Showing posts with label BONGO MOVIE. Show all posts
Showing posts with label BONGO MOVIE. Show all posts

"MASTAA WENGI WAMETOKEA KWENYE UCHANGUDOA NA KUVAMIA TASNIA YA FILAMU"...KAULI YAMPONZA DUDE...SOMA ZAIDI

WASANII wa kike wanaotamba kwenye filamu za Kibongo, hivi karibuni wamembwatukia staa mwenzao, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na kuipinga kauli yake kwamba mastaa wengi wa kike wametokea kwenye uchangudoa na kuvamia tasnia hiyo, shuka na mistari uipate habari hii.
Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Wakizungumza na Risasi Jumamosi, mastaa hao wamemtaka Dude kuacha tabia ya kuropoka kwani kauli yake imewavunjia heshima mbele ya jamii.
Baadhi ya mastaa waliotoa kauli za kumbwatukia Dude na kauli zao ziko hapa chini ni hawa wafuatao:
Tamrina Poshi ' Amanda".
TAMRINA POSHI ‘AMANDA’
“ Ni heri Dude aache kuzungumza vitu visivyokuwa na maana, ajifunze  mambo mazuri kwani ni mtu mzima sasa. Kila mara anatuponda wasanii wa kike, kila mtu ana maisha yake kama wapo wanaofanya uchangudoa hao ni hulka zao, sina tabia hiyo na sanaa nimeianzia kwenye vikundi .”
Upendo Mushi 'Pendo'.
UPENDO MUSHI ‘PENDO’
“Kauli ya Dude siyo ya kweli kama wapo ni  baadhi na siyo wote, sijaingia kwenye sanaa kwa rushwa ya ngono na sina tabia hizo, sijaipenda kauli yake.”
BABY MADAHA
“Siyo kweli kwamba sisi ni machangudoa . Wasanii wa kike wenye tabia hizo wanatoka katika maisha duni na wale wanaolipwa malipo duni kwenye filamu lakini wengine tumetokea kwenye familia   za hadhi na tunaishi kwa kufuata maadili.”
HALIMA YAHAYA ‘DAVINA’
“Sijaipenda kauli ya Dude, ametukosea sana ingawa watu wengi wanaona tasnia hii ni kama  ya kihuni lakini siyo wote wenye tabia hizo za kihuni, wengine tunajiheshimu na tuna familia zetu tunaithamini sanaa  tunaichukulia kama kazi.”
SNURA MUSHI
“Dude ameongea uongo, binafsi siko hivyo na sina maisha ya kuzurura, starehe na pombe na sitarajii kuwa na maisha hayo, ili heshima yake iendelee, angetuomba radhi na kuifuta kauli yake.”
MIRIAMU JOLWA ‘JINI KABULA’
“Huo ni mtazamo wa Dude, wasanii wa kike tunatakiwa kumuombea kwa Mungu ili ampe akili za kuweza kuzungumza vitu vya maana na siyo hivyo vya kutushushia heshima kwenye jamii.” 

USHOGA WA DK.CHENI HUU HAPA...!! SOMA HAPA KUJUA KIUNDANI...

SIKU chache baada ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) kuzuia filamu ya mkongwe katika sinema za Kibongo, Mahsein Awadh Said ‘Dk. Cheni’ ijulikanayo kwa jina la Nimekubali isiingie sokoni kwa madai kuwa imekiuka maadili ya Kitanzania, msanii huyo ameibuka na kueleza kinagaubaga, Risasi Jumamosi limenasa sauti yake.
Akizungumza na mwandishi wetu Jumatano ya wiki hii maeneo ya Mlimani City jijini Dar, msanii huyo alisema amesikitishwa na maamuzi ya bodi hiyo huku akidai kuwa lengo la filamu hiyo ni kukemea tabia za kishoga zinazoendelea kuibuka kwa vijana ikiwa ni pamoja na kupinga uhalali wa ndoa za jinsia moja.
Mkongwe wa sinema za Kibongo, Mahsein Awadh Said ‘Dk. Cheni’.
Katika maelezo hayo, DK. Cheni ambaye huzitendea haki filamu zake kwa kuvaa uhusika halisi, alisema moja ya kigezo ambacho bodi hiyo imekitumia kuzuia filamu hiyo ni pamoja na muonekano wa bango la filamu hiyo ambalo linamuonesha msanii huyo akiwa amevaa vazi la shera huku akiwa amejiremba kwa madai kuwa ni kuchochea ushoga jambo ambalo msanii huyo amelipinga vibaya.
“Eti ushoga wangu uko kwenye kujiremba sana, hakika wamenionea sana, lengo letu ni kuonya na kukemea vikali vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja, huwezi kuelimisha bila kuonesha madhara yake kwa vitendo kama ilivyo ndani ya filamu hiyo.
Mkurugenzi wa bodi ya filamu,  Joyce Fissoo.
“Lakini, ndani ya filamu hiyo, kuna kipande ambacho kinaonesha kiongozi wa serikali akikemea kitendo hicho, sasa hapo ushoga wangu uko wapi? Kuvalia shera kwenye kava? Siyo sahihi,” alisema Dk. Cheni.
Mbali na kava hilo, msanii huyo alidai haoni kosa lolote katika filamu hiyo hivyo ataendelea kupigania haki yake na kwamba hayuko tayari kuonewa.
Jitihada za kumpa mkurugenzi wa bodi ya filamu,  Joyce Fissoo ili kuelezea juu ya sekeseke hilo, ziligonga mwamba hadi gazeti hili linaingia mtamboni lakini imedaiwa kuwa bodi hiyo itasimamia msimamo wake. 
b

STEVE NYERERE ATAKIWA KUJIUZULU BONGO MOVIE...

Hali si shwari katika klabu ya wasanii wa filamu za Kibongo, Bongo Movie Unity ikidaiwa kuwa baadhi ya ‘memba’ wake wanashinikiza mwenyekiti wake, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ajiuzulu.


 
Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.

Habari zilizoifikia Stori Extra wikiendi iliyopita zilidai kuwa, baadhi ya wasanii wa klabu hiyo akiwemo mwenyekiti huyo walilamba mshiko kutoka kwa mwanasiasa mmoja wa CCM mkoani Mbeya ili wamfanyie kampeni katika uchaguzi ujao jambo ambalo wenzao walilipinga vikali kwa kuwa wao hawajihusishi na siasa bali wasanii na jamii.

Alipotafutwa Steve kujibu tuhuma hizo hakupatikana lakini katibu wake, William Mtitu alikiri kuwepo kwa ishu hiyo.

WEMA, KAJALA, AUNT WACHAFUA HALI YA HEWA TRIPLE A JIJINI ARUSHA...TAZAMA PICHA HAPA WALICHOKIFANYA...

Kajala, Wema, Aunt na Zamaradi wakiwa katika pozi tofauti.
....Wakiwa pamoja na Mirror tayari kwa ajili ya kwenda kwenye Show, klabu ya  Triple A.
Wema Sepetu, Aunt Ezekiel na Kajala Masanja tayari kwa ajili ya kwenda ukumbini.
Kajala akipanda stejini.
Wema akipanda jukwaani huku akiacheza.
...Wakiwa katika picha ya pamoja.
...Wakicheza na Mirror.
Wema katika pozi.
Msanii Dyana Kimaro katika pozi.
Wema Sepetu pamoja na Meneja wake Martin Kadinda muda mfupi baada ya kuwasili jijini Arusha.
  

Wema Sepetu, Zamaradi na Martin Kadinda katika picha ya pozi.

Kajala Masanja na Aunt Ezekiel wakiwa wamepozi hotelini.

 MASTAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Kajala Masanja pamoja na wasanii wa Bongo Fleva Chid Benz na Miraji Hussein ‘Mirror’ hivi karibuni  walitinga katika jiji la Arusha kwa ajili ya kumtambulisha msanii Mirror kwenye klabu ya Triple A.

KAJALA AJIBU TUHUMA ZOTE ZA SKENDO ZINAZOMKABILI,PAMOJA NA KUNASWA NA DAWA ZA KULEVYA NA KUNASWA NA MUME WA RAFIKI YAKE NCHINI CHINA...SOMA ZAIDI

kajala
Hii ni interview ya kwanza ya mwigizaji Kajala, yani ndio kwa mara ya kwanza kahojiwa kwenye chombo cha habari  baada ya kumiliki headlines kwa ishu zake tatu ambazo ni kuchukua mume wa mtu, kudaiwa kukamatwa na dawa za kulevya na safari yake kwenda China.

Yafuatayo ni maswali ya millardayo nyumbani kwake Dar es salaam.
millardayo : Ni kweli kuhusu hii ya mume wa mtu?
Kajala: Hapana, niliambiwa mtu wa kwanza kuandika hii alikua mtu wa blog ndio magazeti na mitandao mingine ikafata ila sio kweli… sikufatilia manake ukweli naujua mwenyewe, niliumia na hata mama yangu aliumia na aliniuliza.
Kwenda club au kukutana na mtu na kupiga nae picha sio kwamba umeiba mume wa mtu, huyo dada kama kweli yule angekua mume wake angenifata manake haya kuniona hivi hajawahi… yeye yuko Hongkong mi niko China ananiambia nimeiba mume wake…. huyu Mwanaume anaishi hukohuko, China nilikwenda mwenyewe na wala sio kwamba nimetoka nae Tanzania.
millardayo : Siku unapigwa picha ukiwa na huyu mwanaume Club ulikua unajua unachukuliwa picha?

kajala mume wa mtu
Kajala: Siku hii ilikua ni birthday ya mwenye club, mimi sikujua kama napigwa picha ndio zikasambazwa kwenye mtandao, wale wadada wamezichukua huko ndio wakaanza kunitukana.
millardayo : Vipi kuhusu hii iliyoandikwa ya wewe kukamatwa na dawa za kulevya Airport?
Kajala: Sio kweli manake hata dawa zenyewe za kulevya sijui zilivyo zaidi ya kuziona tu kwenye TV, sasa hivi kila staa akipita kwenye uwanja wa ndege Dar ni lazima asachiwe sana kwa sababu wanasema ‘nyinyi mastaa mnatuharibia sana kazi’ kwa hiyo lazima wakuweke pembeni kukukagua.
millardayo : Safari yako ya China ilihusu nini?
Kajala: Nilikwenda kufanya shopping tu sababu ya movie yangu naanza kushoot January 2014 kwa hiyo nikaenda kununua vitu vya kuvaa, sio Camera wala vifaa… ni nguo tu, shopping inazidi milioni kumi.

kajala 12
millardayo Inaweza kutokea siku moja tukasikia Kajala kaolewa?Kajala: Ndoa yangu ni ya kanisani ila sijui kama nitaruhusiwa kuolewa tena kwahiyo namsubiria labda mume wangu akitoka Jela, sina mpango wowote wa kuolewa kwa sasa japo napata usumbufu ila nawaambia tu mume wangu yuko jela, huwa namtembelea kila weekend…. kukaa kwake jela kumeniathiri sana, tulikaa kwenye ndoa miezi sita tu kabla ya misukosuko kuanza, nilikua nampango wa kupata mtoto mwingine wa pili ili niwe nimemaliza ila sasa hivi siwezi kuzaa, nimekaa tu namsubiria…..

MH..NI PICHA TU

Staa wa Filamu za Kibongo, Mahsein Awadh almaarufu Dokta Cheni akiwa katika pozi tata na staa mwenziye, Elizabeth Michael 'Lulu'.

KAJALA: KIYOYOZI CHA CHINA KIMENIFANYA NIWE MZURI ZAIDI KWA KUIBADILISHA NGOZI YANGU

MWIGIZAJI Kajala Masanja amekanusha vikali suala la kujipodoa badala yake amesema kiyoyozi cha nchini China kimeifanya ngozi yake ibadilike.

Kajala Masanja.
Akizungumza na paparazi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita, Kajala akiwa katika harakati za kuelekea China alisema amekuwa akiipenda nchi hiyo kwani akiwa huko ni ‘full’ kiyoyozi ambacho kimemfanya aonekane mweupe.
“Ngozi yangu inabadilika na kuwa nzuri sana, China kunanipenda. Kiyoyozi mwanzo mwisho lazima uwe mweupe,” alisema mwigizaji huyo.

Rose Ndauka Ajifungua mtoto wa Kike..!!

STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka amejifungua mtoto wa kike kwa njia ya upasuaji mwanzoni mwa wiki hii katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar.

Akizungumza na Ijumaa, Rose Ndauka alisema anamshukuru sana Mungu kwa kumjaalia kujifungua salama huku mwanaye huyo akiwa na afya njema.
 
Ki ukweli kabisa namshukuru sana Mungu kwa zawadi ya mtoto kwa maana nimejifungua salama kabisa,mimi na mtoto tuko vizuri na nafurahi sana kuingia kwenye ulimwengu mwingine kabisa wa cheo kipya cha kuitwa mama,” alisema Rose.
 
Akasema hivi sasa ataweka shughuli zote pembeni kwa ajili ya kuanza kumlea mtoto mpaka atakapofisha umri ambao anastahili kuachwa ndipo ataendelea na shughuli zake za sanaa.

RAY AONA AIBU KUMBUSU LULU KWA SABABU BADO NI MTOTO...

STAA wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amesema alipata wakati mgumu kumpanga mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwenye filamu yake ambayo walipaswa kucheza kama wapenzi kwa kuhofia kumbusu.

Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza katika kituo kimoja cha runinga cha jijini Dar hivi karibuni, Ray alisema licha ya kuwa Lulu alikuwa anastahili kuigiza katika sinema ya Woman Principle miaka kadhaa iliyopita, aliona Lulu anafaa kutokana na umakini wake lakini akaona bora amchukue Miss Tanzania namba 3, 2003, Nargis Mohammed kwa kuhofia kupata aibu ya kuoneshana malavidavi na Lulu.
 

Vincent Kigosi ‘Ray’.

Lulu alikuwa na uwezo wa kumudu kipengele hicho, kipindi hicho alikuwa mdogo sana, niliona ni jambo la aibu kidogo kumbusu mdomoni mtoto mdogo kama yeye halafu ni kitu ambacho jamii itakaa ikitazame nikaona bora nimchukue Nagris, Lulu nikampa sini nyingine,” alisema Ray.

Aliongeza kuwa, kikubwa kilichomfanya avutiwe kucheza na Nagris ni kwa sababu ni mwanamke ambaye katulia na hana skendo hivyo itamuongezea heshima na mvuto wa kazi yake katika jamii. 

AUNT EZEKIEL AKIRI MUMEWE KUKAMATWA DUBAI..

STAA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amekiri mumewe kukamatwa na kupata misukosuko lakini si kufungwa kama baadhi ya watu wanavyoeneza uzushi.

 
Aunt Ezekiel.
Akipiga stori na mwandishi wetu hivi karibuni, Aunt alisema mumewe, Sunday Demonte alikamatwa kutokana na viza yake kuisha ambapo alishikiliwa kwa muda na alipokamilisha taratibu za ‘kurinyuu’, aliachiwa.

“Nashangaa sana mambo haya yamevuma kuwa mimi nimemuacha mume wangu amefungwa, ukweli ni kwamba mume wangu yuko huru na hata sasa ukitaka ongea naye, ni mwanamke gani atakuwa na furaha hivi wakati mumewe ana matatizo?” alihoji Aunt.

http://api.ning.com/files/MN6ZNqVOIKOj4UGweglrZ7yo2eHgFV0ZU-eQnP5tErLW4PbZZ9Zb84QoA41aCDvL26jOJJb5G7i9cBqgodCdlcfPSY-h3SI8/AUNTNADEMONTE.jpg?width=650


Aunt akiwa na mumewe.
Katika mistari mingine, Aunt alisema watu wengi wanatamani kuona ameachika au kujua mwenendo wa maisha yake na mumewe lakini wanajidanganya kwani yeye ni mwanamke aliyeamua kuolewa na amefundwa hivyo wataambulia patupu.

Siyo  rahisi mimi kutoa siri ya maisha ninayoishi na mume wangu, ni makubaliano yetu. Kimsingi ndoa yetu iko imara, watasubiri sana na watachoka wenyewe,” alisema Aunt.

SNURA AMWAGIA SIFA KIBAO WEMA SEPETU.NI BAADA YA KUHUSIKA KWENYE VIDEO YAKE YA NIMEVURUGWA

clip_image001Hatimaye baada ya ukimya mrefu kuhusu urafiki wao, leo hii Snura ameamua kufunguka, na kukumbuka fadhila na ukarimu wa Wema kwake kipindi cha nyuma na hasa alipotoka mara ya kwanza kabisa kimuziki. Kupitia ukurasa wake wa Instagram mwimbaji huyo wa NIMEVURUGWA ame andika kifuatacho:clip_image001clip_image001[5]Hakuna kitu kizuri kama kushukuru na kukukumbuka fadhila no matter what. Well done Snura.

"Natamani kuokoka.... !Natamani kumrudia yesu kristo"...Aunt Ezekiel Asaema..


 
Licha  ya kubadili dini na kuwa muislam kisha kupewa jina la Rahma, staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amesema sasa anatamani kurejea ‘ulokoleni’ na kumrudia Yesu kwa kuokoka. 
 
Akizungumza na gpl hivi karibuni nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, msanii huyo ambaye alibadili dini kutoka ukristo na kuwa muislam baada ya kuolewa na mumewe, Sunday Demonte alisema anajisikia kurudi kwenye ukristo kwa madai ya kumtumikia Mungu kikamilifu.
 
Akionesha msisitizo katika hilo, Aunt alisema moyo wake umekuwa ukitamani kusikiliza mafundisho na mahubiri ya kikristo pamoja na kusikiliza nyimbo mbalimbali za injili.
Wakizungumzia mawazo ya kuokoka ya msanii huyo, baadhi ya mashabiki wake walimshangaa huku wakionesha wasiwasi wake juu ya kusilimu na kudai huenda kubadili kwake dini ilikuwa danganya toto.
 
“Huyu si aseme tu uislam umemshinda? Kasilimu juzijuzi tu hapa na kudai ameanza kusali msikitini, leo anatuambia anatamani kuokoka, hawa mastaa wetu wanamchezea sana Mungu,” alisema Rahma wa Kinondoni jijini Dar.

-gpl


MASKINI MAMA KANUMBA..!HALI NI MBAYA, SASA ATEMBEZA BAKULI.NASIKITISHA, MSAADA WAHITAJIKA.

Mama mzazi wa marehemu ‘Seven Kanumba’ Frola Mtegoa.

MAMA wa msanii nguli wa filamu nchini marehemu ‘Steven Kanumba’ Frola Mtegoa amesema yuko katika mkakati wa kuandaa filamu inayohusu maisha ya mwanaye kiasi cha kufikia hatua ya kuomba msaada ‘kutembeza bakuli’. Akizungumza na paparazi wetu mama huyo alisema kwamba, anapata wakati mgumu kukamilisha jambo hilo kutokana na kukwama na kutaka asaidiwe ili kufanikisha jambo hilo.
 “Nimekwama na nawaomba wadau wajitokeze kunisaidia nikamilishe hili, nahitaji msaada wa kifedha na hata ushauri,”alisema.
Mama huyo alisema lengo la kuandaa kazi hiyo ni kutaka kufikisha ujumbe katika jamii kwa kuamini kwamba wengi watajifunza kupitia maisha ya mwanawe.

Marehemu Steven Kanumba.
Amemtaka yeyote ambaye atakayeguswa na jambo hilo asisite kuwasaliana naye na kumsaidia.

KWELI RAY KACHEMKA, ANGALIA MAKOSA KWENYE MOVIE MPYA YA RAY ,HII NDIO BONGO MOVIE BWANA!!NOMA SANA



kwenye scene hii anaonekana camera man kwa mbali ukiangalia kwenye viio vya nyumba io ni baada tu ya wazee wao kurudi kutoka Zanzibar 

....


Wakati Ray anaongea na mpenzi wake wa siri wakati mpenzi wake huyo akiogelea huku akimueleza Ray historia yakeya maisha kwa ufupi.....




 Wakati Ray amepigiwa simu na mwanasheria wake kwamba anatakiwa aende ili aelezwe jambo fulani alilolifanya mama yake..... picha ya upande wa kulia inaonesha ray akiongea..... na kwa nje utaona ukuta mrefu na mweupe  lakini shot ya pili yani baada ya sekunde tu inaonesha yupo sehemu nyingine kabisa lakini akiendeleza mazungumzo yale yale.

NISHA APATA GONJWA LA AJABU LINALOMPA MAUMIVU MAKALI,USHIRIKINA WAHUSISHWA


Maskini! Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ anateseka baada ya kupata gonjwa la ajabu linalomsababishia maumivu makali.
Hali ya Nisha ilivyo kwa sasa. Hapa akilazimishwa kula chakula.
Akizungumza rafiki yake ambaye pia ni msanii mwenzake, Happy John ‘Nyatawe’ alisema Nisha alianza kulalamika kwamba anasikia vitu vikimtembea mwilini na maumivu makali ya kichwa kinachomuuma mfululizo.
“Alianza kulalamika kuumwa kama mchezo lakini siku zinavyozidi kusonga ndivyo hali yake inavyozidi kuwa mbaya, hata hatuelewi ni nini,” alisema Nyatawe.
Paparazi wetu alifanikiwa kuzungumza na Nisha akiwa nyumbani kwake huku akilishwa chakula kama mtoto ambapo alisema anasikia maumivu makali ya kichwa na tayari ameshaenda hospitali akapewa dawa lakini ugonjwa unaomsumbua haukujulikana.
 
 Nisha akilishwa chakula.
“Kichwa kinaniuma sana na vitu vinanitembea mwilini sijielewi kabisa, muda mwingine ninakandwa na maji ya baridi kutokana na maumivu makali, nimeenda hospitali nimepima kila kitu lakini ugonjwa hauonekani,” alisema Nisha akitokwa machozi kutokana na maumivu aliyokuwa akiyasikia.
Wakati paparazi wetu akiendelea na mazungumzo hayo alimshuhudia Nisha akiweweseka kama mtu aliyechanganyikiwa.
KUNA MKONO WA MTU?
Baadhi ya wasanii ambao hawakutaka kutajwa walisema kutokana na hali aliyonayo Nisha inawezekana kuna mkono wa mtu kwani wasanii wamezidi kwa kulogana hivyo anatakiwa kuombewa kwa Mola kwani hali ya afya yake si shwari.

Baada ya kulinasa Penzi la BOND, Wastara aonywa kuhusu Ngono za Kinyume na Maumbile ...!!!


Msanii nyota kwenye kiwanda cha Bongo muvi Wastara amepewa tahadhari kubwa na mshabiki wake kuhusu mpenzi wake mpya ambae ni prodyuza wa filamu aliyefahamika kwa jina la Bond Bin Sinnon kuwa amekuwa akipenda sana mapenzi kinyume na maumbile hakuna mfano.  

Habari za uhakika zilitua ndani ya ofisi  zilizopo Mwananyamala Komakoma zilisema Bond ambae aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa zaidi ya Miaka 4 na nusu na Mtangazaji Lulu Semagongo ambae kipindi flani aliwahi kukiri kwenye vyombo vya habari hasa magazeti pendwa kuwa yeye mzuka wake ni kufanya mapenzi na maumbile tangu akiwa mdogo.Hivyo basi hali imetiliwa shaka na mashabiki wa Wastara kuwa kwa vile wawili hao wameonekana kuwa na mahusiano ya kimapenzi basi ni dhahiri kuwa Wastara wame makini la sivyo kijana huyo anaweza kuendeleza tabia yake hiyo aliyokuwa anaifanya kwa Lulu. 

Chanzo chetu kiliendelea kuilza Xdeejayz kuwa Bond ambae tangu aachane na Lulu hakuwahi kuwa na mpenzi hata siku moja" Huyo Bond anaogopwa sana na mabint kwa sababu ya kauri ya Ant Lulu alipotangaza kuwa yeye mzuka wake ni  kifanya mapenzi kinyume na maumbile hivyo hakuna msichana yeyote anaemkubari kwa hofi hiyo hivyo hata Wastara tunashangaa wamepatana kiasi hicho" Kilisema chanzo hicho.Mahusiano ya Bond na Wastara yalianza kwa siri sana lakini hivi sasa kila kitu wazi hadi ndugu wa Wastara wanamjua bond kama shemeji yao, 


Mapaparazi wa Xdeejayz walifunga safari hadi Tabata jirani kabisa na anapoishia Wastara ili kupata umbea ambapo majirani hao walifunguka" Aaah na nyie waandishi mko wapi siku zote bwana? Wastara na Bond ni mke na mume mbona wala hakuna kificho tena Wastara sasa amerejesha furaha ya maisha kwa malavidavi ya Bond ambapo wanaishi pamoja kupika na kupakua" Alisema jirani huyo aliyejitambulisha kwa jina la Amina Aidha mwanzo wa mahusiano ya wawili hayo hayana tofauti na yale ya Pennie na Diamond ambao walianza kufanyia interview kwenye kipindi na baadae wakageuza na kuwa wapenzi kabisa hivyo ndivyo ilivyotokea kwa Wastara na Bond

 Credit: XDEEJAYZ

HACKERS WAVAMIA UKURASA WA FACEBOOK WA NISHA NA KUWEKA PICHA ZA NGONO..

Mwanadada Salma Jabu ‘Nisha’ anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo amekubwa na balaa baada ya ukurasa wake wa Facebook kuingiliwa na watu ambao wanautumia vibaya kwa kuweka picha za ngono na picha ambazo hazina maadili, tukio hilo limemfanya msanii huyo kuwa katika wakati mgumu baada ya kupigiwa simu na jamaa zake. 


“Jamani kuna watu wana majaribu sana wameingia katika page yangu ya facebook na wanatuma picha za ajabu ajabu ambazo kwa mtu ninayejiheshimu kama mimi siwezi kuweka picha hizo kwani nina wapenzi wengi wanaohitaji kuchati na mimi kwa kazi zangu,”alisema Nisha.
























Nisha anawalaumu watu ambao wameingia na kuchukua password yake na kuposti picha mbaya kwa nia ya kumharibia ukurasa wake ambao yeye utumia kwa ajili ya kuwasiliana na wapenzi wa filamu ambao wamekuwa wakipata taarifa zake kupitia ukurasa huo,

Msanii huyo anaomba watu wanaohusika na udhibiti wa mitandao ya kijamii kutafuta njia ya kuwakamata watu ambao wanatumia teknorojia vibaya kwa kuwaharibia wengine, baadhi ya wasanii wamekuwa wakikumbana adha mbalimbali kama matumizi mabaya ya picha zao na hata majina yao, pia kwa kurasa ambazo haziwahusu.

MASHABIKI WA BONGO MUVI WAUPONDA MWONEKANO MPYA WA RAY...WADAI KUWA AMECHEMKA...


Huu  ni  muonekano  mpya wa  Vicent  Kigosi ambao ni moja ya maandalizi ya movie  yake  mpya ...
Ni  muonekano  ambao  kwa  kiasi  flani  umewachefua  mashabiki  wake  ambao  dakika  chache  baada  ya  picha  hizo  kuwekwa  walijimwaga  kwa  comment  ambazo hazikumuunga  mkono  kwa  asilimia  zote. 

“Je nageukia bongoflava au kuna nini kinakuja?”. Aliadika  Ray  kwenye  moja  ya  picha  zake.
 
 

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger