Showing posts with label Jamii. Show all posts
Showing posts with label Jamii. Show all posts

Club ya usiku ya nyimbo za Injili yafunguliwa maeneo ya Mbezi Tangibovu jijini Dar.....Ukiwa nusu uchi, ukilewa hamtaruhusiwa kuingia


 
 Imezoeleka kuwa klabu za usiku zimekuwa zikitumika kwa mambo ya starehe huku viongozi wa dini wakizichukulia kama maeneo hatari kwa waumini wao.

Tofauti na maeneo mengine ya starehe, klabu za usiku huwa na kumbi za muziki zenye taa za kumweka za rangi mbalimbali huku giza likitawala. Wakati huo huo muziku hupigwa kwa sauti ya juu.


Mbali na muziki, klabu hizo husheheni vileo vya kila aina huku watu wakiruhusiwa kuingia na mavazi yoyote wakiwemo wale wanaopenda kuvaa nuzu uchi.

Hata hivyo kwa watumishi wengine wa Mungu, klabu sasa ndiyo pamekuwa mahali pa kuvunia waumini.

Mchungaji Harris Kapiga wa kanisa la Nchi ya Ahadi lililoko Sinza Kamanyola, ameamua kuanzisha klabu ya usiku kama zilivyo klabu nyingine za starehe.

Klabu hiyo iliyozinduliwa hivi karibuni maeneo ya Mbezi Tangibovu katika hoteli inayoitwa MakHotel, imeonekana kuvutia vijana wengi ambao walionekana wakifurahia mandhari na muziki uliokuwa ukipigwa ndani yake.

Tofauti na klabu nyinginezo, Mchungaji Kapiga anasema kutakuwa na udhibiti wa vishawishi vya dhambi ikiwa ni pamoja na ulevi, mavazi yasiyo na staha na aina ya muziki unaopigwa.

Anasema tangu alipoanzisha wazo hilo, watu wengi hasa wachungaji walikuwa na wasiwasi kuhusu vishawishi hivyo.

“Tangu nimeanza wazo langu hili nimekumbana na vikwazo vingi. Imeshtua watu wengi, japo wengi wamelikubali na kuna baadhi hawakubali ila hawawezi kusema wazi,” anasema na kuongeza:

“Wengine wanajiuliza nitawezaje kudhibiti  hali ya klabu kwa sababu maeneo haya kunakuwa na anasa, ulevi na masuala ya mavazi watu watavaaje, na mimi nawajibu.”

“Mtu akija hapa na mavazi mabaya hataingia, tutakuwa makini sana katika hili. Mtu avae nguo yenye staha, siyo mtu aje nusu uchi, tutamtoa kwa nia njema tu. Hata mtu aliyelewa tutamtoa labda tusimgundue.”

Kwa nini ameanzisha klabu ya usiku? Mchungaji Kapiga anasema alianza kupata wazo hilo siku alipokuwa kwenye sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa Clouds Media ambako pia ameajiriwa kama mtangazaji

credit: teenzchoice

HatimayeMtoto wa Sheikh Yahya Hussein atabiri Jinamizi la Kifo kuendelea kuwatafuna wasanii na Wanahabari Nchini..!!

MTOTO wa  aliyekuwa mtabiri  maarufu nchini, Shehe Yahya Hussein, Maalim Hussein Yahya ametoa utabiri wake wa mwaka na kusema kwamba vifo zaidi vitaendelea kutokea kwa mastaa wa filamu, muziki, waandishi wa habari, viongozi wa dini pamoja na wanasiasa, Risasi Jumamosi linaweka bayana. 

Aliyekuwa mtabiri  maarufu nchini, Shehe Yahya Hussein.
  


Akifafanua kuhusu utabiri wake huo, Maalim Hussein alisema kwamba pamoja na vifo hivyo lakini mwaka huu utakuwa ni wa mafanikio kwa baadhi ya mastaa na wanahabari.



Pamoja na kwamba vifo vitatokea kwa mastaa na wanahabari lakini wapo kati yao watakaopata neema ya uongozi na kuwa watu wakubwa  kwa kushika nyadhifa mbalimbali,” alisema Maalim Hussein.
Akizungumzia kwa upande wa siasa, Maalim Hussein alisema nyota zinaonesha kwamba kuna kiongozi mmoja  kwenye vyama vikubwa vya siasa atavuliwa uongozi ghafla na kutokana na sakata hilo ataanguka na kufariki dunia.
Kama vile haitoshi, Maalim Hussein alisema baadhi ya  viongozi wa dini watapata kashfa ambazo zitawasababishia umauti pamoja kuvuliwa uongozi katika nyadhifa walizonazo.
Maalim huyo ameongeza katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajiwa kufanyika mwaka huu kutatokea vuguvugu kubwa litakalosababisha mapigano ya jamii kwa jamii na jambo hilo huenda likasababisha vifo.
Mbali na misiba hiyo, Maalim Husseina alisema kwamba mwaka huu kutakuwa na msiba utakaoligusa taifa moja kwa moja na kuongeza kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete atafanya tukio kubwa la kutikisa nchi ambalo litaleta neema kubwa kwa jamii.
Huu ni utabiri wangu kwa mwaka, natarajia kufanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza mengi kwani haya ni baadhi ya  mambo machache kati  ya mengi,” alisema Maalim Hussein.
Mwaka jana, Maalim Hussein alitabiri kutokea vifo vya baadhi ya  mastaa ambavyo vilitokea na kuufanya utabiri wake kutimia.


EHE MUNGU OKOA MAISHA YANGU...!! KIJANA WA MIAKA 19 ALIA KWA UCHUNGU..

 Haruni Kayombo.

KIJANA Haruni Kayombo (19), mkazi wa Mbalizi, Mbeya anaishi kwa mateso makubwa tangu mwaka 2006, baada kushikwa na ugonjwa wa ajabu uliomuanza ghafla.

Katika mahojiano na gazeti hili akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam, Kayombo alisema bado hajui hatima ya maisha yake kutokana na mateso anayoyapata usiku na mchana huku akitoa simulizi ya majonzi namna gonjwa hilo lilivyomtokea.

Alisema awali akiwa na umri wa miaka 11 alilazwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya lakini baadaye wazazi wake walifariki dunia na hakupata kuwajua ndugu zake jambo ambalo anaona hakuna haja ya kuwa binadamu huku akionekana mwenye mateso makubwa.

“Sioni faida ya kuwa binadamu, niliugua kama utani, ilifika wakati nikajua kitu cha kawaida, nilishangaa kuona linazidi kuongezeka nilijua utakuwa ugonjwa wa muda mfupi,  lakini nikashangaa usiku na mchana mateso yanazidi.

“Ni tatizo ambalo hata mimi mwenyewe sijui chanzo chake, lilianza kama kauvimbe ka kawaida, sikutambua mapema na sikuwa na hela kwenda kwenye kituo cha afya kwa matibabu zaidi.

“Nilijipa moyo kuwa ipo siku nitakuwa sawa lakini kwa mpaka sasa nimeshakata tamaa, sina baba wala mama, hapa kweli kuna haja ya mimi kuitwa binadamu? Sina kazi na sikubahatika kusoma ni nani atakayeokoa maisha yangu?

“Maisha haya ni Mungu tu anayeweza kuniokoa, inaniuma sana! Ningekuwa na ndugu wangeweza kunisaidia japo hata pesa ya matumizi. Eee... Mola okoa maisha yangu (analia). Napenda kuishi kama binadamu wengine lakini kwa hali hii sina amani kabisa.

“Zamani wakati tatizo linaanza nilikuwa na tabia ya kusali mara kwa mara lakini nimefika hatua ya kukata tamaa na kuona hakuna haja.

Namuomba rais aje anitembelee ajionee mateso ninayoyapata usiku na mchana, nimepangiwa kwenda kufanyiwa operesheni India lakini sijui lini na itakuwaje!” alisimua Kayombo na kumaliza na kilio tena.


Kama utakuwa umeguswa na tatizo la Haruni Kayombo basi usisite kutoa mchango wako kwenye namba yake ya simu, mtumie kwa njia ya M-PESA ama wasiliana naye moja kwa moja akiwa ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa namba +255764548607.

MTOTO ANUSULIKA KULAWITIWA NA KIJANA KWA KUMDANGANYA KWA PIPI MITAA YA MBEZI DAR...ANGALIA PICHA ZA KILICHOTOKEA KICHAKAI HUKO BAADA YA MTUHUMIWA KUKUTWA

Huyu ni mtoto Julius mwenye umri wa miaka 8, alikuwa nyumbani wakati wazazi wake wote wakiwa hawapo, Alikuwa yeye na kaka yake mwenye umri wa miaka 12.Ndipo swahibu lilipomkuta mpaka kufanya aumizwe kiasi hiki 
 
 Sura ya mtoto imefichwa kutokana na maadili

 Huyu ndio mtuhumiwa.
Alifika Nyumbani na kumlaghai mtoto Julius kwa pipi na kumuita uncle, uncleAkamvuta mpaka vichakani na kutaka kuanza kumlawiti
Mtoto alipoona hivyo akaanza kupiga kelele na kupambana na mtuhumiwa
Muasi alikuwa tayari ameshavua nguo, alipoona mtoto anapiga kelele akaanza kumng'ata na meno mashavuni
Na kumpiga na jiwe kwenye paji la uso.
Bahati nzuri, MUNGU saidia, kuna mama alikuwa anashusha matofali akaskia kelele hizo kabla ya tendo baya kufanyika.
Akaita watu wakamkuta mtuhumiwa akiwa anaendelea kujaribu kumlawiti mtoto huyo wa kiume
Alifanikiwa kumwaga haja zake tu, ila hakufanikiwa kumuingia kimwili
Watu wenye hasira walimpa adhabu yake na yeye, kabla Police hawajafika na kumtia mbaroni


Inasemekana kuwa mtuhumiwa huyu ndio tabia yake, ila hii ndio ilikuwa arobaini yake
Mitaa ya Mbezi ya Kimara, amezunguka sana kuharibu watoto wa watu.
Kila Nyumba akifika anauliza baba na mama wapo?? akiambiwa tu hawapo anaanza shughuli zake
Hivi sasa yuko Hospitali ya TUMBI mahututi, akingojea kusomewa mashtaka
Kama kuna lolote la ziada tutaendelea kufahamishana.
Anaonekana pia kuwa ni shabiki wa Manchester United, Mashetani wekundu
Au labda kajivalia tu t-shirt tu na maushamba yake, mimi nimeudhika sana sijui wewe msomaji

Kama atapona, maana kipigo alichopata sio cha kitoto

MTOTO ALIYELELEWA NA MBWA AZIDI KUTESEKA....!! SOMA HAPA KWA TAARIFA ZAIDI..

MTOTOKulendya Rojason (3) ambaye siku za nyuma aliwahi kuripotiwa na vyombo vya habari kuwahi kulelewa na mbwa baada ya wazazi wake kumtelekeza yeye na ndugu zake, bado anazidi kuteseka kwa kukosa msaada wa chakula.


Mtoto ( kulia ) aliyelelewa na mbwa.

Akizungumza kwa niaba ya mtoto huyo nyumbani kwao, Nyerere B, Mabatini Mwanza, dada wa mtoto huyo, Recho Rojason (18) alisema kuwa mdogo wake bado anateseka kwani hapati malezi ya kutosha kutokana na maisha yao kuwa magumu.
 
Baba wa mtoto.

Recho alisema kuwa, maisha yao yamekuwa magumu baada ya mama yake kuwatelekeza na kuolewa na mwanaume mwingine huku akimwacha baba yao ambaye ametopea kwenye ulevi na kushindwa kutoa msaada wowote.

Recho ambaye ni hausigeli anayefanya kazi kwa ujira mdogo maeneo ya Mwanza Mjini, alisema wamekuwa wakipata fedha kidogo kutoka Halmashauri ya Jiji ambapo hazikidhi mahitaji yao na kuwaomba watu wajitokeze kuwasaidia.
 
Nyumba anayoishi mtoto huyo.

Aliomba msaada wa kupata fedha kwa ajili ya matibabu, masomo na malazi kwa kuwa yote hayo ni mahitaji yao yeye pamoja na wadogo zake watano akiwemo Kulendya.

Akizungumzia sakata hilo jirani anayeishi na watoto hao, Chausiku Ibra alisema kuwa watoto wa familia hiyo wamegeuka machokoraa kutokana na huduma hafifu na kuongeza kuwa mtoto wa mwisho (Kulendya) ndiye yupo hatarini zaidi. 

“Huyu mtoto wa mwisho ndiye aliye hatarini zaidi kwa kuwa tangu alivyokuwa mtoto alikuwa akiletewa chakula na kutunzwa na mbwa.

Mpaka anakuwa hivi ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kweli. Watoto hawa wanahitaji msaada jamani,” alisema jirani huyo.

Waandishi wetu walijionea, nyumba wanayoishi watoto hao ambayo imeonekana kuharibika kwa kiasi kikubwa sehemu za paa na kuta jambo ambalo ni hatari kwa watoto hao huku taarifa zikieleza kuwa, baba wa watoto hao, Rojason Ernest amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando akiuguza nyonga baada ya kuanguka akiwa anatokea kilabuni.

Kama umeguswa na unataka kuwasaidia watoto hao, wasiliana nao kwa namba ya jirani yao, Chausiku: 0767445683.

-gpl 

Mwonekano wa Mabasi Mapya yaendayo Kasi Jijini Dar, Mwonekano wa Nje na Ndani..!

Muonekano wa nje na Ndani.



Mabasi ya mwendo kasi 2014 kimara kivukoni.  Picha kwa hisani ya Deo Mutta Mwanatanga 

Hatimaye Denti wa miaka 8 Afunguka na kusema "Nimechoka kubakwa na Baba"..!!

AMA kweli dunia sasa inaserereka! Katika hali ya kusikitisha, baba mzazi mwenye familia ya watoto watatu, mkazi wa Kambi ya Fisi jijini hapa, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka binti yake wa kumzaa hadi mtoto akafungua kinywa na kusema: “Nimechoka kubakwa na baba.”

Mtoto aliyebakwa na  baba yake mzazi.
Tukio hilo lililobumburuka hivi karibuni limewaacha watu vinywa wazi kwa sababu mtoto huyo ana umri wa miaka minane na kwamba alianza kufanyiwa ukatili huo mwaka jana akiwa na umri wa miaka saba alipokuwa darasa la pili katika shule moja ya msingi jijini hapa (jina tunalo).
AFUMWA LAIVU!
Inadaiwa kwamba mtuhumiwa huyo aliyetajwa kwa jina moja la Pelejai (34) ambaye ni mfanyabiashara wa mkaa, amemwingilia mwanaye huyo kwa mwaka mmoja.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba.
Taarifa zinasema, mwaka jana baba huyo aliwahi kufumwa laivu na mkewe akimtendea ubaya huo binti yake huyo.
Hata hivyo, inasemekana kuwa baada ya kunaswa chumbani kwake na mtoto, alimuomba msamaha mkewe ambaye alimsamehe kwa sharti la kutorudia tena kufanya tendo hilo la aibu na jambo hilo likawa siri kati yao.
Akizungumza kwa uchungu na gazeti hili akiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru anakopatiwa matibabu, mtoto huyo alisema chanzo cha baba yake kumbaka ni baada ya mzazi huyo kugombana na mama yake ambaye aliondoka nyumbani na kwenda kwao.

                                    
MARA YA KWANZA
Alisema mara ya kwanza kuingiliwa na baba yake alisikia maumivu makali mno huku akitokwa na damu nyingi.
Alieleza kuwa alijaribu kulia na kupiga kelele usiku huo lakini baba yake alimziba mdomo ili asitoe sauti.
Alisema alipomaliza kumfanyia ‘unyambilisi’ huo alimtishia kuwa endapo atasema popote, yeye atakamatwa na kufungwa na wao watabaki bila baba, hivyo watateseka kwa njaa.
Baada ya muda mtoto huyo alieleza kwamba baba yake huyo aliendelea kumwingilia mara kwa mara wakati kaka yake mkubwa wanayeishi naye akishindwa kusema baada ya kupewa fedha na baba yake.

MY GOD! KITANDA KIMOJA!
Alisimulia zaidi mtoto huyo alisema kwamba alikuwa akilala na baba yake kitanda kimoja kila siku kama mke na mume katika kipindi ambacho mama yake alipokwenda kijijini kwao Nduruma wilayani Arumeru kujifungua na kukaa kwa zaidi ya miezi mitatu.

“Ukweli nilichoka kubakwa na baba yangu lakini chanzo cha yote ni mama kutokuwepo nyumbani,” alisema mwanafunzi huyo.
Kwa upande wake, mama mzazi wa mtoto huyo alisema kuwa aligundua tukio la kubakwa kwa mwanaye tangu Machi mwaka huu na baada ya tukio hilo mumewe alimwomba tena msamaha kwa mara nyingine  na yeye kumsamehe.

Mama huyo alisema kwamba alilazimika kwenda nyumbani kwao baada ya ujauzito aliokuwa nao kuwa mkubwa.
Alisema baada ya kujifungua aliendelea kuishi huko hadi Novemba 28, mwaka huu alipolazimika kurejea na kichanga chake baada ya kupata taarifa za kupotea kwa mtoto wake huyo anayedaiwa kubakwa na baba yake.
Alisema aliporejea nyumbani kwake Kambi ya Fisi alimuuliza mtoto wake mkubwa iwapo baba yake alirudia tabia ya kumbaka mwanaye lakini mtoto huyo hakusema chochote.
IGP - Said Mwema.
Akiwa anatafakari sehemu alipokuwa mwanaye ndipo alipopata taarifa kwamba alikuwa kituo cha polisi alikopelekwa na walimu wake baada ya watoto wenzake kutoa taarifa kwa walimu kuwa mwanafunzi mwenzao amekuwa akibakwa na baba yake mzazi.
SHULENI
Mmoja wa walimu katika shule hiyo alithibitisha kubakwa kwa mwanafunzi huyo baada ya kumhoji na kumkagua na kugundua kwamba ameharibika sehemu nyeti na kuwa kama za mtu mzima.

                                                                                  
HOSPITALINI
Mama wa mtoto huyo akisaidiwa na walimu walitoa taarifa kituo cha polisi na kupatiwa hati ya matibabu (PF-3) na kumpeleka Hospitali ya Mount Meru.

Mwalimu wa shule hiyo alisema baada ya vipimo, daktari alithibitsha kwamba mtoto huyo alibakwa na kuharibiwa sehemu zake za siri.
Baada ya taarifa hizo kulifikia jeshi la polisi, vijana wa Inspekta Said Mwema walimtia mbaroni mtuhumiwa huyo na kumfungulia kesi ya ubakaji kwa hati ya mashtaka AR/RB/16064/2013-

UBAKAJI
Uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

INAUMA SANA!
Hivi karibuni kumeibuka vitendo vingi vya ubakaji na unyanyasaji kwa watoto, hivyo Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na taasisi nyingine za utetezi wanaombwa kuingilia kati ili kuwanusuru watoto.


Credit: GPL

Wito watolewa kwa wanaume wanaonyanyaswa na wake zao kujitokeza ili waweze kupata Msaada...!!

Ni siku nyingine shughuli zinaendelea, kila mmoja anahangaika kutafuta riziki hata hivyo mamia ya wanaume kati ya wale wanaoonekana wakitembea barabarani na kuendelea na shughuli zao kama kawaida wana siri nzito inayowatafuna…ndani ya maisha yao.
Imezoeleka kuwa wanawake ndiyo viumbe pekee wanaopata manyanyaso toka kwa wenza wao, jambo ambalo lilisababisha vita kali kuanza…vita ya kumtoa mwanamke katika manyanyaso, ukatili, udhalilishaji na kadhia zote zinazotajwa kusababishwa na maumbile yake.
Hata hivyo, ukifuatilia kwa karibu, pengine kusikiliza visa vingi vinavyotokea katika mitaa ya hapa nchini, utagundua kuwa wanaume nao, wananyanyasika kwa kiasi kikubwa kama wanawake wanavyonyanyasika.
Kwa bahati mbaya, wengine wamekuwa wakificha manyanyaso hayo kwa sababu ya aibu au kwa sababu tu wao wanaamika kuwa ni jinsia shupavu, basi wanaona si vyema kuliweka wazi tatizo linalowaumiza na kuwafadhaisha.
Pengine wanaona ni fedheha, aibu au labda si jambo lililozoeleka katika jamii hasa za Kiafrika. Lakini huu ni wakati mwafaka wa kuuweka wazi ukweli kuhusu manyanyaso mnayoyapata.
Kwa mfano, nilipigiwa simu hivi karibuni na mwanamume wa miaka 42 ambaye jina lake nalihifadhi. Alisema kuwa mwaka 2010, aliugua ugonjwa wa kisukari ambao ulimsababisha kupoteza nguvu zake za kiume. Mke wake, hakuvumilia mabadiliko hayo, bali alianza kutoka nje ya ndoa.
“Mwanzoni alificha, lakini baadaye aliona ni haki yake kufanya hivyo na alianza kuwa jeuri, akinitukana na akirudi usiku au wakati mwingine ninasikia gari likimshusha nje,” anasema.
Anasema, alijaribu kumkanya kuhusu tabia hiyo, lakini alikuwa na kiburi kupita kiasi. Kadri siku zilivyoendelea alianza kumsimanga kutokana na hali aliyonayo. “Kibaya zaidi nilipokuwa nikimkanya, alitishia kuwa atawaambia ndugu na rafiki zangu kuwa mimi si mwanamume kamili,” Anasema mwanamume huyo kwa masikitiko.
Wapo wanaume wengi wanaopitia changamoto kama hizi au za aina nyingine, lakini wamezimeza na kuzifungia katika uvungu wa mioyo yao, wakiogopa fedheha.
Umefika wakati wa kusema ukweli kuwa wanaume nao wanapata manyanyaso, ili kama ni vita kwa ajili yao, ianze tena kwa makali kama ile inayofanyika kwa ajili ya wanawake.
Pia, wanaume walio wengi wananyanyasika zaidi pindi wanapoanguka kiuchumi, kwa mfano, mwanamume mwingine alizungumza na gazeti hili na kusema jinsi mke wake alivyomtupia virago nje ya nyumba mara baada ya kufukuzwa kazi katika benki moja hapa nchini.
“Wakati namuoa, nilikuwa ni meneja wa NMB. Tulipendana sana, lakini baada ya miaka mitatu ya ndoa, nilifukuzwa kazi kwa sababu ambazo sitaki kuzitaja. Alipoona nimekaa nyumbani mwaka mzima sina kazi, alianza vituko. Akaamua kunifukuza akidai mali zote nilizochuma ni zake,” anasema mwanamume huyo.
ata kutoka Ofisi ya Takwimu kutoka Uingereza, zinaonyesha kuwa, asilimia 40 ya wanaume duniani kote wanapata manyanyaso kutoka wake zao. Takwimu hizo za 2010 zinaonyesha idadi ya wanaume wanaonyanyaswa na wenza wao ilianza kupanda kuanzia 2004 hadi 2009.
Ukimya huu katika ndoa au uhusiano, ipo siku utaleta madhara kama vifo, ulemavu na uharibifu mkubwa. Kaka, baba zangu simameni…pazeni sauti zenu, wekeni wazi yanayowasibu ili Tanzania ibadili mtazamo wa unyanyasaji wa kijinsia.


JE, UNATAMANI KUACHA KUANGALIA PICHA ZA NGONO NA UNASHINDWA..?? SOMA HAPA UFAHAMU NJIA SAHIHI ZA KUKUSAIDIA KUACHA KABISA..

 

Kuacha kutazama picha za ngono kunahitaji nidhamu, 
ujasiri na imani ndani yake.
Kwani bado madhara yake huwa hayaonekani mbele ya macho ya mtumiaji.
Je, kuangalia picha za ngono kuna madhara gani?

1.MAHUSIANO:

Si tu katika mahusiano yako na mchumba wako bali hata kwa marafiki,
 familia, wanafunzi wenzako, na hata wafanyakazi wenzako.


Uchunguzi wa kisayansi unaonyesha wazi kuwa watu wanaoangalia picha za ngono,
 wana msongo mkubwa wa mawazo na kujihisi wapweke kuliko wasioangalia.

2.UBONGO:

Sehemu ya ubongo inaathirika na mihemko bandia inayotengenezwa  na anayeangalia,
 na hivyo kusababisha unalemaa na kushindwa kabisa kujibu mihemko halisi.
Picha hizi zitakufanya ujitenge na jamii yako, kwani kila muda utataka uwe peke, 
yako eneo unalokaa ili upate wasaa wa kuangalia vizuri kwa kujinafasi.
Maisha yanakosa shauku ikiwa ubongo utazoeshwa kujibu mihemko ya bandia
 kwa kiwango cha juu.

3.KUFURAHIA MATUKIO:

Unaweza ukajikuta kila kitu kwako kinachukiza kuangalia au kujihusisha nacho,
hata ukiangalia kitu kingine utaona bora kiishe ili uangalie picha zako.
Na hii ni hatari kubwa sana kwani utaufanya ubongo ukose taarifa za ziada na zile za ngono ndio zitatawala.

Fuata hatua zifuatazo kujiachisha na tabia hii:

1.AMUA KUACHA LEO USISEME KESHO:

Mara kwa mara watu ambao wamebobea katika uangaliaji wa picha hizi,
 wanapomaliza kuangalia hujipa ahadi kwamba kesho tu nitaacha kuangalia.
Baadaye wanajikuta kesho haifiki,
 kwani kila siku ina kesho yake.
Ukitaka kweli kuacha amua muda uliopo sasa usipange kesho ambayo hujaifikia.

2.USIKAE KARIBU NA MAZINGIRA YA PICHA HIZO:

Ukitaka kujisaidia kuondokana na tatizo hili, hakikisha una kaa mazingira
 ambayo hayajatawaliwa 
na picha za ngono.
Kama unatumia kompyuta, simu au 
hata iPad ambayo 
ndani yake umehifadhi picha hizo zifute sasa,
na ikiwa unatumuia 
DVD au CD ziharibu usikae nazo ndani,
 na hata katika 
historia ya anwani ya 
mitandao uliyotembelea,
 kama zipo zifute kabisa kwani ukiziona utarudi kule kule.

3.USIHESABU SIKU AMBAZO HUJAANGALIA:

Mara nyingi kama umebobea kuangalia huwa haipiti siku bila 
kutupia jicho picha hizo.
Na kuna muda mwingine unabanwa na shughuli nyingi kukupelekea 
kufikisha siku kadhaa hujaangalia,
sasa usikae chini kuanza 
kuhesabu siku ambazo hujaangalia utajikuta unajipa kibali cha 
kutaka kuziangalia haraka iwezekanavyo.

4.USIKAE MAZINGIRA YA PEKE YAKO:

Mara nyingi kama uliwahi kuangalia picha za ngono na ukajikuta uko 
mazingira ya peke yako,
 ya ama unaangalia tamthilia au 
kusoma kitabu chochote kitakachokuwa na habari ya masuala ya watu 
kujamiana itakukumbusha kamchezo kako.
Usichague pia kuangalia
 peke yako picha ziliwekwa
 alama ya miaka 18 zitakuchochea urudi ulipotoka.

5.EPUKA MAZUNGUMZO MACHAFU NA MARAFIKI:

Mara nyingi tunapokaa na marafiki zako ambao wanapenda kuhadithia 
masuala ya ngono tu watakuchochea.
Maana kuna wengine ni mafundi wa kuhadithia hizo vitu,
 kana kwamba wao ndiyo watengenezaji,
sasa unapoona wanaanzisha hizo habari kama huwezi kuwasimamisha basi ni heri ujitenge nao.

6.EPUKA HISIA CHOCHEZI ZA NDANI:

Siri kubwa katika hizi picha zinampa hisia nzuri mtazamaji,
 na kuona hakuna chenye thamani yoyote muda huo.
Kwa hiyo epuka hisia za hasira, 
upweke, na huzuni kwani 
zitakufanya uone eneo pekee la kwenda kujipumzisha ni kuangalia picha hizo.

7.FUTA FIKRA POTOFU:

Achana na fikra potofu za mtaani kuwa kuangalia picha za
 ngono ni kujifurahisha nafsi na hazina madhara.
Lakini kiuhalisia madhara yanayoambatana na tukio lake utayaona baadaye.
Kuna wengine watakwambia kuwa usipoangalia hizo picha utakuwa mshamba na hauendi na wakati.

8.USIJISEMESHE KUWA HUWEZI KUACHA:

Unapokuwa unaangalia hizi picha mara nyingi akili yako inajizoesha,
 na kuona ni utaratibu 
wake wa kila siku.
Kwa hiyo moyoni utakuwa unajisemesha kuwa kuacha kitendo hiki 
hautaweza kamwe,
kitu ambacho kitakufanya uwe dhaifu wa kujitawala.

9.ACHA KUJIKUMBUSHA PICHA ULIZOANGALIA:

Mara nyingi unapokuwa mazingira fulani ya kuwaza mambo mbali mbali, 
mawazo ya picha ulizoangalia ukiyatanguliza kwanza utajifanya 
uwe na shauku ya kwenda kuangalia upya.
ukiona kuna kazi unafanya kazi
 katika kompyuta au umeshika kifaa chochote chenye uwezo wa kukuonesha 
picha hizo ni heri ukizime 
kwa muda huo halafu fikiria kitu kingine kwa haraka.

LINAPOKUJA SUALA LA KUACHA TABIA,
 HII NI VYEMA UKAFIKIRIA ZAIDI KAMA KUNA FAIDA YOYOTE UNAYOPATA.
 NA JE KUNA SIKU UTAKAYOKAA CHINI KUJIVUNIA ULICHOPATA KWA KUANGALIA HIZI PICHA? 

CHUKUA LEO HATUA YA KUACHA ILI KUEPUKA MADHARA YATAKAYOKUJA KUTOKEA SIKU ZIJAZO.



WEKA NIA, UNAWEZA.

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger