Home » , » USHAURI ,,,! JE, NIFANYEJE ILI KUWEZA KUEPUKANA NA VITIMBI VYA PROFESA HUYU....?? HELP PLEASE..

USHAURI ,,,! JE, NIFANYEJE ILI KUWEZA KUEPUKANA NA VITIMBI VYA PROFESA HUYU....?? HELP PLEASE..

Mimi ni mwanafunzi wa chuo fulani hapa nchini Tanzania.  Kuna Profesa mmoja wa hapa chuoni kwetu ameanzisha uhusiano na mpenzi wangu ambaye nilikuwa nampenda sana na nilitegemea awe mama wa watoto wangu. Pamoja na kwamba nilikuwa nampenda sana lakini nililazimika kuachana naye ili kuepuka migogoro ambayo ingenisababishia matatizo katika masomo yangu.

Baada ya miezi mitatu binti yule amenifuata na kuniambia heti ana ujauzito wangu. Nilikubaliana naye lakini nilipochukua jukumu la kwenda kupima, ujauzito ule ukakutwa na ukubwa wa miezi miwili. Niliikataa mimba ile na kumwambia haikuwa yangu.

Binti yule alilia sana na kunibembeleza nikubali heti kwasababu alikuwa ametumwa na Profesa aniletee mimi. Nilikana kwa herufi kubwa na kumfukuza kama mwizi.

Ilipofika mitihani ya majaribio nikaona performance yangu inashuka na baadhi ya mitihani yangu ikapotea na kuambiwa heti sikufanya test. Hata hivyo somo la yule Profesa nikawa ninafauru vizuri ingawa nilikuwa sijiandai ipasavyo kama masomo mengine.  Nimefuatilia sana lakini sikuambulia kitu zaidi ya kuambiwa heti nisubiri kurudia masomo ambayo sikuwa nimeyafanyia test. Nimeumia sana kwasababu nilikuwa mwaka wa mwisho.

Pamoja na kwamba nimeumia sana kurudia mwaka lakini kinachonichanganya zaidi ni kwamba mwalimu yule bado yupo pale chuoni. Sijajua kitu ambacho kinaweza kutokea katika mwaka huu mpya wa masomo ambao sikustahili kuwa chuoni.

JE, NIFANYE NINI ILI KUWEZA KUEPUKANA NA VITIMBI VYA PROFESA HUYU?
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger