Home » , » AFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KOSA LA KUMNAJISI MTOTO...!!

AFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KOSA LA KUMNAJISI MTOTO...!!

MKAZI wa mtaa wa Nsemulwa, Athuman Mussa (54) amehukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumnajisi mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne mdomoni.


Hukumu.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Chiganga Ntegwa baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka uliongozwa na Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Ally Mbwijo.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Juni 26 mwaka jana saa 12:00 jioni nyumbani kwake katika mtaa wa Nsemulwa katika Mji wa Mpanda.

Kumnajisi Mtoto

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Ntengwa alieleza kuwa siku hiyo ya tukio mshitakiwa alimkuta mtoto huyo ambaye wazazi wake ni jirani zake akiwa anacheza na watoto wenzake karibu na nyumba yake akamwita na kuingia naye ndani akiahidi kumpatia zawadi ya pipi aina ya jojo.
Baada ya mtoto huyo kuingia ndani ya nyumba, Athumani alimvuta kwenye kochi sebuleni na kisha alimwingizia uume wake kwenye mdomo wa mtoto huyo hadi hapo alipomaliza haja yake kisha akamwamuru aondoke nyumbani kwake ndipo mtoto huyo alipotoka mbio na kurejea kwao akilia.

 Kumnajisi
Aliiambia mahakama baada ya mtoto huyo kufika nyumbani kwao mama yake alimuuliza kilichomfanya alie ndipo alitema mbegu za kiume ambazo zilikuwa mdomoni mwake na kisha alimwelezea mama yake kila kitu alichotendewa na mshitakiwa.
Baada ya mama kuelezwa unyama huo wa Kumnajisi mtoto wake, naye alianza kulia kwa nguvu na kusababisha majirani kufika nyumbani hapo ambapo walielezwa alichofanyiwa mtoto huyo ndipo majirani walikwenda nyumbani kwa mshitakiwa wakamkamata na kumfikisha kwenye kituo cha polisi Wilaya ya Mpanda Jijini DAR.
Source: Habari L

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger