Home » , » HACKERS WAVAMIA UKURASA WA FACEBOOK WA NISHA NA KUWEKA PICHA ZA NGONO..

HACKERS WAVAMIA UKURASA WA FACEBOOK WA NISHA NA KUWEKA PICHA ZA NGONO..

Mwanadada Salma Jabu ‘Nisha’ anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo amekubwa na balaa baada ya ukurasa wake wa Facebook kuingiliwa na watu ambao wanautumia vibaya kwa kuweka picha za ngono na picha ambazo hazina maadili, tukio hilo limemfanya msanii huyo kuwa katika wakati mgumu baada ya kupigiwa simu na jamaa zake. 


“Jamani kuna watu wana majaribu sana wameingia katika page yangu ya facebook na wanatuma picha za ajabu ajabu ambazo kwa mtu ninayejiheshimu kama mimi siwezi kuweka picha hizo kwani nina wapenzi wengi wanaohitaji kuchati na mimi kwa kazi zangu,”alisema Nisha.
























Nisha anawalaumu watu ambao wameingia na kuchukua password yake na kuposti picha mbaya kwa nia ya kumharibia ukurasa wake ambao yeye utumia kwa ajili ya kuwasiliana na wapenzi wa filamu ambao wamekuwa wakipata taarifa zake kupitia ukurasa huo,

Msanii huyo anaomba watu wanaohusika na udhibiti wa mitandao ya kijamii kutafuta njia ya kuwakamata watu ambao wanatumia teknorojia vibaya kwa kuwaharibia wengine, baadhi ya wasanii wamekuwa wakikumbana adha mbalimbali kama matumizi mabaya ya picha zao na hata majina yao, pia kwa kurasa ambazo haziwahusu.

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger