Tukio hilo limetokea hivi karibuni ambapo wafanyakazi hao waliweka mgomo kwa takriban siku mbili chanzo kikiwa ni wafanyakazi hao kudai kulipwa mishahara yao chini ya kiwango kilichotamkwa na serikali.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mmoja wa wafanyakazi hao alimshuhudia mzee huyo ambaye jina lake halikupatikana akizungumza na simu chooni kumjulisha kigogo wa kiwanda hicho hatua ambazo wafanyakazi hao wamekusudia kuzifanya dhidi ya uongozi.
Jamaa huyo baada ya kumsikia akitoa umbea huo, aliwatonya wenzake waliokuwa na hasira ambao walimvamia na kumshushia kichapo cha cha nguvu hadi pale polisi walipofika na kumuokoa.
Katika madai mengine, wafanyakazi hao walishinikiza kuondolewa kwa afisa mwajiri wa kampuni hiyo, Gaspal Mwakatuma ambaye amedaiwa kushindwa kutetea maslahi yao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Mashambani na Kilimo Tanzania (TPAWU), Donda Ligonga alpozungumza na waandishi wa habari, alisema mgomo huo si halali na kuwataka wafanyakazi hao kurudi kazini.
Mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazeti, alisema suala la mgomo linaweza kuzungumzika na kuwataka wafanyakazi kurejea kazini wakati mazungumzo