Showing posts with label utafiti. Show all posts
Showing posts with label utafiti. Show all posts

KWA WANAWAKE: FAHAMU DALILI KUMI ZA AWALI ZA KUGUNDUA KAMA UNA UJAUZITO (MIMBA)...




MWANAMKE anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.Maumivu kwenye matiti:

Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.

Maumivu mwilini:

Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.

Kutokwa damu bila kutegemea:


"Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,” anasema Goist. Ambaye anaendelea kusema kwamba iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito..

Kuchoka:


Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.

“Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingizi” anasema Goist.

Chuchu kuwa nyeusi:


Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, Goist anasema: “Wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.”

Kichefuchefu:


Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha. 

Mwili kuvimba:


Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.

Kwenda haja ndogo mara kwa mara:


Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.

Tamaa ya vitu mbalimbali:

Kutokana na mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.

Kuumwa kichwa:

Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususani katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.

Kufunga choo:


Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.

Kuwa na hasira


"Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,” anasema Goist

Kuongezeka kwa joto mwilini:


Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna “mtoto anakuja”.



JE UNAFAHAMU MADHARA YA KUJICHORA TATTOO.....!!

 
Producer Pharrell Williams alishawahi kukiri kuwa alipata maumivu makali sana wakati anafuta tatto alizochora wakati wa ujana wake na akajutia kitendo hicho. Alikuwa muoga wa magonjwa atakayopata baada ya tattoo kufutwa na mionzi mikali kwenye mwili wake inayoweza kusababisha saratani na magonjwa mengine.

Picha Zingine Ziko Hapa
Angelina Jolie alibidi afute tattoo ya mpenzi wake wa awali Billy Bob aliyoichora wakati wako pamoja.



Huyu ni mwigizaji Matt" Damon alijichora tattoo kabla hajawa B list Super Star wa filamu marekani na kuamua kuifuta ili kujenga heshima zaidi.

Jamaa aliweka midomo ya rapper Trina kwenye shingo yake wakati wako pamoja na baada ya kuachana nae alibidi afute tattoo, Maumivu yake sasa.

Baada ya kuachana na mke wake Jennifer Lopez, Mac Anthony alibidi afunike tattoo ya jina la Jennifer na kitu kingine. Aliogopa maumivu ya kufuta.


50 Cent kashazoea kufutwa na kuchora tattoo zingine kwenye maisha yake. Akiwa na jambo jipya huongeza tatto anavyo jiskia.

JE UNAJUA KWA NINI WATU HUOTA WAKIWA WANAFANYA MAPENZI...?? SOMA HAPA NIKUJUZE CHANZO CHA NDOTO NYEVU...


Miongoni wa makundi ya vijana hasa wenye umri wa kati miaka 15-23 wengi wao huota wakifanya mapenzi ndotoni, lakini mbali na hao kuna watu wazima pia ambao hukumbwa na tukio hili. Uotaji wa ndoto hii umekuwa ukitafsiriwa na wengi kwa maana tofauti tofauti, huku wengine wakiuhusisha na ufanyaji mapenzi na Majini.

Uchunguzi unaonyesha kuwa uotaji ndoto za kimapenzi huwatokea hata watu ambao hawajawahi kufanya kitendo hicho kabisa, huku watu wanaofanya nao wakiwa ni wale wanaowafahamu kwa sura au wasiowafahamu. Wengi wamekuwa wakijiuliza maswali mengi juu ya nini kinachangia uotaji huu wa ndoto za kimapenzi?

Kitaalamu ndoto hizi hutokana na mawazo ya mtu husika ambayo yanaweza kugawanywa katika sehemu mbili ambazo ni MAWAZO YALIYO WAZI au YALIYOJIFICHA. Mtaalamu wa masuala ya ndoto Daktari Gillian Holloway anaeleza kuwa ndoto hizi hufumbua maamuzi na hisia zilizojificha nyuma ya ubongo.

Pamoja na tendo hili kuwa baya katika mitazamo ya wengi hasa kiimani, lakini bado si kitaalamu halina ubaya kwa kiwango hicho kwani mara nyingine husaidia kutafsiri yale ambayo wahusika hawakupata kuyafahamu kabla. Kwa mfano vijana ambao hawajafanya mapenzi hupata kutambua raha itokanayo na kitendo hicho na hivyo kuwaamshia hisia za kimapenzi ambazo pengine hawakuwa nazo hapo awali.

Wachunguzi wa masuala ya ndoto wanasema ndoto hizi zikitumika vizuri zinaweza kusaidia kumpata mchumba anayegusa hisia za moyo, aina ya mapenzi yanayokufurahisha, haiba ya mpenzi umpendaye na wakati mwingine huchangia kuongeza uzalishaji wa homoni na kupunguza msongo wa mawazo sawa na mtu aliyefanya mapenzi laivu.

Hata hivyo watu wanaotajwa kutokewa na kitendo hicho mara kwa mara ni wenye tabia ya kuogopa wanaume/wanawake na hivyo kuzikandamiza hisia zao, pamoja na wale wanaochochea hamasa za kingono na kutokuzikata, (mfano kufanya romance na kuachana bila kuingiliana), wanaotazama picha za ngono, wanaozungumzia sana mambo ya kimapenzi na wale wanaowaza sana wapenzi wao walio mbali.

Kwa maana hiyo ili mtu asiweze kutokewa na ndoto hizo hana budi kujizuia na mambo hayo yanayotokana na uamshaji na ukandamizaji wa hisia za kingono. Hii ina maana ya utashi wa mtu wa kutopenda kuota, lakini si kwamantiki kuwa uotaji huu unauhusiano na mambo ya kishirikina au kichawi kama ambavyo watu wengine wanavyoaminishwa.

Mwisho kama kuna wanaodhani kuwa ndoto hizi zimewadhuru kwa namna moja au nyingine, wafahamu kuwa kilichowadhuru si kuota ndoto hizo bali ni wasiwasi wao unaotokana na kusikia na wala si madhara kwa maana ya kuota kwenyewe, kwani ikiwa ni ndoto hata wanyama kama Mbwa, Paka na Sungura nao huota wakifanya mapenzi, ushahidi ambao unatosha kutupilia mbali hoja ya ndoto kutokana na majini.

KWA WAPENDANAO: ZIFAHAMU SIFA 10 ZA WANAWAKE WANAOPENDWA ZAIDI NA WANAUME DUNIANI..!! JE WEWE MWANAMKE UNAZO..?? SOMA HAPA NIKUJUZE...

WENYE MSIMAMO

Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, walio makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio. 
WAPENDA USAWA
 Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50. 

WANAOJUA MAPENZI 
Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa kuwatosheleza wenzi wao katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani.

MARAFIKI 
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, ni waungwana na wapenda amani. 

WAPENDA UWAZI 
Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na wapenda uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo. 

WANAOJITEGEMEA  

Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina ‘naomba vocha’ kila siku. Uchunguzi unaonesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja. WASIO NA PRESHA Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi. 
 
MARIDADI 
 Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje lakini pia ni waelewa wa mazingira, si washamba. Wanapendeza kwa mwonekano. WANAORIDHIKA Wanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume. Hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.  

WA MMOJA  

Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo, wanahitajika sana. “Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana."


JE UNATAMBUA KUWA DAWA ZA HOSPITALI NDIZO ZINAGEUZWA KUWA DAWA ZA KULEVYA ..??


Matumizi ya dawa za kulevya nchini yamechukua sura mpya, baada ya kubainika kuwa watumiaji wengi wa dawa hizo aina ya heroin na cocaine sasa wanatumia dawa za hospitali zenye uwezo wa kulevya kuwa mbadala.
Matumizi hayo mabaya yamebainika kutokana na kuwapo ongezeko la matumizi ya dawa za hospitali zilizo na nguvu inayoelezwa kulingana na dawa za kulevya ikiwamo heroin, cocaine na amphetamine.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Uhalifu na Dawa za Kulevya (UNODC) ya mwaka 2013, inathibitisha ongezeko hilo la matumizi ya dawa hizo, ambazo kitaalamu zinaitwa ‘new psychoactive substances (NPS).
“Dawa mbadala za dawa za kulevya zimezua wasiwasi mkubwa siyo kwa sababu ya ongezeko la matumizi yake, bali hata ukosefu wa utafiti wa kisayansi na uelewa wa matumizi yake,” ilisema sehemu ya ripoti ya UNODC.

Katibu Mkuu UNODC, Yury Ferdotov alieleza katika ripoti hiyo ya hali ya dawa za kulevya mwaka 2013 kwamba, changamoto kubwa iliyopo katika kudhibiti dawa hizo duniani ni matumizi ya dawa za hospitali na kemikali zinazotumika kuzitengeneza kutumika kama dawa za kulevya.
Alisema nchi nyingi duniani hazina sheria wala uelewa kuhusu kemikali hizo, jambo linalosababisha wafanyabiashara wakubwa kuendelea kusafirisha kemikali hizo au kutumia teknolojia kulima mimea inayotumika kutengeneza dawa hizo.
UNODC limefafanua kuwa matumizi mabaya ya dawa hutokea wakati dawa za hospitali zinapotumika kwa malengo mengine kinyume na tiba.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa aina tisa ya dawa za hospitali ni miongoni mwa dawa zinzouzwa kwa njia ya panya kama mbadala wa heroin na cocaine.
Dawa hizo ni pamoja na mephedrone, ketamine, benzodiazepine, tramadol na dextromethorphan.
Nyingine ni piperazines, phencyclidines, trypitamines na aminoindance.
Uchunguzi huo umebainisha kwamba unaweza kuzipata dawa hizo kwa wafamasia wasio waaminifu katika hospitali kubwa ambapo huuzwa kwa bei nafuu na wakati mwingine katika maduka ya dawa muhimu.
Mwananchi Jumamosi lilipita katika baadhi ya maduka ya dawa na kufanikiwa kuzinunua dawa hizo zilizothibitishwa kutumika mbadala wa dawa za kulevya bila ya kuwa na cheti cha daktari.
Dawa zilizonunuliwa na gazeti hili ni pamoja na dawa aina ya Tramadol, morphene, phencyclidines na valium.
Pamoja na matumizi hayo pia, ilibainika kuwa dawa za kifua au za pumu ambazo zina kemikali aina ya codeine na zile zenye mchanganyiko wa dextromethorpen, pia zinatumiwa kama dawa za kulevya.
Pamoja na dawa hizo kutoruhusiwa kuuzwa bila cheti cha daktari, watu wengi wamekuwa wakizipata kwa urahisi na bei nafuu katika maduka ya dawa maeneo mbalimbali nchini hasa mijini.
Gazeti hili limebaini kuwa dozi moja ya dawa aina ya Tramadol inayotumika kutuliza maumivu lakini inatumika kama heroin, huuzwa katika maduka ya dawa bila cheti cha daktari na bei ndogo.
Kitaalamu dawa hiyo inaelezwa kumfanya mtu kupata kilevi kinachoweza kulingana na mtumiaji wa dawa za kulevya.
TFDA wazungumza
Msemaji wa Shirika la Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza alikiri dawa hizo kutumiwa vibaya na watumiaji wa dawa za kulevya jambo alilosema linakuzwa zaidi na ukosefu wa maadili.
“Kama wafamasia wanauza dawa hizo kwa siri basi watakuwa wanavunja ile Sheria ya Famasia ya Mwaka 2001 ya Dawa Muhimu,” alisema Simwanza.
Alisema TFDA inachunguza kwa umakini matumizi mabaya ya dawa hizo na endapo watabaini wafamasia wanaouza dawa hizo kinyume na taratibu, watachukuliwa hatua kali.
Hata hivyo, Simwanza alisema kuwa kuna changamoto kubwa katika usimamizi na udhibiti wa ununuzi wa dawa.
Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya
Mchambuzi wa Masuala ya Mifumo ya Kompyuta kutoka Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, January Nkisi naye alikiri kuwepo kwa dawa mpya za hospitali zinazotumika kama mbadala wa dawa za kulevya.
Nkisi aliongeza kuwa kutokana na kuwepo dawa hizo, tume hiyo kwa sasa inafanya kazi kwa ukaribu na TFDA, Ofisi ya Mkemia Mkuu na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha kuwa kemikali hizo zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya zinajulikana na hazipitishwi katika mipaka ya nchi.
Nkisi alisema kuwa tume hiyo inaendelea kufanya kazi kwa kasi katika kupata taarifa kutoka vyombo vya kimataifa ili kujua namna dawa za kulevya zinavyopitishwa, pamoja na mbinu mpya zinazotumiwa na wasafirishaji wa dawa za kulevya.
Akitoa mfano wa vilevi aina ya pombe, sigara na mirungi alisema kuwa vyote hivyo vina madhara na athari za muda mrefu kama zilivyo dawa za kulevya na kwamba sheria hazina budi kuundwa kwa kuangalia mifumo ya matumizi ya vilevi hivyo.
Naye Asia Gregory ambaye ni mfamasia kutoka duka la dawa baridi Buguruni alisema kuwa mtu anayetumia dawa kama ketamine, tramadol na kundi la dawa aina ya benzodiazepine hupata matokeo sawa na anayetumia heroin au cocaine.
“Hata mtu wa kawaida akitumia dawa hizi kwa muda mrefu huanza kumfanya awe tegemezi. Akizikosa hupata athari kama kuwashwa, mate kumdondoka, kupata hali kama ya degedege, kutetemeka, kutokwa jasho jingi na ili aondokane na hali hiyo, basi huhitaji dawa hizo tu,” alisema.
Gregory alitoa mfano wa dawa aina ya morphene ambazo ni za maumivu makali akisema zina uwezo wa kulevya sawa na heroin.
Alizitaja pia dawa za usingizi aina ya ketamine ambazo hutumika katika upasuaji kuwa nazo hutumiwa na waathirika wa dawa za kulevya.
Alitoa angalizo kuwa hata wagonjwa ambao hawakuwa na nia ya kutumia dawa hizo kama mbadala wa dawa za kulevya huathirika, hivyo lazima utafiti wa kina ufanyike.
Utafiti uliofanywa Tanzania
Utafiti uliofanywa na Erasmus Mndeme wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), kuhusu matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana mkoani humo ulibaini kuwa, vijana wengi wanatumia dawa aina ya benzodiazep kuwa mbadala wa dawa za kulevya.
Utafiti mwingine uliochapishwa mwaka huu ulibaini kuwa, dawa mbadala wa dawa za kulevya zinazotumiwa zaidi ni zile dawa zenye codeine.
Dawa hizo hutumiwa na vijana kwa asilimia 59.6, huku valium na morphine zikitumika kwa asilimia 1.8 huku mbadala mwingine unaotumiwa na vijana ukitajwa kuwa ni glue na petroli.
Aidha, utafiti huo ulibaini kwamba vijana wengi wameanza kutumia dawa mbadala wa dawa za kulevya wakiwa na umri wa kuanzia miaka 12.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili na mtaalamu wa waathirika wa Dawa za Kulevya, Augustine Godman, alithibitisha kuwa watu wengi wamegundua matumizi ya dawa za hospitali kama dawa za kulevya.
Alisema kuwa chanzo kikubwa cha hali hiyo ni uuzaji holela wa dawa hizo katika maduka ya dawa.
“Sheria zingekuwa zinafuatwa vijana wasingeharibika kiasi hiki. Sasa wanauziwa dawa hizo katika maduka ya dawa bila kuhojiwa chochote,” alisema.
Dk Godman alisema kuwa amekuwa akitibu vijana wengi walioathirika kwa dawa za kulevya katika kliniki yake, chanzo kikubwa kikiwa ni dawa za kulevya ambazo ndani yake kuna chembechembe ya dawa aina ya benzodiazepine na morphine.
“Unajua watu wanadhani dawa za kulevya ni heroin na cocaine pekee, lakini vijana wanavuta petroli, gundi, dawa za maumivu na za kifua ambazo zina codeine, vyote hivi vinaathiri,” alisema.
Aliongeza kuwa ulevi wa aina yoyote ni sawa na dawa za kulevya ikiwemo bangi, mirungi na mimea yoyote inayolevya.
“Hili ni janga. Unawaacha watu wanaathirika kwa kutumia Sh2,000 au 3,000, lakini unapata kazi ya kuwatibu ya zaidi ya Sh100 milioni,”alisema akisikitika Dk Godman.
Mfamasia Charles Lymo wa Hospitali ya Amana wilayani Ilala alisema kuwa mtu anapokunywa dawa ya benzodiazep hujisikia hali ya raha na maisha mazuri.
“Mtu anaweza kujisikia ana mali nyingi, amani humwingia moyoni, yaani anapata faraja ya kina na anasinzia,” alieleza Lymo.
Alisema kuwa dawa nyingine ambazo huweza kufanya kazi kama mbadala wa dawa za kulevya ni amephetamine na phenobabiton.
Joshua Joseph (siyo jina halisi), ambaye ni mwathirika wa dawa za kulevya, mkazi wa Tabata Dar es Salaam alisema kuwa anapokosa cocaine, hununua dawa aina ya tramadol na kuchanganya na valium, kisha kuzisaga na kuvuta kama wanavyovuta dawa nyingine za kulevya.
“Unakuwa ‘high’ kama kawaida lakini tunazitumia zaidi kama tumekosa unga wa kawaida,”alisema.
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Imeeleza kuwa idadi kubwa ya watu wanaougua maradhi ya akili wanaofika katika hospitali hiyo huonyesha historia ya kutibiwa kimakosa au kutumia dawa aina ya benzodiazepine kabla ya kupelekwa hospitali.


Je, ni sahihi kufanya mapenzi wakati mkeo akiwa na MIMBA?. Je, mimba yaweza kutoka? Vipi kuhusu afya ya mtoto tumboni..!! BOFYA HAPA KUFAHAMU ZAIDI..

  
Ni kawaida kwa mwanaadamu aliye mzima kupenda kuwa na mtoto, na kwa namna ya upekee katika kuumbwa kwa mwanaadamu, hakuna njia nyingine yoyote ile ambako mtoto anaweza kupatikana bila ya maingiliano ya kimwili baina ya watu wa jinsia mbili tofauti (ukiachilia mbali instances chache ambapo mambo ya test tube na artificial insemination hutumika).
Kifupi ni kwamba, kama mwanamke atataka kubeba ujauzito ni lazima akubali kuingiliwa, Vivyo  hivyo kama mwanaume anataka kumbebesha mwenza wake ujauzito ni lazima ahakikishe kuwa amemwiligilia mke  

Hata hivyo, licha ya ukweli wa kuwa ili ujauzito upatikane ni lazima kuwe na kufanya mapenzi, kumekuwa na mkanganyiko sana juu ya tendo hili la kufanya mapenzi au kutiana kama wengine wanavyosema, pindi inapotokea mwanamke ameshashika ujauzito.

Je, ni sahihi kufanya mapenzi wakati mwanamke wako ni mjamzito?

Je, ni hadi muda gani kabla ya kujifungua, ambapo mwanamke mjamzito anaweza kuwa anaingiliwa kimwili na mwenza wake? 


Kwa maswali haya na mengine kadhaa, hebu twende pamoja mdogo mdogo kama ifuatavyo:- 

(1).  Je, ni sahihi kufanya mapenzi ikiwa mwanamke wako ni mjamzito?

Ndio, hakuna tatizo lolote kwa mwanamke kuendelea kufurahia mapenzi na mumewe au mpenzi wake wakati anapokuwa mjamzito.  
 

 Wataalamu wanaeleza kuwa, ikiwa ujauzito ulioubeba haukupi shida yoyote ile na unajisikia uko poa, basi hakuna hatari yoyote ile ikiwa utataka kufanya. 
 

Tatizo pekee ambalo huwa linawakumba wengi wa wanawake wakiwa wajawazito ni kuwa, huwa wanapoteza hamu ya tendo lenyewe wanapokuwa katika hali hii, au kushindwa kumudu kutokana na kujisikia uchovu muda mwingi. 

Ingawa pia wapo wanawake ambao wakiwa katika hali hii ndio kwanza, wanakuwa wanajisikia kukereketwa huko kwenye ki**i kupita maelezo, na wanatamani muda wote wafanye mapenzi. 

Wapo baadhi ya wanawake ambao wanakuwa wako normal kimwili, lakini kisaikolojia wanakuwa na ile hofu ya kuwa kufanya kunaweza kuwaharibia mimba zao, fikra ambazo huwatoa kabisa katika mstari wa kufurahia tendo hili.  


Kwa hiyo, ikiwa mwili wako uko poa, na madaktari wamekwambia kiumbe kinakua bila shaka, na unaweza kwenda kazini, huna haja ya kujibania utamu wa mumeo au kumbania mumeo.  

(2). Je, kufanya wakati wa ujauzito kunaweza kusababisha ujauzito kuharibika?

Hili pia ni miongoni mwa maswali na hali ambazo zimekuwa zikiwachanganya watu wengi, waume kwa wanawake.  
Ila ukweli ni kwamba, kufanya hakuhusiani na kuharibika kwa mimba au kujifungua kabla ya wakati muafaka. 

 Kwa kawaida, kuharibika kwa mimba hutokana na sababu zingine tofauti kabisa, ikiwa ni pamoja na kizazi cha mwanamke kuwa na matatizo hasa katika kuhimili ukuaji wa kiumbe tumboni na sababu zingine za kimazingira. 
 

Wala sio kwa sababu ya kitu ambacho unakifanya au hukifanyi.


(3). Je, kufanya wakati wa ujauzito kunaharibu au kumdhuru mtoto?

Kiumbe kilicho tumboni wakati wa ujauzito huwa kinakingwa na ute maalum unaojulikana kitaalamu kwa jina la "amniotic fluid" ndani ya mji wa uzazi, pamoja na kuta za mji wenyewe wa uzazi. 

Hakuna namna ambavyo muhogo unaweza kupita na kufika mahali mtoto anapokuwa anakua huko ndani, au zile mbegu kuwa zitapita moja kwa moja na kwenda kumdhuru mtoto. 

 Kumekuwa na ule msemo wa kuwa kufanya wakati wa ujauzito ni kulea mimba, watu wakiamini kuwa mbegu huwa zinakwenda moja kwa moja kwenye kiumbe.
 

 Dhana hii ni potofu. Kama kilivyo chakula cha kawaida mtu anapokula, ndivyo ambavyo mbegu nazo huwa hivyo.
 
Kila kitu kwanza lazima kiingie katika mfumo wa kawaida wa usafirishaji wa virutubisho vilivyo sahihi kuelekea kwenye kiumbe husika. 

 Hii ikimaanisha kuwa mbegu nazo huingia katika mfumo huo huo, huchujwa na kile kinachoonekana kuwa ni kirutubisho kitasafirishwa kwenda kulea kiumbe, ilhali yale makapi lazima yatatoka.
 

 Tofauti pekee hapa ni kuwa, "mbegu  za kiume  zina protini  nyingi", hii ikimaanisha kuwa sehemu kubwa ya kile kinachomwagwa kwenye uke wa mjamzito, kina nafasi ya kutumika kwa ajili ya kuongeza rutuba kwa kiumbe kinachokuaa ndani ya tumbo.
 

 Na nyingine zinaweza kutoka tu zenyewe bila matatizo yo yote.


(4). Ni mikao ipi (staili) ambayo ni mizuri zaidi kuitumia kufanya wakati wa ujauzito?

Hakuna mkao maalum. Ujauzito sio ulemavu kwamba mnalazimika kujipanga upya namna ya kuridhishana, wala sio ugonjwa pia. 

 Ikiwa mwanamke unajihisi uko fresh kuendelea kutumia staili ya mwanzo ambayo mlikuwa mnaitumia na unafikishwa na mwenzio, huku huyo mwenzio naye akiwa yuko ok kuitumia staili hiyo na anaimudu hata unapokuwa na tumbo lako, hakuna  shida
 

 Jichumishe mboga, jifanye mbuzi ulogoma kwenda, jifanye namna yoyote ile unayoona uko poa, na mambo yatakuwa vizuri.
 

(5). Vipi kuhusu kitu ule mtandao wetu na or*l s*x? (chumvi)

Or*l s*x ni salama kabisa wakati wa ujauzito. Hata hivyo, ni muhimu kuepuka hewa kuingia ndani ya uke wako wakati ukiwa katika hali hii.  

Wapo wale watu watundu ambao hugeuza uke kama pulizo na kujitia umahiri wa kutaka kulijaza hewa wakati wa kupeana raha.  

Katika mazingira ya kawaida, ikiwa mnafurahia hili, hakuna tatizo, ila wakati wa ujauzito, hii ni hatari kwani inaweza kuleta madhara katika mishipa fulani ndani ya uke, ambayo iko na uhusiano na mishipa ya kuelekea kwenye mji wa uzazi. 

Kuhusu ule mtandao wa  vijana (Tigo), ambao kwa kawaida hauruhusiwi kutumika, hakuna wakati unaokuwa mbaya zaidi kuutumia kama wakati huu wa ujauzito. 

 Katika wakati huu, uke wa mwanamke mara nyingi unakuwa sensitive zaidi ya wakati akiwa hana ujauzito, na kuendekeza kuf**ana, kunaongeza hatari ya bakteria kuhamia kwenye uke na kusababisha magonjwa ambayo yatadhuru kiumbe kilichobebwa ndani.
 

(6). Kuna umuhimu wa kutumia kondomu?
Kama nilivyodokeza hapo awali, wakati wa ujauzito uchi wa mwanamke unakuwa sensitive zaidi kwa magonjwa. 
 Unaweza tu kuguswa na mwenzako ambaye hakuwa amenawa mikono uzuri na ikakusababishia tatizo fulani, hivyo basi, inashauriwa kutumia kondomu ikiwa:
  • mwenza wako aliwahi au ana maradhi ya maambukizi
  • uko kwenye mahusiano na zaidi ya mtu mmoja
  • umeamua kungonoka na king'asti kipya wakati wa ujauzito

(7). Je, kukojoa au ku-squi*t mara kwa mara kunaweza haribu mimba?
Hapana. Licha ya ukweli kuwa wakati wa ujauzito uke huzalisha kemikali ambazo ni mahususi kwa ajili ya kumkinga mjamzito na uvamizi wa bakteria wowote wanaoweza kuwa tishio kwa ujauzito wake, na kwamba kemikali hizi wakati mwingine huweza kuhitilafiana na lile bao analopiga mwanamke na hivyo kumletea hali fulani ya kukwaza, kwa ujumla wake hakuna baya linaloweza kusababishwa na kukojoa au kufika kileleni . 

Na wala kufanyana hakuwezi kuathiri kwa namna yoyote ile muda wako wa kujifungua (kuuchelewesha au kuuwahisha)
  

(8). Je, ni wakati gani mwanamke mjamzito anatakiwa kuacha kufanya mapenzi?
Ijapokuwa wapo wanawake wengi ambao wanaweza kabisa kuendelea kufurahia kufanywa hadi siku wanakwenda kujifungua , kuna baadhi ya nyakati mshauri wako wa afya anaweza kukushauri kuacha ngono kutokana na moja au yote kati ya yafuatayo:
  • umekuwa na tatizo la kujifungua kabla ya muda muafaka kabla ya ujauzito ulio nao
  • umetokewa na tatizo la kutokwa na damu kwenye uke
  • umekuwa ukitokwa na ute fulani ambao wataalamu wanauita kwa jina la "amniotic fluid"
  • umekuwa na tatizo la kwenye mlango wa uzazi, ambalo kitaalamu linajulikana kama cervical incompetence
  • kondo la nyuma limesambaa na kuziba kabisa mlango wa uzazi na kuanza kujitokeza kwa nje (placenta previa)

(9). Je, kuna tatizo lolote ikiwa huhitaji kufanya?
Hapana, na hii ni hali ya kawaida sana kwa baadhi ya wanawake wanapokuwa wajawazito, ama kutokana na hofu inayokuwa vichwani mwao kuwa atapata madhara kwa kufanya hivyo, au kutokana tu na aina ya homoni zinazozalishwa mwilini wakati huo.  
 
Kuna mengi mnaweza kufanya bila kuhusisha maingiliano ya kimwili na ambayo yanaweza kumfanya mwanamke kuridhika anapokuwa katika hali hiyo.
  

(10). Ni baada ya muda gani toka kujifungua mwanamke anaweza kuendelea kufanya mapenzi?
Iwe kwa njia ya upasuaji au kwa njia ya kawaida, inaeleweka wazi kuwa baada ya kujifungua, mwanamke anakuwa na hali fulani ya mwili kuchoka, hali ambayo ni ya kawaida. 

 Ingawa wapo ambao wanaweza kujihisi wanamudu kushiriki tendo la ndoa kabla, lakini wataalamu wanashauri kuwa wakati mzuri wa kurejea kufanyana na mwenzio baada ya kujifungua, inakuwa ni baada ya kupita wiki sita.

UTAFITI: HAYA NDIO MADHARA YA UVUTAJI WA SIGARA...


MADHARA YA UVUTAJI WA SIGARA
Katika moshi wa sigara, zaidi ya kemikali 400
zimegundulika kuwa na madhara makubwa
katika afya. Mvutaji mdogo hutumia nusu ya
pakiti ya sigara kwa siku na kujikuta akiathiri
mwili wake kwa kemikali hizi mara 3500 kwa
mwaka. Hata hivyo,

VITU VITATU HATARI ZAIDI
KATIKA SIGARA NI:

1. Tar: hiki ni kisababisha kansa katika mwili.

2. Nicotine: Hiki ni kitu chenye sumu ambacho
kwa muda mrefu san akimetumiwa kama
dawa ya kuuwa wadudu na sumu ya panya.
Inachukua nafasi ya pili kama sumu kali
kabisa kwa athari yake mbaya katika mwili
wa binadamu.

3. Carbonmonoxide: Hii ni gesi
inayopatikana katika moshi wa sigara.
Madhara mbalimbali ya vitu vinayopatikana
katika moshi wa sigara ni kama yafuatayo:
1. Kuharibika kwa utando mlaini katika njia za
hewa: katika njia ambayo pumzi hupita kuna
kama tabaka fulani ambalo ni laini
limezunguka katika njia.
 Tabaka hili hufanyakazi ya kuzuia vumbi vumbi linaloingia
pamoja na hewa. Ile tabia ya uvutaji hufanya
vile vitu vinavyopatikana katika moshi wa
sigara kuganda katika utando huu na
kusababisha njia kuwa nyembamba kwa kule
kuongezeka kwa takataka na kemikali katika
njia, hivyo kumfanya mvutaji apate shida ya
pumzi hapo baadaye.

2. Vidonda vya tumbo: uvutaji wa sigara
huchochea utengenezaji wa acid ambayo
huweza kumletea mvutaji huyo vidonda vya
tumbo.

3. Matatizo katika mfumo wa upumuaji:
wavutaji hupata shida katika koo na mapafu
hivyo kupata kifua mara kwa mara na
maumivu na mwishowe kupata madhara
makubwa katika mfumo mzima wa upumuaji
kutokana na kuharibika kwa mapafu kama
tutakavyozungumzia katika pointi namba 7
hapo chini. Hali ya hewa huwaathiri sana
wavutaji sigara kwani hupata pneumonia na
asthma.

4. Udhaifu katika mifupa (Osteoporosis):
katika moshi kuna metali ijulikanayo kama
cadmium ambayo inaweza kusababisha
matatizo katika mifupa, hii husababisha
kupoteza asilimia 30 ya calcium katika mifupa.
Kwa wanawake uvutaji wa sigara
umeonekana kuzuia shughuli ya estrogen na
kitu chochote kinachozuia estrogen kufanya
kazi husababisha udhaifu katika mifupa
(Osteoporosis) na hii huweza kusababisha
maumivu ya mara kwa mara katika mifupa.

5. Kuwahi kumaliza kufikia mzunguko wa
mwezi (Menopause): Menopause ni ile hali ya
mwanamke kufikia mwisho wa mzunguko
wake wa kila mwezi ambao humpelekea
kushika ujauzito, hali hii huanza kutokea
akifikia umri wa miaka 45 – 55, hutofautiana.
wanawake wanaovuta sigara hufikia
menopause miaka mitano mapema zaidi ya
wasiovuta.

6. Athari kwa wenye mimba: wanawake
wanaovuta sigara huwa katika hatari kubwa
sana ya mtoto kutoka kabla ya siku zake
(Abortion) au kuua mtoto tumboni. Au hata
mtoto kufa mapema zaidi pindi
atakapozaliwa.

7. Kuharibika kwa Alveoli za mapafu
(Emphysema): ile harufu kali ya moshi
huharibu alveoli ndogo ndogo katika mapafu.
Hii kwa kiasi kikubwa sana hupunguza eneo
ambalo Oxygen hukutana na damu na hivyo
kusababisha hali inayoitwa Emphysema. Hali
hii hujitengeneza taratibu sana na kimya kwa
muda mrefu.
Wavutaji wote wana
Emphysema kwa kiwango fulani Lakini
kutokana na eneo kubwa wanaloishi ambalo
hupatikana Oxygen, watu wengi hawajui
kwamba wana hali hii. (watu wengi wana
takriban alveoli milioni 300 katika mapafu
yao) hivyo ni vigumu kugundua hali hii na
baadhi hujijua pale wanapofanya mazoezi
kwa mfano, na kuhisi ugumu wa pumzi.

8. Upungufu wa uwezo wa kubeba oxygen
katika damu: Carbon Monoxide (CO)
inapatikana katika moshi. Uhusiano wa
Carbon Monoxide kwa Haemoglobin ni
mkubwa mara 200 zaidi ya Oxygen. Hivyo
baadhi ya haemoglobin ya damu huzuiwa na
Carbon Monoxide kwa wavutaji kwani
haemoglobin badala ya kuchukua Oxygen
huenda katika Carbon Monoxide na hivyo
uwezo wa kubeba oxygen katika damu
hupungua.

9. Kansa/ Saratani: Katika asilimia kubwa ya
watu wenye kansa hupatikana kutoka kwa
wavutaji wa sigara, saratani za ngozi, koo,
utumbo, kibofu, mdomo n.k. vilevile saratani
ya figo, kongosho, tumbo na kizazi
imeonekana mara chache kwa wavutaji wa
sigara.

10.Kupungukiwa na vitamin: Uvutaji wa
sigara husababisha upungukiwaji wa Vitamin
hasahasa Vitamin C. ule uvutaji wa sigara
moja tu unaweza kupunguza kiasi cha
Vitamin C ambacho kinaweza kulingana na
ukubwa wa kutumia chungwa moja tu. Hivyo
inashauriwa kula sana Vitamin C ili
kurekebisha hali hii.

11. Uvutaji wa sigara unaweza kusababisha
kisukari: Nicotine huchochea sukari katika
damu kwa kuilazimisha au kuichochea
Adrenaline na Non Adrenaline ambayo
hufanya ini na misuli kupeleka sukari katika
mishipa ya damu. Hii hufanya kongosho
ifanye kazi ya kutoa Insuli mara kwa mara ili
kudhibiti sukari kama kawaida yake na
kutokana na kufanya kazi huku mara kwa
mara hufanya kongosho ichoke haraka na
kushindwa tena kudhibiti sukari, hivyo
humsababishia mtu huyu kisukari.
Kwa upande wangu hizo ndizo athari
zinazotokana na uvutaji wa sigara, hivyo basi
jaribu kulinganisha yale manufaa ya muda
mfupi anayoyapata mvutaji na hasara zake.
Hapo utaona kwamba uvutaji wa sigara ni
hatari sana kwa afya yako, na ni bora ujitahidi
sana uache ili kuboresha afya yako

JE UNA TATIZO LA KUTOKWA NA CHUNUSI USONI...?? SOMA HAPA KUPATA SULUHISHO LA TATIZO LAKO...

Tatizo la kutokwa na chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hushambulia sehemu za usoni  na kuharibu sura ya mwanadamu hasa wanawake.

Ugonjwa huu umekuwa ukiwachukiza baadhi ya wanawake na wanaume kutokana na kuharibika kwa uso wao na matokeo yake kujikuta wakienda kununua vipodozi  vyenye kemikali kali ambazo ni hatari kwa afya ya ngozi zao.

Vipodozi hivyo ni hatari kwani vingine huweza kuchubua na kusababisha ngozi kukosa kinga,hivyo kuleta madhara  makubwa mwilini.
  
Chunusi huwatoka na kuwasumbua watu wengi hasa vijana wenye umri wa kubalehe  lakini pia hushambulia hata watu wazima.

Ukitokwa na chunusi maana yake una mchanganyiko wa magonjwa tofauti ya ngozi sehemu za usoni kwani vipele vidogo vinavyotoka husababisha maumivu na muwasho kwa muathirika.
Vipele hivyo baadaye hutunga usaha na kuwa chunusi ngumu.

Kitaalamu  ili mtu awe na chunusi kuna vijidudu hushambulia vitezi vya ngozi ya uso vijulikanavyo kwa jina la Pilosebaceous na Sebaceous gland.

 Tezi hizi hutoa mafuta mengi usoni na yakizidi huwa chakula cha vijidudu (bacteria)wanaokaa kwenye ngozi na kusababisha uingiaji wa vidudu hivyo kwenye hizo tezi  na kusababisha chunusi.

Chunusi hutokea baada ya tezi za Pilosebaceous kuziba (obstruction), huzibwa na mgando wa mafuta ya usoni na kusababisha wadudu kuingia kwenye tezi za usoni ambapo wadudu hao hushambulia ngozi ya usoni. 





Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria.


  Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris.Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni kumi na sa-ba..

Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wa-kati wa balehe (adolescents) .
  Karibu asilimia 85 ya vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi 25 hupata chunusi na zaidi ya asilimia 20 ya wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka ishirini hupata chunusi wakati mwingine hata watoto wadogo pia huweza kupata chunusi hii ni tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuwa chunusi ni dalili ya balehe.
  Chunusi ni ugonjwa unaoathiri vifuko au glandi za ngozi.Katika ngozi ya binadamu kuna glandi ziitwazo Sebaceous ambazo zipo chini ya ngozi na kazi yake kubwa ni kutoa mafutamafuta yaitwayo Sebum ambayo hu-saidia kuiweka ngozi kuwa nyevu na yenye mvuto. 
Wakati wa balehe mwili wa binadamu hutoa Sebum kwa wingi na kwa sababu wakati huu vikemikali vya mwili yaani sex hormones hutolewa kwa wingi hasa hormone ya kiume iitwayo androgen husababisha utoaji wa sebum kuwa mwingi zaidi kuliko kawaida. Sebum inapotolewa kwa wingi huungana na seli za ngozi zilizo-kufa na kutengeneza mchanganyiko mzito kama nta uitwao comedo ambao huziba vishimo vya kutolea joto.   
   Maambukizi zaidi hutokea pale ambapo vijidudu yaani baktaria vinaposhambulia vishimo vilivyoziba hapo kivimbe ambacho watu wengine huita Pimple hujitokeza pale ambapo Sebum, bacteria, seli za ngozi na seli nyeupe za damu zinapo-changanyika na kujikusanya katika vishimo vya jasho vilivyoziba na eneo husika hupata vivimbe au vipele ambavyo tunaviita chunusi.
 
  Ukubwa wa kipele hutegemea ngozi ya mtu au kiasi cha mchanganyiko nilioeleza hapo juu katika eneo husika.Vipele vinaweza kuwa vidogo au vikubwa. Chunusi wakati mwingine husababisha mabaka katika ngozi hali hii hutokea pale ambapo seli za ngozi zilizoharibika huondolewa na seli mpya kutengenezwa.
  Ngozi mpya hutengenezwa kirahisi tu mahali palipokuwa na chunusi hali hii husababisha mlingano usiosahihi wa ngozi na hutoa kidonda ambacho baadaye hubaki kama baka. Chunusi hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega na mgongoni kwa sababu maeneo hayo yana vifuko au glandi za Sebaceous nyingi.
CHANZO CHA CHUNUSI
Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo baadhi ya vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;
1.    UMRI – Kama nilivyosema hor-mone/vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa kubale-he.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa nta (sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
2.  VIPODOZI –Baadhi ya vipodozi kama Make-up za kina dada na Sprays za ny-wele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.
3.  CHAKULA- Chunusi hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufan-ya chunusi kuwa nyingi zaidi.
4.  DAWA-Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,steroids na tranquilizers.Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na ma-kusudio ili kuongeza unene wa misuli yao.
5.  MAGONJWA- Magonjwa yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana.
6.  MAZINGIRA- Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye mafuta,grisi au hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa katika mazingira ya joto huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.
7.  JINSIA-Wavulana hupata sana chunusi kuliko wasichana.
8.  FAMILIA- Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana kwa wanafamilia wa familia kadhaa kuliko nyingine.
9.  HOMONI- Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au mwanamke anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata chunusi.
10.               USAFI WA MWILI- Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au vipele hu-sababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwi-lini au kutooga huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi
11. MAWAZO AU STRESS-Mtu anapokuwa na mawazo mengi vimkemikali kadha hutolewa mwilini ambavyo huwe-za kuchangia au kusababisha chunusi
DALILI ZA CHUNUSI
Vipele au vivimbe vidogo vidogo ambavyo pengine husababisha mwasho au vinavyouma ni dalili ya chunusi.

Wakati mwingine huweza kujitokeza kama baka dogo na wakati mwingine mtu anaweza utambuzi wa chunusi unaweza kuwa mgumu kutokana na watu walivyomakini au wanavyojenga wasiwasi kubwa katika mwonekano wao hasa usoni.Ikumbukwe kuwa kutokana mwonekano wa chunusi ni rahisi sana
 
Daktari kuzigundua, japokuwa katika familia zetu ni mara chache sana mtu akaenda kumwona daktari au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa sababu ya chunusi.

Pale inavyotokea hivyo basi hali inakuwa ni mbaya zaidi.Hata hivyo si vibaya kumwona daktari ambaye atakuuliza kuhusu chakula, ngozi, dawa unazotumia na vitu vingine vinavyowe-za.kuchangia mtu kupata chunusi
MATIBABU
Matibabu ya chunusi yanajumuisha kupunguza utoaji wa anta (sebamu ), kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani bacteria.
Matibabu huweza kutofautiana kutokana na wingia au ukubwa wa tatizo. Suala la kuzingatia ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha chunusi kama nilivyoeleza hapo juu.
DAWA ZA KUPAKA
Kuna dawa za kupaka ambazo hupaka katika eneo la ngozi lililoathirika kwa chunusi. Dawa hizi hupatikana kama cream,lotion,gel au pad. 
Dawa hizi hutumika kutibu chunusi ambazo haziko katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo tu. 

Mojawapo ya dawa hizi ni antibi-otic kama zenye mchanganyiko wa gentamyicin na betamethasone au dexame-thasone kama vile Gentrisone au Gentriderm cream,Erythromycin,B-Tex na kadhalika.Pia Persol forte Gel husaidia hasa ukianza na asilimia ndogo (2.5%) na kuen-delea kadri ngozi yako inavyohimili dawa. 

Gentamycin huua wadudu wanaosababisha chunusi wakati dawa nyingine huondoa mwasho.
Dawa nyingine ni zile zinzolainisha nta au Comedolytics na kufanya vishimo vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza kasi ya utengenezwaji wa seli mpya za ngozi
Dawa hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara mbili au tatu kila siku hasa baada ya kusafisha kwa maji safi na sabuni ya kawaida na kukausha kwa taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua wiki kadhaa.
DAWAZA KUMEZA
Wakati mwingine daktari anaweza kumshauri mgonjwa kutumia dawa za kumeza kulingana na wingi au ukubwa wa tatizo.
Dawa kama antibiotics huua wadudu na huzuia chunusi ,dawa hizo ni kama vile Erythromycin topical, Accutane (isotret-inoin), Benzamycin Cleocin T (clindamycin phosphate), Desquam-E (benzoyl peroxide) Minocin (minocycline hydrochloride) na
”Si vema kujinunulia mwenyewe tu na kuanza kutumia bila ushauri wa daktari au mtaal-amu wa magonjwa ya ngozi.”
Wanawake wenye chunusi zisizotibika wanaweza kupewa Anti-androgens kama vile baadhi ya vidonge wa uzazi wa mpango.Chunusi sugu hutibiwa kwa ciorticosteroids na anti-iflammatory drugs ambazo hutibu chunusi sugu ambazo huitwa Acne fulminans na hupatikana zaidi kwa vijana.
MATIBABU MENGINE
Kwa nchi zilizoendelea matibabu yanaweza kuwa hata upasuaji mdogo (skin grafting) au plastic surgery kama chunusi imesaba-bisha baka kubwa na kuna njia kama vile Chemical peel ambapo kemikali hupakwa kwenye ngozi na inapokauka kipande au gamba la juu la ngozi huondolewa na kuondoa baka.
MATIBABU MBADALA
Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu nakuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.
Watu wenye chunusi wanashauriwa kulAa mlo kamili wenye vyakula vyenye madini ya zinki,nyuzinyuzi, matunda, mboga za ma-jani,vitamin B complex na Chromium.

 Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya maziwa, tumbaku, sukari, vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi
MUHIMU
Chunusi haziwezi kutibika kabisa japokuwa iwapo matibabu Yatakuwa sahihi watu 60 kati ya 100 hupona na unapokuwa unatumia dawa usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi miwili kupata nafuu na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia dawa.

Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha mabaka ambayo kwa hapa nchini hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali huweza kuondoka kadri muda unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na madhara katika ngozi.
MAMBO YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI
Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;
1.    Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu choichote kigumu.
2.  Tumia make-up au vilainisha ngozi visivyo na mafuta mgando
3.  Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)
4.  Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.
5.  Usibinye au kutoboa vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.
6.  Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D
7.  Punguza mawazo
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger