Showing posts with label maajabu. Show all posts
Showing posts with label maajabu. Show all posts

TAZAMA MAAJABU...!HUYU NDIYE DADA ANAYETOKA MACHOZI NA JASHO LA DAMU.ANGALIA PICHA NA STORY YAKE



Miaka minne iliyopita msichana huyu mwenye umri wa miaka 19, Delfina Cedeno, alianza kupata tatizo hili la ajabu, lililokuwa likimfanya alie na kutoka jasho la damu. Kwa kuongeza zaidi, wakati mwengine damu zimekuwa zikitoka hata kwenye kucha na kitovu.ANGALIA PICHA ZAIDI







Hali hii ilipomuanza, alianza kwa kulia machozi mekundu, kutokwa na damu puani na kunyunyukwa nywele kichwani.

Hali ilipokuwa mbaya, alikuwa akienda hedhi kwa siku 15 mpaka ikafika kipindi alihitaji kuongezwa damu kutokana na hali hiyo iliyokuwa ngumu. Licha ya vipmo vingi alivyofanya, madaktari wa mji wake wa Veron, kwenye Jamhuri ya Dominica, walishindwa  kumsaidia.

Cedeno alisema: 'Hali hii ilipoanza kwangu sikuwa najua nini cha kufikiri - nilishtushwa na kuogopa.

Anasema alijisikia vibaya kutokana na hali aliyokuwa nayo mpaka ikambidi aondoke nyumbani kwao alipokuwa akiishi na mama yake aitwaye Mariana, 36.

Aliacha shule huku marafiki zake wengi wakimtenga kutokana na hali hiyo wakihofu kupata maambukizo au usumbufu kutokana na hali yake.

'Nilitengwa, ila Mungu mkubwa. Kwa sasa najisikia poa maana baada ya muda mrefu nimeanza kujisikia vizuri.'

Miezi michache baadae alifanikiwa kupata boyfriend, Recaris Avila, ambaye alimtembelea hospitali mara baada ya kusikia stori yake.





Sasa, miaka minne baada yote kuanza, madaktari wa wamefanikiwa kutatua tatizo lake.




MAAJABU ...!! TAZAMA KIATU CHENYE AC NDANI...!

7 Hydro-Tech ambayo ni kampuni ya Japan ndio imetengeneza hiki kiatu ambacho bei yake ni dola za Kimarekani 75 ambazo ni kama laki moja na 20 za kibongo. As MobileMag explains, the way these shoes work is a bit different from our conventional understanding of “air conditioning”: The shoes don’t have a mini air conditioner integrated inside, but rather rely on a new filter technology that releases heat and humidity and allows air to flow, for your feet to feel refreshed and clean 4 1

MAAJABU...!! HII NDIO MASSAGE INAYOFANYWA KWA KUTUMIA NYOKA HUKO NCHINI INDONESIA..! TAZAMA PICHA

Unapenda kufanyiwa massage na nyoka? Unaweza kukaza roho na usiogope kung’atwa? Kama ndio basi nenda nchini Indonesia utaipata kwa raha zako.
snake-spa-2

Massage hiyo inapatikana Bali Heritage Reflexology and Spa huko Jakarta, Indonesia ambako wanaweza kukuondolea uchovu wako wa siku nzima kwa massage ya nguvu inayofanywa na nyoka mkubwa.
snake-spa-1
Massage hiyo inafanyika kwa nyoka huyo kuwekwa juu ya mwili wa mteja na mengine huachiwa yeye nyoka afanya yake. Ili kupata huduma hii mteja hutakiwa kulipa dola 47 ambazo ni zaidi ya shilingi 76,000 za Tanzania.

kutoka- Bongo5.com

MAAJABU YA DUNIA...! VIDEO: MTAZAME MCHUNGAJI ALIYEWEKWA KWENYE RECORD YA DUNIA KUTOKANA NA KUPIGA DRUMS SET NYINGI KWA WAKATI MMOJA..

Dr. Mark Temperato (aka Rev M) – Creator of the largest drum-set

“I am so grateful and honoured. It has been a labour of love and one of my greatest pleasures. It gives me a chance to encourage others to make some history and do something worthy of world recognition.” maneno haha alinukuliwa akisema 
TAZAMA VIDEO YAKE HAPA...
 

HAIJAWAHI KUTOKEA,HII NDIO MELI KUBWA AJABU ILIYOTUA BANDARI YA DSM NCHINI TANZANIA...!! Itazame hapa..

Meli ya Maersk Line. 

BIASHARA katika bandari ya Dar es Salaam imeanza kushika kasi huku Watanzania wakitarajia kunufaika na punguzo la bei ya bidhaa kutoka nje baada ya meli kubwa yenye urefu wa meta 249 kuanza kutia nanga katika bandari hiyo. 


Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa propaganda kuwa bandari hiyo haina uwezo wa meli zenye ukubwa huo wenye kubeba makontena 4,500 kutia nanga, lakini jana Tanzania iliandika historia kwa meli hiyo kutia nanga asubuhi. 

Meli hiyo ya Maersk Line ilitia nanga ikiwa inaendeshwa na kapteni wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Abdul Mwingamno ambaye alielezea wazi kuwa hakupata tatizo lolote kutia nanga.
Ikiwa katika safari huonekana hivi. 
 
Kutia nanga kwa meli hiyo kulishuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe na kusema kuwa kuanza kutia nanga kwa meli hizo kubwa kutaongeza mizigo kupitia katika bandari hiyo. 
 
“Kwa sasa biashara inazidi kuchanganya kwani nchi za Zimbabwe na Kongo wanapitisha mizigo yao hivyo kwa kutumia meli hizo kubwa gharama zitapungua zaidi ya kuongeza nchi kutumia bandari hiyo,” alisema. 
 
Akizungumzia meli hiyo kutia nanga bandarini, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande alisema kila kitu kinawezekana iwapo kila mtu atafanya juhudi na kuwajibika. 
 
Alisema changamoto watakayokutana nayo sasa ni vifaa vya kupakulia kuendana na ukubwa wa meli ili kuweza kupunguza muda wa kushusha shehena na hivyo kuondoa misongamano bandarini. 
 
Alisema kulikuwa na propaganda ya kuwa meli za ukubwa huo haziwezi kutia nanga katika bandari hiyo hivyo kuishia Mombasa, Kenya na meli ndogo kubeba mizigo mpaka bandarini hapo. 
Pia Madeni alizungumzia mgomo wa malori na kusema ulisababisha mlundikano wa mizigo hivyo kusababisha hasara ya Sh bilioni 1.5 na mpaka jana asubuhi, bado kulikuwa na meli 18 zikisubiri huku tisa zikipakua mzigo. 
 
Alisema wamekuwa katika hatari ya hasara zaidi kwa uchumi kwani idadi kubwa ya mbolea ambazo ni hatari iwapo zingenyeshewa, kwani zilishindwa kusafirishwa. 
 
Naye Meneja mwendeshaji wa kampuni hiyo ya Maersk Line, Amos Mwansumbule alisema meli hiyo iliyotokea katika nchi za Asia na kupitia Afrika Magharibi na kutia nanga Angola, ilisafiri kwa siku 10 kutoka nchini humo hadi Dar es Salaam na ilitarajia kukaa bandarini hapo kwa saa nane.
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger