaka 30.Washitakiwa hao walitiwa hatiani kwa kosa la kuteka gari la chuo kikuu cha SUA na kupora abiria shilingi 8.7 milioni.Washitakiwa hao pia inadaiwa walibomoa jeneza lililokuwa limebeba mwili wa mwanafunzi wa SUA Munchari Lyoba na kulisachi kwa imani kuwa limetumika kuhifadhi mali.(Picha na Nathaniel Limu). 
Mahakama ya wilaya ya Singida imewahukumu vijana wakulima wanne wakazi wa Manispaa ya Singida adhabu ya kutumikia jumla ya miaka 120 jela baada ya kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa shilingi 8.7 milioni kwa kutumia silaha.
Washitakiwa hao kabla na baada ya unyang’anyi huo walitumia silaha aina ya bunduki,nondo,mawe na fimbo katika kufanikisha azma yao hiyo.
Washitakiwa hao vijana ambao kila mmoja atatumikia jela miaka 30,ni Hamisi Ally (23),Hamisi Issa (33),Khalid Hamisi (21) na Abubakari Jumanne (26) wote wakazi wa kijiji cha Kisaki Manispaa ya Singida.
Mshitakiwa aliyekuwa wa kwanza kwenye kesi hiyo Idd Omari (38) mkazi wa kijiji cha Kisaki aliachiwa huru awali baada ya kutokutambuliwa na walalamikaji katika paredi mbili za utambuzi zilizofanywa na Jeshi la Polisi.
Washitakiwa hao pia wanadaiwa kuwa baada ya kufanikiwa kupora mali na fedha taslimu waliweza kubomoa jeneza lililokuwa lina mwili wa mwanafunzi wa SUA, Munchari Lyoba na kuchana chana sada kwa imani kwamba kuna mali iliyokuwa imehifadhiwa humo Mwili wa Lyoba alikuwa ukipelekwa Tarime mkoani Mara kuzikwa.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo,Mwendesha Mashitaka Sajenti wa Polisi,Godwel Lawrence amesema pamoja na washitakiwa wote kutokuwa na rekodi yoyote ya makosa ya jinai lakini kitendo walichokifanya ni cha kinyama na cha aibu mbele ya macho ya jamii.
“Kwa hiyo,Mheshimiwa hakimu naiomba mahakama yako tukufu iwape washitakiwa wote adhabu kali ambayo itakuwa fundisho kwao na watu wengine wanaotarajiwa kufanya makosa ya jinai kwa kutumia silaha au nguvu ya aina yoyote”,amesema Lawrence.
Kwa upande wao washitakiwa kila mmoja kwa nafasi yake walitoa maombolezo yaliyofafana kwamba wana familia zinazowatengea kwa asilimia kubwa na kwamba kosa hilo ni la kwanza kutenda toka wazaliwe Hivyo wakaiomba mahakama hiyo iwape adhabu nafuu.
Akisoma hukumu hiyo iliyochukua saa moja na dakika 45,Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Singida,Flora Ndale amesema usahidi wa upande wa mashitaka umethibitisha bila kuacha chembe chembe ya shaka kwamba washitakiwa wana hatia kama walivyoshitakiwa.
“Walalamikaji wote ambao walikuwa abiria kwenye gari lililokuwa likisafirisaha mwili wa marehemu mwanafunzi wa SUA maelezo yao yanafafana wote waliweza kuwatambua vema washitakiwa kwa msaada wa taa za gari na mbalamwezi”,amesema.
Ndale amesema kiongozi wa msafara huo Makaranga Nona,aliiambia mahakama kwamba mshitakiwa wa pili na wa tatu walimwamuru kufungua ‘brief case’ mbele ya gari huku mwanga wa taa za gari ukiwamulika.
“Kama hiyo haitoshi,dereva wa gari hilo Kalistus Malipula ameiambia mahakama hii kwamba mshitakiwa wane alimbebeleza kwa muda mrefu ampe simu mbili za marehemu na maombi hayo alikuwa akiyatoa huku mwanga wa taa za gari ukimmulika”.
Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka Lawrence washitakiwa hao wametenda kosa hilo Desemba sita mwaka jana saa saba usiku huko katika barabara kuu ya Dodoma – Singida eneo la kijiji cha Kisaki.
CREDIT : MO DEWJI

UKATILI..!! MUME AMUUA MKEWE NA KISHA KUMTUMBUKIZA KWENYE SHIMO LA CHOO ...!!

MKAZI wa Kijiji cha Msanzi wilayani Kalambo katika Mkoa wa Rukwa , Festus Sungura (37) anadaiwa kumuua kikatili msichana Janeth Mwanandenje (10) na kisha kutumbukiza mwili wake ndani ya shimo la choo. Inadaiwa choo hicho kilikuwa kikitumiwa na mkewe waliyetengana naye na lengo lilikuwa aweze kukamatwa na kufungwa kwa kosa la mauaji. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Alibainisha kuwa lilitokea Oktoba 18 mwaka huu saa 11 katika Kijiji cha Katuka Kata na Tarafa ya Matai wilayani Kalambo.
Mwaruanda alidai Oktoba 13 mwaka huu saa mbili usiku Janeth (marehemu) alikwenda kwenye ukumbi uliokuwa ukionesha mikanda ya video katika Kijiji cha Msanzi na hakurudi tena nyumbani kwao hadi mwili wake ulipogunduliwa ndani ya shimo la choo, kijiji jirani cha Katuka .
Inadaiwa siku iliyofuata, baba mzazi wa marehemu huyo aitwaye Mussa Mwanandeje , alitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Matai ya kupotea kwa binti yake huyo.
Kwa mujibu wa Mwaruanda, Oktoba 18 mwaka huu jirani wa wazazi wa marehemu huyo katika Kijiji cha Msanzi, aitwaye Festus Sungura (37), alikwenda Kijiji cha Katuka, ambacho ni jirani na kijiji cha Msanzi.
Alikwenda kumfuata mkewe Rosemary Arusha, ambaye alirudi kwao kijijini hapo baada ya kugombana na mumewe huyo miezi kadhaa iliyopita.
Baada ya Sungura kufika Katuka, alikutana na binti yake aitwaye Digna Sungura (15), ambapo alimhoji iwapo mama yake mzazi ( mke wa Sungura) akifungwa, kwa kuwa anamchukia yeye baba yake, ataenda kuishi kwa nani? Binti yake huyo, alimjibu kuwa ataishi na bibi yake kijijini hapo Katuka.
Ndipo Sungura alipomwagiza binti yake huyo, akamwambie mama yake atoe miti mitatu, iliyowekwa juu ya shimo la choo wanachotumia, waone alichofakifanya yeye.
Mama ya binti huyo, alitoa taarifa kwa viongozi wa kijiji hicho cha Katuka, ambapo kwa kushirikiana na wakazi wengine, walitoa miti chooni hapo na kuuona mwili wa marehemu uliotumbukizwa humo.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, mtuhumiwa huyo ameshakamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani upelelezi wa shauri lake utakapokamilika

INASIKITISHA SANA...!! NDUGU WATAKA MTOTO AUAWE ILI KUONDOA NUKSI KWENYE UKOO...!!


MTOTO aitwaye Mwajuma Haji (16) ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anayesumbuliwa na  ugonjwa wa kusinyaa kwa viungo yuko katika hali mbaya baada ya baadhi ya ndugu kudaiwa kutaka auawe ili kutoa uchuro katika familia.

 Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo, Tatu Musa baadhi ya ndugu (siyo wote) wamekata tamaa ya kumuuguza mtoto huyo na kupendekeza heri mtoto huyo akatishwe maisha yake.
  
“Mwanangu haumwi wala hajawahi kuumwa ila ghafla alianza kusinyaa na kukosa nguvu, kinachoniuma baadhi ya ndugu zangu wamekata tamaa wanataka wamuue, waniachie mwanangu,” alisema mama huyo huku akilia mfululizo.


Mwandishi wetu amemshudia mtoto huyo akiwa amesinyaa viungo kiasi cha kutoweza kufanya kitu chochote zaidi ya kulala.
  
Mama mzazi wa mtoto huyo alisema kuwa alijifungua mtoto huyo akiwa na afya njema lakini alipofikisha umri wa miaka mitatu hali ikabadilika na viungo vyake kuanza kusinyaa.
  
Mama huyo amedai kwamba  kutokana na hali hiyo hakuweza tena kufanya shuguli za kumwingizia kipato zaidi ya kukaa na mwanaye kijijini kwao, Kiamange, Bagamayo mkoani Pwani bila ya kupata matibabu ya uhakika.
  
Alisema kwamba   maisha ya mtoto wake yameendelea kuwa mabaya bila ya kupata msaidizi kutokana kutengwa na baadhi ya ndugu zake waliokata tamaa ya kumuuguza.
  
Aidha, Mama Mwajuma amedai kwamba kuna wakati alikuwa akimfungia ndani mwanaye  kuanzia asubuhi ili aende kulima na kupata chochote, lakini aliporudi nyumbani alimkuta katika hali mbaya sana.

Kutokana na mazingira kuwa magumu, mama huyo alidai kwamba hakuwa na msaidizi wa kuweza kumwachia mwanaye  ili aweze kuhangaikia kipato.
  
Mbali na mtoto huyo, mama huyo alibahatika kupata mtoto mwingine ambaye sasa ana umri wa mwaka mmoja na nusu lakini baada ya kujifungua mwanaye mkubwa akatokwa na vidonda mgongoni.

Baada ya mtoto huyo kusumbuliwa na ugonjwa huo kwa muda mrefu alishauriwa kumpeleka Muhimbili na kumuacha mwanaye  mdogo kwa majirani.

Baada ya muda alipata taarifa kwamba mtoto wake mdogo anaumwa, ikabidi akamchukue na kumleta Muhimbili ili aishi naye ingawaje hairuhusiwi kwa mtoto kuishi wodini.

“Nina wakati mgumu, kwa kuwa nina watoto wawili sina cha kufanya kwa kuwa huyu mwingine hajiwezi kwa chochote zaidi ya kumsaidia  kwa kila kitu, mbaya zaidi  ndugu wamenitenga,” alisema   huku akibubujikwa machozi.
  
Ndugu Mtanzania mama Mwajuma yuko katika hali mbaya sana, kama unataka kumsaidia mtoto wake tuma mchango wako kupitia namba 0754 021 301.

UKATILI..!! MWANAMKE MWENYE UKIMWI AMWIBA MTOTO WA JIRANI NA KWENDA KUMNYONYESHA...!!

zim wom Wickedness: HIV positive woman arrested for breastfeeding neighbour’s baby (PICTURED)
Mwanamke mmoja mzimbabwe ambaye alimnyonyesha mtoto wa jirani yake bila kibali/ruhusa ya mama yake anakabiliwa na miaka miwili gerezani kwa kumwambukiza mtu mwingine HIV kwa kukusudia kwasababu yeye ni mwathirika.

Mwanamke mwingine mwenye umri wa miaka 39Annie Mpariwa alifika mahakama ya Gaborone jumatano na kesi ilipangwa october 24 ili wafanye vipimo vya HIV kwa mara ya pili kwa mtoto huyo. 
Vipimo vya kwanza vilionyesha kuwa mtoto hajaathirika.

Mpariwa alikamatwa wiki iliyopita kwa kufanya kosa dogo kwa makusudi (ambalo ni kumnyonyesha mtoto bila kibali kutoka kwa mama yake) ila mtoto akipimwa kwa mara ya pili na kukutwa ni mwathirika adhabu itaongezwa na kuwa ya 'kumwambukiza mtu mwingine HIV makusudi'.
Mama wa mtoto huyo mwenye miezi 14 alisema kumuona jirani yake akimnyonyesha ilikuwa ni jambo la kushitusha sana kwake.
Aliendelea kusema kuwa jirani yake alimchukua mtoto wake aliyekuwa nje na kwenda kumficha chumbani kwake alikokuwa amepanga. Baada ya kumtafuta mtoto wake kwa muda mrefu,alienda kugonga hodi kwenye chumba cha Mpariwa lakini hakujibiwa.
Alipochungulia dirishani alimuona jirani yake huyo ambaye ni mwathirika wa ukimwi akimnyonyesha mtoto wake.
"Nilipochungulia dirishani nilimuona akimnyonyesha mtoto wangu.Nilipata mshituko mkubwa karibu nizimie",aliongezea kusema kwamba maziwa ya jirani huyo yalikuwa bado yanavuja na inashangaza kwasababu kwa muda huo yeye hakuwa na mtoto ambaye anamnyonyesha(hakuwa mzazi) wala hakuwa mjamzito.
Tukio hilo limekuja kwenye mwamko wa sheria mpya zilizowekwa kuhusu HIV na AIDS ambazo zimekuja na adhabu kali kwa wale wanaowaambukiza wenzao virusi vya ukimwi makusudi.

Ila jamani kuna watu wakatili kweli duniani,sasa jirani alikuwa anataka amwambukize ili iweje? Au anapata faida gani? Such an innocent child,kafanya nini to deserve such a bad,horrifying and unbearable thing on her life(HIV)? Kwanini watu hawana huruma siku hizi?!! Inasikitisha sana.....


newsdzezimbabwe

UNYAMA..MTOTO WA MIAKA SITA ABAKWA NA DALALI WA NYUMBA...!

Dalali wa viwanja na nyumba eneo la Mbezi Makabe, jijini Dar es Salaam anatuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka sita na kumjeruhi vibaya sehemu zake za siri.
Tukio hilo limetokea Septemba 3, mwaka huu, ambapo mtoto huyo (jina linahifadhiwa) alifanyiwa unyama huo na dalali huyo anayejulikana kwa jina moja la Mgosi.
Akizungumza kwa masikitiko na gazeti hili, mama mkubwa wa mtoto huyo, Elizabeth Aloyce (28), alisema Mgosi ambaye ni dalali wa viwanja na nyumba katika eneo hilo, alikuwa akimfanyia kitendo hicho kwa muda mrefu.
Alisema kugundulika kwa tabia hiyo chafu ilikuja baada ya mtoto huyo kushindwa kutembea kutokana na maumivu makali.
Elizabeth alidai kwamba siku ya tukio alirudi nyumbani mapema kutoka kwenye biashara zake, alipoingia ndani alimkuta mtoto huyo amelala huku akiugulia.
Alipomuuliza kitu gani anachoumwa, mtoto huyo alianza kulia huku akificha sehemu zake za siri.
"Nilishtuka sana kuona hali ile, nilimshika na kuanza kumchunguza ndipo nikagundua sehemu zake za siri zimeharibika na kibaya zaidi mbegu za kiume zilikuwa zimeenea kila mahali," aliongeza kusema.
Kutokana na hali hiyo, aliamua kuwaita majirani na baada ya kushuhudia walikiri mtoto huyo amebakwa.
Baada ya kugundua suala hilo walimbana mtoto huyo amtaje mtu aliyemfanyia kitendo hicho, ndipo alipomtaja jina la mtuhumiwa na kwamba ilikuwa siyo mara yake ya kwanza kufanyiwa kitendo hicho.

MTOTO ANENA
Mtoto huyo akiongea na NIPASHE alisema kabla ya kufanyiwa unyama huo, mtuhumiwa huyo alikwenda kumchukua wakati akicheza na watoto wenzake.
"Nilikuwa nacheza alikuja Mgosi na kunichukua hadi chumbani kwake na kunilalia juu, kila siku ananifanyia hivyo na kuniambia nisiseme kwa mtu atanipiga," alisema mtoto huyo.
Alisema siku ya mwisho mtuhumiwa huyo mara baada ya kumaliza haja zake alimwambia arudi nyumbani kwao haraka.
"Nilirudi nyumbani niliogopa mama atanikuta nikitoka kwa mgosi, lakini niliona maumivu makali," aliongeza kusema.

POLISI WAMKAMATA
MTUHUMIWA
Baba mzazi wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa) alisema tukio waliliripoti kituo cha Polisi Mbezi kwa Yusufu baada ya kumaliza taratibu zote za kumpatia matibabu Hospitali ya Rufaa ya Tumbi.
Polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na kukaa ndani kwa siku kumi, kisha kuachiwa kwa dhamana.
Hata hivyo, alisema hajaridhishwa na mwenendo wa suala hilo baada ya polisi wa kituo hicho kumzungusha kwa muda mrefu na hakuna dalili ya kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.
"Tumekatishwa tamaa na utendaji wa polisi, hivi sasa imefikia muda wa mwezi mmoja hakuna kilichofanyika huku mtuhumiwa ameachiwa huru," alisema.
POLISI YATOA TAMKO
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Camilius Wambura, alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alisema halifahamu na kuahidi kulifuatilia kwa kina ili aweze kutolea ufafanuzi.
Hata hivyo, aliwataka wananchi kutambua wajibu wa jeshi hilo siyo tu kumfikisha mahakamani mtuhumiwa, badala yake inawajibika kufanya upelelezi kisha jalada husika kulipeleka kwa mwanasheria wa serikali kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.
"Naomba wananchi wafahamu kwamba polisi kazi yao ni kupeleleza tu, kazi ya kufikisha mahakamani ni Ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali (DPP), hivyo kutupa lawama ni kutuonea," alisema Kamanda Wambura.
Alisema hata suala la mtu kupewa dhamana lipo kisheria na kila mtu ana haki ya kudhaminiwa, bali kwa makosa machache ya jinai kama kuua, wizi wa matumizi ya nguvu, biashara ya madawa ya kulevya ndiyo mtuhumiwa wake hawezi kupewa dhamana.

UKATILI...!BINTI WA MIAKA 12 APEWA UJAUZITO KWA KUBAKWA JIJINI DAR...MTUHUMIA AENDELEA KUDUNDA MTAANI ...

BINTI wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kilimani iliyopo Kipunguni, Dar mwenye umri wa miaka 12 (jina tunalihifadhi kwa sababu za kimaadili) amejikuta akishindwa kuendelea na masomo baada ya kupewa ujauzito na kijana wa mtaani aliyejulikana kwa jina moja la Roja.
 
Binti wa darasa la sita mwenye miaka 12 aliyepewa ujauzito na Roja.
Akizungumza kwa huzuni mama wa mtoto huyo, Aziza Mohammed alisema kuwa mwishoni mwa mwezi uliopita ndiyo aligundua kuwa binti yake huyo ni mjamzito na ilikuwa ni baada ya kukataa kwenda shule huku akitapika mara kwa mara.
Mama huyo alisema, baada ya kuona dalili hizo  aliamua kwenda kununua kifaa cha kupimia mimba lakini mwanaye huyo alikimbilia kwa mama yake mdogo, Temeke ambako waligundua kuwa ni mjamzito.
 “Alipofika kwa mama yake mdogo ilibainika kuwa ana mimba, wakanipa taarifa, nikawaomba wamlete kisha tukampeleka hospitali ambako tulithibitishiwa na daktari kuwa kweli ana ujauzito wa miezi mitano,” alisema mama huyo na kuongeza:
“Nilimbana aniambie mwenye mzigo huo ambapo alimtaja kijana aitwaye Roja. Akaniambia kijana huyo ambaye ni jirani yetu amekuwa akimbaka na kumtishia kumuua ikiwa atasema.
“Kwa maelezo hayo ilibidi tumtaarifu mjumbe wa mtaa wa Kipunguni B, Bakari Issa ambaye tulikwenda naye kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Stakishari na kufungua jalada la kesi lenye namba STK/RB/18639/2013 KUMPA

MWANAFUNZI MIMBA
“Jamani naomba taasisi husika zinisaidie kwa sababu baada ya kutoa ripoti polisi nimekuwa nikuzungushwa tu...mtuhumiwa hakamatwi.”

SIMULIZI YA KUSIKITISHA
Binti aliyepata dhahama hiyo alipata kuzungumza ambapo alisimulia simulizi ya kusikitisha sana ikionesha jinsi mchezo mzima ulivyokuwa.
Alisema: “Wadogo zake Roja ndiyo walikuwa marafiki zangu...Roja alikuwa akiwatumia wao kuniita kila siku jioni na nilipoenda alikuwa akinifungia chumbani kwake na kunilazimisha kufanya naye mapenzi huku akinitishia kuwa nikisema ataniua.
“Pamoja na vitisho hivyo alikuwa akinipa shilingi elfu tatu hivyo nikawa naogopa kumwambia mama na nilipogundua nina mimba nilimtuma wifi yangu (dada wa Roja) akamwambie lakini akakataa na kusema mimba siyo ya ndugu yake, mimi sijawahi kufanya mapenzi na mwanaume mwingine zaidi yake,” alisema binti huyo.

KUTOKA KWA MWANDISHI
Tukio hili linaumiza na kusikitisha. Ni wito wetu kwa taasisi husika kufuatilia sakata hili na kumsaidia binti huyu ambaye ndoto zake zimezimwa ghafla akiwa bado mdogo.
Aidha, ni vyema wazazi wakawa makini katika kufuatilia nyendo za watoto wao kabla mambo mabaya hayajawakuta.


-Gazeti la ijumaa via Gpl

VIDEO:MADEREVA WA BODABODA WALIVYOMKANYAGA KIJANA MWENZAO MPAKA KUFA,INASIKITISHA SANA




                 Huu  ni  unyama  uliopitiliza.Tumezoa  kuyaona  matukio  kama  haya  yakitokea  huko  Nigeria.Leo  hii  tunajiona  kwa  macho  yetu  hapa  hapa  nchini  Tanzania.
  
Huu ni unyama walioufanya madereva boda boda kwa kijana ambaye haikuweza kujulikana mara  moja  kuwa kosa lake ni nin. 

Kijana huyu amefungwa mikono kamba na madereva boda boda wanamshambulia kwa zamu kwa kumgonga .

Tazama Video yenyewe hapa chini  kisha  toa  maoni  yako
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger