Showing posts with label AGNES MASOGANGE. Show all posts
Showing posts with label AGNES MASOGANGE. Show all posts

MSANII SENGA ATADATISHWA NA MZIGO WA AGNESS MASOGANGE ALIOJAALIWA,CHEKI MAPICHA MWENYEWE


http://distilleryimage6.ak.instagram.com/39c3b4a870c311e387350e22d49cfb46_7.jpghttp://distilleryimage2.ak.instagram.com/257628ec70c211e3be040e37929c2f0e_7.jpg



  http://distilleryimage2.ak.instagram.com/b5f3da2270a411e3b0fe1213113368a2_7.jpg 

http://distilleryimage1.ak.instagram.com/b8df1ab270a411e3ae0e12ea8b4c068d_7.jpg 

 http://distilleryimage8.ak.instagram.com/fee47aee70a311e3958f12eb3ce597d4_7.jpgMwigizaji mkongwe nchini Ulimboka Mwakilasa al-maarufu kama “Senga” alishindwa amenaswa laivu na kamera ya mdau mmoja akishangaa laivu mzigo (wowowo) la mwanadada Agness Masogange wakati wakishoot filamu mpya ya mwanadada Nisha ambayo mwigizaji huyo ameshirikishwa. Tazama picha.


ILE VIDEO YA AGNESS MASOGANGE NA NISHER WAKISHINDANA KUONESHA MAKALIO HII HAPA,ITAZAME UJIONEE

Duh si mchezo hawa masupastaa wa kibongo wakikosa kazi za kufanya wanakuwa na vituko sana niaje.....Video hizi zinawaonesha Agness Gerald "Masogange Nisher wakikata mauno...HATARI SANA

 
VIDEO YA HATARI ZA MASOGANGEFINEASS



VIDEO YA NISHERBEBE

HUKUMU YA MASOGANGE YAPINGWA KWASABABU NI NDOGO NA HAIENDANI NA KOSA ALILOLIFANYA....


MAKAMANDA wa vitengo vya kudhibiti madawa ya kulevya kwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamemaliza kikao chao jana kujadili mustakabali wa uhalifu ikiwemo hukumu iliyotolewa kwa Mtanzania Agness Gerald ‘Masogange’ aliyekamatwa na malighafi haramu aina ya Ephedrine, Julai 5, 2013 nchini Afrika Kusini kwamba ni ndogo.
Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi Tanzania zimeeleza kuwa makamanda wa nchi hizo 15 walikutana jijini Arusha kuanzia Jumatatu iliyopita lengo kubwa likiwa kutokubaliana na adhabu zinazotolewa na baadhi ya nchi wanachama kwa wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’.

WALICHOJADILI
Kwa mujibu wa chanzo kilicho ndani ambacho kiliomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji, makamanda wa nchi hizo walikuwa na kibarua kizito cha kujadili mbinu mbalimbali za kukabiliana na uhalifu pamoja na hukumu inayotolewa kwa watu wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na unga.
“Walijadili matukio mengi ya uhalifu likiwemo suala la madawa ya kulevya, wakajadili mbinu za kukomesha biashara hiyo haramu ili waweze kupata suluhisho la kudumu,” kilisema chanzo hicho.

NZOWA
           WATAKA HUKUMU KWA NCHI WANACHAMA IWE MOJA
Ilidaiwa kuwa, malighafi aliyokamatwa nayo Masogange na mwenzake kwa nchi nyingine kifungo chake kinafanana na kile cha mtu aliyekamawa na madawa ya kulevya, lakini kwa Afrika Kusini ni cha chini sana.

Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, miongoni mwa masuala yaliyokuwepo kwenye ajenda ni pamoja na umoja katika suala zima la hukumu hususan kwa watuhumiwa wa madawa ya kulevya kwani kumekuwa hakuna uwiano baina ya nchi moja na nyingine ndani ya Jumuiya hiyo.
“Tumeona ilivyokuwa kwa Masogange, nchi nyingi zimepinga kabisa ile hukumu kwani ilikuwa haifanani na kosa husika. Mtu anatozwa faini ya shilingi milioni nne na laki nane (Sh. milioni 4.8) kitu ambacho hakiingii akilini kabisa, makamanda wengi wameonesha kupinga hukumu ile,” kilisema chanzo hicho.
MASOGANGE AJIFICHA
Wakati makamanda wa nchi hizo wakimaliza kikao chao, habari zenye utata zimesambaa kwamba, Masogange alitua Bongo katikati ya mwezi uliopita lakini anaishi Dar au Mbeya kwao kwa kujificha.
Agness Gerald ‘Masogange’.
Baadhi ya watu, wakiwemo marafiki zake wamekuwa wakisema kwa mkato staa huyo yupo Dar huku wengine wakisema baada ya kutua Dar alikwenda kwao Mbeya kwa sababu hataki kujulikana kuwa amesharudi Bongo.
Mwenyewe anapopatikana kwenye simu na kuulizwa amekuwa akijibu bado yupo Afrika Kusini lakini siku yoyote atatua Dar.

NZOWA ATOA UFAFANUZI
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alipoulizwa kwa njia ya simu juzi kuhusu mkutano huo alijibu kuwa yupo safarini kikazi akiwa katika mazingira mazuri atatoa ufafanuzi.
“Nipo safarini kikazi, naomba unitafute siku nyingine nitakupa ufafanuzi mzuri sana,” alisema Kamanda Nzowa ambaye naye ilidaiwa alikuwepo kwenye kikao hicho.

KUMBUKUMBU
Masogange na Mellisa Edward walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg  nchini humo wakidaiwa kuingiza madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Hata hivyo, mahakama kuu nchini humo ilidai madawa hayo si ya kulevya bali ni malighafi haramu iitwayo Ephedrine ambapo kwa sheria za Afrika Kusini mtu akipatikana na hatia ya kuyaingiza nchini humo ni kifungo cha miezi 32 jela au faini ya shilingi milioni 4.8 kama alivyohukumiwa Masogange ambayo ni ndogo.

MASOGANGE "ALIENITUMA MZIGO WA MADAWA SOUTH AFRIKA ITABAKI KUWA SIRI YANGU MPAKA KUFA... "

VIDEO Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ alitarajiwa kutua nchini juzi Jumatano akitokea Afrika Kusini huku siri nzito ya mzigo aliodakwa nao ikitawala, Amani linakujuza.
Masogange anakuja Bongo baada ya kumaliza kulipa deni lote la randi 30,000 (shilingi milioni 4.8) alizoamriwa kulipa na Mahakama Kuu ya Gauteng iliyopo Kempton Park jijini Johannesburg nchini humo baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuingiza kemikali haramu, Julai 5, mwaka huu.

Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, Masogange anarejea na Melisa Edward ambaye alikamatwa naye lakini mahakama ikamwona hana hatia.



SIRI NZITO
Ujio wa Masogange bado una siri nzito kwani licha ya mahakama hiyo kumtia hatiani kwa faini au kifungo cha miezi thelathini jela, lakini bado serikali ya Tanzania inahaha kutaka kujua mzigo aliodakwa nao alitumwa na nani!
“Masogange ameahidi kutowataja watu waliompa mzigo akidai kuwa itaendelea kuwa siri yake mpaka anakufa,” kilipasha chanzo chetu.



WATOTO WA VIGOGO
Watoto wa vigogo ndiyo wamekuwa wakitajwa zaidi kuhusika na kumtuma Masogange ingawa hakuna jina la moja kwa moja la mtoto yeyote wa kigogo lililowahi kutajwa.
ANAYEMJUA MWAKYEMBE
Mpaka sasa, Serikali ya Tanzania kupitia kwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe iliwahi kumtaja kijana aitwaye Mangunga ambaye ndiye anadaiwa kuwa na Masogange ndani ya ndege kwenda Afrika Kusini.



Mwakyembe aliamuru kijana huyo asakwe na kukamatwa ili kujibu mashitaka ya kusafirisha madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine kwa Tanzania huku Afrika Kusini ikisema unga huo ni ephedrine ambao si wa kulevywa bali ni kemikali haramu.
KAMATI YA MAPOKEZI YAMWANDALIA PATI YA MAMILIONI
Habari za kifukunyuku zinadai kuwa, jijini Dar baadhi ya mastaa wameunda kamati ya mapokezi ya Masogange, Jacqueline Wolper Massawe akiwa mwenyekiti wake, katibu na wajumbe hawakupatikana majina.
KAZI YA KAMATI
Kazi ya kamati hiyo inadaiwa ni kukusanya mamilioni kutoka kwa mapedeshee wa mjini ili kuwezesha kufanyika kwa pati ya nguvu ya kumshukuru Mungu kwa kumsaidia staa huyo kutoka jela na kurudi Bongo.
“Kamati iko chini ya uenyekiti wa Wolper, si unajua huyu dada hata hivi karibuni alimfanyia birthday Masogange japo mwenyewe hakuwepo?
“Sherehe itaandaliwa kwenye ukumbi mmoja uliopo ufukweni mwa Bahari ya Hindi lakini kwa sasa sitautaja ili kuepuka wazamiaji,” kilisema chanzo chetu.


NZOWA: HIYO PATI ITAFANYIKIA WAPI, SINZA KWA DADA’KE AU?
Kufuatia kuwepo kwa madai kwamba, Masogange akitua tu Bongo atadakwa na Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, juzi Amani lilimsaka kamanda wa kikosi hicho, Godfrey Nzowa na kumuuliza kuhusu madai hayo.
Amani: Afande, naomba unisaidie mawili matatu. Yule msanii Masogange aliyekamatwa na madawa ya kulevya na kuhukumiwa Afrika Kusini anarejea nchini kesho Jumatano (jana) Je, ninyi mna mpango wowote wa kumkamata akitua?
Nzowa: Sisi hatuna shida naye tena. Alishahukumiwa kule, sasa tumkamate huku kwa sheria gani?
Amani: Basi kuna habari kwamba mmepanga kumkamata maana tumeambiwa na chanzo chetu kuwa atafanyiwa pati ya kumshukuru Mungu kwa kumtoa katika mazito.
Nzowa: Hiyo pati ataifanyia wapi, Sinza kwa dada’ke au?
Amani: Bado hawajaweka wazi.
Nzowa: Sisi hatuna shida naye.
WOLPER ASAKWA KUULIZWA
Juzi asubuhi, Amani lilimtafuta Wolper kwa njia ya simu yake ya mkononi na kumuuliza ukweli wa kuwepo kwa kamati ya sherehe ya mapokezi ya Masogange ambapo  alijibu:
“Nipo shooting (narekodi) Arusha, nitawatafuta baadaye kuhusu hilo suala kama lipo au halipo.”
MASOGANGE NAYE
Juzi Jumanne, Amani lilimpigia simu Masogange akiwa Afrika Kusini na kumuuliza kuhusu ujio wake wa jana.
Masogange: Ni kweli narudi huko (Bongo) Jumatano, mipango yote ya safari tayari, namshukuru Mungu kwa yote.
WENGINE WANASOTA!
Wakati Masogange akiwa ameponea tundu la sindano, mrembo mwingine wa Bongo Fleva, Sandra Khan ‘Binti Kiziwi’ anateseka gerezani huko China alipofungwa kwa miaka mitatu kwa msala wa madawa ya kulevywa wakati Saada Kilongo yuko mahabusu Bongo kwa kesi ya aina hiyohiyo.
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger