Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe leo ametinga Mahakama Kuu ya Tanzania,Kanda ya Dar es Salaam kuweka pingamizi la kisheria kuzuia Mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA uliopangwa kufanyika kesho tarehe 3/1/2014.
Zitto
kupitia kwa Wakili wake Albert Gabriel Msando,aliwasilisha pingamizi
hilo kwa Hati ya dharura iliyosainiwa na Wakili Msando. Pingamizi hilo
limesikilizwa leo na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Jaji
Uttamwa.CHADEMA iliwakilishwa na jopo la Mawakili lililoongozwa na
Wakili Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA.
Hoja
za Zitto zililenga kuzuia mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA uliopangwa
kufanyika kesho ukiwa na ajenda tatu ikiwamo kupokea utetezi wa mdomo wa
wanachama watatu wa CHADEMA wanaotuhumiwa kukiuka Kanuni na Taratibu za
chama: Zitto,Samson Mwigamba na Dr.Kitila Mkumbo.
Hoja
za Zitto ni kuwa kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA cha kesho kitazuia
kusikilizwa kwa rufani yake aliyoiwasilisha Baraza Kuu akipinga kuvuliwa
kwake nyadhifa ndani ya chama bila ya kusikilizwa. Hii ni kusema, Zitto
alishaadhibiwa bila ya kujibu tuhuma dhidi yake.
Wakili
Msando,kiujumla, amejenga hoja kuwa kikao cha CC ya CHADEMA cha kesho
kisijadili jambo lililokwisha kukatiwa rufaa na hivyo rufaa isikilizwe
kwanza na Baraza Kuu. Ya kwamba, tuhuma 11 ni tuhuma mpya na tayari
Zitto ameshaadhibiwa pasipo kutenda jambo lolote na kusikilizwa popote.
Source: Jamii Forum