Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

HUYU NDO MZEE MWENYE HATI MILIKI YA YANGA...ASEMA YEYE NDO MMILIKI HALALI WA YANGA

Mmiliki halali wa Yanga aibuka na kuidai klabu yake kutoka kwa viongozi wa sasa! Asema yeye na Tabu Mangala ndio walioisajili klabu serikalini mwaka 1967. Aongeza tokea Tabu Mangala ajitenge
na kuanzisha Pan Afrika 1975, yeye akabaki na hati zote za klabu na amekuwa akizilipia. Nini maoni yako?
Source: East Africa Television

RONALDO NDIYE MFALME WA SOKA DUNIANI KWASASA ,AWABWAGA MESSI NA RIBERY

MRENO Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka wa FIFA kwa mara ya pili katika historia yake, akimuangusha mshindani wake mkuu, Lionel Messi.
Nyota huyo babu kubwa wa Real Madrid alikuwa anakabiliwa na ushindani wa mbali kidogo kwa nyota wa Barcelona, Messi na wa Bayern Munich, Franck Ribery katika kinyang'anyiro cha Ballon d’Or. 
Akiwa mwenye hisia kali, Ronaldo aliyekwenda jukwaani kuchukua tuzo yake akiwa ameambatana na mtoto wake wa kiume, Cristiano alishindwa kujizuia na kumwaga machozi wakati anapokea taji hilo.
Namba 1: Cristiano Ronaldo ameshinda Ballon d'Or na kutajwa ndiye mwanasoka babu kubwa duniani
Family time: A tearful Ronaldo was on stage with his son Cristiano to collect the award
All smiles: Ronaldo couldn't help but grin broadly when he posed with the trophy
Hisia: Ronaldo alishindwa kujizuia na akamwaga machozi jukwaani wakati anapokea tuzo ya Ballon d'Or
Winner: Pele holds up Ronaldo's son Cristiano as the Portuguese star picks up his award
Mshindi: Pele akiwa amemshika mtoto wa Ronaldo, Cristiano wakati Mreno huyo anapokea tuzo yake

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amepewa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 66 katika mechi 56 za klabu na nchi yake, Ureno mwaka 2013 hatimaye kuirejesha tuzo yake aliyoitwaa awali mwaka 2008.
Pamoja na kwamba Ronaldo hakutwaa taji kubwa mwaka 2013, alifunga mabao yote manne Ureno ikiitoa Sweden katika kinyang'anyiro cha tiketi ya kombe la Dunia baadaye mwaka huu.
"Hakuna maneno ya kusema wakati huu," Ronaldo alisema, huku akifuta machozi. "Nataka kuwashukuru wenzangu wote na washirika pale Real Madrid, katika timu ya Ureno na familia yangu, ambako wako nami,".
"Wale ambao wananifahamu mimi, wanafahamu kwamba  watu wengi wananisaidia: kocha wangu, rais wetu, na sitaki  kusahau kumtaja Eusebio. Mpenzi wangu na mwanangu pia. Nasonga zaidi,". 
Glamorous: Ronaldo with his girlfriend Irina Shark during the awards ceremony
Ronaldo na mpenzi wake Irina Shark katika sherehe za tuzo
Nominees: The trio of Ronaldo, Lionel Messi and Franck Ribery before the ceremony
Washindani: Ronaldo, Lionel Messi na Franck Ribery kabla ya sherehe
Incomparable: Legendary striker Pele won an honourary prize at the Gala in Zurich
Gwiji Pele alipea tuzo katia usiku huo mjini Zurich
Emotional: The Brazilian couldn't keep back the tears
Emotional: The Brazilian couldn't keep back the tears
Mfalme wa soka: Gwiji wa Brazil, Pele alishindwa kujizuia kutoa machozi alipokuwa jukwaani
Out at the top: Retied Jupp Heynckes was named Coach of the Year after winning the Champions League
Retied Jupp Heynckes ameshinda tuzo kocha bora wa mwaka wa dunia baada ya kuiwezesha Bayern Muich kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya
Stunner: Zlatan Ibrahimovic won the Puskas prize for the best goal of the year for his goal against England
Mkali: Zlatan Ibrahimovic ameshinda tuzo ya Bao Bora la mwaka, maarufu kama Puskas 
Unreal: His overhead kick was during Sweden's 4-2 friendly win over England in November 2012
Bao lake tik tak Sweden ikiifunga 4-2 England Novemba mwaka 2012 ndilo bao bora la mwaka
Recognised: German keeper Nadine Angerer won the women's Player of the Year award
Kipa wa Ujerumani, Nadine Angerer ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa kike wa mwaka wa Dunia
Duo: Ronaldo and Angerer pose side-by-side after being named the best players in the world
Wawili: Ronaldo na Angerer baada ya kutajwa wanasoka bora wa dunia 
Shot stopper: Angerer in goal for the German national team during a friendly against Japan
Prize: She was part of the Germany team that won the women's European Championships last year
Taji: Angerer alikuwemo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichoshinda Kombe la ubingwa wa Ulaya kwa wanawake

WENGI WAJITOKEZA KUUGAGA MWILI WA ALIYEKUWA KOCHA WA MAKIPA SIMBA MAREHEMU JAMES KISAKA



 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kocha wa makipa wa Simba, marehemu James Kisaka likiingizwa kwenye basi la klabu hiyo, baada ya kutolewa heshima za mwisho katika misa iliyofanyika katika Kanisa la Muhimbili, Dar es Salaam. Marehemu Kisaka atasafirishwa kwenda kwao wilayani Muheza, Tanga kwa mazishi yatakayofanyika kesho.

Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio', (kushoto) akijadiliana jambo na baadhi ya wachezaji wa soka waliokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.
Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akifarijiana na mtoto wa pili wa marehemu Kisaka, Boniface baada ya kutoa heshima za mwisho.
 Ndugu wa karibu wa marehemu Kisaka akilia alipokuwa akitoa heshima za mwisho
 Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mumewe
 Mtoto wa mwisho wa marehemu Kisaka, Christopher akitoa heshima za mwisho
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, Juma Pinto (kushoto), akisalimiana na Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali.
 Wachezaji soka wa zamani wakijadiliana jambo nje ya Kanisa la Muhimbili walipokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka. Kutoka kushoto ni Madaraka Selemani, Peter Tino, Khamis Kinye, Bakari Malima na Thomas Kipese.
 Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio', (kushoto) akijadiliana jambo na baadhi ya wachezaji wa soka waliokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.
 Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu James Kisaka akisoma wasifu wa marehemu kakake
 Msanii wa filamu Jacob Steven JB akitoa heshima za mwisho
 Mchezaji wa zamani wa Simba Malota Soma akitoa heshima za mwisho kwa mchezaji mwenzie marehemu Kisaka.
 Mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula akitoa heshima za mwisho
Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu, akitoa taarisha ya usafiri wa kwenda kwenye msiba baada ya kutoa heshima za mwisho.

HUYU NDO SHABIKI WA SIMBA ALIYEFUTIA MAKALIO YAKE JEZI YA YONDANI

Shabiki mmoja wa Simba alitoa kali ya mwaka baada ya kuchukua kipande cha jezi ya beki Kelvin Yondani na kujifutia makalio.

SHABIKI WA SIMBA AKIJIFUTIA MAKALIO YAKE KIPANDE CHA JEZI YA YONDANI HUKU AKIWAONYESHA MASHABIKI WA YANGA.




Yondani aliyewahi kukipiga Simba kabla ya kutua Yanga, aliwarushia mashabiki hao jezi wakati akitoka uwanjani baada ya kupewa kadi nyekundu.


HAPA MASHABIKI HAO WAKIIGOMBEA JEZI HIYO WALIYORUSHIWA NA YONDANI, BAADAYE WALIICHANA VIPANDE KAMA INAVYOONEKANA.


Nao wakaigombea kwa takribani dakika mbili na kuichana vipande, halafu shabiki huyo akachukua kipande chake na kuanza kujifuta makalio huku akiyaelekeza kwenye upande wa mashabiki wa Yanga.

HATARII..MUONE HUYU MWANACHAMA WA YANGA AKICHOMA KADI YAKE YA UWANACHAMA LIVE...

 
Tired of humiliation! A Yanga SC fan, Khalfan Kipingu, sets his club membership card on fire after 
the Jangwani Street outfit lost 3-1 to rivals Simba in a ‘friendly’ match at the National Stadium on Saturday. Photo | Michael Matemanga



Roy Keane amponda Ferguson na Kudai kuwa ana tamaa ya Madaraka makubwa ndio maana Man utd inaboronga...!!

Nahodha wa zamani wa Manchester United, Roy Keane amesema kwamba kocha aliyeng’atuka katika klabu hiyo, Sir Alex Ferguson bado ana uchu wa madaraka. Keane aliyeondoka baada ya kukosana na klabu hiyo na pia amekuwa akitupiana maneno na Fergie amedai kwamba Ferguson anatafuta nguvu za kimadaraka na kimamlaka ili adhibiti mambo Old Trafford. Fergie alistaafu Mei mwaka huu na kumpendekeza raia mwenzake wa Scotland, David Moyes aliyekuwa Everton kuchukua nafasi yake, huku Fergie akiingia kwenye bodi kama mkurugenzi. Tangu hapo Manchester United wamefanya vibaya kwenye ligi, ambapo sasa wanashika nafasi ya tisa baada ya kupoteza mechi tano, jambo ambalo si kawaida kwao. “Kila kitu hapo 


Ferguson anafanya kwa ajili ya udhibiti na mamlaka,” anasema Keane aliyecheza hapo chini ya Ferguson tangu 1993 hadi 2005 akacheza mechi 326 kama mmoja wa viungo bora zaidi na akafunga mabao 33. “Bado anapigania kupata mamlaka hadi sasa hivi ili awe na sauti kwenye timu japokuwa sio kocha tena – kuna ubinafsi mkubwa sana unaohusishwa hapa,” anasema Keane. Mchezaji huyo wa zamani na mchambuzi wa masuala ya soka kwa sasa ni kocha msaidizi wa Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Ireland na anasema hawana tena uhusiano hata kidogo na Fergie.


g

STARS yang'olewa nusu fainali ya Kombe la CHELENJI na KENYA kwa kufungwa goli 1-0


TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' imeondolewa kwenye michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea nchini Kenya baada ya kufungwa na timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars' bao 1-0 katika mechi iliyomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Nyayo uliopo jijini Nairobi! Bao la Harambee Stars limefungwa na Miheso dakika ya 5

GHANA yapangwa Kundi la kifo kwenye droo ya Kombe la Dunia 2014..!!

Makundi yamejulikana , na pia imejulikana nani atamenyana na nani.
Hapana shaka wapenzi wa soka barani Afrika pamoja na kuomboleza kifo cha Nelson Mandela wamekuwa wanafuatilia Droo ya kombe la dunia kufahamu nani wapinzani wa timu tano zinazowakilisha bara hilo.
Cameroon wamejikuta katika kundi gumu la A pamoja na wenyeji Brazil, Mexico na Croatia.
Mabingwa watetezi Uhispania watakuwa katika kundi B pamoja na Netherlands waliokutana nayo fainali kombe lililopita, na timu zingine ni Chile na Australia.
Dua ya Ivory Coast ya kuepuka kundi gumu sana wakati huu inaonekana imesikika, wako katika kundi C pamoja na Colombia, Japan na Ugiriki.England watakuwa na kibarua kigumu kwenye kundi D ambapo wapinzani wao ni Italia, Uruguay na Costa Rica.
Kwenye kundi E Ufaransa inacheka usiku huu kwani imepangwa pamoja na Uswizi, Ecuador na Honduras.Mabingwa wa Afrika Nigeria wako katika kundi F pamoja na Argentina Iran na Bosnia Harcegovinia, ambayo inashiriki kombe la dunia mara ya kwanza.
Ghana ndiyo inayoonekana kuwa matatizoni miongoni mwa timu za Afrika. Wamejikuta katika kundi G ambapo watapamaba na na Ujerumani, Marekani na Ureno.Timu ya tano ya Afrika Algeria itakuwa kwenye kundi H na wapinzani hapo ni Ubelgji, Korea Kusini na Urusi.

Source: BBC

SIMBA wampokonya Gari KIBADENI mara baada ya kutimuliwa klabuni hapo.


ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni, amenyang’anywa gari aina ya Toyota Mark 11 GX 110 alilopewa na uongozi wa timu hiyo akiwa anakinoa kikosi hicho.
Kocha huyo hivi karibuni alisimamishwa na uongozi wa timu hiyo yeye na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, kabla ya yeye mwenyewe kutangaza kujiuzulu kuendelea kukinoa kikosi hicho.
Tetesi zilizopo hivi sasa ni kwamba, gari hilo anatarajiwa kupewa kocha mpya wa timu hiyo, Zdravok Logarusic, raia wa Croatia, aliyetua jijini Dar es Salaam jana asubuhi.
Kocha huyo anatarajiwa kukabidhi gari wakati wowote kuanzia hivi sasa, mara baada ya kukamilisha baadhi ya vitu, ikiwemo kusaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo.
Uongozi huo utampa kocha huyo gari hilo kwa ajili ya matumizi ya timu na binafsi katika mizunguko yake mbalimbali nchini.
Gari hilo analotarajiwa kupewa, awali lilikuwa likitumiwa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Milovan Cirkovic, raia wa Serbia, kabla hajatimuliwa.
Alipotafutwa Kibadeni kuzungumzia hilo, alisema: “Nimeshakabidhi kila kitu kwa Simba, sitaki kuzungumza masuala yoyote ya timu hiyo kwa sasa.”

JE UNAJUA KILICHOMTIMUA RAGE SIMBA..! SOMA HAPA..!


Kamati ya  utendaji ya klabu ya Simba iliyokutana jana usiku imempiga stop Ismail Aden Rage kuendelea na ubosi katika klabu ya Simba na kulibadilisha benchi la ufundi isipokuwa nafasi ya meneja Madaktari wa timu .
 
 Akizungumza kwa niaba ya kamati ya utendaji, mjumbe wa kamati ya utendaji Joseph Itangare amesema wamemsimamisha mwenyekiti kutokana na kufanya maamuzi yake binafsi bila kushirikisha kamati ya utendaji ikiwemo kutoitisha vikao vya kamati ya utendaji kwa mujibu wa Ibara ya 31 (1)ya katiba ya simba.
 
Kingine alichosema Itangare ni  kuwa  mwenyekiti huyo amesaini mkataba wa kukiuuza kipindi cha Simba tv bila kushirikisha kamati ya utendaji..  
"Kwa sasa lazima twende kikatiba, Mwenyekiti kama hayupo ngazi inayofatia inapanda juu na tunachagua Mjumbe mwingine ili kukaa kwenye nafasi iliyobakia, kwa muda huu wa matayarisho ya mkutano mkuu ujao mimi nitakaimu kama Mwenyekiti wa Simba na Swed atakaimu kama makamu Mwenyekiti..."Alisema  Itangare  na  kuongeza  kuwa:
"Mwenyekiti tumemsimamisha lakini tusubiri maamuzi ya mkutano mkuu ambao utafanyika kwa ajili ya marekebisho ya katiba, kuna mengine yamekiukwa hivyo yatawasilishwa kwenye mkutano mkuu tarehe 1 December.
 
"Kutokana na timu yetu kutofanya vizuri, tumeamua kwamba benchi la ufundi tulifumue ili tulijenge upya, sasa litaongozwa na kocha aliekua na Gor Mahia ZDRAVOK LOGARUSIC"

UKATILI WA KIJINSIA MBEYA, MTOTO WA MIAKA 10 ATUMIKISHWA KWA KUUZA MBOGA WAKATI WENZAKE WAPO DARASANI WAKISOMA...

Zdravko Logarusic raia wa Croatia. 

Baada ya kuwatimua makocha wake, Abdallah Kibadeni na msaidizi wake, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’, Simba sasa imemchukua kocha Zdravko Logarusic raia wa Croatia.

Tayari Simba imemaliza mazungumza na kocha huyo na anatarajia kutua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kusaini mkataba na mara moja kuanza kazi.Kabla ya hapo, Logarusic alikuwa kocha wa Gor 

Mahia ya Kenya aliyoifundisha kwa misimu miwili akisha nafasi ya pili.

Msimu huu ulikuwa wa mwisho, lakini aliondoka katikati na nafasi yake kuchukuliwa na Bobby Williamson ambaye kuna gazeti liliandika anajiunga na Simba, kitu ambacho hakikuwa sahihi.Baadaye Bobby alikanusha kuwa amefanya mazungumzo na Simba na ataendelea kubaki Kenya.

Source GPL

MBWANA SAMATTA AWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA WA AFRIKA...

  


Mtanzania anayecheza klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta.

SHIRIKISHO la soka barani Afrika CAF limetangaza majina ya wachezaji wa Kiafrika watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2013 na Mchezaji bora wa Afrika anayechezea vilabu vya ndani ya Afrika mwaka 2013.

Katika majina hayo yapo majina mawili ya wachezaji wanaotoka Afrika Mashariki ambao ni Victor Wanyama raia wa Kenya anachezea Southampton FC ya England ambaye ni miongoni mwa wachezaji 25 watakaowania tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika, huku Mbwana Samatta raia wa Tanzania anayechezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo yeye ameteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika anayechezea timu za Afrika.

Wachezaji 25 watawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika na 21 Mchezaji bora wa Afrika anachezea timu za ndani ya Afrika.

Washindi wa tuzo hizo wanatarajiwa kutangazwa Januari 9, mwaka 2014 mjini Lagos nchini Nigeria.
Orodha kamili ya wachezaji waliotangazwa na CAF na timu wanazotoka hii hapa chini.
Mchezaji wa bora wa CAF Afrika
1. Ahmed Musa - Nigeria - CSKA Moscow
2. Asamoah Gyan - Ghana - Al Ain
3.Dame N'Doye - Senegal - Locomotiv Moscow
4. Didier Drogba - Cote d'Ivoire - Galatasaray
5. Emmanuel Emenike - Nigeria - Fenerbahce
6. Islam Slimani - Algeria - Sporting Lisbon
7. John Mikel Obi - Nigeria - Chelsea
8. Jonathan Pitroipa - Burkina Faso - Stade Rennais
9. Kévin Constant - Guinea - AC Milan
10. Kwadwo Asamoah - Ghana - Juventus
11. Luís Carlos Almada Soares (platini) - Cape Verde - AC Omonia
12. Mehdi Benattia - Morocco - AS Roma
13. Mohamed Aboutrika - Egypt - Al Ahly
14. Mohamed Salah - Egypt - Basel FC
15. Nicolas Nkoulou - Cameroon - Marseille
16. Pierre-Emerick Aubameyang - Gabon - Borussia Dortmund
17. Ryan Isaac Mendes da Graça - Cape Verde - Lille
18. Saladin Said - Ethiopia - Wadi Degla FC
19. Seydou Keita - Mali - Dalian Aerbin F.C
20. Sofiane Feghouli - Algeria - Valencia
21. Sunday Mba - Nigeria - Warri Wolves
22. Victor Wanyama - Kenya - Southampton FC
23. Vincent Enyeama - Nigeria - Lille
24. Yao Kouassi Gervais 'Gervinho' - Cote d'Ivoire - AS Roma
25. Yaya Toure - Cote d'Ivoire - Manchester City

Mchezaji bora Afrika anacheza vilabu ndani ya Afrika

1. Adane Girma - Ethiopia - St George
2.Ahmed Fathi - Egypt - Al Ahly
3. Alexis Yougouda Kada - Cameroon - Coton Sport
4. Ali Machani - Tunisia - CAB
5. Bapidi Fils Jean Jules - Cameroon - Coton Sport
6. Daine Marcelle-Klate - South Africa - Orlando Pirates
7. Fakhreddine Ben Youssef - Tunisia - CSS
8. Getaneh Kebede - Ethiopia - Bidvest Wits
9. Idrissa Kouyate - Cote d'Ivoire - CS Sfaxien
10. Iheb Msakni - Tunisia - Esperance
11. Luyanda Lennox Bacela - South Africa - Orlando Pirates
12. Mbwana Samatta - Tanzania - TP Mazembe
13. Moez Ben Cherifia - Tunisia - EST
14. Mohamed Aboutrika - Egypt - Ahly
15. Rainford Kalaba - Zambia - TP Mazembe
16. Senzo Meyiwa - South Africa - Orlando Pirates
17. Soumbeila Diakite - Mali - Stade Malien
18. Sunday Mba - Nigeria - Warri Wolves
19. Tresor Mputu - DR Congo - TP Mazembe
20. Waleed Soliman - Egypt - Al Ahly
21. Yannick N'djeng - Cameroon - EST

CHANZO: BBCSWAHILI

YANGA,AZAM SASA WAKO MBIONI KUMSAJILI OKWI ..

YANGA na Azam kama zinamtaka straika wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ni fedha yao tu, lakini kuna sharti lazima walifanye.

Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) limetoa masharti na muongozo wa klabu zinazomtamani mchezaji huyo aliyesitisha mkataba na Etoile du Sahel ya Tunisia.

Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba aliiambia Mwanaspoti kuwa: “Hakuna kinachoizuia klabu kutaka kumsajili Okwi, cha muhimu wanatakiwa kuongea na Etoile du Sahel ya Tunisia, wakimalizana nao basi watamchukua, hivyo ni ruksa cha muhimu ni kufuata sheria na haki.”

Okwi ameidhinishwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuichezea SC Villa ya Uganda kwa muda wa miezi sita huku sakata lake la Etoile likifanyiwa ufumbuzi.

Mchezaji huyo anaidai Etoile malimbikizo ya mishahara pamoja na dau lake la usajili huku Simba iliyomuuza kwa Waarabu hao nayo ikidai dau lake Sh 480 milioni.

Suala hilo lipo Fifa na Kawemba amewahakikishia Simba kwamba wasiwe na wasiwasi watapata haki yao.

MAJANGA TENA KWA MAN UNITED! WELBECK ASUBIRIA UPASUAJI ....!!

KLABU ya Manchester United lazima iamue kumpeleka Danny Welbeck kufanyiwa upasuaji wa goti ambao utamuweka nje mshambuliaji huyo wa England kwa wiki nyingine tano.
United tayari inamkosa kiungo Michael Carrick, ambaye atakuwa nje hadi Krisimasi kwa majeruhi.
Majeruhi: Danny Welbeck atalazimika kufanyiwa upasuaji wa goti ambao utamuweka nje kwa wiki nyingine tano
Blow for United: Michael Carrick is sidelined until Christmas with an achilles injury
Pigo United: Michael Carrick atakuwa nje hadi Krisimasi kwa majeruhi

Matatizo yanayomsumbua Welbeck tayari yamemfanya amekosa mechi sita zilizopita za United. 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anapatiwa matibabu yanayompa matumaini anaweza kuepuika upasuaji, lakini United inahofia italazimika kumpeleka kwenye upasuaji ikiwa hali yake haitaimarika.
Welbeck amekwishafanyiwa upasuaji wa goti mara mbili. Marouane Fellaini pia anaweza kuwa nje kwa wiki hadi 10 atakapofayiwa upasuaji wa mguu wake wa kulia.
Stroll: Carrick walked all 18 holes at the DP World Tour Championship in Dubai
Carrick alikwenda kwenye ziara ya mashindano ya dunia ya DP Dubai
Michael Carrick
Michael Carrick
Carrick aliungana na Caroline Wozniacki kumtazama Rory McIlroy akicheza
Crunch time: David Moyes will be without Carrick and possibly Welbeck for games with Spurs and Everton
David Moyes atawakosa Carrick na Welbeck katika mechi na Spurs na Everton


 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger