Kanali Makenga alizoea kutembea na bakora, ishara kuwa alikuwa mfugaji na pia kamanda wa kijeshi aliyetaka majeshi yake kuwa na nidhamu na kumtii.
Showing posts with label WAASI. Show all posts
Showing posts with label WAASI. Show all posts
HUU NDIO WASIFU WA KAMANDA MKUU WA WAASI WA M-23 KANALI MAKENGA....USOME HAPA...!!
Kanali Makenga alizoea kutembea na bakora, ishara kuwa alikuwa mfugaji na pia kamanda wa kijeshi aliyetaka majeshi yake kuwa na nidhamu na kumtii.
Mrefu
na mwembamba , Makenga alikulia katika maeneo ya milimani mkoani Kivu
Kusini ndani ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, na alisifika sana kwa
kuwa mlenga shabaha na mtu mwenye maarifa na mwenye ujuzi wa kupanga
mambo ya kijeshi.
AL SHABAAB TENA!!!: 'WAKIRI KUHISIKA KULIPUA HOTELI....WATU 6 WAUWAWA....SOMA ZAIDI
Wapiganaji wa Kiislam wa Al Shabaab nchini Somalia
Wapiganaji
wa Kiislamu wa Al Shabaab nchini Somali wamesema wao ndio waliotekeleza
shambulizi la bomu la kujitoa muhanga nje ya hoteli katika mji mkuu wa
Mogadishu nchini Somalia ambapo watu sita waliuawa wakiwemo maafisa wa
polisi.
Kundi hilo la Al Shabaab ambalo lilifurushwa na majeshi ya Somalia yakishirikiana na yale ya Umoja wa Mataifa AMISOM miaka miwili iliyopita wameapa kuendeleza harakati zao za kufanya mashambulizi.
Hapo awali Waziri wa Mambo ya ndani wa Somalia Abdikarim Hussein Guled aliiambia BBC kuwa watu sita waliuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika shambulio hilo la kujitoa muhanga.
Mwandishi wa BBC Ibrahim Mohamed Adan ambaye yupo Mogadishu amesema sauti ya mlipuko ulisikika katikati ya mji huo wa Mogadishu.
-BBC
WAASI WA M23 WAAMUA KUSALITI AMRI MARA BAADA YA KUELEMEWA HUKO MASHARIKI YA CONGO..!!
Wanajeshi wa serikali katika Jmauhuri ya kidemokrasi ya Congo, wanashambulia ngome ya mwisho ya waasi wa M23 katika maeneo ya milimani ,msituni Mashariki mwa nchi.
Mamia ya wakimbizi wanatoroka vita karibu na mpaka wa Mashariki mwa Congo na kuingia nchini Uganda.
Viongozi wa kundi hilo la M23 walitoa wito kwa wapiganaji wao kusitisha vita na kuruhusu mazungumzo ya amani na serikali.
Kiongozi wa wapiganaji hao Mashariki mwa nchi ametangaza kuwa watasitisha mapigano katika vita vyao na jeshi la serikali.
Bertrand Bisimwa alisema kwenye taarifa kwamba anawasihi wapiganaji wote haraka waache uhasama na wanajeshi, ili kuwezesha mazungumzo ya amani kuendelea.
Wanajeshi wa serikali, wakisaidiwa na kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa Mataifa, hivi karibuni wamewasukuma nyuma wapiganaji na kuwatoa katika ngome zao nchini.
Mazungumzo ya amani yanafanywa mjini Kampala, Uganda.