Leo tarehe 26 november 2013 familia inafanya kisomo kwa ajili ya kumkumbuku ya Sharo milionea huku nyumbani kwao Lusanga-Muheza,Tanga.
wanafunzi wa madrasa wakiimba kaswida kwenye mkesha huu wa kumuombea marehemu Sharo Milionea
Jana tarehe 25 november kulikua na mkesha maalum,Mkesha huu umeambatana na kaswida mbalimbali zinazoimbwa na wanafunzi wa madrasa,Miongoni mwa watu waliohudhuria kisomo hiki ni pamoja na Kitale ambae alikua rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea.
Mama mzazi wa sharo milionea katikati ya kitale na rafiki wa kitale
millardayo.com imepiga exclusive interview na mama mzazi wa Sharo Milionea pamoja Kitale juu ya kazi zilizoachwa na marehemu Sharo Milionea ikiwemo mikataba mbali mbali na makampuni kama ya Airtel,Azam pamoja na movie ambazo aliziacha marehemu sharo.
‘Dhumuni la mkesha huu ni kumkumbuka mwanangu,kwa kutaka kumsomea dua ili mwenyezi Mungu ampunguzie mazito na kumpunguzia madhambi yake,Mpaka sasa mtandao wa Airtel peke ake ndo walinipatia pesa ambapo walinipa jumla ya milion 10,lakini wengine kama Azam wao walikuja kutoa rambi rambi zao nikasikia kule wamefuta mkataba’.
‘Nimefatilia juu ya kiwanja chake kilichokua bunju alichotafutiwa na mjomba wake,nikamwambia mjomba wake akiuze kwa sababu ya usumbufu maana mi nipo mbali huku,maana nilikua kila siku nasikia mara wamekichota’.
‘Kuhusu Gari ya Marehemu alikua nayo mudy suma ambaye ni rafiki wa marehemu kwa hiyo Mudy Suma nilimwambia aliuze lile gari,na kweli Mudy Suma kaliuza lile gari na pesa akaniletea.
‘Kwa hiyo bado movie tu ndo ninayoijua katika vitu walivyonambia rafiki zake kuwa marehemu alikua na hiki na hiki ni pamoja na movie kwa hiyo movie bado ndo sijapata hela,nimeambiwa ni movie moja ambayo amecheza yeye na kitale na mudy suma’.Mama sharo