Jeshi
la Polisi mkoani Ruvuma linafanya uchunguzi kuhusu tukio la mume na mke
kumshambulia mtalaka wake Faustina Komba (35) mkazi wa jiji la Mbeya
kwa kumpiga ngumi, makofi na kumng'ata mdomo wake wa chini na kuuondoa
wote.
Habari
zilizopatikana mjini hapa na kuthibitishwa na kamanda wa polisi wa Mkoa
wa Ruvuma, Deusdebit Nsimeki zimewataja watuhumiwa hao kuwa ni Hamidu
Mapunda na Regina Mpangala wakazi wa Mshangano, nje kidogo ya
Halmashauri ya manispaa Songea.
Imedaiwa
Desemba 7, jioni huko Faustina alishambuliwa kwa kupigwa ngumi, makofi
na kung'atwa mdomo wake wa nchini ambao uliondolewa kabisa na Regina
ambaye alishirikiana na mume wake Mapunda.
Inadaiwa chanzo cha ugomvi wao Faustina na Mapunda ambaye alikuwa mume wake wa zamani ni kugombea mtoto wao Mussa Mapunda (5).
Imeelezwa kuwa wakati wakigombana mke wake wa sasa (Regina) aliingilia kati akiwa na lengo la kumsaidia mume wake Mapunda.
Kamanda
Nsimeki alifafanua zaidi kuwa wakati ugomvi unatokea mke wa sasa wa
Mapunda alikuwepo na alishuhudia Mapunda akipigwa kipande cha tofali
kichwani ambacho kilisababisha atokwe na damu nyingi, ndipo alipoingilia
kati na kuanza kumsaidia mume wake lakini Faustina inadaiwa alimkamata
Regina na kumng'ata sehemu ndogo ya mdomo wake wa chini ndipo naye
Regina aliamua kumng'ata sehemu ya mdomo wake wa chini na kuundoa wote.
Kamanda
Nsimeki alisema kuwa Faustina na Regina wamelazwa katika hospitali ya
mkoa Songea kwa matibabu na shauri hilo linasubiri wao wapate nafuu.