Showing posts with label Madawa. Show all posts
Showing posts with label Madawa. Show all posts

MTANDAO WA UNGA WA JACK PATRICK UNATISHA ...SOMA ZAIDI HAPA

Na Mwandishi Wetu
BADO habari ya mjini ni skendo ya kunaswa na madawa ya kulevya ‘unga’ inayomtafuna Video Queen wa Bongo, Jacqueline Clifford Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ ambaye inadaiwa kuwa mtandao wake wa biashara hiyo ni wa kutisha, Ijumaa limetonywa.

Habari kutoka kwa rafiki wa karibu wa Jack ambaye aliomba chondechonde asitajwe, alidai kwa sasa vigogo wanaojihusisha na biashara hiyo haramu wamekuwa wakihaha kwa hofu kuwa modo huyo anaweza kuwataja hivyo wanafanya kila linalowezekana ili wamnusuru kama ilivyokuwa kwa Agnes Gerald ‘Masogange’.

Ilisemekana kuwa katika mtandao huo, vigogo hao wenye maskani jijini Dar, Rwanda, Uganda, Kenya, Dubai, Thailand, Italia na Hong Kong wamekuwa wakihaha kumuokoa Jack bila mafanikio.
“Unajua China siyo rahisi kumchomoa kama ilivyokuwa kwa Masogange (Agness Gerald) aliyenaswa Sauz (Afrika Kusini) kwa sababu wale (China) Tanzania haikuwasaidia kupata uhuru kama ilivyokuwa kwa Sauz.

“Ile ngoma ni mbichi, hakuna upenyo wa rushwa pale. Ngojeni tusubiri hukumu maana itakuwa kali sana, nazijua vizuri sheria za China juu ya madawa ya kulevya,” alisema rafiki huyo wa Jack na kuongeza:

“Hakuna ishu iliyoniuma kama ya Jack kwa mwaka uliomalizika.”
Katika nusanusa za gazeti hili, ilidaiwa kuwa bosi aliyemtuma Jack ni mwanamke mmoja tajiri aishie jijini Dar ambaye ana mtandao mkubwa wa biashara hiyo duniani.

Ili kuthibitisha kuwa mtandao uliodaiwa kumtuma Jack unatisha na una watu wazito, ilielezwa kwamba mrembo huyo hakuwa peke yake kwani alifuatana na warembo wawili, mmoja Mtanzania na mwingine raia wa Rwanda ambao wao walifanikiwa kuwatoroka polisi wa China.

Mbali na timu hiyo ya watu watatu waliokuwa na mzigo mwilini, pia kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa akiwasindikiza

"Natamani na naomba sana Jack Cliff ANYONGWE na afe kabisa "...Hii ni kauli ya Ray C


Rehema Chalamila amekasirika na kwa jinsi ambavyo anawachukia wauza unga, hana hata chembe ya huruma kwa Jackie Cliff aliyekamatwa na madawa ya kulevya huko Macau, China mwezi December mwaka jana, 2013.
 
Awali Ray C aliweka picha Instagram ya Jackie akiwa amekamatwa na vyombo vya dola nchini humo bila kuandika chochote, lakini mizuka ya kufunguka ilikuja kupanda baada ya baadhi ya followers wake kumtetea Jackie.
 
“Wewe tulia mi na hasira maana najua walichonifanya Hawa wauzaji!?!niliingia kwenye madawa na niliwapa kila Kitu hawa wauzaji ili nipate unga maana tayari nilikuwa nimeshaathirika,hawakunionea huruma pamoja na aibu yote walichotaka wao ni pesa ili nipone ndio niheme!!!!!!

"Nilipokuwa na hela walinithamini ila nilipoishiwa walinilaza kwenye box na arosto!!!niliwaomba hata kidogo ili nisiumwe but hawakunielewa ingawa nilishawapa mamilioni ya hela Na nyumba nikauza!!!!!!!

"Sikia tu arosto na omba isiwahi kutokea kwa ndugu yako wala mtoto wako!!!!!!jinsi mama yangu alivyohangaika Na Mimi k**aninA huyu jacky afe tu mbwa mkubwa!!!!na muuaji...
"Ndugu za watu wanalala barabarani mmpaka tunaimbwa teja wa mapenzi!!!!yani acha kabisa!!!wafe wanyongwe,mafirauni wenye dhambi kubwa mbele ya mungu!!!ktk jina la yesu!!!!Wanyongwe!!!!!!!Kill them,” aliandika Ray C.
 
Ray C akiwa taabani  baada  ya  madawa  ya  kulevya  kumfanya  kichaa

HATARI SANA: MTANZANIA ALIYEMEZA MADAWA YA KULEVYA AFA NCHINI INDIA...


The Air Intelligence Unit (AIU) of Mumbai Customs is on a sticky position on the death of one Tanzanian national.

After getting a tip-off, officials of Mumbai customs and Narcotic Control Board (NCB) arrested three Tanzanian nationals at Chatrapati Shivaji International Airport for attempting to smuggle cocaine by ingesting capsules.

Out of these three, two were mules who were flying on Ethiopian Airlines Flight 610, which landed early in the morning, were
taken in for questioning. After five hours of questioning, these men had still not admitted to anything.

Source says, officials offered these foreigners food and water, a common trick. Drug mules who ingest capsules always refuse to eat or drink because sudden bowel movements rupture the capsules leading to death. If the man refused, they would know for sure that the person is smuggling drugs. One of them ate the offered food.

"One man ate the omlette pao offered to him. Later, all three were taken to the court, but the person who had eaten food resisted and tried to escape. In a scuffle, he collapsed outside the court. He died of a sudden cardiac death, typical of a cocaine overdose," an officer said on request of anonymity. He was carrying 20-25 capsules in his body.

The second man's condition was deteriorating and he has been admitted at JJ Hospital on Monday night. After X-ray and CT-scan, it was found that he was carrying around 100 capsules in his body. "He is carrying around 100 capsules in his body. His condition is serious, but he is not in ICU," T P Lahane, dean of JJ Hospital confirmed to Headlines Today.

The third person - an elderly lady - is being questionned separately. She had apparently not ingested any capsules, but was accompanying the men.

Source says, as of now, Mumbai Customs is taking statements of its officials who were present in this operation.

When contacted, no senior custom commissioners made any official statement on this case. One said, "as of now, we could not give any confirmation or any details. But yes, the mattter is under investigation."

Ideally, all three are likely "foot soldiers" also known as 'mules' - who smuggle across a national border, including bringing into and out of an international plane, especially a small amount, transported for a smuggling organisation. The organisers employ these mules to reduce the risk of getting caught themselves.
CHANZO: VIJIMAMBO BLOG

MAITI YA KIJANA MMOJA YAKUTWA NA KETE 65 ZA DAWA ZA KULEVYA MKOANI MBEYA.. !!TAZAMA PICHA ZA MAITI IYO HAPA

 Kete inayosadikika kumuua kijana huyo baada ya kupasukia tumboni.

 Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari nje ya ofisi yake huku akiwa na baadhi ya askari wa jeshi hilo mkoani hapa.
 Pasi ya kusafiria kijana huyo alizokutwa nazo...

 Kete zilizokutwa tumboni mwa kijana huyo baada ya kufan yiwa upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

 Kulia ni kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, akiwa amevalia mavazi maalum, kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Mbeya kwa ajili ya kuona maiti hiyo.


 Maiti ya kijana Kassim Said Mboya ukiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Mbeya baada ya kufanyiwa upasuaji na kutolewa dawa zinazodhaniwa kuwa ni za kulevya.


*Wananachi watakiwa kufika Rufaa Mbeya kuitambua
*Ni maiti ya tatu kukamatwa ikiwa na kete za namna hiyo


MAITI ya kijana Kassim Said Mboya(36), mkazi wa Jijini Dar es Salaam, imekutwa na kete 65 za zinazodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya.

Taarifa zilizolifikia Tanzania daima tangu jana jioni, zilieleza kuwa maiti ya kijana huyo, ilikutwa katika basi la kampuni ya Taqwa eneo la Kasulumu lililokuwa likitokea Jijini Dar es Salaam nchini Tanzania na kuelekea nchini Malawi.

kalulunga blog ilifuatilia na kujua ukweli wake kisha kuwasiliana na kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani leo asubuhi, ambaye pia alikiri kuwepo kwa maiti hiyo na kumwambia mwandishi wakutane eneo la chumba cha maiti cha hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya kuona mwili wa marehemu huyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, alisema kuwa kijana huyo kabla hajafariki, alikamatwa Novemba 7, mwaka huu akiwa ndani ya basi hilo lenye namba za usajili T 319 BLZ akiwa na tiketi yenye jina la Kassim Mueck Michael.

‘’Awali basi hilo kabla ya kufika mpakani Kasumulu na abiria kushuka na kuanza kufanya taratibu za kuvuka mpaka na kuingia nchini Malawi, marehemu alibaki kwenye gari huku afya yake ikizidi kudhoofika’’ alisema Kamanda Dwani Athumani.

Alisema baada ya kuona hivyo, wahusika wa basi hilo walitoa taarifa kituo cha polisi ambapo kijana huyo alichukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya wilaya ya Kyela na kabla hajapata matibabu alifariki dunia.

Alieleza kuwa, kwa kuwa kijana huyo kabla hajapasuka alikuwa na dalili zilizogundulika kuwa alikuwa na dawa za kulevya, iliamuliwa mwili huo kusafirishwa mpaka hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambako ulipasuliwa na kukutwa na pipi 65 zinazodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya na moja ikiwa imepasuka.

‘’Natoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya na nchi nzima kwa ujumla kufika hospitali ya rufaa ya Mbeya kwa ajili ya utambuzi wa mwili wa marehemu na kwamba ijulikane kuwa usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya ni hatari kwa afya ya mtumiaji’’ alisema Kamanda Diwani.

Alipoulizwa kuwa kutokana na mkanganyiko uliowahi kujitokeza katika upotevu na kuwa dawa zilizowahi kukamatwa awali hazikuwa dawa, alisema kuwa kikosi kazi chake kimejipanga vema na jitihada za kupeleka kwa mkemia mkuu zinafanywa chini ya kikosi kidogo cha ulinzi na usalama cha mpaka wa Kasumulu.

Hii ni maiti ya tatu kukamatwa na dawa zinazodhaniwa kuwa ni za kulevya mkoani Mbeya, ambapo shehena ya kwanza ya dawa hizo ilikamatwa mwaka mjini Tunduma mkoani hapa mwaka 2006 ikiwa kwenye tumbo la marehemu Kombo Siriri.

Shehena ya pili ya dawa hizo ilikamatwa Desemba 5, 2011 katika hotel ya High Class mjini Tunduma, ikiwa katika tumbo la maiti ya Mshanga Mwasala.

Licha ya ukamataji wa dawa hizo na baadhi ya watuhumiwa wakiwa haia, hakuna mtuhumiwa aliyewahi kupatikana na hatia tangu mfululizo wa ukamata dawa hizo zinazodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya mkoani Mbeya.


 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger