Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Showing posts with label ELIMU. Show all posts

UPDATE: MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YATANGAZWA RASMI LEO...!! YATAZAME HAPA..


Baraza la Mitihani la Tanzania limetangaza matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 na kiwango cha ufaulu Kimeongezeka kwa asilimia kati ya 0.61 na 16.72 ukilinganisha na mwaka 2012. 

Jumla ya watahiniwa laki 235,227 sawa na asilimia 58.25 ya waliofanya mtihani wamefaulu.  

Wanafunzi 74,324 sawa na asilimia 21.09 wamefaulu katika madaraja ya I -III.

Wavulanawaliopata daraja la kwanza (division one) ni 5,030 na wasichana ni 2,549 
 
Waliopata daraja la pili (Division 2) Wavulana ni 14,167 na wasichana ni 7,561

Waliopata daraja la pili (Division 2) Wavulana ni 14,167 na wasichana ni 7,561.  Wavulana waliopata daraja la tatu (Division 3) ni 27,904 na wasichana ni 17,113.

Jumla ya wanafunzi waliopata daraja la 4 (division 4) ni laki 126,828, wasichana wakiwa 62,841 na wavulana 63,987. 
 
Jumla ya wanafunzi laki 151,187 wamepata '0' (division ziro) . Wasichana ni 72,237 na wavulana ni 78,950.



 Bofya  hapo  juu  kuyatazama

YABAINIKA..!! MTIHANI WA KIDATO CHA NNE- 2013 WAVUJISHWA..!! HII NI AIBU KWA TAIFA..

 

















MTIHANI wa Taifa wa Kidato cha Nne, umeingia dosari baada ya walimu wawili akiwamo Mkuu wa Shule, kushikwa wakishiriki kutoa majibu kwa wanafunzi wao.


Tayari Polisi mkoani Singida, inashikilia walimu hao wa Sekondari ya Nkinto wilayani Mkalama kwa tuhuma ya kuvujisha mtihani huo unaoendelea kufanyika nchini kote hivi sasa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, alitaja watuhumiwa hao kuwa ni Mkuu wa Shule, Monica Sebastian (30) na msimamizi wa mtihani huo, Agaloslo Otieno (32).
Alisema watuhumiwa hao walivujisha mtihani huo juzi kati ya saa 3 na 3:30 asubuhi katika shule hiyo iliyopo Kata ya Mwangeza Tarafa ya Kirumi.
Alidai kuwa Mwalimu Agaloslo aliyekuwa akisimamia mtihani katika shule nyingine ya Mwangeza, aliandika baadhi ya maswali ya Kiswahili na Uraia kwenye simu yake ya mkononi na kumtumia Mkuu wa Shule yake ya Nkinto, Monica aliyekuwa shuleni kwake.
Baada ya Monica kupata maswali hayo, inadaiwa alitafuta majibu akiwa chooni huku wanafunzi wakimfuata huko huko na kupewa majibu.
Kamanda Kamwela alisema lengo lao lilikuwa kusaidia wanafunzi, wafanye vizuri katika mtihani wao wa kidato cha nne mwaka huu. Alisema wanafunzi waliishaambiwa wadanganye wanakwenda chooni, ili wakapewe majibu na Mkuu wa Shule.
"Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa uvujishaji huo ulifanyika kwa nyakati tofauti kati ya Monica na Mwalimu Agaloslo akiwa anasimamia mtihani huo katika shule tofauti.
“Baada ya Mkuu wa Shule kutumiwa maswali, alijificha chooni na watahiniwa kwa nyakati tofauti waliomba ruhusa kwa wasimamizi kwenda kujisaidia na hapo walimkuta Mkuu wa Shule na kuwapa maelekezo ya namna ya kujibu maswali hayo," alisema Kamanda Kamwela.
Alisema baada ya Polisi kupata taarifa ya siri kutoka kwa wasamaria, iliweka mtego katika Sekondari ya Nkinto na kumkamata Mwalimu Monica huku simu yake ikiwa na baadhi ya maswali ya mtihani.

-Habari Leo

MULUGO "HATUJAFUTA ALAMA SIFURI MATOKEO YA MITIHANI "

Dodoma.Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema Serikali haijafuta daraja sifuri katika matokeo ya mitihani taifa ya shule za sekondari na kwamba ilichokifanya ni kuondoa mrundikano wa madaraja.

Mulugo aliyasema hayo jana bungeni, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Magige (CCM).

Magige alitaka kufahamu kama kushusha madaraja ni suluhisho la kuwaokoa vijana waliofanya vibaya katika mitihani ya kidato cha nne mwaka jana.

Mapema katika swali lake la msingi, Magige, alitaka kufahamu kama Serikali ina mkakati wa kuanzisha mpango maalumu hasa wa ufundi kwa wanafunzi waliofanya vibaya katika mitihani ya kidato cha nne mwaka jana.

Akijibu swali hilo, Mulugo alisema hawajashusha madaraja wala kuweka viwango tofauti na ilivyokuwa awali.

“Tumeongeza madaraja ili kuwatambua watoto, kulikuwa na mrundikano katika daraja moja. Serikali haijafuta division ziro na wala hakuna division V, ipo division I, II,III, IV na ziro kama kawaida,” alisema.

Alisema uamuzi wa kushusha madaraja, hauna lengo la kuwaokoa wanafunzi wanaofanya vibaya na badala yake, unalenga katika kuondoa mrundikano wa alama katika daraja moja.

Alitoa mfano wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kuwa lilikuwa linapanga daraja F kuanzia alama 0 hadi 34.

Alisema kulikuwa hakuna ufuatiliaji wa maendeleo ya mwanafunzi kama kanuni inavyosema kuwa lazima kuwe na ufuatiliaji wa asilimia 50 kwa 50 .

Alisema kanuni hiyo inataka kutunzwa kwa alama 50 katika ufuatiliaji wa maendeleo ya mwanafunzi na katika mtihani ya kumaliza shule asilimia 50.

Alisema wameanza kuyaweka madaraja kwa kutofautiana kwa alama 10 kila daraja.

Alisema bado daraja la ufaulu litaendelea kuwa 40 ama alama C.


ata hivyo, baada ya kumaliza kujibu swali hilo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, aliiagiza Serikali kupeleka bungeni kauli ya waziri kuhusiana na suala hilo.

“Naibu Waziri nenda mtuletee kauli ya Serikali kuhusiana na utaratibu huo ili kupata majibu yanayoridhisha,” alisema

Kuhusu wanafunzi waliofanya vibaya mwaka jana katika mitihani yao, Mulugo alisema Serikali haitaanzisha mpango maalumu wa ufundi kwa vijana hao.

Alisema badala yake, Serikali inawashauri wazazi kuwashawishi watoto kurudia mtihani wa kidato cha nne.

Kwa mujibu wa Mulugo, kwa mwaka huu, jumla ya watahiniwa 60,507 wa kujitegemea wamejisajili kufanya mtihani wa kidato hicho.

HATIMAYE MATOKEO DARASA LA SABA YATANGAZWA,KIWANGO CHA UFAULU CHAPANDA,BOFYA HAPA KUYATAZAMA

Dar es salaam Tanzani Matoke ya Darasa la Saba yametangazwa hivi punde hivi punde na mwaka huu ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 30.72 mwaka jana mbaka asilimia 50.61 mwaka huu kutokana na wanafunzi walio fanya mtihani mwaka huu wa darasa la saba wamefaulu zaidi ukilinganisha na wanafunzi wa mwaka jana Kaimu mtendaji wa Baraza la Mtihani Charles Msonda amesema ufauru katika masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya 6.01 na 28.06 ukilinganisha na mwaka 2012 Mwaka huu watainiwa wamefahulu zaidi katika somo la Kiswahilin kwa asilimia 69.06 na somo walilio faulu kwa kiwango kidogo zaidi ni somo la Hisabati wamefaulu kwa asilimia 28.62 Msonda amesema jumla ya watahiniwa 427,606 kati ya 844,938 walio fanya mtihani huo wamepata alama ya 100 kati ya alama ya 250 idadi hiyo nisawa na asilimia 50.61
                               <<BOFYA HAPA KUYATAZAMA MATOKEO HAYO>>
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger