Showing posts with label BONGO FLEVA. Show all posts
Showing posts with label BONGO FLEVA. Show all posts

JE UNAJUA SABABU YA KUFUNGIWA KWA VIDEO YA DULY SYKES....SOMA HAPA....!

Wote tumemsikia jana Prince Dully Sykes akiongelea kufungiwa kwa video yake ya kabinti special na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) . Kuna sababu kuu mbili zilizosababisha video hii kufungiwa na ya kwanza  ni kitendo cha msanii Diamond Platnumz kuvaa T-shirt iliyoandikwa neno ambalo ni tusi  . Hii ingekua kwa nchi za mbele basi ungekutwa t-shirt hii wanaifanyia kitu kinaitwa “blurring” yaani wanayafanya maneno yasisomeke lakini wabongo wakaona isiwe tabu na director akaamua kuacha video irushwe ikiwa katika hali hii.
Sababu ya  pili ni vazi la ufukwe yule demu alilovaa kitu ambacho dully ameona haikua mbaya.
Je, Unadhani ni haki video hii kufungiwa na kama ni haki je unafikiri  ifungiwe ni kwasababu ipi ya msingi?

YOUNG DEE NDIO MFANO WA KUIGWA... AFANIKISHA KULIPA DENI LA MAREHEMU BABA YAKE LA SHILINGI MILIONI 37 KUPITIA MZIKI..!!

Wakati ambapo rappers wengi wa Tanzania wanalalamika kuwa muziki hauwalipi kivile kutokana na kazi kubwa wanayofanya, kuna baadhi ya rappers ambao wana mtazamo tofauti na kwao rap ya Tanzania imewawezesha kufanya vitu vikubwa kuanzia katika ngazi ya familia, na wanaushukuru muziki wa Tanzania kwa hatua hiyo.
Rapper mwenye uwezo mkubwa wa kurap kwa Kiswahili fasaha, Young Dee, ni mmoja kati ya rappers ambao kwao muziki umewatendea haki na hawaoni haja ya kulalamika.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Young Dee amesema anauheshimu sana muziki wa Tanzania kwa kuwa umeweza kusaidia kuirudisha heshima ya familia yake baada ya kuweza kutumia kipato anachokipata kwenye muziki kuikomboa nyumba ya familia yao iliyotakiwa kuuzwa ili kufidia deni la marehemu baba yake la kiasi cha shilingi million 37 .
“Marehemu baba yangu alikuwa ana deni kubwa ambalo hakuna mtu ambaye alikuwa anaweza kuilipa hilo, kwa hiyo ilikuwa ni nyumba ambayo iliikuwa imekaa imetelekezwa na imeharibika japo ilikuwa imejengwa kwa mfumo wa kisasa kidogo lakini bado inahitaji kuongezewa nguvu. Young Dee ameiambia tovuti ya Times Fm.
“Kwa hiyo niliweza kutumia pesa yangu kuclear hilo deni na kuweza kuiregister upya kama nyumba yangu sasa. Kwa sababu ilikuwa na madeni na ilikuwa iuzwe kwa thamani ya million 37. Kwa hiyo hilo deni limeweza kuli-clear, kwa hiyo hicho ni kikubwa zaidi kwa hiyo sasa hivi iko pale inanisubiri mimi nikusanye tena nguvu nimalizie mambo machache niweze kuhamia.” Ameongeza.
Amesema kwa kuzingatia hilo, mama yake ameweza kuwa na furaha zaidi na muziki anaoufanya hata kuliko yeye mwenyewe (Young Dee). Ameongeza kuwa kuwa kwa muda mrefu yeye amekuwa akiishi katika nyumba za kupanga lakini kufikia mwezi wa nane atakuwa amemaliza kuikarabati nyumba hiyo na kuhamia.
“Kufikia mwezi wa nane naweza kumpigia simu mama yangu na kumwambia, mama njoo ukae kwangu.”
Kwa upande mwingine, Young Dee amesema video ya Kijukuu ilimlipa zaidi ya gharama alizotumia kuifanya na kwamba ana mpango wa kufanya video nyingine kali ya wimbo wake ‘Fununu’ aliofanya na mwana FA na kwamba ana ma-director wawili kichwani kwake akiwemo Nisher aliyefanya video ya ‘Kijukuu’.

KWA UNAFUATILIA MAISHA YA MASTAA, SNURA ATAVAA MAVAZI YA AINA HII...!! MWAKA 2014..SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

IMG-20140102-WA0039

Miongoni mwa wasanii wa Bongo fleva ambao hawatoweza kuusahau mwaka 2013 pengine Snura nae yupo kwenye list na hii ni baada ya meneja anayesimamia kazi zake za muziki Hemed Kavu au HK kuzungumza na paparazi wetu na kuelezea mafanikio yote ya mwaka 2013 aliyoyapata staa huyu mwa ‘Majanga

IMG-20140102-WA0033

Hk anaanza kwa kusema>>>Kiukweli mwaka 2013 tulifanya vitu vingi vikubwa kwa sababu naamini msanii wangu ni msanii pekee wa kike aliyefanya show nyingi hata kwa wanaume hakuna anayemfikia Snura,kuna show tunafanya hadi j’4.j’5 hadi alhamisi tumekua tukizifanya show hizo.


‘Kwa ujumla kuhusu pesa tulizoingiza kwa mwaka 2013 ni mpunga mrefu kwa sababu tumefanya show zisizopungua 180 kwa mfano tunapiga Njombe,tunapiga Songea,tunapiga na Mbinga so kwa wiki tuna uhakika kwa wiki tunafanya show zisizopungua 4 hadi 5

‘Ngoma ya Majanga imehit mwez wa 3 ndo tukaanza kukamata show lakini kabla ya hapo tulikua na nyimbo ya shogaake mama na debe la vanga na tulikua tunafanya show pia,tuna jumla ya show kama 20 za makampuni na hizi ni zile tunalipwa milion 3 hadi milion 4.

‘Kwa siku tunaweza kupiga show hadi 3 kwa mfano kuna siku tulikua na show Z’bar tukaja Dar kulikua na show ya kampuni pale Amana,tukatoka hapo tukawa na show mchana huo huo na usiku tukapiga tena show,Mpunga ni mrefu ni zaidi ya Milion 100′.

‘Kuna dili tulikua tumepata ya Snura kuwa balozi wa kampuni fulani lakini mkataba ndo tunaweza kusaini mwezi huu a,mbao utakua ukihusisha pia na show kwa Snura ambapo watatoa shows 30 ambazo kila show moja tutakua tukifanya kwa milioni 7 kwa hiyo kuna Milion 210 zipo’.

‘Kwa Snura mwaka 2014 amekuja na mavazi yake ambayo tumebuni wenyewe kwa hiyo kuna style mpya ya mavazi na moja kati ya wasanii wanaovaa nguo za heshima ni pamoja na Snura japo mwili wake ndo una tetemesha lakini ndo kaumbwa hivyo inabidi tukubali’.Hk.



LADY JAY DEE AWEKA WAZI NDOTO ZAKE ZA KUPIGA COLABO NA DR DRE NA USHER

clip_image001Tunaendelea kuzihesabu siku kadhaa kuikamilisha mbio ya kuumaliza mwaka 2013 Mungu akipenda huku mengi yakiwa yamekamilika na mengine yakiwa pending.
Binti Komando, Anaconda, Lady Jay Dee bado hajakamilisha mpango wa kuuweka wazi wosia wake, lakini hivi karibuni watanzania na wadau wa muziki wanaweza kuushuhudia wosia huo kabla hatujauanza mwaka 2014.
Hii inatokana na tweet ya Jide ya December 18,2013.clip_image002
Katika hatua nyingine, Yahaya hit maker ameweka wazi moja kati ya ndoto ambazo anatamani sana kuzitimiza ikiwa ni pamoja na kukutana na daktari wa midundo duniani ‘Dr. Dre’, na mkali wa R&B Usher Raymond.
Jide ameandika kwenye blog yake:
“Kati ya NDOTO zangu mbili kubwa zilizobakia hapa duniani ni kukutana na watu hawa wawili Dr. Dre na Usher Raymond 2013 hiyoooo inayoyoma ndoto imekuwa ndoto, hebu tusaidiane kusali tujaribu tena 2014.”

ALIYEOKOTA FLASH YA SHILOLE AMKATA MOOD, AMEVUJISHA NGOMA MOJA KUTOKA KWENYE FLASH HIYO...

Audio: Aliyeokota flash ya Shilole amkata Mood, amevujisha ngoma moja kutoka kwenye flash hiyo

Shilole aka ‘ShiShi Baby’ amejikuta akiwa na ngoma mpya hewani bila kupenda, huku akipokea simu za watangazaji kadhaa wakitaka auelezee wimbo huo hali ambayo imemkata mood kiasi flani.

Shilole amesema kuwa hakufahamu chochote kuhusu kutoka kwa wimbo wake na kwamba chanzo cha kuvuja wimbo huo flash yake iliyopotea.
“Ndo nashangaa, nishipigiwa simu nashangaa sielewe mimi lakini hiyo sio ngoma niliyokuwa nimepanga kuachia. Imevuja hiyo ngoma bila shaka, kwa sababu mimi sijategemea kabisa, ila nimepoteza flash na ilikuwa na ngoma zangu.” Amesema Shilole.
Hata hivyo Shilole ameipa baraka ngoma hiyo iendelee kupigwa tu redioni. Lakini kwa kuwa flash imepotea na ngoma kadhaa, huenda aliyeikota akaamua kuwa anaachia moja moja! Ni wazo tu, aliyeiokota amtafute ShiShi arudishe mood yake kiroho safi

SNURA Kuwavuruga mashabiki wake na nyimbo yake ya 'NIMEVURUGWA' kwenye fainali za EBSS Leo Usiku..!!


MAMA wa Majanga, Snura Mushi leo anadondoka katika Ukumbi wa Escape One,  Mikocheni jijini Dar katika fainali za Shindano la Epic Bongo Star Search.
Kwenye fainali hizo ambazo mshindi anatarajiwa kuondoka na kitita cha Sh. Mil. 50, wasanii mbalimbali wanatarajia kutumbuiza akiwemo Barnaba, Young Killer, Shaah, Msechu na Walter Chilambo.
Akizungumzia viingilio, jaji mkuu wa shindano hilo, Rita Paulsen ‘Madam’, alisema kuwa kutakuwa na vitu maalum  kwa Sh: 50,000 ambapo watapata na vinywaji na pia kutakuwa na viti vya kawaida 20,000 na tiketi zinapatikana Shear Illusion ya Mlimani City, Best Bites, Steers ya mjini na Zizzou Fashion ya Victoria na Sinza Africa Sana pamoja na Escape One.
Madam alisema mshindi atakayepatikana leo atakuwa akisimamiwa na studio ya MJ na kufanyiwa kila kitu kwa sababu washindi wengi wanapopata fedha wanajali kufanya vitu vingine kuliko kuendeleza vipaji vyao. 



----GPL

TAZAMA PICHA ZA RAYUU AKIWA NA NJEMBA KITANDANI WAKING**N**K** ZAVUJAA NA KUSAMBAA MITANDAONI..!!

WAKILA BATA KWA RAHA ZAO




HUYU NDO JAMAA MWENYEWE ANAYE KAMATIA MZIGO

Angali hapa video ya "NIMEVURUGWA" yake SNURA Uone jinsi alivyovurugwa kweli....Ni mauno kwa kwenda mbele

snura 234  August 2013 ndio Snura aliishusha single yake ya ‘nimevurugwa’ kwenye radio za bongo ikiwa ni miongoni mwa single zinazopata airtime bila kuwa na video lakini leo November 22 2013 kaishusha video on AyoTV… itazame hapa chini na uache maoni yako mtu wangu, atapita hapa baada ya saa 6. Snura alisema kwenye video ya ‘majanga’ hakuweza kucheza kama inavyotakiwa lakini huku kwenye ‘nimevurugwa’ ndio kajiachia

MSANII BERRY WHITE APIGA KIBERITI GARI LA MPENZI WAKE, NI BAADA YA KUGUNDUA MPENZI WAKE KUGAWA URODA KWA MWANAUME MWINGINE...

Artist anayewakilisha Zenji ktk game ya bongo flava Berry white inasemekana amelichoma Moto garI la mpenzi wake na Gari Hilo likateketea kama unavyoona hapo, kwa mujibu wa cha chanzo chetu cha habari kinadai kuwa chanzo cha tukio Hilo ni baada ya Berry kushtukia dem wake ameenda kufanya mambo ya chumbanI na mwanaume mwingine, ndo huku Nyuma jamaa akaamua kupiga kiberiti Gari, bado tunaendelea kumtafuta berry white ili na yeye atoe ya moyoni.... 
Artist Berry White


Hii ndo ndinga iliyopigwa Moto na Msanii Berry White, nia aina ya Spacio na mwanzo lilikua lina rangi Nyekundu

JIONEE YALIYOJIRI JANA BAADA YA SNURA KUWAVURUGA WAKAZI WA KIGAMBONI..

Wakazi wa Dodoma kaeni tayari kumpokea mwanadada snura na kumpatia company ya kutosha j pili ijayo ya tar 24 /11 kwa mara ya kwanza atakuwa pale @New maisha Club kuzindua kichupa '' NIMEVURUGWA'' hii siyo ya kukosa Mauno kwa sana yatahusika pale kati:

HATIMAYE P SQUARE KUWASHA MOTO JUKWAA MOJA NA LADY JAY DEE PAMOJA PROFFESSOR JAY

Tarehe 23 pale Leaders Club patakuwa hapatoshi baada ya EastAfrica TV kutangaza kwamba wakali wawili walioimba joto hasira watapiga show pamoja na P Square.
Kupitia ukurasa wa facebook wa EATV walisema “HABARI MPASUKO: Lady Jay D, Prof J kupafomu na P-SQUARE


Yaani zile JOTO HASIRA zikikutana na ALINGO lazima PERSONALLY utasema CHOP MY MONEY hadi YAHAYA apatikane maana tupo KAMILI GADO!!!

Wale wakali wa muziki hapa Bongo toka enzi hizo, mwanadada Lady Jay Dee (ANACONDA) na Professor Jay watapafomu jukwaa moja na P- SQUARE siku ya Novemba 23 pale Leaders Club.
Endelea kusikiliza East Africa Radio kwa habari zaidi pia kumbuka Zimebaki siku 2 tu za kununua tiketi yako kwa M-PESA kwa elfu 30!!”

AIBU....!MATONYA ATEKWA NA MASELA NA KUNYANG'ANYWA GARI, NI BAADA YA KUKATAA KULIPA DENI LA WATU HAPO JANA...

Mwanamuziki nyota wa muziki wa kizazi kipya usiku wa kuamkia Jumatatu alionja joto ya kiwe baada ya kutekwa na kusurubiwa kisha kunyang'anywa kila kitu pamoja na gari yake.



Mwanamuziki huyo akiwa kwenye viunga vya Club ya usiku ya Kibo iliyopo Tegeta Jijini Dar pamoja masista du wakila bata ghafra kundi la watu watano lilimvamia na kumkamta msobe msobe hadi nje ya ukumbi pamoja na kumrukisha kichurachura huku wakina dada waliokuwa wamendamana nao wakilia kwa uchungu kwa kumuonea huruma.

Habari zaidi toka kwa chanzo chetu kilichoshuhudia timbwiri hilo kilisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni kudaiwa kwa Matonya na mtoto wa mjini aliyefahamika kwa jina la Evance" Huyu Evance ni mtoto wa mjini na huwa anawakopesha pesa wanamuziki mbalimbali pamoja na wasanii wa bongo movie hivyo miezi ya hivi karibuni alimkopesha shilingi laki nne msanii huyo kwa madai kuwa hakuwa na pesa ya kula bata wikiendi ambapo baada ya kumkopesha msanii alianza kuzungusha kurudisha hali iliyomfanya Evance kuchukua hatua za kumfanyia unyambilisi huo" Kilisema chanzo chetu

Hata hivyo baada ya kumkamata msanii huyo Evance alimpelekwa Oysterbay ambapo aliiacha gari na simu kwa makubaliano atakapoleta pesa hiyo atapewa gari yake.

HATIMAYE MASWALI YA LADY JAY DEE KWA YAHAYA YAPATA MAJIBU, SIKILIZA WIMBO WA HARD MARD ALIYOMJIBU LADY JAY DEE ..

Maswali ya Lady Jay Dee kwa Yahaya yamemgusa Hard Mard na kuamua kuyatolea majibu.Hardmard ameachia wimbo alioupa jina ‘Naishi Ghetto’ akiwa amejivika u-Yahaya .
Wimbo huo uliotumia mdundo uleule wa hit ya 'Yahaya', umetayarishwa katika studio za Over Classic jijini Mwanza ambapo ni ndipo yalipo maskani ya Hard Mad hivi sasa.
Haijajulikana bado kama Hard Mad aliongea na Jide ama vipi, endelea kufuatilia hapa.

Isikilize hapa 'Naishi Ghetto'

KUMBE HUYU NDIYE MSANII WA BONGO FLEVA AMBAYE BABA YAKE ANA UMRI MKUBWA KULIKO WASANII WOTE,ANAMIAKA 107

 
Ukimuona Timbulo akiwa na baba yake, ni rahisi kuwa na imani kuwa huyo ni babu yake kutokana na Uzee wake. Ukweli ni kwamba, baba mzazi wa msanii huyo, ana umri wa miaka 107. Akiongea kwenye kipindi cha Sunrise cha Times FM, leo, Timbulo alisema wazazi wake wamekuwa wakiugua mara kwa mara kutokana na umri wao. Katika hatua nyingine, leo ni siku ya kuzaliwa ya mama yake mzazi, ambaye hata hivyo mama yake huyo hakumbuki mwaka aliozaliwa. Kupitia Instagram, Timbulo ameandika: “Kiukweli upendo wako kwangu ni unreplaceable, cjapata na am sure cwez kupata mwanamke mwenye upendo wa dhati kama ule unaonipa, furaha na nuru hii hugeuka huzuni na giza kila nikifikiri cku utakayoniacha ntakuwa katika hali gani, daaaaah mola nipe la hili swali maana,,,, happy birthday mama yangu mie japo umri na muonekano wako ni kama bibi yangu na hata umri wako hujui ni miaka mingapi ila cwez kuubadili ukweli huu ur my mother, am proud of n I love u so much.” 
Source: Times Fm

VIDEO MPYA YA BABY MADAHA "SQUEEZE ME TIGHT" YAZUA UTATA

Video ya muziki ya mwanadada Muigizazji na mwanamuziki Baby Madaha “Squeeze me tight” imeanza kuzua utata kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutazamwa na watu wengi sana kwa muda mfupi tangu ilipowekwa hewani kwenye mtandao wa youtube.
Video hiyo ambayo imerekodiwa huko nchini Kenya chini ya Studio za Candy n’ Candy Records ina mahadhi ya kijamaika flani hivi  na pia ukiichunguza kwa umakini zaidi ina vionjo flani vya “kizombie” na pia ipo “too sexy” kitu kilichotafsiriwa kama mambo yale  ile “dini ya wavaa suti” na sababu ya video hii kutazamwa sana. Tuliamua kumtafuta baby Madaha mwenyewe ili ajibu tuhuma hizi lakini kwa bahati mbaya simu yake ya mkononi likuwa inatumika muda wote tuliompigia. Tutaendelea kumtafuta na kuwajulisha atakayosema.

HUU NDIO UJANJA WA DIAMOND PLATINUM NA UZEMBE WA WASANII WENGINE HAPA BONGO

Hata kama sio shabiki wa diamond ila kuna kitu lazima uwe kinakuvutia kutoka kwake.Unaweza kujitahidi kumchukia labda kutokana na skendo zake za nje ya muziki wake ila ukirudi kwenye muziki wake nadhani anastahili kuwa pale alipo.
Kuanzia muonekane wake mpaka anavyoweza kuji-brand kimataifa na anavyojua kucheza na akili za mashabiki.

Wasanii wengi wa bongo flava wana tabia ya kurithika kwa mafanikio yao ila Diamond toka atoke na Kamwambie mwaka 2009 mpaka 2013 amezidi kwenda juu bila kuonyesha kusuasua wala kutetereka.
Angalia video ya number 1.Wimbo unaweza sema ni wa kawaida kabisa ukilinganisha na mbagala, kamwambie au nitarejea ila akili ya kwenda kufanya video cape town,south africa kumeifanya nyimbo iwe number 1 kama jina lake lilivyo.

Ushawahi kujiuliza Ali kiba yupo wapi pamoja na kuwa kila mtu anajua ni mkali kuliko diamond?Ali kiba toka atoe my everything mwisho wa mwaka jana amepotea hata video ajatoa.Tukaja kumuona kwenye kidela na Abdu kiba bila kurefusha maneno Ali anashindwa kuufanya mziki wake kama mashabiki wake wanavyotarajia labda pengine angekuwa anafukuzana na diamond ila matokeo yake vijana wake kama Rich mavoko na Dimpoz ndio wapo nyuma ya Diamond huku Ali akibaki msanii mkali ambae ameshindwa kuendelea kutuonyesha ukali wake sijui anawaza nini!

Ushawahi kujiuliza kama ule wimbo wa airtel hands across the world waliopiga wakina r.kelly,fall ipupa,2 face kama nafac ile angeipata diamond leo angekuwa wapi?
Diamond leo anatuletea remix ya number 1 f.t Davido kila mtu anaisubiri kwa hamu ila Ali alishindwa hata kutuletea remix ya Dushelele f.t Fally ipupa pamoja kukaa nae wiki nzima wakifanya wimbo pamoja.
Diamond ni mjanja anaejua biashara ya mziki ilivyo labda pengine ni management yake inayomsimamia.Diamond kaweza kuubadilia mziki wetu kwa kiasi chake leo ndio msanii anaelipwa pesa nyingi kwa show.

Nampenda ali kiba,naipenda sauti yake,anajua mziki kuliko Diamond ila Ali ameshindwa kubadilika na kukubali soko la mziki linataka nini.

Amka Ali huyu Diamond hakuwezi ila usipokuwa makini utajikuta nyuma ya rich,barnaba,dimpoz na ben pol maana mziki sio kuimba peke yake mziki ni biashara pia

"NAJUA WANACHOKIPENDA MASHABIKI KUTOKA KWA DIAMOND NDO MAANA NAONEKANA NOMA ZAIDI YAKE"...RICHIE MAVOKO

Hitmaker wa Roho Yangu, Richie Mavoko amesema anajua kile ambacho Diamond Platnumz anawashikia watu, na yeye anajua kipi cha kufanya, ndio maana anaonekana kuwa tishio kwake.

page
Richie Mavoko amesema alianza kumsikia Diamond tangu akiwa shule na kwamba hakatai kuwa kuna vitu alijifunza kutoka kwake.
Mimi Diamond anatoka, mimi nipo shule, kwahiyo kuna vitu vingi nimeviona, labda yeye amepitaje, amekosea nini na mimi nifanyeje ndio maana mara nyingi mimi naonekana noma kwasababu mimi nishajua wao wanataka nini. Yaani mimi nishajua anapowashkia watu halafu mimi nshajua natakiwa nifanye nini,”alisema.
Mavoko aliendelea kudai kuwa muziki wake na wa Diamond haufanani hata kidogo. “Mimi na huyo jamaa hatufanani kabisa yaani, sisi ni watu wawili tofauti. Wote tunaimba Bongo Flava, Wote tunafanya kitu kimoja lakini makoo tofauti sababu koo la Diamond sio koo langu mimi tuko tofauti kabisa.
Muimbaji huyo aliongeza kuwa hana urafiki wowote na Diamond licha ya kwamba wakikutana husalimiana.
Mimi nachoamini sina ushkaji naye, sio lazima kuwa na ushkaji naye lakini ni mtu ambaye ananijua, namjua ‘hi mambo, vipi poa, salama’ hatuna matatizo yaani.

VIDEO: MDOGO WAKE DIAMOND ATOA VIDEO YA KUONYESHA MAISHA YA DIAMOND KABLA HAJATOKA..


NUSU UTUPU YA LINAH YAWADATISHA WANAUME..!


Linah akiwa jukwaani wakati wa shoo ya Fiesta 2013 jijini Dar.

Mavazi ya nusu utupu ambayo msanii Esterlina Sanga ‘Linah’ hupenda kuyavaa hasa kwenye matamasha yamekuwa yakiwadatisha wanaume na wengine kuomba kupiga naye picha kwa lengo la ‘kujipoza’ kama ilivyotokea kwenye Fiesta, Dar hivi karibuni.
 

 
Linah akipozi na baadhi ya wanaume walioomba kupiga naye picha.
 
Ijumaa limekuwa likimfuatilia Linah na kubaini kuwa kila mara hupenda kuvaa nguo zinazoacha wazi mapaja na kitovu chake na watu ambao amekuwa akipiga nao picha ni wanaume ambao wengi huonekana wakiwa wamemshika kimahaba.

Hata hivyo, licha ya mwenyewe mara kadhaa kueleza kuwa, hayo ni mvazi ya kikazi zaidi, baadhi ya mashabiki wamemponda na kumtaka kubadilika hasa ikifahamika kuwa ni mtoto aliyetokea kwenye familia iliyoshika dini na kwamba kuvaa hivyo ni kujidhalilisha. 
GPL

KUTOKA KIMAPENZI NA BOSI WAKE KWAMSABABISHIA BALAA BABY MADAHA ...!!

Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’.

Mwanamuziki na mwigizaji Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’, amemshukia mwanamuziki memba mwenzake wa Candy n’ Candy, Top C na kumtaka asimuingilie katika maisha yake.

Kupitia kipindi cha redio hivi karibuni, Top C alisema tangu Baby Madaha asajiliwe katika kampuni hiyo ya muziki iliyopo nchini Kenya, memba wengine wamekuwa wakipuuzwa na bosi wao, Joe Kairuki kiasi kwamba hawasikiki kabisa na kuainisha kuwa Baby anatamba kwa sababu amekuwa ‘kiburudisho’ cha bosi huyo.
Alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo, Baby alikanusha:
“Top C na wenzake ni wazushi, sina uhusiano na Joe. Mimi nina kipaji kikubwa na nina nidhamu ya kazi kuliko wao ndiyo maana ninapewa nafasi. Wanaendekeza uzushi kwa nini wasipigwe chini?”

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger