Home » » UNYAMA:MWANAMKE ABAKWA KWA AMRI YA WAZEE WA KIJIJI HUKO NCHINI INDIA..!

UNYAMA:MWANAMKE ABAKWA KWA AMRI YA WAZEE WA KIJIJI HUKO NCHINI INDIA..!

Polisi nchini India wamewakamata wanaume 13 waliohusishwa na genge la wanaume waliombaka msichana mwenye umri wa miaka 20 katika jimbo la Benghal Magharibi.

Inadaiwa wanaume hao walimbaka mwanamke huyo kufuatia amri ya wazee wa kijiji ambao wamejipa wenyewe mamlaka ya mahakama ya kitamaduni. Msichana huyo amelazwa hospitalini kwa matibabu akiwa katika hali mahututi.

Inaarifiwa kuwa amri ya kumbaka mwanamke huyo ilitolewa na wazee wa kijiji ambao walipinga uhusiano wake na mwanamume kutoka katika jamii tofauti.

Hiki ndicho kisa cha hivi karibuni cha genge la wanaume kumbaka mwanamke nchini India. Tangu kisa cha ubakaji wa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23 uliofanywa na genge la wanaume mjini Delhi mwaka 2012 , swala la ubakaji limekuwa likiangaziwa sana nchini India.

Hasira ya mamilioni ya watu iliyotokana na kisa hicho ilipelekea vyombo vya habari nchini India kuanza kuangazia tatizo hilo , swala ambalo wengi walihisi lilikuwa limepuuzwa kwa muda mrefu.
RAPE1

Serikali nayo ilianza kuweka sheria kali kuhusu dhuluma za kingono dhidi ya wanawake. Lakini utekelezwaji wa sheria hizo bado ni changamoto katika nchi ambayo ustawi wa kijamii unakuwa kwa kujikokota na ukosefu wa usawa likisalia kuwa tatizo jengine kubwa.
Wengi wameshangazwa kuwa katika kisa hiki, ubakaji umeamrishwa na kikundi cha wazee wa kijiji ambao wamejipa mamlaka kama viongozi wa kijamii.

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger