Showing posts with label DIAMOND. Show all posts
Showing posts with label DIAMOND. Show all posts

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA DIAMOND PLATINUMZ BAADA YA NYIMBO YAKE YA MY NUMBER ONE FT DAVIDO KUFIKA NAFASI YA KWANZA KATIKA STESHENI YA TRACENIGERIA.

Leo ni siku kubwa sana kwa msanii wa kizazi kipya Diamond Platinumz na washabiki wake, pamoja na wana-Bongo flava, ambao kila siku tunatamani kuona mziki huu wa nyumbani unavuka mipaka na kwenda mbali, nakuleta heshima nyumbani kwetu, kukuza mapato ya watu wetu na kuzidi kujivunia kilicho chetu...

Haya ni maneno machache ya Diamond Platinumz aliopost leo mchana kwenye account yake ya instagram,... soma hapa chini.
"Need i say More...???? My Prayers are slowly been answered... Trust me! we getting there... S/O to @trace_inter for keeping that pace of promoting African Music Constant Cc @TraceNigeria #numberOne #1 #wasafi

DIAMOND PLATNUMZ AWAJIA JUU WALE WANAOSEMA KAMPONDA ALI KIBA, SOMA HAPA ALICHOKISEMA...

Photo: kiukweli, nasikitishwa sana  jins baadhi ya wasanii kutwa  wanavyolazimisha kunitengenezea ugomvi wa kilazima pasipo kuwa na sababu, mara wengine wakizusha eti Nimewatusi kwenye Media, Mara sjui Nimepost kuwakashif, yaani ilimradi tu....kwanini Wanamuziki wa Tanzania Tunashindwa kubadilika... mbona mi nahangaika na muziki wangu kimpango wangu... Mnasema nyie ndio mnaojua kuimba mie sijui "sinatatizo"... Mnasema nyie ndio wenye sauti nzuri yangu mbaya "Sina tatizo"... sasa mbona tena bado mnanifatilia na kutokujua kwangu... Nafkiri ni vyema mkaanza kutumia ujuzi wenu kukuza sanaa ya nchi yetu na kuleta heshima na maendeleo nchini, kuliko kupika majungu..... Watu wanataka kazi!

Kiukweli, nasikitishwa sana jins baadhi ya wasanii kutwa wanavyolazimisha kunitengenezea ugomvi wa kilazima pasipo kuwa na sababu, mara wengine wakizusha eti Nimewatusi kwenye Media, Mara sjui Nimepost kuwakashif, yaani ilimradi tu....kwanini Wanamuziki wa Tanzania Tunashindwa kubadilika... mbona mi nahangaika na muziki wangu kimpango wangu... Mnasema nyie ndio mnaojua kuimba mie sijui "sinatatizo"... Mnasema nyie ndio wenye sauti nzuri yangu mbaya "Sina tatizo"... sasa mbona tena bado mnanifatilia na kutokujua kwangu... Nafkiri ni vyema mkaanza kutumia ujuzi wenu kukuza sanaa ya nchi yetu na kuleta heshima na maendeleo nchini, kuliko kupika majungu..... Watu wanataka kazi!

-diamondplatnumz

MODEL WA TANZANIA HAMISA AZUNGUMZIA KUTOA PENZI KWA MWANAMUZIKI DIAMOND...HUYU HAPA

MREMBO anayedaiwa kuliingilia penzi la staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, aliyewahi kushiriki Shindano la Miss Tanzania, Amisa Mabeto amefunguka kuwa  mwanamuziki huyo ni shemeji yake tu, hakuna chochote kati yao.
Amisa Mabeto.

Akipiga stori na safu hii kuhusiana na madai hayo, Amisa alisema alistaajabu kwani hana mazoea na Diamond Kama ni kuonana waliwahi kuonana miaka ya nyuma, tena siyo kimapenzi.

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

“Kamwe siwezi kutembea na Diamond na haitatokea kwani jamii nzima inajua yupo na Wema na mimi huyo mtu ni rafiki yangu mkubwa, hana chake hapa, siwezi kutembea naye kamwe, namheshimu kama shemeji yangu,” alisema Amisa.

Amisa aliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano na Diamond akiwa ni shosti mkubwa wa Wema.

HII SASA IMEKUWA SIO KIFICHO TENA...!! TAZAMA KAMERA ILIVYO WAFUMA DIAMOND & WEMA WAKILA BATA USIKU WA JANA...


Hii ndo habari ya mujini......Wacha movie iendeleeeeeeeee.............
-jestina-george



KWELI DIAMOND ANATISHA SANA, HEBU CHEKI PART YA INTERVIEW YAKE NA KISS TV NA WAANDISHI WA MAGAZETI.

 Hii ni sehemu ya pili,ya mahojiano na media mbali mbali
Hapa Nairobi,baada ya kufanya mahojiano na
 Tuva wa Mambo mseto..nilifanya mahojiano na
Kiss Tv kisha nikafanya na waandishi kutoka vyombo vingine  vya habari waliokuwa wakinisubiri nje...
kama ilivyokuwa kwenye mambo mseto...kikubwa
 walitaka kufahamu kuhusu mipango yangu ya baadae
kimziki,collabos,na maisha yangu..
 Director wa kipindi,Kiss Tv akiniwekea Mike
 Mahojiano na Kiss Tv yakaanza

 Waandishi kutoka vyombo vingine vya habari wakinisubiri
 Mahojiano yakaanza na wwaandishi wamajarida  na magazeti

ANGALIA HOTEL YA KIFAHARI ALIYOFIKIA DIAMOND HUKO NCHINI KENYA JIJINI NAIROBI ....


 Baada ya kuwasili toka airport
 Hotel naitwa EKA,ipo mjini Nairobi

WEMA ANYANG'ANYWA KILA KITU, KISA KURUDIANA NA DIAMOND..

ZILE tambo, mbwembwe na majigambo ya Miss Tanzania 2006/07, aliye pia msanii wa filamu Bongo, Wema Isaac  Sepetu, zimefika mwisho kufuatia kunyang’anywa samani za ofisi yake ya Endless Fame Film Production na aliyekuwa mpenzi wake, Clement ‘kigogo wa ikulu’ na sasa amebaki mweupe.....
 

Wema Isaac  Sepetu.

 Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo la aibu lilijiri hivi karibuni kwenye ofisi hiyo ya Wema iliyopo Mwananyamala-Komakoma jijini Dar
.
 KIGOGO WA IKULU AVAMIA NA MABAUNSA

Habari za uhakika zinadai kuwa, siku ya tukio, Clement akiwa ameongozana na watu waliosadikiwa kuwa ni mabaunsa, walivamia ofisi hiyo aliyomfungulia mlimbwende huyo na kukomba vitu vyote vya thamani alivyomnunulia wakati wa mapenzi motomoto (hakuna lenye mwanzo lisilo na ncha).

KUMBE ALIKODI CANTER

Kama njiwa apelekaye ujumbe muhimu wa huba, mtoa taarifa huyo alizidi kumwaga ‘upupu’ kuwa, siku hiyo Clement mbali na gari lake la kifahari, pia alitinga akiwa na gari aina ya Canter ambapo bila maswali wala maelezo achilia mbali ufafanuzi, alikusanya vifaa vyote na kuvirundika kwenye gari.
 
Wema akiwa katika ofisi yake kabla ya kunyang'anywa samani zilizomo.

IDADI YA VITU VILIVYOBEBWA

Vifaa hivyo ni tarakishi (computer), kamera ya kurekodi sinema (video camera), vifaa vya kurekebisha hali ya hewa (air conditioner), vifaa vya kuhifadhia umeme wa ziada, uninterruptible power supply  (ups) pamoja na vifaa vingine zikiwemo nyaya za umeme na kuiacha ofisi nyeupe kama uwanja wa mpira.

 “Hali ni mbaya sana, jamaa (Clement) alichukua kila kitu ndani ya ofisi hiyo kuanzia kompyuta, kamera hata nyaya! Hivi tunavyoongea, ofisi haina kitu kabisa,” kilisema ‘kikulacho’ hicho.

 CHANZO NI DIAMOND

Mpashaji huyo alizidi kuyapa utulivu masikio ya mwandishi wetu kuwa, chanzo cha kigogo huyo kufanya ‘umafia’ huo ni kitendo cha Wema kurejesha penzi lake kwa ‘mtemea maiki’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.
 
Ofisi ya Wema kwa ndani.

 Taarifa hizo zilieleza kuwa, kitendo hicho kilichochea hasira za Clement, hasa pale Diamond alipohojiwa kuhusu kuingilia penzi hilo na kujibu hamwogopi mtu, “ndiyo maana Clement akaamua kumwaga ugali baada ya wawili hao (Wema na Diamond) kumwaga mboga,” kiliongeza chanzo.

HEBU MSIKILIZE WEMA

Ili kujua yapi ni maziwa na lipi ni tui juu ‘niuz’ hizo, mwandishi wetu alimtafuta Wema na kukutana naye laivu juzi ambapo alikiri kukumbwa na zahama hiyo huku akionesha mshangao wa wazi kwa kitendo alichofanyiwa na ‘zilipendwa’ wake huyo.
 

Geti la kuingia katika ofisi hiyo.

 “Ni kweli kabisa Clement amefanya hivyo, lakini nashangaa na ni mara yangu ya kwanza kuona wapenzi wakiachana mwanaume anaamua kuchukua vitu vyote alivyowahi kumnunulia au kumpa.
“Huo ni ushamba na unyanyasaji, akumbuke kwamba alipokuwa na mimi alinitumia pia,” alisema Wema na kuongeza:

 “Hata hivyo, namshukuru Mungu, vitu vyote alivyochukuwa Clement, baby (Diamond) kasema ataninunulia, wiki mbili hazitapita.”

Wema alikwenda mblele zaidi kwa kuonesha machungu yake kwa kigogo huyo pale aliposema: “Kwanza nasikia vitu vyenyewe alipofika nyumbani kavimwaga nje maana ndani hakuna nafasi.”
Wema akiwa na mpenzi wake Diamond aliyesababisha mpaka akanyang'anywa samani hizo.

KAANZA MWAKA VIBAYA

Mwanzoni mwa mwaka huu, Wema alikumbwa na mkasa wa kunyang’anywa lile gari la kifahari alilodai ni lake, Audi Q7 baada ya kusemekana kuwa halikuwa lake.

Kumbe gari hilo alipewa na Clement ambaye naye alilikopa kwa thamani ya shilingi milioni 90 kutoka kwa mtu aliyejulikana kwa jina la Shadrack Tweve.

 Tweve, baada ya kuzungushwa sana kulipwa fedha hizo, alikimbilia Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo hakimu aliamuru gari hilo likamatwe na kurejeshewa mlalalamikaji huyo.

 PENZI LA WEMA, KIGOGO WA IKULU

Uhakika ni kwamba, penzi kati ya Wema na kigogo huyo halipo tena na kwa sasa jamaa ana demu mwingine (jina tunalo) ambapo mapaparazi wetu wanaendelea kufuatilia kwa karibu ili kuwanasa katika mazingira yoyote yale.

CREDIT: GPL

DIAMOND KAMPA MIMBA WEMA SEPETU?SOMA HAPA UJE UKWELI WA JAMBO HILI

MSANII maarufu wa Bongo Movie, mrembo na mwenye pesa pengine kuwazidi wengi na ambaye hivi karibuni amezua mijadala mikubwa baada ya kurudiana na mpenzi wake wa zamani Diamond, ambaye pia ni maarufu katika muziki wa kizazi kipya nchini na mwenye kuongoza kwa mapato nchini, imegundulika kuwa ana ujauzito wa miezi kadhaa.
Wema ambaye alishindwa kuficha hisia zake na hatimae kuweka kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa instagram,” …mmmmmh jamani hichi kitumbo… hakifichiki now…” kuashiria kuwa mabadiliko ya mwili yameshaanza kuonekana (Picha chini inaonesha ujumbe huo kamili).

Mtandao wa huu ulianza kuhisi taarifa hizo na kuamua kuzifuatilia kwa karibu ili kujua nini haswa kinaendelea au ni hisia tu. Ndipo mwandishi alipochukua jukumu la kumtafuta mlimbwende huyo Wema Sepetu na kugonga mwamba.

Hata hivyo jitihada hizo hazikuishia hapo ndipo kilipopatikana chanzo cha karibu na Wema na kudai kuwa “ amekuwa akilalamika mabadiliko hayo na hata kusikika akisema anaihisi ameconsive…” kilisema chanzo hicho bila kutaka kutambulika hadharani.
“Ni kweli itakuwa hivyo na ndio maana Diamond aliamua kumtangaza rasmi siku hile ya chrismas” aliongeza.

Diamond ambaye alimtupilia mbali mpenzi wake Penny na kurudiana na Wema mapenzi yao hayakufichika kwani wakiwa China walipiga picha za mahaba na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii na kuzua hisia tofauti.

Hivi karibuni wamekuwa karibu sana kimapenzi na kuamua kuonesha siri zao za ndani bila kuficha, “mwenye macho haambiwi ona… juzi tu wameweka video zao wakiwa kitandani kila mtu ameziona, lakni pia Diamond kumnunulia nyumba baada ya kusikia mkataba wake umeisha na kwamba hautoongezwa, na mambo mengine kibao” kiliongeza chanzo hicho

“lakini tusubiri miezi tisa tu sio mingi na mimba huwahaifichiki bana tutaona

Wema Sepetu na Diamond wajirekodi wakifanya yao kitandani



Penzi lenye historia ya kushamiri, kumwagana na kurudiana limezidi kuchukua sura mpya, safari hii, Wema Sepetu  amenaswa akimrekodi video baby wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Chanzo cha  kuvuja kwa scene hiyo mpya ilitokea Ijumaa iliyopita ambapo bila hiyana, bibie Wema aliamua kuitupia video katika Mtandao wa Instagram ambayo alimrekodi Diamond aliyekuwa akiandika mashairi kitandani, akamsumbua kwa kumrekodi huko na kusindikiza kwa ujumbe uliosomeka:
 
“In da middle of his writing session…just had to disturb him a little”(Katikati ya muda wake wa kurekodi...nikamsumbua kidogo).
 
Diamond aliyekuwa akiandika mashairi, alisumbuliwa na Wema kwa kumrekodi huku akimtaka aweke mapozi tofautitofauti hali iliyomfanya ‘boyfriend’ wake huyo waliyerudiana siku chache zilizopita, apoteze umakini wa kuendelea kuandika mashairi.
 
Baada ya muda mfupi, ‘posti’ hiyo ya Wema ilipata maoni kibao huku kila mmoja akiweka mtazamo wake. Kuna ambao walimpongeza kwa kufurahi kuona uhusiano wao huku wengine wakiponda kuwa wamechoka ‘drama’ zao za kila siku.

VIDEO IKO HAPO CHINI 

NYUMBA MPYA YA DIAMOND NI NOMA SANA...CHEKI PICHA

Imefikia mahala flani hivi ambapo kweli kila mtu anaweza ku-agree kuwa muziki wetu huu wa bongo maarufu kama bongo fleva unalipa kwa kweli,tofauti kabisa na hapo mwanzo ulipokuwa unaonekana tu ni mziki wakihuni,na mzazi akijua unataka kufanya bongo fleva wakati unasoma.mtu unakuta unachezea stick zakutosha au kufukuzwa hadi home ikiwa mshua mtata zaidi,hivi sasa wasanii wengi wamekuwa wanapata maendeleo mbalimbali makubwa wengine magari na wachache sana wanaokumbuka mpango mzima wakujenga hivyo ikitokea mtu anajenga inabidi apewe hongera zake.
04dec2c0788211e3a1741240743416c5_8
Kupitia mtandao wa instagram msanii maarufu star wa nyimbo ya Mynumber1 Diamond platnums ame-share moja ya picha ya sehemu ya mjengo wake mpya ambao bado upo under construction,noma zaidi katika mjengo huo anaoushusha msanii kutakuwa na bonge la sweaming pool ambalo itakuwa kwenye backyard tu ya house hilo,kupitia mtandao huo wa instagram alitupia hiyo picha na kuandika haya.huku akionyesha uzalendo flani hivi kwa nchi yake.
Capture

Licha ya Kutoswa na Diamond, Penny Afunguka na kusema "Naapa kwa Mungu wangu katika maisha yangu haitatokea kamwe nikamdharau Diamond, thamani yake kwangu itabaki palepale"

MTANGAZAJI wa Kituo cha Televisheni cha DTV, Peniel Mungilwa ambaye ni zilipendwa wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnum’ amesema katika maisha yake haitatokea akamdharau kwa kumkashifu hata kama si wake tena.


Akipiga stori na paparazi wetu, mwanadada huyo alisema japo kwa sasa ametofautiana na Diamond aliyeweka wazi kwamba yupo na Wema Sepetu hawezi kuwa na chuki dhidi yao. “Naapa kwa Mungu wangu katika maisha yangu haitatokea kamwe nikamdharau Diamond, haijalishi yupo na nani kwa sasa, thamani yake kwangu itabaki palepale hamuwezi jua namheshimu kiasi gani yule mtu,” alisema Penny.

BAADA YA WEMA NA DIAMOND KURUDIANA..!! KIGOGO WA WEMA ATANGAZA VITA NA DIAMOND...SOMA ZAIDI HAPA..

YULE kigogo au taita aliyekuwa akimpa jeuri ya fedha Wema Isaac Sepetu ajulikanaye kwa jina moja la Clement anadaiwa kutangaza vita na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.

Habari ‘hoti’ zinadai kuwa Clement anataka Diamond arudishe gharama alizomgharamia Wema ndipo waendeleze mapenzi yao.
Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na Wema Isaac Sepetu katika pozi.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa kigogo huo, Clement anadai kwamba gharama alizotumia kwa Wema ni kubwa mno lakini bidada hakujali chochote na kuukabidhi moyo wake kwa ‘Mtoto wa Tandale’ ambaye ndiye barafu wa moyo wake.
Wema Isaac Sepetu.
“CK (Clement) anaumia sana kuona kuwa ameteketeza fedha nyingi kwa Wema lakini bila hiyana, mrembo huyo akabwaga manyanga kisha akarudisha mpira kwa kipa na kuanza moja huku kaka mkubwa akiachwa kwenye mataa,” alitonya mnyetishaji huyo bila kufafanua kama Clement aliachwa mataa ya eneo gani.

Akiendelea kutiririka bila kuweka nukta au ya mkato, mtu huyo alisema kuwa kiasi ambacho kinadaiwa kuteketea kwa Wema kinakaribia Sh. milioni 279.6 ambazo gharama hizo zinahusisha vitu kadhaa alivyowekeza kwa Wema.

“Kuna gharama za utengenezaji wa Filamu ya The Super Star ambayo haijulikani kilichotokea kwani hadi leo haionekani sokoni.

“Kama hiyo haitoshi kwenye uzinduzi wa filamu hiyo akamleta staa wa filamu wa Nollywood, Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde na sherehe mbili za uzinduzi zilifanyika katika hoteli kubwa mbili tofauti, ikasemekana milioni arobaini na nane ziliteketea.
 
Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.
“Kuna kodi ya pango la ofisi ya Wema ya Endless Fame iliyopo Mwananyamala Koma-koma, Dar, jamaa alilipa milioni nane na laki nne kodi ya miaka miwili ambayo kwa mwezi ni laki tatu na nusu.

“Ukiachana na gharama za nyumba na ofisi, kuna gari aina ya Audi Q7, inadaiwa kanunua Clement kwa Sh. milioni 98, Toyota  Harrier Lexusya Sh. milioni 48 na Toyota Mark X iliyomtoa Sh. milioni 25.

“Usisahau hata lile Toyota Noah ‘kitimoto’ la ofisi alinunua Clement kwa Sh. milioni 10, faini aliyolipiwa Kajala Masanja mahakamani Sh. milioni 13, gharama za kuirekebisha ngozi yake alipoenda nchini China iligharimu Sh. milioni 14, yaani jumla ni kama Sh. milioni 279 na ushee. Na hiyo ni kwa vitu vinavyojulikana ukiachia mbali shopping za Dubai,” alitiririka kikulacho huyo.

Baada ya kujazwa data, Paparazi wetu alijaribu kumtafuta kigogo huyo lakini licha ya juhudi zote hizo hakuweza kupatikana ndipo alipogeukiwa Diamond:

 “Sitishiki kwa lolote lile kwani huko nyuma kabla sijawa maarufu kivile enzi ya Nenda Kamwambie (wimbo) niliwahi kukaa mahabusu kwa siku kadhaa na sababu ilikuwa mapenzi kwa hiyo kwa hili siogopi kitu kwanza mimi ndiyo alinichukulia na mwana mpotevu amerudi kundini,” alisema Diamond anayekimbiza na Ngoma ya Number One.

Baada ya kumwagwa na Diamond Penny azawadiwa Keki yenye maneno 'Peni Ukome Kuchukua Mabwana wa Rafiki zako'..!!

KATIKA staili ya aina yake ya kuuaga mwaka na kuukaribisha 2014, mtangazaji Peniela Mungilwa ‘Penny’, ambaye ni zilipendwa wa Nasib Abdul ‘Diamond’ alipewa zawadi ikiwemo keki yenye maandishi ya kumsuta.
 
Peniela Mungilwa ‘Penny’.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumatano hii nyumbani kwake Mwananyamala Mwinjuma alikohamia hivi karibuni, baada ya watu wanaosadikika kuwa ni wadau wa Wema Sepetu, kufika hapo wakiwa na ‘mzigo’ huo uliojumuisha pia kadi, shampeni na maua.
 
Mmoja wa wapangaji wa nyumba anayoishi Penny, aliliambia gazeti hili kuwa msafara wa magari matatu ulifika hapo na kugonga mlango wakimuulizia mtangazaji huyo wa kituo cha televisheni cha Channel Ten.
 
Walivyofika sisi tulijua labda leo ni bethidei ya Penny, maana tuliwaona wakiwa na maua, keki, shampeni na kadi, walipomuulizia tukawaambia ametoka, wakaacha mzigo huo wakisema apewe atakaporudi,” alisema shuhuda huyo.
 
Juu ya Keki iliyopelekwa kwa mtangazaji huyo kulikuwa na maandishi yaliyomsuta na kumtaka kuachana na tabia ya kuchukua mabwana wa rafiki zake pamoja na dada zake, hali inayoonyesha kuwa waliompelekea ujumbe huo ni wabaya wake.
Juhudi za kumtafuta Penny kuzungumzia tukio hilo hazikuweza kuzaa matunda hadi gazeti hili linakwenda mtamboni.

Credit: GPL
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger