Showing posts with label mauaji. Show all posts
Showing posts with label mauaji. Show all posts

TAZAMA PICHA ZA WATUHUMIWA WALIOHUSIKA KATIKA MAUAJI YA BILIONEA ERASTO MSUYA WAKIWA MAHAKAMANI KWA AJILI YA KESI YA MAUAJI..!!


Mtuhumiwa namba 8 katika kesi ya mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini ya
Tanzanite Erasto Msuya, aliyekamatwa hivi karibuni Ally Musa "Majeshi"
akipelekwa katika chumba cha mahakama ya hakimu mkazi mjini Moshi kwa
ajili ya kuunganishwa na watuhumiwa wenzake katika kesi hiyo.
Mtuhumiwa namba mbili, Shaibu Shaibu Jumanne Saidi maarufu kama Mredi(38) anayetuhumiwa kushiriki Mauaji ya mfanyabiashara wa madini Erasto Msuya wakipelekwa katika jengo la mahakama.
Mmoja wa askari akijaribu kutoa maelekezo kwa mtuhumiwa wa mauaji ya
mfanyabiashara wa madini Erasto Msuya wakati akielekea chumba cha
mahakama ya hakimu mkazi mjini Moshi.
Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa nje ya jengo la mahakama ya
hakimu mkazi mjini Moshi wakitizama watuhumiwa wa mauaji ya ndugu yao.
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini Erasto Msuya
wakitolewa katika chumba cha mahakama mara baada ya kuahirishwa kwa
shitaka linalo wakabili.
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini Erasto Msuya
wakitolewa katika chumba cha mahakama mara baada ya kuahirishwa kwa
shitaka linalo wakabili.
Mtuhumiwa namba mbili, Shaibu Shaibu Jumanne Saidi maarufu kama Mredi (38) anayetuhumiwa kushiriki Mauaji ya mfanyabiashara wa madini Erasto Msuya, akisaidiwa kupanda katika gari mara bada ya kuahirishwa kwa shitaka linalo wakabili. 
MTUHUMIWA “Muhimu” katika kesi ya mauaji ya Bilionea wa madini ya Tanzanite, Erasto Msuya (43), Ally Mussa “Majeshi” (42) amepandishwa mahakamani LEO katika Mahakama ya hakimu mkazi Moshi, mkoani Kilimanjaro. 

Mtuhumiwa huyo aliyekamatwa Oktoba 8, mwaka huu, alinaswa mkoani Kigoma akijaribu kutorokea nchini Burundi baada ya kufanikiwa kukimbia mitego ya polisi katika mikoa ya Arusha, Dodoma na Mwanza na kurudishwa mkoani kilimanjaro ambapo jana aliunganishwa katika kesi ya Mauaji ya Msuya.

Akisoma Mashtaka yanayomkabili Mtuhumiwa huyo mbele ya Mahakama ya Hakimu Munga Sabuni, Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali, Janet Sekule alisema Mshtakiwa huyo pamoja na wenzake Saba, wanashtakiwa kwa kosa la kuua kwa kukusudia kinyume cha kinyume cha kanuni namba 16,kifungu cha 196 ya sheria za makosa ya jinai, “Kinyume cha sheria ya makosa ya jinai, kanuni ya 16, kifungu cha 196, Ally Mussa au kwa jina lingine Majeshi, walimuua Erasto Msuya katika maeneo ya Mjohoroni, njia panda ya Arusha na KIA kwa kumpiga risasi,” alisema Sekule.

Aidha baada ya kusoma maelezo ya shtaka hilo, upande wa Jamhuri, ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Janet Sekule iliiomba Mahakama ya Hakimu Sabuni kuipa muda kuweza kukamilisha upelelezi ambapo kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 28, mwaka huu, itakapo tajwa tena. 

Ally Mussa “Majeshi”, anayedaiwa kuwahi kulitumikia Jeshi la kujenga Taifa (JKT), kabla ya kufukuzwa anaungana na Sharif Mohamed Athuman (31) mchimbaji mdogo wa madini na mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, Shaibu Jumanne Saidi maarufu kama Mredi (38), mkazi wa Songambele Wilaya ya Simanjiro. 

Wengine ni Joseph Damas Mwakipesile maarufu kama Chusa (36), mfanyabiashara wa madini na mkazi wa Arusha, Jalila Zuberi Said (28), mkazi wa Babati, Sadiki Mohammed Jabir ‘Msudani’ au ‘Mnubi’(32), mkazi wa Dar es Salaam na Lang’ata wilayani Hai na Karim Kihundwa (33) mkazi wa Kijiji cha Lawate Wilaya ya Siha na Mussa Juma Mangu (30), mkazi wa Shangarai kwa Mrefu mkoani Arusha. 

Hata hivyo Mwandishi wa Habari hizi alishuhudia kesi hiyo ikisomwa katika hali ya utulivu tofauti na ilivyozoeleka kwani katika mara zote kesi hiyo ilipofikishwa Mahakamani hapo kulikuwa na umati mkubwa wa watu wakiwemo ndugu za Marehemu Erasto Msuya.

Mfanyabiashara Erasto Msuya, aliuawa Agosti 7, mwaka huu majira ya 6:30 mchana kwa kupigwa risasi 13 kifuani, kando ya barabara kuu ya Arusha– Moshi katika eneo la Mjohoroni, Wilaya ya Hai, karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Credit: kijiwe

KUFUATIA KUPIGWA RISASI KWA UFOO SARO, MAZITO YAIBUKA...!!!

 MAZITO yameibuka kufuatia kupigwa risasi kwa Mtangazaji wa Independent Television (ITV), Ufoo Saro na mtu anayedaiwa ni mzazi mwenzake, Ateri Mushi, Risasi Mchanganyiko lina mkanda mzima. 
Ufoo alipigwa risasi na mwanaume huyo na kujeruhiwa tumboni na mguuni katika tukio lililotokea Oktoba 13, mwaka huu nyumbani kwa mama yake mzazi, Anastazia Saro, Kibamba, Dar es Salaam kufuatia kutoelewana kati ya wawili hao. 
Katika tukio hilo la kutisha, Ateri pia alimuua kwa risasi mama wa Ufoo na kujiua mwenyewe na maiti zao kupelekwa Muhimbili.


MAZITO YALIYOIBUKA
Juzi, Shekilango, Ubungo jijini Dar, Risasi Mchanganyiko lilizungumza na rafiki mmoja wa marehemu Ateri aliyejitambulisha kwa jina moja la Urassa ambaye aliweka wazi mambo anayoyajua kuhusu marehemu kabla ya kujiua kwa risasi.
Alisema tangu mwaka huu (2013) uanze, marehemu Ateri alikuwa akilalamika kwamba, anampenda sana Ufoo lakini hamuelewielewi.
“Tangu mwaka huu ulipoanza nimekuwa nikiwasiliana na Ateri. Alikuwa akisema anampenda sana Ufoo lakini kama hamuelewielewi katika mambo fulani ya uhusiano.
“Alisema kukaa kwake mbali (Sudan) na mchumba wake huyo anahisi kama mambo yanakwenda kufikia mwisho wa uchumba wao. Kwa jumla Ateri alishajua nini atakifanya mwaka huu kuhusu uhusiano wake na yule mtangazaji maana maneno yake mengi yalikuwa ni malalamiko tu,” alisema Urassa.

MAREHEMU ALISEMA AMECHOKA KUISHI
Akienda mbele zaidi, Urassa alisema Septemba, mwaka huu marehemu alimpigia simu na kumwambia anahisi amechoka kuishi kwenye dunia hii yenye maumivu ya mapenzi kila kukicha.
“Nilimuuliza amechoka kuishi kivipi? Akanijibu anaona kuna mambo hayaendi sawa kama anavyotaka yeye kwa huyo mchumba wake. Lakini kwenye simu hakuniambia kama hayo mambo ni yapi? Ila nahisi ni mapenzi yao,” Urassa alizidi kutoboa.

ALIIBUA TABIA YA KUPENDA KUSALI
Katika mazungumzo na Urassa, pia alimgusia marehemu kwamba kwa siku za karibuni aliibua tabia ya kusali kila wakati kuliko siku za nyuma.
“Siku moja akiwa Sudan alinipigia simu, akasema anapenda kama mahali anapoishi kule pangekuwa na kanisa karibu ili awe anasali alfajiri, mchana na jioni lakini akaniambia kule hakuna makanisa.
“Nilimuuliza mbona amepanga kusali mara tatu zote hizo kwa siku, akanijibu binadamu tunatakiwa kujiandaa kwani saa yoyote roho inaweza kutoka,” alisema Urassa. 

MAREHEMU ALIKUWA AKILIA WIVU
Risasi Mchanganyiko: Kwa hiyo unawaza nini kuhusu marehemu kumuua mama mkwe wake na kumjeruhi mchumba wake kisha na yeye kujimaliza?
Urassa: Kwa kweli ninavyojua mimi ni wivu tu. Unajua yule alikuwa yuko kikazi Sudan, mchumba wake yupo Dar. Mfano siku moja aliniambia anatamani apate mtu wa kumfuatilia Ufoo kwenye nyendo zake za kila siku kwani anahisi anaibiwa japo hakuniambia kama ana uhakika.

DALILI ZA MAUAJI ZILIONEKANA MAPEMA
Kwa mujibu wa ndugu, licha ya kwamba hawakujua litakalotokea mbele, lakini baada ya kutokea ndiyo wamebaini kwamba marehemu Mushi alishabadilika roho muda mrefu.
Walisema uchangamfu na utani aliokuwa nao siku za nyuma alipokuwa akienda kuwatambelea viliisha ghafla kwani hivi karibuni alikuwa akienda, baada ya salamu hakuwa akiongeza neno.

LENGO LA MAREHEMU
Kwa mujibu wa watu waliofika nyumbani kwa mama Ufoo mapema, marehemu alionesha dalili za kuteketeza familia hiyo.
“Huyu bwana (marehemu) nahisi alitaka kutekeza familia, maana kabla ya kujiua yeye, alipiga risasi mtungi wa gesi ukiwa na nguo, ukalipuka. Sasa hapo unadhani lengo lake lilikuwa nini kama si kuiangamiza familia yote ya mzee Peter Saro?” alisema jirani mmoja kwa mtindo wa kuhoji.

UFOO ALILIJUA HILO
Habari zinasema baada ya Ufoo kupigwa risasi, akiwa anatambaa na damu zake tumboni aliwataka ndugu zake kutotoka kwani shemeji yao alikusudia kuwaua wote. Kauli ya Ufoo inakwenda sambamba na madai ya mzee aliyesema dhamira ilikuwa kuiangamiza familia hiyo. 

ALIKUWA HAELEWANI NA BABA WA UFOO
Godluck Saro ni mdogo wa Ufoo, yeye akizungumza na gazeti hili juzi, nyumbani kwao, Kibamba, Dar alisema marehemu shemeji yake alikuwa haelewani kabisa na baba wa Ufoo, marehemu mzee Peter Saro aliyefariki dunia Julai 16, 2011 kwa shinikizo la damu.
“Kwanza shemeji alianza kufika hapa nyumbani baada ya baba kufariki, kabla ya hapo alikuwa hafiki maana walikuwa hawaelewani kabisa. Baba alikuwa anasema shemeji ni mkorofi, hawezi kuwa mume wa dada,” alisema kijana huyo.  

MAJIRANI WA KWA UFOO
Juzi, Risasi Mchanganyiko lilipata bahati ya kuzungumza na baadhi ya majirani wa kwa Ufoo, Mbezi jijini Dar es Salaam ambapo karibu wote walidai kusikia majibizano ya muda mrefu usiku wa kuamkia siku ya tukio.
“Tulisikia majibizano kwa muda mrefu ule usiku, lakini si ya wazi sana kiasi cha kumfanya mtu ajue nini kilikuwa kinaongelewa,” alisema jirani mmoja.
“Mimi alfajiri wakati wanaondoka niliwasikia, lakini sikujua wanakwenda wapi na nilijua wapo na amani tu kwani hakukuwa na mazungumzo ya ugomvi,” alisema jirani mwingine.

UFOO NA MAREHEMU
Ufoo yeye bado amelazwa Hospitali ya Muhimbili kwa matibabu. Yeye na marehemu walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume, Alvin Ateri Mushi.

MAZISHI YA WOTE
Juzi, ndugu wa marehemu Mushi walikutana katika kikao cha ratiba ya mazishi pale 92 Hotel, Shekilango - Ubungo, Dar ambapo walisema mwili wa marehemu utasafirishwa kabla ya Ijumaa kwenda kijijini kwao Uru, Moshi kwa mazishi.
Mwili wa marehemu Anastazia ulitarajiwa kusafirishwa jana kwenda Machame, Moshi ambapo mazishi yake yalipangwa kufanyika leo katika eneo hilo.

Mwenyezi Mungu aziweke pema peponi roho za marehemu. Amina.

-GPL
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger