Home » » DOKII: AFUNGUKA NA KUSEMA KUWA HATEGEMEI SANAA YA BONGO KATIKA MAISHA YAKE...

DOKII: AFUNGUKA NA KUSEMA KUWA HATEGEMEI SANAA YA BONGO KATIKA MAISHA YAKE...


MSANII wa filamu za ‘kikwetukwetu’ Ummy Wenslaus ‘Dokii’ amekiri kutotegemea sanaa ya filamu na muziki kupeleka mkono kinywani kwa madai kuwa hailipi kabisa, Ijumaa linakushushia.
Ummy Wenslaus ‘Dokii’.
Akizungumza kwa njia ya simu na Ijumaa, Dokii alisema sanaa peke yake hailipi endapo kama mhusika hatajishughulisha na biashara nyingine, huku akiwaasa wasanii wenzake kutotegemea fani hiyo tu kwani kufanya hivyo ni kujichimbia shimo la umaskini.
“Kwangu mimi sanaa hailipi, ndiyo maana unaona wasanii wengi wanaishi maisha ya tofauti na thamani yao katika jamii, hapa kwetu sanaa hasa filamu haithaminiki ukilinganisha na baadhi ya wenzetu kama Nigeria, India na kwingineko, mimi sitegemei kazi hiyo tu na hata wengine nawaasa kujiwekea milango mingine halali ya kujiongezea kipato,” alisema Dokii.
-GPL
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger