Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

PICHA 5 : RONALDO APIGA PICHA ZA NUSU UCHI KWASABABU YA MBUNIFU GIORGIO ARMANI


 
Kutoka Majuu uko Tunamwangazia Mchezaji Mpira Maarufu  Duniani na mwenye Bei ghali kuliko wachezaji mpira wote Duniani namzungumzia  Cristiano Ronaldo mchezaji wa Real Madrid ya Uhispania lakini hapa tunaangazia kwenye maswala
 ya yeye kujiingizia pesa kama staa duniani.....Akiwa na umri wa miaka 25Cristiano  Ronaldo usiku wa Kuamkia
siku chache zilizo pita ameweza kumwaga wino wa Mkataba wa kupiga picha  na  Mbunifu Giorgio Armani mbunifu toka Italia wa kutangaza nguo za ndani kwa wanaume  na suruali aina ya jeans  za mbunifu huyo.....
Unajua hii imetokanaje!? kutokana na Ronaldo ni mchezaji  maarufu na mzuri duniani
so ameamua kumtumia kutangaza biashara yake akijua fika  shabiki yoyote wa Ronaldo akiona Ronaldo anazitanga ni lazima atanunua yule shabiki  wa Staa huyo duniani.... Giorgio Armani ameweza kumpa Ronaldo dola za kimarekani
 Milioni 20 kwa Kutangaza  Nguo hiyo ya ndani na Jeans hiyo na hapa meamua kukuwekea picha hizi uweze kuona taswira ya  kile nachokizungumzia....!1 Hongera kwa Staa huyo kuvuta mkwanja mwingi kwa kazi hiyo...!! Boxer hizo na jeans hizo zitaanza kuwa kwenye store mnamo tarehe 6.8.2014 kwa gharama ya boxer dola $98 na  jeans kwa dola $240 sawa sawa na boxer kwa pesa taslimu ya kitanzania itauzwa kwa 142,000/= na jeans itauzwa kwa Tsh 366,000

KWA HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE: IKULU YA RAIS SOMALIA YASHAMBULIWA...

Al Shabaab
Wapiganaji wa kundi la wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia meshambulia Ikulu ya Rais katika mji mkuu Mogadishu.
Umoja wa mataifa unasema umefahamishwa kuwa rais wa nchi hiyo hakujeruhiwa na yu salama na kwamba shambulizi la wanamgambo hao lilitibuka.
Waziri wa mambo ya usalama wa nchi hiyo Abdi Karim Hussein, amesema baadhi ya washambuliaji wamefariki na wengine kukamatwa.

Kundi la Al- Shaabab linalopigana na utawala nchini humo limedai kuhusika na shambulio hilo na kusema makabiliano yangali yanaendelea.

Walianza mashambulizi yao, kwa kutumia gari lililokuwa na bomu ndani yake kwa kuliegesha kando ya ukuta na kisha kuanza kupigana ili kuweza kuingia ndani.

Milipuko mikubwa ilisikika pamoja na milio ya risasi.
Majeshi ya muungano wa Afrika yamekuwa yakipambana na wapiganaji hao na hata kuwafurusha kutoka mji mkuu Mogadishu. Hata hivyo bado wanadhibiti sehemu nyingi nje ya Mogadishu

HATIMAYE...!! FACEBOOK WAINUNUA RASMI WHATS APP, WAMILIKI WAWA MABILIONEA..













San Fransisco. Mtandao wa kijamii wa Facebook umenunua programu ya huduma za meseji ya WhatsApp kwa dola za marekani bilioni 19 (TSh 30.9 trilioni) katika taarifa iliyotoka mapema leo.
Ununuzi huo wa WhatsApp umetengeneza mabilionea wapya angalau watatu, akiwemo mwanzilishi wa WhatsApp, Jan Koum, ambaye atajiunga na bodi ya wakurugenzi ya Facebook.
Mwanzilishi mwenza wa WhatsApp, Brian Acton, naye anaingia katika orodha ya mabilionea wapya vijana.
Miaka 4 iliyopita, Acton alijaribu kuomba kazi Facebook na Twitter baada ya kupunguzwa kutoka Yahoo, inaripoti blogu ya teknolojia ya Techcrunch.
Hakufanikiwa.
Leo hii, program aliyoitengeneza na rafikiye wa Yahoo, Koum, inagombaniwa na kampuni zilezile zilizomkataa na hatimaye, imenunuliwa kwa mabilioni ya dola na Facebook.
Wengine walioula ni wawekezaji wa kwanza wa WhatsApp toka kampuni ya uwekezaji ya Sequoia.
Techcruch inaripoti vijana wa Sequoia wametengeneza zaidi ya dola bilioni 3 (TSh 4.9 trilioni) – mara 50 ya pesa waliowekeza – katika ‘dili’ hilo.
Facebook, ambao ni mtandao mkubwa kuliko yote duniani ukiwa na wanachama zaidi ya bilioni 1, inaamini kuwa WhatsApp itasaidia kuongeza uwepo wake katika masoko mbalimbali duniani, hasa katika nchi zinazoendelea Afrika, Asia na Amerika Kusini ambapo teknolojia ya simu za mkononi imeshika hatamu.
Uamuzi huo unaipa Facebook nafasi ya kuongeza idadi ya watumiaji wa mtandao wake, itarithi zaidi ya watumiaji milioni 450 wa WhatsApp.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook, Mark Zuckerberg anaamini uamuzi wa kuinunua WhatsApp kwa dola bilioni 19 ni wa busara, kwa kuwa “[WhatsApp] ni mtandao unaokuwa kwa haraka, ambayo itafikia watumiaji zaidi ya bilioni moja hivi punde

MUSWAADA WA KUPINGA USHOGA KUSAINIWA UGANDA...

ug_e861f.jpg
 
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema atasaini muswaada tata unaopinga ushoga na kuwa sheria kamili.
 
Hatua hiyo inaelezwa kuwa ni onyo kwa wanaotetea vitendo vya mahusiano ya jinsia moja kuwa watashughulikiwa vikali nchini humo.
 
Mwezi uliopita kiongozi huyo alipanga kuachana na muswaada huo ambao umekuwa ukikosolewa vikali na wahisani kutoka mataifa ya Magharibi na wanaharakati wa haki za binaadamu tangu ulipowasilishwa mwaka 2009. Mapenzi ya jinsia moja ni mwiko katika mataifa ya Afrika na kinyume cha sheria kwa mataifa 37.
 
Wasiwasi wa mashoga wa Afrika
Wanaharakati wa haki za binaadamu wanasema Waafrika wachache waliojitangaza kuwa mashoga, wanahofu ya kufungwa, kukabiliwa na vurugu na kupoteza ajira zao.

Wakati wa mkutano wake na chama tawala nchini Uganda NRM kundi la wanasayasi liliwasilisha utafiti wao kuhusu mapenzi ya jinsia moja kwa rais Museveni. Msemaji wa mkutano huo, wa NRA Anite Evelyn katika taarifa yake alisema kuwa "Museveni alitangaza atasaini muswaada huo kwa vile swali lile la iwapo mtu anaweza kuzaliwa shoga au hapana limejibiwa".
 
Uchunguzi wa mawaziri
Katika taarifa yake kamati ya mawaziri iliyokuwa ikilifanyia uchunguzi suala hilo ilisema Ijumaa (14.02.2014) hakuna vinasaba vya mapenzi ya jinsia moja na kwa hivyo si ugonjwa lakini ni tabia isiyo ya kawaida ambapo mtu anaweza kujifunza tu kwa kupitia uzoefu katika maisha.
 
Katika mkutano na chama tawala cha NRM, Mshauri wa Rais katika masuala ya Kisayansi, Dokta Richard Tushemereirwe alimwambia kwamba "mapenzi ya jinsia moja yana athari kubwa kwa afya za watu kwa hivyo si jambo la kuachwa liendelee hata kidogo".
 
Muswaada wa kupinga uhusiano wa jinsia moja uliwasilishwa bungeni mwaka 2009, ambapo awali ulikuwa ukipendekeza adhabu ya kifo kwa wanaoshiriki vitendo vya ngono kwa watu wa jinisia moja, lakini ukafanyiwa marekebisho kwa kuweka adhabu ya vifungo vya awamu gerezani na maisha kwa kile kilichotajwa kuwa mapenzi ya jinsia moja ya kuchochewa.
 
Rais Museveni alisisitiza kuwa , wahamasishaji, wanaojionesha na wote wanaoshiriki vitendo vya ngono kwa watu wa jinsia moja kwa sababu za ukaidi wa kutumwa , hawatavumiliwa na watakabiliwa vikali.
Chanzo, dw.de/swahili

WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUVUNA MILIONI 21...TSH 300,000/ KWA SIKU..SOMA ZAIDI HAPA...


HATIMAYE serikali imeweka hadharani kwamba kila mjumbe katika Bunge la Katiba ataweka kibindoni posho ya sh 300,000 kwa siku.


Kwa maana hiyo, kila mjumbe katika Bunge hilo atakuwa amelipwa sh milioni 21 kwa siku 70 za uhai wa Bunge hilo, na kama serikali itaongeza siku 20 zaidi kwa mujibu wa katiba na kufikia siku 90, kila mjumbe atavuna sh milioni 27.


Awali gazeti hili liliwahi kuripoti majadiliano ya ndani serikalini kabla ya jana kuthibitishwa rasmi ambapo kulikuwa na pendekezo la kutaka kila mjumbe alipwe sh 700,000 kwa siku.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashililah, alisema kuwa kila mjumbe katika Bunge hilo atalipwa sh 300,000 kwa siku.

Alisema malipo ya wajumbe hao ni pamoja na posho zote za vikao ikiwa imeunganishwa na posho za madereva.

Pia alieleza kuwa gharama zote ambazo zimetumika katika matengenezo ya ukumbi na sehemu nyingine ni sh bilioni 8.2 na fedha hizo ni bajeti ya kawaida ambayo ilipitishwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2013/14.

Mbali na hilo, Kashililah alisema kuwa kutokana na umuhimu wa kuwepo kwa Bunge Maalumu la Katiba, Bunge limehakikisha linafanya ukarabati ikiwa ni pamoja na kufunga mitambo mbalimbali ya usalama na kurekebisha mifumo ya kiutendaji.

Alisema matengenezo yaliyofanyika ni pamoja na kurekebisha paa la jengo la ukumbi wa Bunge ambalo awali lilikuwa likivuja wakati wa mvua.

Akitoa ufafanuzi zaidi katika ufungaji wa viti ndani ya ukumbi wa Bunge hilo, alisema  kuna viti 678 na kurekebisha vipaza sauti ambapo kazi hiyo pekee imegharimu dola za Kimarekani milioni moja.

Kuhusu maandalizi, alisema yamekamilika na wajumbe wameishaanza kufika bungeni kwa ajili ya usajili.

Alisema vikao vya Bunge vitaanza  rasmi Februari 18 majira ya saa nane mchana na wataanza kwa kumchagua mwenyekiti na makanu wake.

Alisema ratiba ya Bunge la Katiba itaanza na mkutano wa maelekezo kwa wajumbe Februari 18 asubuhi na Bunge lenyewe litaanza siku hiyo hiyo saa nane mchana.

Kwa mujibu wa katibu huyo, shughuli nyingine zitakazofanyika ni pamoja na mwenyekiti wa muda kusimamia uandaaji  na upitishwaji wa kanuni.
Alisema mwenyekiti wa muda atasimamia uchaguzi wa mwenyekiti na baada ya kupatikana mwenyekiti na makamu wake, ndipo atakapopatikana katibu ambao wataapishwa na Rais Jakaya Kikwete.
Uhai wa Bunge hilo utakoma Aprili 30 au kwa ridhaa ya rais.
-Tanzania Daima

UNYAMA:MWANAMKE ABAKWA KWA AMRI YA WAZEE WA KIJIJI HUKO NCHINI INDIA..!

Polisi nchini India wamewakamata wanaume 13 waliohusishwa na genge la wanaume waliombaka msichana mwenye umri wa miaka 20 katika jimbo la Benghal Magharibi.

Inadaiwa wanaume hao walimbaka mwanamke huyo kufuatia amri ya wazee wa kijiji ambao wamejipa wenyewe mamlaka ya mahakama ya kitamaduni. Msichana huyo amelazwa hospitalini kwa matibabu akiwa katika hali mahututi.

Inaarifiwa kuwa amri ya kumbaka mwanamke huyo ilitolewa na wazee wa kijiji ambao walipinga uhusiano wake na mwanamume kutoka katika jamii tofauti.

Hiki ndicho kisa cha hivi karibuni cha genge la wanaume kumbaka mwanamke nchini India. Tangu kisa cha ubakaji wa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23 uliofanywa na genge la wanaume mjini Delhi mwaka 2012 , swala la ubakaji limekuwa likiangaziwa sana nchini India.

Hasira ya mamilioni ya watu iliyotokana na kisa hicho ilipelekea vyombo vya habari nchini India kuanza kuangazia tatizo hilo , swala ambalo wengi walihisi lilikuwa limepuuzwa kwa muda mrefu.
RAPE1

Serikali nayo ilianza kuweka sheria kali kuhusu dhuluma za kingono dhidi ya wanawake. Lakini utekelezwaji wa sheria hizo bado ni changamoto katika nchi ambayo ustawi wa kijamii unakuwa kwa kujikokota na ukosefu wa usawa likisalia kuwa tatizo jengine kubwa.
Wengi wameshangazwa kuwa katika kisa hiki, ubakaji umeamrishwa na kikundi cha wazee wa kijiji ambao wamejipa mamlaka kama viongozi wa kijamii.

SUNGURA ANAYEONEKANA KWENYE SIKIO LA SANAMU LA NELSON MANDELA AZUA UTATA HUKO AFRIKA KUSINI

sungura

Msanii aliyetengeneza sanamu la Nelson mandela huko south africa ameingia kwenye matatizo makubwa, baada ya serikali hiyo ya south African kugundua kwamba kwenye sikio la sanamu hilo kuna ka sanamu pia kadogo ka panya, kama inavyo onekana kwenye picha. Serikali hiyo imeamuru panya huyo atolewe haraka kwani haileti picha nzuri au maana yoyote kuwepo na kitu kama hicho.

       Msanii huyo aliomba radhi kwa kutuma email kadhaa kwa serikali, lakini hakuna iliyojibiwa, baadae alipewa msamaha ila pia alijibu makosa kwanini aliamua kuweka kitu kama hicho kabla ya kutoa taarifa kwa serikali na pia kutoa maana yak

RONALDO NDIYE MFALME WA SOKA DUNIANI KWASASA ,AWABWAGA MESSI NA RIBERY

MRENO Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka wa FIFA kwa mara ya pili katika historia yake, akimuangusha mshindani wake mkuu, Lionel Messi.
Nyota huyo babu kubwa wa Real Madrid alikuwa anakabiliwa na ushindani wa mbali kidogo kwa nyota wa Barcelona, Messi na wa Bayern Munich, Franck Ribery katika kinyang'anyiro cha Ballon d’Or. 
Akiwa mwenye hisia kali, Ronaldo aliyekwenda jukwaani kuchukua tuzo yake akiwa ameambatana na mtoto wake wa kiume, Cristiano alishindwa kujizuia na kumwaga machozi wakati anapokea taji hilo.
Namba 1: Cristiano Ronaldo ameshinda Ballon d'Or na kutajwa ndiye mwanasoka babu kubwa duniani
Family time: A tearful Ronaldo was on stage with his son Cristiano to collect the award
All smiles: Ronaldo couldn't help but grin broadly when he posed with the trophy
Hisia: Ronaldo alishindwa kujizuia na akamwaga machozi jukwaani wakati anapokea tuzo ya Ballon d'Or
Winner: Pele holds up Ronaldo's son Cristiano as the Portuguese star picks up his award
Mshindi: Pele akiwa amemshika mtoto wa Ronaldo, Cristiano wakati Mreno huyo anapokea tuzo yake

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amepewa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 66 katika mechi 56 za klabu na nchi yake, Ureno mwaka 2013 hatimaye kuirejesha tuzo yake aliyoitwaa awali mwaka 2008.
Pamoja na kwamba Ronaldo hakutwaa taji kubwa mwaka 2013, alifunga mabao yote manne Ureno ikiitoa Sweden katika kinyang'anyiro cha tiketi ya kombe la Dunia baadaye mwaka huu.
"Hakuna maneno ya kusema wakati huu," Ronaldo alisema, huku akifuta machozi. "Nataka kuwashukuru wenzangu wote na washirika pale Real Madrid, katika timu ya Ureno na familia yangu, ambako wako nami,".
"Wale ambao wananifahamu mimi, wanafahamu kwamba  watu wengi wananisaidia: kocha wangu, rais wetu, na sitaki  kusahau kumtaja Eusebio. Mpenzi wangu na mwanangu pia. Nasonga zaidi,". 
Glamorous: Ronaldo with his girlfriend Irina Shark during the awards ceremony
Ronaldo na mpenzi wake Irina Shark katika sherehe za tuzo
Nominees: The trio of Ronaldo, Lionel Messi and Franck Ribery before the ceremony
Washindani: Ronaldo, Lionel Messi na Franck Ribery kabla ya sherehe
Incomparable: Legendary striker Pele won an honourary prize at the Gala in Zurich
Gwiji Pele alipea tuzo katia usiku huo mjini Zurich
Emotional: The Brazilian couldn't keep back the tears
Emotional: The Brazilian couldn't keep back the tears
Mfalme wa soka: Gwiji wa Brazil, Pele alishindwa kujizuia kutoa machozi alipokuwa jukwaani
Out at the top: Retied Jupp Heynckes was named Coach of the Year after winning the Champions League
Retied Jupp Heynckes ameshinda tuzo kocha bora wa mwaka wa dunia baada ya kuiwezesha Bayern Muich kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya
Stunner: Zlatan Ibrahimovic won the Puskas prize for the best goal of the year for his goal against England
Mkali: Zlatan Ibrahimovic ameshinda tuzo ya Bao Bora la mwaka, maarufu kama Puskas 
Unreal: His overhead kick was during Sweden's 4-2 friendly win over England in November 2012
Bao lake tik tak Sweden ikiifunga 4-2 England Novemba mwaka 2012 ndilo bao bora la mwaka
Recognised: German keeper Nadine Angerer won the women's Player of the Year award
Kipa wa Ujerumani, Nadine Angerer ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa kike wa mwaka wa Dunia
Duo: Ronaldo and Angerer pose side-by-side after being named the best players in the world
Wawili: Ronaldo na Angerer baada ya kutajwa wanasoka bora wa dunia 
Shot stopper: Angerer in goal for the German national team during a friendly against Japan
Prize: She was part of the Germany team that won the women's European Championships last year
Taji: Angerer alikuwemo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichoshinda Kombe la ubingwa wa Ulaya kwa wanawake

IKULU ya Rwanda yakanusha Uzushi wa Kifo cha KAGAME..!!

Ikulu ya rais wa Rwanda imekanusha leo ijumaa uvumi kuhusu kifo cha rais Paul Kagame, ambao umepelekea raia wa mji wa Goma kuandamana mabarabarani wakisheherekea kwa furaha taarifa hio. Rwanda iliingia kijeshi mara kadhaa kwenye aridhi ya Congo, hasa ikiwaunga mkono waasi dhidi ya utawala wa Kinshasa wakati wa vita viliyoibuka nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiitwa Zaïre wakati huo, katika miaka ya 1996-1997 na katika miaka ya 1998 hadi 2003.

Rwanda imeelezea mshangao wake kuona uvumi huo ukizagaa, huku raia wa mashariki ya Congo wakiandamana wakionyesha furaha kuhusiana na na taarifa isiyokua ya kweli.
Afisa m'moja anaefanya kazi kwenye Ikulu ya rais wa Rwanda, amefahamisha AFP kwamba taarifa ya kifo cha rais Paul Kagame ilikua uvumi mtupu.

“ Rais wakati huu tunaongea, anakutana kwa mazungumzo na wanafunzi wa chuo kikuu kutoka Marekani. Muko huru kuja kuhudhuria kikao hicho, na muweze kukutana nae, ameendelea kusema afisa huyo.

Paul Kagame, mwenye umri wa miaka 56, ni rais wa Rwanda tangu mwaka wa 1994, baada tu ya waasi wa RPF kushinda jeshi la Rwanda lilokua likimuunga mkono rais Juvenal Habyarimana. Chanzo cha kushindwa kwa jeshi la Rwanda ni mauaji ya kimbari, ambayo lilihusishwa jeshi hilo.
Watu laki nane, wengi wao kutoka jamii ya watutsi waliuawa.

Wafuasi wa rais Paul Kagame wanamsifu kwamba ni mtu mwenye mtazamo katika masula ya uchumi, na lengo lake ni kuliendeleza taifa la Rwanda, huku wapinzani wake wakimtuhumu kujihusisha na tabia mbovu ya kufuta vyama vya upinzani.

Paul Kagame amevaa lawama, kwa mujibu wa Jumuiya ya Kimataifa, kutokana na kuunga mkono makundi ya wapiganaji mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha ya kua Kigali imeendelea kukanusha madai hayo.

HII NI BAADA YA BANGI KURUHUSIWA KISHERIA...SOMA ZAIDI NA PICHA

 
Hawa hapa juu ni baadhi tu ya wateja waliojinunulia bangi yao toka ipitishwe kisheria huko Colorado Marekani ambapo hii picha walikua wakiukaribisha mwaka mpya 2014.
bangi 9
Kwenye hii picha hapa juu na hii ya chini ni foleni ya watu wakiwa kwenye foleni kuingia kwenye duka la kuuzia bangi, hii ni foleni kwenye siku ya kwanza kabisa hawa walikua miongoni mwa wateja kwenye moja ya maduka ya kuuzia hizo bangi ambazo ziko kwenye ladha tofauti mfano strawberry.
Foleni ya kununua bangi mazee
Foleni nje ya duka la kuuzia bangi mazee.
Huko Colorado Marekani dawa ya kulevya aina ya bangi imeruhusiwa kisheria kuuzwa na kuvutwa lakini kununua ni lazima uwe na umri wa miaka 21, nimeona maduka mengi ukiingia kuna mlinzi mlangoni ambae ni lazima umuonyeshe kitambulisho.
Bangi hii inafungwa kwenye mfuko maalum ambapo hauwezi kufunguliwa kirahisi na mtoto mfano akiikuta mahali ambapo kuna duka moja niliona Wafanyakazi wanasema wamepata wateja zaidi ya mia tano toka bangi iruhusiwe siku chache zilizopita na wanayo bangi ya kutosha kwa ajili ya wateja wengine.
Denver prepares for marijuana legalizationHii picha hapa juu ni bango lililowekwa huko Denver Colorado kuwakumbusha watalii pamoja na wakazi kuhusu bangi kuruhusiwa kisheria pamoja na vitu vingine vinavyohusiana na hii ishu.
New Year Celebration
bangi 7
bangi 6Surrounded by a swarm of media in a small retail marijuana sales room, the first official recreational marijuana purchaser ,Sean Azzariti of Boston, reaches for his first marijuana selection handed over by store owner Toni Fox at the 3D Cannabis Center. Photograph: UPI/Landov/Barcroft Media
bangi 4Maduka mbalimbali yaliyo na kibali cha kuuza bangi.
bangi 3
bangi 2bangi 11
bangi 14
bangi 13

USOME UJUMBE ALIOUANDIKA JACK CLIFF KWA MARTIN KADINDA ENDAPO ATANYONGWA HUKO CHINA

Baada ya kukamatwa na kilo 1.1 za heroin nchini China,
mrembo Jackie Cliff kwa sasa anasubiria hatima yake kutokana na kosa hilo la kusafirisha madawa ya kulevya. Ikiwa nchini humo kuna adhabu tofauti za kuwahukumu watu wanao jihusisha na madawa ya kulevya.kc
Jackie Cliff Amuachia Maagizo Ya Wosia Martin Kadinda …

Baadhi ya adhabu ni kifungo cha kuanzia miaka mitatu mpaka kumi na tano (3-15) na adhabu hii hutolewa katika mji wa Macau ambapo mrembo Jackie Cliff… Lakini kwa upande mwingine kuna adhabu ya kuhukumiwa kunyongwa au kifungo cha maisha katika miji mingine na pia hutegemea na aina za dawa za kulevya na uzito wa mzigo aliokamatwa nao mtuhumiwa.
Kupitia Personal Message ya BBM aliyoiandika mwana dada Jackie Cliff  inayosema … ” Ikitokea nimekufa wosia Martin Kadinda ana maagizo ya nini cha kufanya … dnt ask pls.” inasemekana kuwa kama mrembo huyo atashindwa kujikwamua katika tatizo hilo basi, rafiki yake wa karibu ana maagizo yote ya nini cha kufanya kama yeye hatokuwepo tena
IMG-20131228-WA0000


MWANAMITINDO NA VIDEO QEEN "JACKY CLIFF" AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI CHINA...SOMA ZAIDI HAPA

Nchi ya Tanzania imeingia tena kwenye headline kuhusiana na suala la Madawa ya kulevya baada ya kukamatwa tena kwa Mtanzania mwingine akisafirisha Madawa hayo toka Thailand kuelekea Macao nchini China jumanne iliyopita.
Mtanzania huyo ni msichana ana jumla ya umri wa miaka 28 aitwae  Jackie Clief alikamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya Heroin huko Macao nchini China
a3853fb3862d450baca5a4282c0c0d81
Dawa hizo zimekutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na wana usalama kisha kufanyiwa X-ray ambapo baada ya kufanyiwa X-ray alikutwa na jumla ya vidonge 66 vikiwa na thamani ya dola za kimarekani 137,72.
fe5c726676e94e5fadbe9356a9ec599f
Msichana huyu aliliambia Jeshi la Polisi nchini China kwamba alikua akisafiri kuelekea Guangzhou ambao ni mji ulio chini ya jimbo la Guangdong huko China,Inasemekana Msichana huyu amewahi kushiriki video mbalimbali ikiwa ni pamoja na video ya Nataka kulewa ya Diamond.
Hii ni picha imepigwa akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Macao.
0f5d40554df94bcb9c99d45b4ef29b6a
     
Jack Cliff mwenyewe ndio huyu hapa

Jackie Cliff ambaye ni video queen wa Bongo anadaiwa kukamatwa na dawa za kulevya  nchini China. Star mmoja nchini aliyekataa kutajwa jina lake aliutonya mtandao wa  swahiliworldplanet  bila kufafanua zaidi kwa kusema kuwa Jackie amekamatwa na madawa ya kulevya China:
 
 "Jackie Cliff amekamatwa na unga China". alisema star huyo huku akitutumia na picha za mwanamke aliyefungwa kitambaa usoni baada ya kukamatwa na dawa hizo na mwanamke huyo anadaiwa ni Jackie Cliff. Angalia picha hizo hapo chini..........  
Hata hivyo baadhi ya mitandao jana  iliweka habari za mwanamke mmoja wa kitanzania kukamatwa na dawa za kulevya huko china lakini bado habari hizo hazikubainisha mwanamke huyo ni nani na usiku huu ndiyo ikasemekana ni Jackie Cliff. Habari hiyo inasomek  kama  ifuatavyo:

 
"Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya vidonge 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720.

 
"Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.

 
"Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake kwenye press conference huko Macau, Disemba 19, 2013."


MWANAMITINDO NA VIDEO QEEN "JACKY CLIFF" AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI CHINA...SOMA ZAIDI HAPA

Nchi ya Tanzania imeingia tena kwenye headline kuhusiana na suala la Madawa ya kulevya baada ya kukamatwa tena kwa Mtanzania mwingine akisafirisha Madawa hayo toka Thailand kuelekea Macao nchini China jumanne iliyopita.
Mtanzania huyo ni msichana ana jumla ya umri wa miaka 28 aitwae  Jackie Clief alikamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya Heroin huko Macao nchini China
a3853fb3862d450baca5a4282c0c0d81
Dawa hizo zimekutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na wana usalama kisha kufanyiwa X-ray ambapo baada ya kufanyiwa X-ray alikutwa na jumla ya vidonge 66 vikiwa na thamani ya dola za kimarekani 137,72.
fe5c726676e94e5fadbe9356a9ec599f
Msichana huyu aliliambia Jeshi la Polisi nchini China kwamba alikua akisafiri kuelekea Guangzhou ambao ni mji ulio chini ya jimbo la Guangdong huko China,Inasemekana Msichana huyu amewahi kushiriki video mbalimbali ikiwa ni pamoja na video ya Nataka kulewa ya Diamond.
Hii ni picha imepigwa akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Macao.
0f5d40554df94bcb9c99d45b4ef29b6a
     
Jack Cliff mwenyewe ndio huyu hapa

Jackie Cliff ambaye ni video queen wa Bongo anadaiwa kukamatwa na dawa za kulevya  nchini China. Star mmoja nchini aliyekataa kutajwa jina lake aliutonya mtandao wa  swahiliworldplanet  bila kufafanua zaidi kwa kusema kuwa Jackie amekamatwa na madawa ya kulevya China:
 
 "Jackie Cliff amekamatwa na unga China". alisema star huyo huku akitutumia na picha za mwanamke aliyefungwa kitambaa usoni baada ya kukamatwa na dawa hizo na mwanamke huyo anadaiwa ni Jackie Cliff. Angalia picha hizo hapo chini..........  
Hata hivyo baadhi ya mitandao jana  iliweka habari za mwanamke mmoja wa kitanzania kukamatwa na dawa za kulevya huko china lakini bado habari hizo hazikubainisha mwanamke huyo ni nani na usiku huu ndiyo ikasemekana ni Jackie Cliff. Habari hiyo inasomek  kama  ifuatavyo:

 
"Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya vidonge 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720.

 
"Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.

 
"Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake kwenye press conference huko Macau, Disemba 19, 2013."


 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger