Mtu
aliyetuhumiwa kujaribu kuiba pikipiki aina ya Bajaj maeneo ya Coco
Beach Dar es Salaam akiwa tahabani baada ya kupata kipigo cha mbwa mwizi
maeneo ya
Msasani jirani na Hospitali ya CCBRT hivi karibuni. Kwamujibu
wa mashuhuda wa tukio hilo kijana huyo alikubwa na mkasa huo alipokuwa
katika harakati za kukimbia na inadaiwa alikuwa na hirizi inayomsaidia
kuendelea kupumua. Askari wa Kituo cha polisi cha Oysterbay walifanikiwa
kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala na tutawajuza kama anaendelea na
hali gani. Kwa mujibu wa askari wa Kituo hicho wamethibitisha kumfikisha
hospitalini na kwa kuwa hakuna anayemtuhumu baada ya kupata kipigo
kikali watafanya mchakato wa kumlinda mpaka atoke hospitalini.