Showing posts with label Afya. Show all posts
Showing posts with label Afya. Show all posts

Taarifa ya Dk. Kitila Mkumbo kwa Umma kuhusu Kuvuliwa nafasi za mamlaka ndani ya CHADEMA


Taarifa ya Dk. Kitila Mkumbo kwa Umma kuhusu Kuvuliwa nafasi za mamlaka ndani ya CHADEMA

1. Katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kilichofanyika tarehe 20-22 Novemba 2013, pamoja na mambo mengine, kulijadiliwa waraka wa siri unaojulikana kama Mkakati wa Mabadiliko 2013. Waraka huu ulilenga kujenga hoja ya kufanya mabadiliko ya uongozi na kuanisha mikakati ya ushindi kwa mgombea mlengwa katika uchaguzi mkuu ndani ya CHADEMA. Nilikiri kuwa nilikuwa naufahamu waraka huu, na kwamba nilishiriki kuuandaa na kuuhariri, na kwamba mimi ni mmoja wa wanachama wanaoamini kwamba kuna haja ya kubadilisha uongozi wa juu wa chama katika uchaguzi ujao ndani ya chama.

2. Katika mjadala, maudhui ya waraka huu yalionekana kwa wajumbe kwamba yalikuwa na mapungufu na yalikiuka misingi na kanuni zilizoanishwa katika Katiba ya Chama. Kwa kuwa katika chama cha siasa hoja za watu wengi ndizo hupewa uzito, na kwa kuwa dhamira na nia yangu ndani ya chama hiki imekuwa ni kusukuma mabadiliko ambayo watanzania wanayatazamia nje ya mfumo wa sasa wa utawala, nilikiri makosa yangu na kuwaomba msamaha wajumbe wa Kamati Kuu na viongozi wakuu wa chama, na kueleza kwamba nilikuwa tayari kujiuzulu na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida. Wajumbe walikataa kukubali ombi langu la kujizulu bali walipitisha azimio la kunivua mimi na Mhe. Zitto Zuberi Kabwe nafasi zetu za uongozi. Nilipokea kwa unyenyekevu adhabu ya kuvuliwa nafasi zote za mamlaka nilizokuwa nazo ndani ya chama hiki na kueleza kuwa nitaendelea kutoa mchango wangu kama mwanachama wa kawaida hadi hapo chama kitakapoona ninafaa kukitumikia katika nafasi yeyote.

3. Kufuatia mkutano wa waandishi wa habari siku ya Ijumaa tarehe 22 Novemba 2013 ambapo, pamoja na mambo mengine, ilielezwa na viongozi wa CHADEMA kwamba mimi na wenzangu (Samson Mwigamba na Zitto Kabwe) tumehujumu chama na tumefanya uhaini kwa kuandaa mkakati wa ushindi kwa mgombea tunayemtaka, ningependa nieleza mambo yafuatayo:

a. Siamini hata kidogo kwamba kugombea nafasi yeyote iliyo wazi ndani ya chama cha siasa ni uhaini na hujuma. Msingi namba moja wa CHADEMA ni demokrasia na hakuna namna ya kudhihirisha mapenzi kwa demokrasia zaidi ya kuruhusu ushindani katika nafasi za uongozi na hasa uongozi wa juu kabisa. Hiki kinachoitwa uhaini ni wasiwasi wa siasa za ushindani katika chama chetu.

b. Sijawahi na sitarajii kushiriki vitendo vyovyote vya kuhujumu chama changu cha CHADEMA na harakati za mabadiliko hapa nchini. Chama hiki kiliniamini katika nafasi nyingi nyeti sana na kama mie ningekuwa mhujumu nilikuwa na fursa nzuri za kufanya uhujumu huo. Nimeshiriki kuandaa ilani ya chama ya 2010-2015, kuratibu kampeni za mwaka 2010 nikiwa makamu mwenyekiti wa kampeni chini ya Profesa Baregu na nilishiriki kutengeneza na kusimamia utaratibu mzuri wa kupata wabunge wa viti maalumu katika chama chetu. Zote hizi ni nafasi nyeti mno ambazo kamwe huwezi kumkabidhi mtu ambaye ni ‘mhaini’ na ‘mhujumu’. Nilishiriki katika shughuli za chama kwa kiwango ambacho nilijisababishia matatizo makubwa katika familia yangu na kazini, lakini sijawahi kutetereka na sijaterereka. Nilifanya yote haya kwa mapenzi yangu ya dhati na imani yangu kwa CHADEMA kwamba ndicho chama kinachostahili kuongoza harakati za mabadiliko hapa nchini kwa sasa.

c. Nasikitika kwamba nimesababisha usumbufu kwa viongozi wangu wa CHADEMA kutokana na dhamira yangu ya kutaka mabadiliko ya uongozi ndani ya chama chetu kwa njia halali za kidemokrasia. Nilifanya hivi kwa imani niliyo nayo kwa misingi ambayo CHADEMA inasimamia, ikiwemo demokrasia, na imani yangu kwamba chama hiki kinahitaji kufanya mabadiliko makubwa katika uongozi wa juu wa chama, ikiwa ni maandalizi muhimu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Nasisitiza tena kwamba siamini hata kidogo kwamba matamanio ya mabadiliko ya uongozi ndani ya chama, na kuandaa mikakati ya kufikia matamanio hayo kwa njia za kidemokrasia ni uhaini.

d. Tunaweza kujifunza kutokana na historia. Siasa za ushindani ndani ya vyama katika nchi hii sio kitu kigeni. Enzi za TAA na kabla TANU haijazaliwa wanachama walikuwa wanagawana nafasi za uongozi mezani. Lakini mwaka TANU ilipozaliwa (mwaka 1954) kulikuwa na uchaguzi mkali sana kwa nafasi ya uenyekiti. Mwalimu Nyerere alimshinda Mzee Skyes kwa kura chache sana. Rais Obama wa Marekani alianza mkakati wa kushinda uteuzi wa kugombea nafasi ya urais kupitia chama chake cha Democrat mapema kabisa mwaka 2006 kupitia waraka maalumu wa siri ulioainisha mikakati yake. Waraka huu uliandaliwa na watu wanne tu bila yeye mwenyewe kujua. Waandaji wa mkakati huu walikuja kumshirikisha baadaye mwaka 2007 na kumshawishi yeye ajitokeze kugombea dhidi ya Hillary Clinton aliyekuwa anachukuliwa kama mrithi halali wa kiti cha urais. Yaliyobaki ni historia. Hivi ndivyo ambavyo siasa za ushindani ndani ya vyama hatimaye huzaa wagombea na viongozi imara katika nchi.

e. Zitto Zuberi Kabwe hajafukuzwa kwa sababu ya waraka huu kwa sababu yeye hakuhusika kwa namna yoyote kuuandaa, ingawa alikuwa ni mlengwa mkuu. Yeye amefukuzwa kwa sababu ambazo yeye atazieleza na ambazo viongozi wa CHADEMA hawakuzieleza katika mkutano na waandishi wa habari.

f. Napenda ijulikane kwamba sikuomba kujiuzulu kwa sababu ya kuogopa aibu ya kufukuzwa. Niliomba kujiuzulu kwa sababu nilitambua kwamba wenzangu katika Kamati Kuu walikuwa hawana imani nami tena, na ni uungwana kujiuzulu mkifika mahala hamuaminiani. Nilitambua vilevile kwamba, kwa mujibu wa Katiba yetu, Kamati Kuu ilikuwa haina uwezo wa kunivua nafasi yangu moja kwa moja.

Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, Sura ya Sita, Ibara ya 6.3.6 (b), inasomeka hivi “Kiongozi aliyeteuliwa na vikao vya uongozi ataweza kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao kilichomteua”. Mimi nilichaguliwa na Baraza Kuu na ni kikao hiki pekee chenye uwezo wa kunivua nafasi niliyokuwa nayo. Ninaamini wajumbe wa Kamati Kuu walipitiwa katika hili kwa sababu siamini kwamba hawajui takwa hili la kikatiba ukizingatia kwamba ndani yake kuna wajumbe waliobobea kabisa katika tasnia ya sheria.

4. Hiki kilichotokea ndani ya chama sio kitu kibaya. Vyama vingi imara hupitia katika migogoro na misukosuko kama hii na zaidi. Naamini tutavuka na tutakuwa imara zaidi. Muhimu ni kwamba ni lazima tuaminiane. Katika kuaminiana sio lazima tufanane kimawazo na kimtazamo kwa sababu hili ni jambo lisilowezekana kibinadamu na zaidi katika siasa.

5. Ninapohitimisha, ninawasihi wanachama wa CHADEMA na wapenzi wa mabadiliko popote walipo wapiganie kwa dhati MISINGI mama ya CHADEMA ikiwemo demokrasia ndani ya chama. Hakuna namna ambavyo chama chochote kinaweza kushawishi umma kwamba kitapigania demokrasia katika nchi wakati kinayahainisha mapambano ya kidemokrasia ndani ya chama chenyewe.

Kukataa siasa za ushindani ndani ya chama ni kuhujumu demokrasia na ni usaliti kwa misingi mama ya chama ambayo ni uhuru wa kweli na mabadiliko ya kweli. Hisia za usaliti na umamluki zilitumika enzi za ukomunisti katika kunyamazisha wapinzani ndani ya vyama vya siasa na katika nchi. Zilikuwa ni njia haramu zilizozoeleka ambazo hatimaye zilizaa udikteta wa kutisha katika mataifa ya kikomunisti. Tusikubali utamaduni wa kuhisiana usaliti na umamluki ukaota mizizi katika chama chetu na katika nchi kwa sababu utaua demokrasia na mfumo wa vyama vingi utakuwa hauna maana tena.

6. Nitafuata taratibu zote za chama kama zilivyoelekezwa na Kamati Kuu na kwa mujibu wa katiba yetu, na nitashiriki kikamilifu katika kutuliza hali ya kisiasa ndani ya chama ili kuhakikisha kwamba tunabaki imara, na CHADEMA inaendelea kuwa tumaini la watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.

Dkt. Kitila Mkumbo
Dar es Salaam
Jumapili, 24 Novemba 2013.

AFYA..!JE UNAFAHAMU UMUHIMU NA FAIDA ZA KULA MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI..?? SOMA HAPA UJIFUNZE..

APPLES Protects your heart, prevents constipation, Blocks diarrhea, Improves lung capacity Cushions joints

APRICOTS Combats cancer, Controls blood pressure ,Saves your eyesight ,Shields against Alzheimer's ,Slows aging process

 ARTICHOKES Aids digestion, Lowers cholesterol, Protects your heart, Stabilizes blood sugar Guards against liver disease

AVOCADOS Battles diabetes, Lowers cholesterol, Helps stops strokes, Controls blood pressure Smoothes skin

 BANANA Protects your heart, Quiets a cough, Strengthens bones, Controls blood pressure, Blocks diarrhea

BEANS Prevents constipation, Helps hemorrhoids, Lowers cholesterol, Combats cancer, Stabilizes blood sugar

 BEETS Controls blood pressure, Combats cancer, Strengthens bones, Protects your heart, Aids weight loss

 BLUEBERRIES Combats cancer, Protects your heart, Stabilizes blood sugar, Boosts memory , Prevents constipation

BROCCOLI Strengthens bones, Saves eyesight, Combats cancer, Protects your heart, Controls blood pressure

CABBAGE Combats cancer, Prevents constipation, Promotes weight loss, Protects your heart, Helps hemorrhoids

CANTALOUPE Saves eyesight, Controls blood pressure, Lowers cholesterol, Combats cancer Supports immune system

CARROTS Saves eyesight, Protects your heart, Prevents constipation, Combats cancer, Promotes weight loss


Baada ya utambulisho wa umuhimu na faida ya kula matunda na mboga kwani kila mboga na kila tunda vina nafasi tofauti ya kujenga na kulinda mwili. Watoto wengi wanasumbua sana kwenye kula hasa mboga majani asilimia kubwa sio wapenzi angalu upande wa matunda watoto wengi hupenda matunda lakini kwa kuchagua sio matunda yote watapenda kula tabia hii hujitokeza kwa kila mtoto hakuna aliekamilika nakumbuka hata mimi nilipokua mtoto nilikua nasumbua sana kula kiasi ikapelekea kua na afya dhaifu wakati wa kukua kwangu mpaka nilipobadili tabia na kuanza kula bila ya kufatiliwa.

Unaweza badilisha tabia ya mtoto wako au mtu yeyote unaeishi nae nyumba moja asiyependa kula mboga majani au matunda kwa kubadilisha muonekano wa chakula hicho au tunda hilo kwa kulinakshi kwa mtindo wowote ule ilimradi kionekane kitu tofauti na kinachovutia hii itakua njia rahisi sana kumvutia mtoto au mkubwa chakula kizuri au upambaji wa chakula sio mpaka hotelini hata nyumbani unaweza fanya sanaa hii na wala haiitaji muda mrefu wa maandalizi muonekano bora wa chakula hutia hamasa kwa mlaji leo tutaangalia utengenezaji wa salad na kuipamba na uandaaji wa mboga ktk muonekano wa kuvutia upande wa kuchonga matunda tutaangalia wakati ujao fata maelezo jinsi ya kutengeneza salad yenye mchanganyiko wa mboga mboga hapo chini
.


Hili ni jokofu la kutunzia mchanganyiko wa mboga katika nyuzi joto 4 hadi 5 tu kwa hali ya usalama sana kwa manufaa na afya ya mlaji tukianzia juu kushoto ni mahindi mabichi ya njano kabla huifadhiwa katika kopo tayari kwa matumizi, karoti iliyokwaruzwa, Lime stone lettuce, chicory, Radish iliyokwaruzwa, zucchin iliyokwaruzwa, rollo nyekundu, rollo ya kijani, matango yaliyokatwa, celeriac salad, curly endive, chicory nyekundu.
Katika sahani yako anza kupanga mboga ambazo zimekatwakatwa  ambazo ni karoti, matango, mahindi machanga ya njano, celeriac salad na  radish nyeupe

Chota kidogo kidogo kila moja panga kwa mtindo wa duara nusu sahani tu kama mduara wa nusu mwezi kati kati acha nafasi kiasi.

Baada ya hapo chukua jani la salad moja moja toka kila aina ya salad pagange sambamba majani hayo kisha zungusha yabane kama unataka kuyafunga kamba kisha kata kiasi upande wa chini utakua umepata kitako safi utakua umetengeneza kama uwa rozi.

Kisha liweke juu ya zile mboga mboga pembei yake kata kipande cha tikiti maji rangi yeyote ile kama ni la kijani, jekundu au rangi ya chungwa pamba kama invyoonekana katika picha.

Kisha kata slice nyembamba ya chungwa katikati yake weka tunda lolote dogo la mviringo kama zabibu au strawbery chomeka toothpick ili ishikilie chungwa juu ya tikiti maji.

Salad hii unaweza mwagia dresing yeyote ile mfano italian dressing, french dressing au siki na chumvi inatosha salad hii unaweza kula na kipande cha kuku, samaki wakuchemsha au wa kukaanga na unakua umekula mlo safi kabisa bila stach kwa watu wanaofanya dayati hapa ni mahala pake mvuto na muonekano wa sahani utamfanya mlaji avutie hata kama si mpenzi wa mboga na matunda.
Hili ni jokofu la kutunzia mchanganyiko wa mboga katika nyuzi joto 4 hadi 5 tu kwa hali ya usafi sana kwa manufaa na afya ya mlaji tukianzia juu kushoto ni nanasi iliyopikwa katika sukari, embe mafuta, cappers, vitunguu vidogo vya kopo,  chopped chives, chopped onion, olives nyeusi, asparagus, matango machanga yaliyosindikwa, olives zakijani, Nyanya
Katika sahani yako anza kupanga mboga ambazo zimekatwakatwa ambazo ni karoti, matango, mahindi machanga ya njano, celeriac salad na radish nyeupe.

Chota kidogo kidogo kila moja panga kwa mtindo wa duara kuzunguka sahani yote katikati acha nafasi.

Baada ya hapo chukua jani la salad moja moja toka kila aina ya salad pagange sambamba majani hayo kisha zungusha yabane kama unataka kuyafunga kamba kisha kata kiasi upande wa chi utakua umepata kitako safi utakua umetengeneza kama uwa rozi.

Kisha liweke pembeni ya zile mboga mboga katikati ya sahani unaweza weka mchanganyiko wowote ule wa nyama ya kuku, ngo'mbe, samaki au sausage iliyochemshwa ikapoa.

Kata saizi ya kuweza kuingia mdomoni kisha changanya na vitunguu vilivyochopiwa safi pamoja chives.

Mchanganyiko huo unaweza malizia na chaguo lako la dresing yeyote uipendayo kisha unamwagia kati kati ya sahani mwisho kata nyanya kipande weka pamoja na tango dogo la kopo na olive moja ya kijani na moja nyeusi kwa kupamba salad yako.
Kwa upande wa mlo kamili baada ya kupika chakula chako kikaiva kama ni ugali au wali

Chemsha njegere zisiive sana

Kisha kata vitunguu vidogo sana kaanga katika siagi dakika 1 tu

Kisha weka hizo njegere zilizoiva katika sufuria kwa dk 2 usiasahau chumvi kisha zitoe

Chukua nyanya nzuri ngumu iliyokwisha iva kata nusu pia kata kidogo katika kitako ili iweze kukaa katika sahaki

Kisha toa mbegu zote katikati ya nyanya tumia kijiko kuchota na jaza zile njegere kwanye nyanya

Kisha save nyanya hiyo yenye njegere kama mboga majani itakayo ambatana na chakula chako kama ni cha mchana au cha usiku.

Muonekano na mchanganyiko wa rangi inakua kivutio kizuri sana kwa mtu asiependa kula mboga majani.

Sasa hapa ndio utawakamata kweli kweli wasiopenda kula mboga za majani,

Chukua maharage mabichi yachemshe kiasi yasiive sana yabaki na rangi yake nzuri ya kijani

Kisha unachukua bacon slice zipo aina mbili zipo bacon za nguruwe na bacon za ng'ombe chaguo ni lako mlaji.

Kisha chukua maharage hesabu kumi na tano kisha zungushia bacon katika maharage hayo weka katika ubao wa kukatia kata ncha za mwisho ili kuweka usawa na muonekano mzuri zaidi.

Ukishamaliza weka kikaango kwenye jiko la moto wa wastani tu weka mafuta kiasi katika kikaango yakishapata moto weka maharage yaliyozungushiwa bacon kaanga kiasi tu ili ile bacona ikauke.

Kisha toa tayari kwa chakula pia sevu kama mboga majani itakayo ambatana na chakula chako kama ni cha mchana au cha usiku. Muonekano na mchanganyiko wa rangi inakua kivutio kizuri sana kwa mtu asiependa kula mboga majani
  
KWA KUFATILIA MAELEZO HAYA YOTE UTAKUA UMEFANIKIWA KUMREKEBISHA KAMA NI MUME AU MTOTO ASIEPENDA KULA MBOGA ZA MAJANI AU MATUNDA IKIWA UMESHAFAHAMU PIA UMUHIMU WA VYAKULA HIVYO KWA BINADAMU




Nashukuru sana mdau aliezungumzia upatikanaji wa bacon ya ng'ombe, nikweli kwa ulaya kupata bacon ya ng'ombe ni adimu sana ila hapa kwetu Tanzania zinapatikana kwa wingi ukienda katika supermaket kubwa au maduka makubwa ya nyama utapata.

Endapo umekosa basi chukua mboga hiyo hapo juu inaitwa leeks kata jani lake lisafishe vizuri kisha zungushia vizuri maharage yako hatua za upishi ni zile zile unaikaanga kidogo tu itaiva na italeta harufu nzuri sana kwahiyo kwa asie kula kabisa nyama atakua nae kafaidika.

AFYA :JE UNAFAHAMU FAIDA ZA KULA MBEGU ZA MABOGA....?? SOMA HAPA UJIFUNZE...

Unaweza kuzidharau mbegu za maboga, lakini ni miongoni mwa mbegu zenye faida kubwa mwilini, zinazoweza kuzuia na kutibu hata magonjwa hatari yaliyoshindikana hospitalini.

 
Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi uliokwishafanyika, zifuatazo ni faida za kifya mtu anazoweza kuzipata kwa kula mbegu za maboga, zikiwa mbichi ama zilizokaangwa:

HUIMARISHA MOYO, MIFUPA
Mbegu za Maboga (Pumkin Seeds), zina kiwango kingi cha madini aina ya Magnesium ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo, uimarishaji mifupa, mishipa ya damu na ufanisi wa utumbo mpana. Magnesium imeonesha uwezo mkubwa wa kuzuia mshituko wa moyo na kiharusi.

KINGA YA MWILI
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini aina ya Zinc, ambayo yana faida nyingi mwilini, zikiwemo uimarishaji wa kinga mwilini, ukuaji wa seli, macho na ngozi ya mwili. Vile vile Zinc huimarisha nguvu za kiume.

SARATANI YA KIBOFU
Kutokana na kuwa na kiwango kingi cha Zinc, utafiti umeonesha kuwa mafuta na mbegu zenyewe za mabogo huweza kutumika kama dawa ya kutibu saratani ya kibofu.

KINGA YA KISUKARI
Utafiti umeonesha pia kuwa mbegu za maboga huweza kuimarisha utokaji wa ‘insulin’ mwilini, hivyo kuwa kinga au kuleta ahueni kubwa kwa wagonjwa wa kisukari.

TIBA KWA WALIOFIKIA UKOMO
Mafuta ya mbegu za maboga hayana madhara, zaidi yana kirutubisho muhimu cha kurekebisha Cholesterol mwilini, kushusha shinikizo la damu, kuzuia uvimbe, maumivu ya kichwa, maumivu ya viungo vya mwili na vile vile huondoa maumivu mbalimbali yanayowapata wanawake wenye umri mkubwa waliofikia ukomo wa hedhi (Menopause).

UGONJWA WA INI
Mbegu za maboga pia zina kamba lishe na kinga kubwa ya kupambana na magonjwa nyemelezi. Mbali na hayo, mbegu zina virutubisho vinavyotoa kinga dhidi ya magonjwa ya ini na moyo.

USINGIZI
Kwa watu wenye matatizo ya usingizi, wanashauriwa kula punje kadhaa pamoja na tunda lolote muda mfupi kabla ya kupanda kitandani, utafiti umeonesha kuwa mbegu za maboga zina kirutubisho kinachochea uzalishaji wa homoni za usingizi kwa wingi.

UVIMBE
Mbegu za maboga zimeonesha kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuzuia magonjwa yote ya uvimbe mwilini, yakiwemo ya kuvimba miguu, vidole na hata majipu.

JINSI YA KULA MBEGU
Hakikisha unakula mbegu ambazo hazijaoza na zilizosafi ambazo hazijakaa muda mrefu. Kwa usalama zaidi, zioshe kwa maji safi kisha zianike, inapendeza zaidi ukila bila kukaanga, lakini pia ukiamua kula za kukaanga bado utapata faida zake, muhimu usiziunguze wakati wa kukaanga. Kwa kawaida hukaangwa kwa muda usiozidi dakika 10 tu.

AFYA :JE UNAFAHAMU KIUNDANI UGONJWA WA PUMU (ASTHMA) NA DALILI ZAKE...

Utangulizi Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia za hewa ambazo huingiza na kutoa hewa katika mapafu. Upatapo ugonjwa wa pumu, kuta za ndani za njia ya hewa hupata maumivu (inflammation) na kuvimba. 

Maumivu katika njia za hewa huzifanya kujihami kwa kusinyaa na hivyo kupunguza kiasi cha hewa kinachopita kwenda kwenye mapafu. Hali hii husababisha muathirika kutoa mlio kama wa filimbi au mluzi wakati wa kupumua. 




Pumu husababishwa na nini? 

Bila shaka mpenzi msomaji umekua ukijiuliza swali hili mara kwa mara. Haifahamiki haswa ni sababu zipi zinazopelekea njia za hewa kupata maumivu na hivyo kupelekea mtu kupata pumu. 

Vyanzo mbali mbali vinaonyesha kuwa inatokana na mseto wa vitu kama tumbaku, maradhi na baadhi ya vizio

Pia kuna vitu katika mazingira ambavyo vinaweza kusababisha mtu kushambuliwa na pumu. Vitu kama vile mazoezi, vizio, viwasho (irritants) na maradhi yatokanayo na virusi. 

Baadhi ya vizio ni kama vifuatavyo: 

-Vumbi 
-Mende 
-Chavua (pollen) kutoka kwenye miti na majani 
-Magamba ya wanyama, manyoya n.k 

Viwasho kama: 
-Moshi wa sigara 
-Uchafuzi wa hewa 
-Harufu kali (kutoka kwenye rangi au chakula) 
-Msongo wa mawazo 
-Dawa kama Aspirin 
-Ugonjwa wa kucheua 
-Viwasho au vizio vitokanavyo na kemikali 
-Magonjwa ya njia ya hewa n.k.

Ieleweke kwamba orodha iliyotajwa hapo juu siyo kamilifu kwa maana kwamba haijasheheni vitu vyote vinavyoweza kuleta dalili za pumu na pia muathirika anaweza kuathirika na kimoja wapo au zaidi. 

Vigezo hatarishi 

Baadhi ya vigezo hatarishi vinavyoweza kuongeza uwezekano wa kusababisha ugonjwa wa pumu ni pamoja na: 

-Kuishi katika miji mikubwa, haswa katikati ya mji ambapo huongeza uwezekano wa kukutana na vizio 

-Kuvuta hewa iliyo na moshi 

-Kemikali zitokanazo na kilimo, dawa za kutengeneza nywele, rangi, vyuma, plastiki au vifaa vya elektroniki 

-Kuwa na mzazi mmoja au wawili wenye pumu 
-Kuathirika na maradhi ya mfumo wa hewa kama kikohozi na mafua wakati wa utoto. 

-Unene wa kupita kiasi (obesity) 

-Ugonjwa wa kucheua na kiungulia (Gastro esophageal reflux disease) 

Dalili za Pumu 

Baadhi ya dalili za kawaida za ugonjwa wa pumu ni kama zifuatazo: 

-Kikohozi: Mara nyingi kikohozi cha pumu huwa kikali nyakati za usiku au alfajiri na hivyo kumfanya mwathirika kutolala vizuri 

-Kutoa sauti ya mfano wa mtu anayepiga mluzi au filimbi wakati wa kupumua 

-Kifua kubana: Mgonjwa husikia kama kitu kinakandamiza kifuani au wakati mwingine husikia kama mtu amemkalia kifuani. 

-Kukosa hewa: Baadhi hujisikia kama hawawezi kupumua na kukosa hewa ya kutosha inayoingia au kutoka kwenye mapafu. 

-Kupumua haraka haraka 

Ikumbukwe kwamba si watu wote huwa na dalili zilizokwisha tajwa hapo juu na dalili zaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu. 

Dalili pia zinatofautiana ukali. Wakati kwa mwingine dalili zinakuwa za wastani, wengine zinakuwa za kukera tu au mbaya kiasi cha kumzuia muathirika kufanya shughuli zake za kila siku. 

Vile vile wapo wengine ambao dalili zinakuwa mbaya kiasi cha kuhatarisha maisha. Dalili pia zaweza kutofautiana kwa kipindi zinapotokea. 

Wengine hupata dalili mara moja tu kwa mwezi, wengine kila wiki na wengine hupata dalili kila siku. Hata hivyo iwapo muathirika atapata matibabu sahihi anaweza kuishi na dalili chache au bila dalili kabisa. 

UTAFITI: HAYA NDIO MADHARA YA UVUTAJI WA SIGARA...


MADHARA YA UVUTAJI WA SIGARA
Katika moshi wa sigara, zaidi ya kemikali 400
zimegundulika kuwa na madhara makubwa
katika afya. Mvutaji mdogo hutumia nusu ya
pakiti ya sigara kwa siku na kujikuta akiathiri
mwili wake kwa kemikali hizi mara 3500 kwa
mwaka. Hata hivyo,

VITU VITATU HATARI ZAIDI
KATIKA SIGARA NI:

1. Tar: hiki ni kisababisha kansa katika mwili.

2. Nicotine: Hiki ni kitu chenye sumu ambacho
kwa muda mrefu san akimetumiwa kama
dawa ya kuuwa wadudu na sumu ya panya.
Inachukua nafasi ya pili kama sumu kali
kabisa kwa athari yake mbaya katika mwili
wa binadamu.

3. Carbonmonoxide: Hii ni gesi
inayopatikana katika moshi wa sigara.
Madhara mbalimbali ya vitu vinayopatikana
katika moshi wa sigara ni kama yafuatayo:
1. Kuharibika kwa utando mlaini katika njia za
hewa: katika njia ambayo pumzi hupita kuna
kama tabaka fulani ambalo ni laini
limezunguka katika njia.
 Tabaka hili hufanyakazi ya kuzuia vumbi vumbi linaloingia
pamoja na hewa. Ile tabia ya uvutaji hufanya
vile vitu vinavyopatikana katika moshi wa
sigara kuganda katika utando huu na
kusababisha njia kuwa nyembamba kwa kule
kuongezeka kwa takataka na kemikali katika
njia, hivyo kumfanya mvutaji apate shida ya
pumzi hapo baadaye.

2. Vidonda vya tumbo: uvutaji wa sigara
huchochea utengenezaji wa acid ambayo
huweza kumletea mvutaji huyo vidonda vya
tumbo.

3. Matatizo katika mfumo wa upumuaji:
wavutaji hupata shida katika koo na mapafu
hivyo kupata kifua mara kwa mara na
maumivu na mwishowe kupata madhara
makubwa katika mfumo mzima wa upumuaji
kutokana na kuharibika kwa mapafu kama
tutakavyozungumzia katika pointi namba 7
hapo chini. Hali ya hewa huwaathiri sana
wavutaji sigara kwani hupata pneumonia na
asthma.

4. Udhaifu katika mifupa (Osteoporosis):
katika moshi kuna metali ijulikanayo kama
cadmium ambayo inaweza kusababisha
matatizo katika mifupa, hii husababisha
kupoteza asilimia 30 ya calcium katika mifupa.
Kwa wanawake uvutaji wa sigara
umeonekana kuzuia shughuli ya estrogen na
kitu chochote kinachozuia estrogen kufanya
kazi husababisha udhaifu katika mifupa
(Osteoporosis) na hii huweza kusababisha
maumivu ya mara kwa mara katika mifupa.

5. Kuwahi kumaliza kufikia mzunguko wa
mwezi (Menopause): Menopause ni ile hali ya
mwanamke kufikia mwisho wa mzunguko
wake wa kila mwezi ambao humpelekea
kushika ujauzito, hali hii huanza kutokea
akifikia umri wa miaka 45 – 55, hutofautiana.
wanawake wanaovuta sigara hufikia
menopause miaka mitano mapema zaidi ya
wasiovuta.

6. Athari kwa wenye mimba: wanawake
wanaovuta sigara huwa katika hatari kubwa
sana ya mtoto kutoka kabla ya siku zake
(Abortion) au kuua mtoto tumboni. Au hata
mtoto kufa mapema zaidi pindi
atakapozaliwa.

7. Kuharibika kwa Alveoli za mapafu
(Emphysema): ile harufu kali ya moshi
huharibu alveoli ndogo ndogo katika mapafu.
Hii kwa kiasi kikubwa sana hupunguza eneo
ambalo Oxygen hukutana na damu na hivyo
kusababisha hali inayoitwa Emphysema. Hali
hii hujitengeneza taratibu sana na kimya kwa
muda mrefu.
Wavutaji wote wana
Emphysema kwa kiwango fulani Lakini
kutokana na eneo kubwa wanaloishi ambalo
hupatikana Oxygen, watu wengi hawajui
kwamba wana hali hii. (watu wengi wana
takriban alveoli milioni 300 katika mapafu
yao) hivyo ni vigumu kugundua hali hii na
baadhi hujijua pale wanapofanya mazoezi
kwa mfano, na kuhisi ugumu wa pumzi.

8. Upungufu wa uwezo wa kubeba oxygen
katika damu: Carbon Monoxide (CO)
inapatikana katika moshi. Uhusiano wa
Carbon Monoxide kwa Haemoglobin ni
mkubwa mara 200 zaidi ya Oxygen. Hivyo
baadhi ya haemoglobin ya damu huzuiwa na
Carbon Monoxide kwa wavutaji kwani
haemoglobin badala ya kuchukua Oxygen
huenda katika Carbon Monoxide na hivyo
uwezo wa kubeba oxygen katika damu
hupungua.

9. Kansa/ Saratani: Katika asilimia kubwa ya
watu wenye kansa hupatikana kutoka kwa
wavutaji wa sigara, saratani za ngozi, koo,
utumbo, kibofu, mdomo n.k. vilevile saratani
ya figo, kongosho, tumbo na kizazi
imeonekana mara chache kwa wavutaji wa
sigara.

10.Kupungukiwa na vitamin: Uvutaji wa
sigara husababisha upungukiwaji wa Vitamin
hasahasa Vitamin C. ule uvutaji wa sigara
moja tu unaweza kupunguza kiasi cha
Vitamin C ambacho kinaweza kulingana na
ukubwa wa kutumia chungwa moja tu. Hivyo
inashauriwa kula sana Vitamin C ili
kurekebisha hali hii.

11. Uvutaji wa sigara unaweza kusababisha
kisukari: Nicotine huchochea sukari katika
damu kwa kuilazimisha au kuichochea
Adrenaline na Non Adrenaline ambayo
hufanya ini na misuli kupeleka sukari katika
mishipa ya damu. Hii hufanya kongosho
ifanye kazi ya kutoa Insuli mara kwa mara ili
kudhibiti sukari kama kawaida yake na
kutokana na kufanya kazi huku mara kwa
mara hufanya kongosho ichoke haraka na
kushindwa tena kudhibiti sukari, hivyo
humsababishia mtu huyu kisukari.
Kwa upande wangu hizo ndizo athari
zinazotokana na uvutaji wa sigara, hivyo basi
jaribu kulinganisha yale manufaa ya muda
mfupi anayoyapata mvutaji na hasara zake.
Hapo utaona kwamba uvutaji wa sigara ni
hatari sana kwa afya yako, na ni bora ujitahidi
sana uache ili kuboresha afya yako
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger