Home » » MATAPELI YATUMIA MGAHAWA WA FRESH COACH MJINI MOSHI KUTAPELI MILIONI 5...

MATAPELI YATUMIA MGAHAWA WA FRESH COACH MJINI MOSHI KUTAPELI MILIONI 5...

Mwanamke mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Rashushi Amani Shembusho, mkazi wa Pasua, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ametapeliwa kiasi cha shilingi milioni 5.4 na watu wasiojulikana asubuhi ya leo, Februari 20. 
 
Bi. Shembusho akilia kwa uchungu baada ya kudangasnywa na watu wawili, wa kike na wakiume ambao majina yao bado hayajafahamika. watu hao walimpeleka katika Hoteli maarufu mjini moshi, Fresh Coach na kumtapeli shilingi milioni 5.4 ambazo alikuwa ametoka kutoa Benki ya Uchumi ya mjini Moshi. 
 
Askari wa Hoteli hiyo inayodaiwa kutumika kumtapeli mwanamke huyo akimtuliza Mama huyo ambaye alionekana kuchanganyikiwa na tukio hilo.
 
Mama akilia kwa uchungu. 
 
Msamaria Mwema aliyefika katika eneo la tukio na kujitolea kumpeleka Mwanamke huyo katika kituo cha Polisi cha Kati cha Mjini Moshi.
 
Mama akisimulia tukio zima kwa wananchi waliofika katika eneo la tukio baada ya kumsikia akipinga ukunga kuomba msaada. 
 
Msamaria Mwema aliyefika katika eneo la tukio na kujitolea kumpeleka Mwanamke huyo katika kituo cha Polisi cha Kati cha Mjini Moshi. 
 
Bi. Shembusho akipanda gari la Msamaria Mwema aliyejitolea kumpeleka Polisi kutoa taarifa hizo. Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger