Showing posts with label UNYAMA. Show all posts
Showing posts with label UNYAMA. Show all posts

UNYAMA:Mwanamke abakwa na kuchomekwa chupa za soda katika sehemu zake za siri na kisha kunyongwa huko Chalinze

 
 Mwanamke mkazi wa Chalinze, Mkoa wa Pwani, Moshi Rashid (43) amefanyiwa unyama uliopitiliza na watu wasiojulikana baada ya kumbaka na kumnyonga...
 
Tukio hilo la kutisha lilijiri usiku wa Desemba 7, mwaka huu Chalinze Kwamwarabu ambapo mwanamke huyo alikwenda kujumuika na ndugu na majirani katika mkesha wa ngoma ya kuwatoa wari siku ya Jumapili.
                                                    
Mkasa huu unasimuliwa kwa majonzi mazito na mdogo wa marehemu ambaye alikuwa mshehereshaji wa shughuli hiyo ‘MC’, Siwema Rashid.
 
Alisema: “Mpaka sasa tunashindwa kuelewa kilichotokea maana siku ya tukio tulikuwa naye kwenye ngoma usiku. Alikuwa mchangamfu sana, aliifanya shughuli ipendeze.
 
“Ilipofika saa nane usiku baadhi ya watu walianza kulala, sasa sijui yeye ilikuwaje mpaka hali hiyo ikamfika maana hao watu walichomfanyia wametuachia historia kubwa sana.

 
“Walimbaka wakaona haitoshi wakamwingiza chupa ya soda sehemu ya siri ya mbele halafu wakamwingiza chupa ya bia sehemu ya siri ya nyuma.
 
“Ili kuzidi kutimiza unyama wao, waliondoka na kumwacha kama alivyozaliwa, inauma sana halafu matukio ya hivyo yamekithiri sana.”
 
Aliongeza: “Marehemu ametuachia jukumu la malezi kwa watoto wake wawili, Sikudhani Juma (18) na Ally Juma (12).”
 
Naye mtoto mkubwa wa marehemu, Sikudhani akisimulia kifo cha mama yake, alisema: “Nasikitika sikuweza kuuona mwili wa mama hata pale watu walipojazana na kumshangaa.
 
“Hata polisi na mganga mkuu wa mkoa walipofika kumchomoa zile chupa sikutaka kusogea kabisa, naamini Mungu atawaonesha jambo hao watu hapahapa duniani.”
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Yurichi Mtei akizungumzia ukatili huo alisema: “Taarifa za tukio hilo bado hazijafika kwangu kutokana na majukumu mengine ya kikazi, isipokuwa nalifanyia kazi kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa.”
 
Tukio hilo lilifunguliwa jalada kwenye Kituo cha Polisi Chalinze kwa namba CH/RB/3767/2013 MAUAJI.
 
Mpaka kifo chake, mwanamke huyo alikuwa akiishi na mwanaume mmoja (jina halikupatikana mara moja lakini si aliyezaa naye watoto hao wawili). Alizikwa Jumapili iliyofuata, Chalinze.
  
 Source: Gpl

UNYAMA ...!! Tazama Video ya mabinti waliovuliwa nguo na kuchomekwa vijiti wakituhumiwa kumtapeli mfanyabiashara milioni 5


 
Mabinti  wawili   pamoja  na  mwanaume  mmoja  raia  wa  Nigeria wamejikuta  wakidhalilishwa  mbele  ya  umati  wa  watu  baada  ya  kuvuliwa  nguo   na  wanakijiji  wakituhumiwa  kumtapeli  mfanyabiashara  milioni 5...
Mbali  na kuvuliwa  nguo, watuhumiwa  hali  pia  walidhalilishwa  kwa  kuchomekwa  vijiti  sehemu  zao  za  siri huku  wakipewa  kichapo  kikali...
Tukio  zima  liko  hapo  chini....Bofya  ujionee  unyama  wa  binadamu

Tukio  zima  liko  hapo  juu...Bofya  ujionee unyama  wa  binadamu


UKATILI...! MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AUAWA KINYAMA NA KUTOBOLEWA JICHO MOJA HUKO TARIME..!!


MWALIMU wa shule ya msingi Nyarero katika tarafa ya Inchage wilayani Tarime mkoani Mara, Joshua Makuri (34), amekutwa amekufa na mwili wake kutelekezwa katika maeneo ya uwanja wa shule ya msingi Turwa Tarime.
Katibu tarafa ya Inchage, Jonathan Machango, alisema jana kuwa mwili wa marehemu uligundulika mwishoni mwa wiki iliyopita na watu waliokuwa wakipita karibu na maeneo ya viwanja vya shule ya msingi Turwa.
Mwili huo kwa mujibu wa Machango, ulikutwa na majeraha ambapo jicho moja lilikuwa limetobolewa.
Machango alisema watu hao walipoona mwili huo, walitoa taarifa Polisi ambapo askari walifika na kuuchukua na baada ya muda ndugu za marehemu walijitokeza kuutambua katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Wilaya Tarime.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa maalumu wa Tarime Rorya ACP, Sweetbelt Njewike, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea kubaini waliohusika na tukio hilo.
Mwalimu Makuri alikuwa akifundisha katika Shule ya Msingi Nyarero na mwili wake ulichukuliwa na ndugu zake kwa maziko yaliyotarajiwa kufanyika katika kijijini cha Nyarero.

---HABARI LEO

UNYAMA...!! MUME ATEKETEZA NYUMBA KWA PETROLI HUKU WATOTO WAKE WAKIWA NDANI...KISA UGOMVI KATI YAKE NA MKEWE..

 Mtoto aliyefariki

Mtoto Matrida Michael mwenye umri wa miaka 9, mkazi wa Mtoni kwa Azizi Ally, wilayani Temeke jijini  Dar es Salaam, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Oktoba 23, mwaka huu kufuatia majeraha ya moto aliyoyapata. 
Marehemu Matrida na watoto wenzake wawili, Tatu Mapunda (9) na Flora Mapunda (7), waliungua moto Oktoba 16, mwaka huu saa tano usiku wakiwa wamelala baada ya chumba chao kulipuliwa kwa petroli na mtu anayedaiwa kwa ni Brighton Mnamwa.
Inadaiwa kwamba chanzo cha Mnamwa kuamua kulipua watoto hao ni ugomvi baina yake na mkewe Janeth Lwena, waliyekuwa katika mzozo wa kumgombea mtoto wao wa miaka mitatu aitwaye Tulizo.


Watoto ambao wako hoi

Mama mdogo wa marehemu Mary Ivo ambaye alikuwepo msibani hapo, alisema kwamba dada yake yupo Muhimbili anawauguza majeruhi wawili waliobakia na kwamba wakati wa ugomvi wao, mke alimzidia nguvu mumewe.
Aidha aliendelea kueleza kwamba baada ya mke kumzidi nguvu, mume alizusha ugomvi mkubwa huku akitishia kumuua kwa panga, hata hivyo mke alimdhibiti.
‘Baadaye mume huyo inadaiwa kwa aliondoka hapo nyumbani na haikujulikana alikoenda, ndipo mke alienda chumba cha jirani na kumuomba Matrida abakie na watoto pale chumbani akatoe taarifa polisi lakini mtoto aliyekua akigombewa alienda naye kituoni,’ alisema mama mdogo.
Habari zinasema kwamba yule mume alienda kituo cha mafuta kununua petroli ili aweze kuwatekezeza wote, lakini hakujua kama mkewe pamoja na mtoto aliyekua akigombewa hawakuwepo.
Taarifa zaidi zinaeleza kwamba baada ya mume huyo kurudi, alimimina mafuta hayo katika chumba hicho kisha kukilipua wakati watoto hao watatu wakiwa katika usingizi na wananchi walipojitokeza walikuta chumba kikiteketea huku sauti ya watoto ikisikika wakiomba msaada.

Wananchi waliokuwepo kwenye eneo la tukio walisema kwamba walipatwa na uchungu hivyo walijitosa kuuzima moto ule na kuwaokoa watoto hao watatu huku wakiwa wameungua vibaya, waliwakimbiza Hospitali ya Temeke na kutokana na hali yao kuwa mbaya walipelekwa Muhimbili ambapo Matrida alifariki dunia.
Naye Michael Melkiori Kess, baba wa marehemu alisema kwamba amesikitishwa na kitendo hicho na amedai ni cha kinyama hivyo ameiomba dola kumsaka mtu huyo hatari kwani huko aliko kwa sasa bado anaweza kusababisha majanga megine.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mtoni Sabasaba, Mwita Mang’ana alisema kwa kitendo hicho ni cha kinyama kwani amesababisha kujeruhi watoto wasiokua na hatia na amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha kuwa mtuhumiwa anapatikana .

Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba msako wa kumtafuta mtuhumiwa unaendelea sambamba na uchunguzi wa tukio

UKATILI..!! MUME AMUUA MKEWE NA KISHA KUMTUMBUKIZA KWENYE SHIMO LA CHOO ...!!

MKAZI wa Kijiji cha Msanzi wilayani Kalambo katika Mkoa wa Rukwa , Festus Sungura (37) anadaiwa kumuua kikatili msichana Janeth Mwanandenje (10) na kisha kutumbukiza mwili wake ndani ya shimo la choo. Inadaiwa choo hicho kilikuwa kikitumiwa na mkewe waliyetengana naye na lengo lilikuwa aweze kukamatwa na kufungwa kwa kosa la mauaji. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Alibainisha kuwa lilitokea Oktoba 18 mwaka huu saa 11 katika Kijiji cha Katuka Kata na Tarafa ya Matai wilayani Kalambo.
Mwaruanda alidai Oktoba 13 mwaka huu saa mbili usiku Janeth (marehemu) alikwenda kwenye ukumbi uliokuwa ukionesha mikanda ya video katika Kijiji cha Msanzi na hakurudi tena nyumbani kwao hadi mwili wake ulipogunduliwa ndani ya shimo la choo, kijiji jirani cha Katuka .
Inadaiwa siku iliyofuata, baba mzazi wa marehemu huyo aitwaye Mussa Mwanandeje , alitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Matai ya kupotea kwa binti yake huyo.
Kwa mujibu wa Mwaruanda, Oktoba 18 mwaka huu jirani wa wazazi wa marehemu huyo katika Kijiji cha Msanzi, aitwaye Festus Sungura (37), alikwenda Kijiji cha Katuka, ambacho ni jirani na kijiji cha Msanzi.
Alikwenda kumfuata mkewe Rosemary Arusha, ambaye alirudi kwao kijijini hapo baada ya kugombana na mumewe huyo miezi kadhaa iliyopita.
Baada ya Sungura kufika Katuka, alikutana na binti yake aitwaye Digna Sungura (15), ambapo alimhoji iwapo mama yake mzazi ( mke wa Sungura) akifungwa, kwa kuwa anamchukia yeye baba yake, ataenda kuishi kwa nani? Binti yake huyo, alimjibu kuwa ataishi na bibi yake kijijini hapo Katuka.
Ndipo Sungura alipomwagiza binti yake huyo, akamwambie mama yake atoe miti mitatu, iliyowekwa juu ya shimo la choo wanachotumia, waone alichofakifanya yeye.
Mama ya binti huyo, alitoa taarifa kwa viongozi wa kijiji hicho cha Katuka, ambapo kwa kushirikiana na wakazi wengine, walitoa miti chooni hapo na kuuona mwili wa marehemu uliotumbukizwa humo.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, mtuhumiwa huyo ameshakamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani upelelezi wa shauri lake utakapokamilika

UNYAMA...!! MUUZA CHIPSI AMTEKA MTOTO NA KUTOKOMEA NAE KUSIKOJULIKANA...

MTOTO wa kike mwenye umri wa miaka mitatu, Maryment Ibrahim ambaye anaishi Tandale jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alipatwa na masahibu makubwa baada ya kutekwa nyara na kutoroshwa hadi Gairo mkoani Morogoro huku mtekaji akidaiwa kutaka apewe shilingi milioni 6 ili amuachie.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Oktoba 16 mwaka huu baada ya kijana mmoja, anayefanya biashara ya kuuza chipsi anayejulikana kwa jina la Issa Ramadhani, kudaiwa kumchukua mtoto huyo aliyekuwa akicheza nyumbani kwao na kutoweka naye kabla ya wazazi wake kubaini na kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’.
Awali, ilidaiwa Ramadhan alikuwa na tabia ya kuwachukua watoto wadogo wa mtaani hapo na kuondoka nao na kuwarudisha baadaye, kitu kilichowafanya wazazi wa mtoto huyo kutokuwa na wasiwasi.
Wakizungumza na mwandishi wetu, wazazi wa mtoto huyo walisema waliamua kutoa taarifa polisi na kufunguliwa jalada nambari KJM/RB/8994/13 baada ya kupashwa kuwa mtekaji ambaye alishaacha kazi yake ya kukaanga chipsi, aliondoka muda mrefu na binti yao na hakukuwa na dalili za kurejea.
Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu, wazazi hao pamoja na majirani walifanya uchunguzi wa chinichini na kufanikiwa kupata namba ya simu ya mtekaji huyo, lakini walifanikiwa kubadilishana naye ujumbe mfupi wa simu kwani hakuwa akipokea simu yake ya kiganjani.
Inadaiwa kuwa katika mawasiliano hayo, mtekaji alikataa katakata ombi la kumtaka amrudishe
mtoto wao na kutaka apewe kiasi cha shilingi milioni 6 ili kutekeleza jambo hilo ingawa baadaye ilibainika jamaa huyo alikuwa Gairo mkoani Morogoro.
Wazazi hao walisema kuwa Oktoba 19 mwaka huu mmoja wa majirani walioguswa na tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Justin Henry alijitolea kusafiri mpaka Gairo kumsaka mtoto na mtekaji wake jambo ambalo lilifanikiwa kwa kumpata mtoto akiwa mzima wa afya japokuwa mtekaji alishtukia na kukimbia.

INASIKITISHA SANA...!! NDUGU WATAKA MTOTO AUAWE ILI KUONDOA NUKSI KWENYE UKOO...!!


MTOTO aitwaye Mwajuma Haji (16) ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anayesumbuliwa na  ugonjwa wa kusinyaa kwa viungo yuko katika hali mbaya baada ya baadhi ya ndugu kudaiwa kutaka auawe ili kutoa uchuro katika familia.

 Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo, Tatu Musa baadhi ya ndugu (siyo wote) wamekata tamaa ya kumuuguza mtoto huyo na kupendekeza heri mtoto huyo akatishwe maisha yake.
  
“Mwanangu haumwi wala hajawahi kuumwa ila ghafla alianza kusinyaa na kukosa nguvu, kinachoniuma baadhi ya ndugu zangu wamekata tamaa wanataka wamuue, waniachie mwanangu,” alisema mama huyo huku akilia mfululizo.


Mwandishi wetu amemshudia mtoto huyo akiwa amesinyaa viungo kiasi cha kutoweza kufanya kitu chochote zaidi ya kulala.
  
Mama mzazi wa mtoto huyo alisema kuwa alijifungua mtoto huyo akiwa na afya njema lakini alipofikisha umri wa miaka mitatu hali ikabadilika na viungo vyake kuanza kusinyaa.
  
Mama huyo amedai kwamba  kutokana na hali hiyo hakuweza tena kufanya shuguli za kumwingizia kipato zaidi ya kukaa na mwanaye kijijini kwao, Kiamange, Bagamayo mkoani Pwani bila ya kupata matibabu ya uhakika.
  
Alisema kwamba   maisha ya mtoto wake yameendelea kuwa mabaya bila ya kupata msaidizi kutokana kutengwa na baadhi ya ndugu zake waliokata tamaa ya kumuuguza.
  
Aidha, Mama Mwajuma amedai kwamba kuna wakati alikuwa akimfungia ndani mwanaye  kuanzia asubuhi ili aende kulima na kupata chochote, lakini aliporudi nyumbani alimkuta katika hali mbaya sana.

Kutokana na mazingira kuwa magumu, mama huyo alidai kwamba hakuwa na msaidizi wa kuweza kumwachia mwanaye  ili aweze kuhangaikia kipato.
  
Mbali na mtoto huyo, mama huyo alibahatika kupata mtoto mwingine ambaye sasa ana umri wa mwaka mmoja na nusu lakini baada ya kujifungua mwanaye mkubwa akatokwa na vidonda mgongoni.

Baada ya mtoto huyo kusumbuliwa na ugonjwa huo kwa muda mrefu alishauriwa kumpeleka Muhimbili na kumuacha mwanaye  mdogo kwa majirani.

Baada ya muda alipata taarifa kwamba mtoto wake mdogo anaumwa, ikabidi akamchukue na kumleta Muhimbili ili aishi naye ingawaje hairuhusiwi kwa mtoto kuishi wodini.

“Nina wakati mgumu, kwa kuwa nina watoto wawili sina cha kufanya kwa kuwa huyu mwingine hajiwezi kwa chochote zaidi ya kumsaidia  kwa kila kitu, mbaya zaidi  ndugu wamenitenga,” alisema   huku akibubujikwa machozi.
  
Ndugu Mtanzania mama Mwajuma yuko katika hali mbaya sana, kama unataka kumsaidia mtoto wake tuma mchango wako kupitia namba 0754 021 301.

BABA AUZA NYUMBA NA KUTOKOMEA KUSIKOJULIKANA....MTOTO MMOJA AFUNGIWA NDANI KWA SIKU TANO....

Na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vimeendelea kushika kasi katika baadhi ya maeneo hususani vijijini, licha ya Serikali na asasi mbali mbali kulipigia kelele ambapo hivi karibuni Baba mmoja aliamua kuuza nyumba ikiwa na watoto ndani na kutokomea kusikojulikana na kuwaacha wasijue la kufanya.
Mkasa huo wa ajabu ulitokea katika kijiji cha Hatwelo, Kata ya Ijombe Mbeya Vijijini ambapo Mkazi huyo aliyefahamika kwa jina la Emmanuel Yuta alipouza nyumba yake na kutokomea yeye na mkewe na kuwaacha watoto wawili wenye umri kati ya miaka 9 na 11 wakikosa mahala pa kuishi.
Akizungumzia sakata hilo kijijini hapo, Mwanaharakati wa haki za Binadamu, Yasin Yuta, alisema majirani waligundua baada ya kusikia kelele za mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Erasto Emmanuel (11) aliyekuwa amefungiwa ndani na kukaa kwa siku saba.

Alisema baada ya kumfungulia mtoto huyo ndipo ilipobainika kuwa nyumba hiyo ilikuwa imeshauzwa huku mtoto akiwa ndani na ndipo mnunuzi alipofunga na kufuli bila kujua kama kuna mtoto ndani huku watoto wengine wakiwa kwa ndugu zao ambao pia hawakuelezwa kama nyumba imeuzwa.
Nyumba hiyo iliuzwa kwa Dati Nsagaje kwa gharama ya shilingi 750,000/= ikiwa ni nyumba mbili pamoja na kiwanja ambapo mnunuzi huyo alilipa kianzio cha shilingi laki nne biashara iliyofanyika tangu April 26 mwaka huu  na kiasi kilichobaki wakiwa wameahidiana kulipana Mwezi Mei 15, Mwaka huu.

Wahanga wa tukio hilo ambao ni watoto walisema hawakuwa na taarifa zozote za kuuzwa kwa nyumba wanayokaa ambapo walisikia kuwa baba yao ameenda Sumbawanga kumfuata  mke wake ambaye inasemekana aliolewa na mwanaume mwingine.
“ Nilikuwa nimelala  ndani ambapo nilipoamka asubuhi nilikuta mlango umefungwa kwa nje hata hivyo nilivumilia hadi njaa ilipoanza kuniuma baada ya siku tano nikaanza kupiga kelele ndipomajirani walipokuja kunifungulia na kuniambia nyumba imeuzwa” alisema mtoto Erasto Emmanuel. 
Mtoto mwingine aliyetelekezwa ambaye siku ya tukio alikuwa ameenda kulala kwa bibi yake Groli Emmanuel (9) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Hatwelo alisema siku akiwa anaondoka aliagwa na baba yake ambaye alimwachia shilingi 3000 lakini hakumwambia kama nyumba imeuzwa.
Kutokana na kitendo hicho kutokukubalika,baadhi ya majirani walisema ni kitendo cha kinyama na hakipaswi kufumbiwa macho ambapo waliamua kuchanga fedha ili kuikomboa nyumba ili irudi mikononi mwa watoto.
Majirani hao walifanikiwa kuchanga shilingi 410,000/= alizokuwa amedai mnunuaji ili aweze kurejesha nyumba ikiwa ni fedha alizokuwa ametoa awali hivyo kukubaliana kuicha nyumba hiyo ambayo kwa mujibu wa majirani na baadhi ya ndugu wamesema itakuwa ni mali ya watoto.
Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida na kuonesha kukosa uwajibikaji kwa baadhi ya viongozi wa Serikali ya Kijiji ambao walishiriki moja kwa moja zoezi hilo huku wakiwa wamesaini kama mashahidi na kugonga mhuri wa Serikali ya Kijiji walipoulizwa kuhusiana na sakata hilo hawakuwa na majibu ya kuridhisha.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Hawelo, Ibrahimu Mponzi, alisema kitendo alichokifanya muuzaji ni cha kawaida kwa sababu ameuza mali yake mwenyewe na kwamba wao kama majirani na serikali ya kijiji hawawezi kuhoji atakako waacha watoto kwa sababu ni mipangilio ya maisha ya kila mtu.
Mbali na mwenyekiti wa Kijiji kuwa shahidi wa upande wa mnunuaji akiwa sambamba na watu wengine wanne akiwepo Mkewe ambaye pia ni Balozi wa nyumba kumi pia waliosaini wengine ni ndugu wa mnunuaji ili hali muuzaji akiwa hana shahidi hata mmoja.
Aidha juhudi za majirani kuikomboa nyumba hiyo na kuwa mali ya watoto zilifanikiwa ambapo mnunuzi Datistani Mwanshinga alibatilisha ununuzi wa nyumba hiyo Mei 9, Mwaka huu baada ya kukiri kurejeshewa fedha zake.

HATIMAYE BABA ALIYETELEKEZA WATOTO AKAMATWA. ...NI WATOTO WA MIAKA (8) NA (7) WANAOJIONGOZA WENYEWE BAADA YA KUKIMBIWA NA WAZAZI WAO

Watoto  Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakifanya usafi katika nyumba wanayoishi 
Hapa ndipo wanapopikia chakula wakati wa usiku  kwakweli ni hali ya hatari sana
Mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango akiwa na watoto hao alipowatembelea nyumbani mara baada ya kuwakosa shuleni mwandishi wetu alipowauliza kwanini hamjaenda shule leo? wakamjibu tulijua leo ni sikukuu ndiyo maana hatujaenda shule,
Hapa wakinawa kutokana na hali ya uchafu waliokuwanayo baada ya kumaliza kufanya usafi nyumba yao
Wakiwa na waalimu wao
Hapa mwandishi wetu Joseph Mwaisango akiwarudisha nyumbani watoto hao mara baada ya maongezi mafupi na waalimu wao

JESHI la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Steven Julias mkazi wa Jakaranda kata ya Iyela Jijini Mbeya akituhumiwa kutelekeza familia kwa miezi mitano bila huduma za msingi ikiwemo chakula na sare za shule.

Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumethibitishwa na mwenyekiti wa dawati la Jinsia Mkoa wa Mbeya, Mary Gumbo ambaye alisema walimkamata Oktoba 11, mwaka huu eneo la nyumbani kwake alikokuwa amewatelekeza watoto hao.

Aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa anafanya maandalizi ya kuwatorosha watoto hao ili kukwepa mkono wa sheria dhidi yake baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa anatafutwa kukabili kesi iliyombele yake.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo alisema hivi sasa uchunguzi unafanyika ili kesi iweze kufunguliwa na hatimaye kufikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake ili vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto vikomeshwe.

Wakati huo huo maisha wanayoishi kwa sasa watoto hao  Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza  shule ya msingi Mapambano iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya maisha ya kujipikia bila huduma za msingi wasamaria wema wameombwa msaada wao wa hali na mali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti watoto hao wamesema hivi sasa wanaishi kwa misaada kutoka kwa walimu na baadhi ya watu ambao huwapa unga na maharage na wao hulazimika kutafuta fedha za kununulia mahitaji mengine kama mafuta ya kula na taa.

Wametaja baadhi ya mahitaji yao muhimu kwa sasa kuwa ni pamoja na Sare za shule kutokana na kuchakaa kwa sare wanazotumia ikiwemo Madaftari, kalamu,Masweta, Viatu, mafuta ya kupikia, mafuta ya kupaka, sabuni, chumvi, mkaa, Unga, Mchele na maharage.

Aidha imeshauriwa kuwa kutokana na mazingira wanayoishi watoto hao kutokuwa mazuri kwa utunzaji wa vyakula ambapo nyumba wanayoishi kutokuwa na mlango vitu hivyo vihifadhiwe Ofisini Kwa Mwalim Mkuu kama vitapatikana.

Kwa yeyote atakayekuwa ameguswa na hali ya watoto hao awasiliane na Mbeya yetu kupitia namba 0754374408
 au Bomba fm redio kupitia 0754 490752.
 
-Mbeya yetu

UNYAMA..MTOTO WA MIAKA SITA ABAKWA NA DALALI WA NYUMBA...!

Dalali wa viwanja na nyumba eneo la Mbezi Makabe, jijini Dar es Salaam anatuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka sita na kumjeruhi vibaya sehemu zake za siri.
Tukio hilo limetokea Septemba 3, mwaka huu, ambapo mtoto huyo (jina linahifadhiwa) alifanyiwa unyama huo na dalali huyo anayejulikana kwa jina moja la Mgosi.
Akizungumza kwa masikitiko na gazeti hili, mama mkubwa wa mtoto huyo, Elizabeth Aloyce (28), alisema Mgosi ambaye ni dalali wa viwanja na nyumba katika eneo hilo, alikuwa akimfanyia kitendo hicho kwa muda mrefu.
Alisema kugundulika kwa tabia hiyo chafu ilikuja baada ya mtoto huyo kushindwa kutembea kutokana na maumivu makali.
Elizabeth alidai kwamba siku ya tukio alirudi nyumbani mapema kutoka kwenye biashara zake, alipoingia ndani alimkuta mtoto huyo amelala huku akiugulia.
Alipomuuliza kitu gani anachoumwa, mtoto huyo alianza kulia huku akificha sehemu zake za siri.
"Nilishtuka sana kuona hali ile, nilimshika na kuanza kumchunguza ndipo nikagundua sehemu zake za siri zimeharibika na kibaya zaidi mbegu za kiume zilikuwa zimeenea kila mahali," aliongeza kusema.
Kutokana na hali hiyo, aliamua kuwaita majirani na baada ya kushuhudia walikiri mtoto huyo amebakwa.
Baada ya kugundua suala hilo walimbana mtoto huyo amtaje mtu aliyemfanyia kitendo hicho, ndipo alipomtaja jina la mtuhumiwa na kwamba ilikuwa siyo mara yake ya kwanza kufanyiwa kitendo hicho.

MTOTO ANENA
Mtoto huyo akiongea na NIPASHE alisema kabla ya kufanyiwa unyama huo, mtuhumiwa huyo alikwenda kumchukua wakati akicheza na watoto wenzake.
"Nilikuwa nacheza alikuja Mgosi na kunichukua hadi chumbani kwake na kunilalia juu, kila siku ananifanyia hivyo na kuniambia nisiseme kwa mtu atanipiga," alisema mtoto huyo.
Alisema siku ya mwisho mtuhumiwa huyo mara baada ya kumaliza haja zake alimwambia arudi nyumbani kwao haraka.
"Nilirudi nyumbani niliogopa mama atanikuta nikitoka kwa mgosi, lakini niliona maumivu makali," aliongeza kusema.

POLISI WAMKAMATA
MTUHUMIWA
Baba mzazi wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa) alisema tukio waliliripoti kituo cha Polisi Mbezi kwa Yusufu baada ya kumaliza taratibu zote za kumpatia matibabu Hospitali ya Rufaa ya Tumbi.
Polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na kukaa ndani kwa siku kumi, kisha kuachiwa kwa dhamana.
Hata hivyo, alisema hajaridhishwa na mwenendo wa suala hilo baada ya polisi wa kituo hicho kumzungusha kwa muda mrefu na hakuna dalili ya kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.
"Tumekatishwa tamaa na utendaji wa polisi, hivi sasa imefikia muda wa mwezi mmoja hakuna kilichofanyika huku mtuhumiwa ameachiwa huru," alisema.
POLISI YATOA TAMKO
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Camilius Wambura, alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alisema halifahamu na kuahidi kulifuatilia kwa kina ili aweze kutolea ufafanuzi.
Hata hivyo, aliwataka wananchi kutambua wajibu wa jeshi hilo siyo tu kumfikisha mahakamani mtuhumiwa, badala yake inawajibika kufanya upelelezi kisha jalada husika kulipeleka kwa mwanasheria wa serikali kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.
"Naomba wananchi wafahamu kwamba polisi kazi yao ni kupeleleza tu, kazi ya kufikisha mahakamani ni Ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali (DPP), hivyo kutupa lawama ni kutuonea," alisema Kamanda Wambura.
Alisema hata suala la mtu kupewa dhamana lipo kisheria na kila mtu ana haki ya kudhaminiwa, bali kwa makosa machache ya jinai kama kuua, wizi wa matumizi ya nguvu, biashara ya madawa ya kulevya ndiyo mtuhumiwa wake hawezi kupewa dhamana.

INASIKITISHA SANA...!! HOUSEGIRL AMNYONGA MTOTO NA KISHA KUMTUPA KWENYE DIMBWI LA MAJI MACHAFU...

NI ukatili uliopitiliza! Hausigeli aliyejulikana kwa jina moja la Ester (14) yupo matatani kwa madai ya kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa kumnyonga shingo na kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kuutumbukiza mwili wake kwenye dimbwi la maji machafu, Risasi Jumamosi limekamata tukio zima.
Tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita Mailimoja, Kibaha mkoani Pwani ambako marehemu alikuwa akiishi na wazazi wake.
Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye, alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili tangu aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo alimkubalia na kumuagiza mboga.
AONDOKA NA MTOTO
Bila mwanamke huyo kujua, msichana huyo alimpitia Arafat kwa jirani alikokuwa akicheza na wenzake na kuondoka naye kwa madai anamsindikiza.
“Nilipoona muda unasonga mbele bila hausigeli kurudi na mtoto nilianza kuwatafuta,” alisema mama wa marehemu.
Akasema aliwatafuta kwa muda mrefu bila mafanikio mwishowe yeye na majirani zake wakaenda kutoa taarifa polisi na kufunguliwa jalada la kesi KB/RB/1154/2013 TAARIFA.
HABARI ZASAMBAA MAITI YA MTOTO KUONEKANA KWENYE DIMBWI LA MAJI
Mama wa marehemu aliendelea kusema kuwa zoezi la kumsaka msichana huyo na mtoto wake liliendelea mpaka Jumanne iliyopita ambapo habari zilisambaa kwamba kuna maiti ya mtoto wa kiume  imekutwa ikielea kwenye dimbwi la maji machafu linalotumika kumwagilia bustani za mboga maeneo hayo.
“Niliondoka na ndugu wengine hadi kwenye dimbwi hilo! Nilipata mshtuko mkubwa kukuta maiti ya mtoto anayeelea ni ya mwanangu Arafat,” alisema huku machozi yakimtoka.
MADAKTARI WAANIKA RIPOTI YA UCHUNGUZI
Baada ya hapo, mwili huo ulipelekwa katika Hospitali Teule ya Tumbi, Kibaha ambapo madaktari waliufanyia uchunguzi na kubaini kuwa marehemu alinyongwa shingo na kupigwa na kitu kizito kichwani hali iliyomsababishia mauti.
MAUAJI YAHUSISHWA NA USHIRIKINA
Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili Jumatano iliyopita akiwemo mama wa marehemu, walisema kwa siku mbili hizo alizofanya kazi hausigeli huyo alionekana kuwa na mambo ya kishirikina kwani asubuhi ya siku ya tukio aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja.
“Siku hiyo ya Jumapili huyo mdada wa kazi aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja, alipoambiwa amalizie zote alikataa akisema atanyoa baada ya kutoka sokoni ambapo hakurudi tena,” alisema mama wa marehemu.
HAUSIGELI AKAMATWA
Jumatatu iliyopita, siku moja baada ya tukio, hausigeli huyo alikutwa akirandaranda stendi akiomba fedha za nauli ili arudi kwao Mbeya lakini alikamatwa na kufikishwa kwenye kituo kidogo cha polisi.
Habari zinasema hali kwenye kituo hicho ilikuwa mbaya kufuatia baadhi ya wakazi wa eneo hilo kujaribu kukivamia ili wamuue mtuhumiwa huyo. Ilibidi mtuhumiwa ahamishiwe Kituo cha Polisi cha Tumbi, Kibaha.
MANENO YA WATU WA KARIBU
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa familia hiyo, msichana huyo aliokotwa na ndugu wa baba wa marehemu baada ya kumkuta barabarani akiomba msaada akidai anateswa na ndugu zake, wakampeleka kwa baba wa marehemu ili wamsaidie ambapo walimpa shughuli ya kazi za ndani.
Baba wa marehemu, Allan hakuweza kuzungumza kutokana na kuwa kwenye hali mbaya katika Zahanati ya Kellen alikolazwa baada ya mwanaye kuzikwa katika Makaburi ya Mailimoja, Jumatano iliyopita.
-RISASI
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger