Showing posts with label Ajali. Show all posts
Showing posts with label Ajali. Show all posts

AJALI..!! KONDAKTA AGONGWA NA LORI NA KUFA AKIWAVUSHA BARABARA WANAFUNZI WA CHEKECHEA...


Marehemu William Francis,28, enzi za uhai wake


Baadhi ya viongozi wa chama cha waendesha daladala wakiendelea kukusanja michango ya rambi rambi leo mchana




Baadhi ya madereva na makondakta wa daladala wakiwa na nyuso za hudhuni baada ya kupokea taarifa za tukio hilo.
NA DUSTAN SHEKIDELE, MOROGORO.
KATIKA hali ya kuhuzunisha kondakta wa Hiace inayofanya safari zake Kihonda - Mjini William Francis,28, jana mchana amegongwa na Lori na kufa papo hapo eneo la Kihonda barabra kuu ya Morogoro-Dodoma, alipokuwa akiwavusha abiria wake ambao ni wanafunzi wa chekechea uapande wa pili wa barabara hiyo isiyokuwa na vituo vya kushusha na kupakia abiria.

Akihojiwa na mwandishi wa habari hizi msemaji wa chama cha madereva na makondakta wa daladala mkoani Morogoro Bw Kigola Pazi alisema marehemu aligongwa na gari hilo alipokuwa akiwavusha abiri wake ambao ni madenti wa shule ya awali 'chekechea'

"Kwa nyinyi waandishi wa habari mtusaidia kufikisha kilio chetu kwa mamlaka husika mwenzetu amekufa akitetea roho za abiri wake kufutia barabara ya Kihonda kukosa vituo vya kushusha na kupakia abiri, Wille aligongwa na gari wakati akirudi upande wa pili wa barabra baada ya kuwavusha watoto wawili wa shule ya chekechea akisema kwa uchungu msemaji huyo wa chama hicho.
 
Mwandishi wa habari hizi alifika kwenye kituo kikuu cha daladala kilichopo katikatika ya mji kasoro bahari 'Morogoro' na kushuhudia baadhi ya madereva na makondakta wakiwa na nyuso za huzuni baada ya kupokea taariza hizo za kifo cha ghafla cha mwenzao.

'Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake libarikiwe Amen'


PICHA: AJALI MBAYA YA BASI LA URAFIKI...!!

0 027b0

1 96a73


2 3f6b3
Wakazi wa kijiji cha Ndolela Tarafa ya Isimani wilaya Iringa vijijini wakiangalia ajali ya Basi la abiria la Urafiki  T 594 ABM lililoanguka kijijini hapo jana likitokea Iringa kuelekea Dodoma. PICHA NA SAID NG'AMILO.

BREAKING NEWS: MSANII PROFESA JAY APATA AJALI MBAYA YA GARI MAENEO YA KIMARA JIJINI DAR..!!

Taarifa zilizotufikia ni kwamba Mwanamuziki wa Hip hop, Joseph Haule 'Profesa Jay' amepata ajali ya gari baada ya kuparamia kifusi akijaribu kumkwepa mtu eneo la Kimara-Baruti, jijini Dar wakati akitoka nyumbani kwake Mbezi! Prof hajaumia sana katika ajali hiyo japo gari lake limharibeika.
Muonekano wa gari baada ya ajali eneo la Kimara-Baruti, jijini Dar.


--GPL

INASIKITISHA SANA ...!! AJALI YA GARI YAUA WALIMU WAKUU WATATU HUKO KILOSA...


WALIMU wakuu watatu waliotajwa kuwa ni Margaret Kimbo, Agrey Kikwesha na Lanford Muhando kutoka shule mbalimbali za Tarafa ya Magole wilayani Kilosa, wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali.
Mbali ya vifo vya walimu hao, ajali hiyo iliyotokea baada ya tairi moja ya nyuma kupasuka, imesababisha majeruhi 17, baadhi yao wakiwa katika hali mbaya.

Walioshuhudia waliliambia gazeti hili kuwa ajali hiyo mbaya ilitokea juzi, majira ya saa 12 jioni katika Kijiji cha Mvumi na Rudewa, eneo la Kisangata mkoani hapa.
Kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Magole, Koletha Mhululu, walimu hao walikuwa wakisafiri kwenda wilayani Kilosa kuitika wito wa ghafla wa mkuu wa wilaya hiyo kwa jambo la dharura ambalo hawakulifahamu mapema.
Mwalimu Koletha alisema tairi la gari hilo  lilipasuka na kusababisha lipinduke  mara nne na kusababisha baadhi yao kupoteza maisha hapo hapo.
"Tulikuwa walimu na waratibu zaidi ya 17 tukielekea wilayani kuitika wito wa mkuu wa wilaya, gari lilikuwa kasi na lilipopasuka tairi,  lilibilingika kama mara nne hivi,” alisema mwalimu huyo kwa uchungu na kushindwa umalizia.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema ajali hiyo ilitokea baada ya gari aina ya Toyota Hiace kupasuka tairi la  nyuma.
TANZANIA DAIMA


AJALI MBAYA YATOKEA MLIMA WA MZALENDO IGAWILO JIJINI MBEYA.

 
Lori baada ya kupata ajali katika eneo la mlima wa Mzalendo Igawilo jijini Mbeya wakati likielekea jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya majeruhi katika ajali hiyo wakipelekwa hospitali.

AJALI ...! DEREVA WA BODABODA AZIRAI BAADA YA KUMGONGA MAMA MJAMZITO HUKO KIGOGO LUHANGA...



Wasamaria wema wakimpepea.


...Akiwa hoi.


Akisogezwa pembeni ya barabara.

Dereva wa bodaboda aina ya Bajaj Boxer yenye namba za usajili T 344 CDJ ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja muda si mrefu amepata ajali na kuzirai baada ya kumgonga mama mjamzito aliyekuwa akikatisha barabara eneo la Kigogo Luhanga bodaboda jijini Dar es Salaam. Mama huyo anayedaiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo alitoka mbio baada ya msala huo.

INASIKITISHA...!! AJALI MBAYA YATOKEA IRINGA, WATU 38 WAJERUHI...

Daladala aina ya Coster yenye namba za usajiri T.960 AQY inayofanya safari zake za Kibwabwa mjini Iringa mara baada ya kugongana na gari aina ya Isuzu Tipa, lenye namba SM 3363 katika Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha Bibi.
l_dd9a2.jpg
m_74746.jpg
Taxi ambayo nayo ilisababishiwa ajari ikiwa katika eneo la tukio, huku askari polisi wakilinda usalama wa mali za abiria na baadhi ya vitu katika eneo la tukio.(A.M)
n_7bc78.jpg
Wananchi wa mji wa Iringa wakitazama ajari hiyo katika mlima wa Ipogolo (Kisima cha Bibi).
o_fbf87.jpg
Basi aina ya Coster linalofanya ruti zake Kibwabwa Manispaa ya Iringa likiwa eneo la tukio, baada ya kugongana na Roli Tipper na kusababisha ajali iliyojeruhi zaidi ya watu 30.
ZAIDI ya abiria 38 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne mjini Iringa, baada ya Bus dogo la abiria aina ya Coster kufeli breki na kuyagonga magari matatu, ajali ambayo imetokea majira ya saa saba mchana wa siku ya jana.
Tukio hilo limetokea katika mlima wa Ipogolo, eneo maarufu mjini Iringa kama "Kisima cha bibi", ambapo ajali hiyo imesababisha majeruhi 38 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Iringa, huku chanzo cha ajali hiyo kikisemekana kuwa na kuferi breki kwa Bus hilo la abiria,lenye namba T. 960 AQY na kuyavaa magari matatu, gari kubwa aina ya Tipper Isuzu SM784 BNA la manispaa ya Iringa, Tax pamoja na Hiace.
Akizungumzia hali ya majeruhi wa tukio hilo , Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa Dr. Deogratius Manyama amesema wamepokea majeruhi 38, na waliolazwa ni 8 huku majeruhi watatu wakiwa na hali mbaya, na kuwa majeruhi wengi wameumia zaidi kichwani na kifuani, huku majeruhi 27 wakiruhusiwa kurudi nyumba kwao kutokana na kutokuwa na majeraha makubwa.
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger