Home » , » RONALDO APIGA HAT TRICK YA 19 LA LIGA REAL IKIUA 5-1...SASA NDIYE KINARA WA MABAO HISPANIA,BAYERN MUNICH WAWEKA REKODI MPYA BUNDESLIGA

RONALDO APIGA HAT TRICK YA 19 LA LIGA REAL IKIUA 5-1...SASA NDIYE KINARA WA MABAO HISPANIA,BAYERN MUNICH WAWEKA REKODI MPYA BUNDESLIGA

RAIS wa FIFA, Sepp Blatter alizomewa ile mbaya jana Uwanja wa Santiago Bernabeu wakati Cristiano Ronaldo anafunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Real Sociadad kwenye Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.
Mashabiki wa Real Madrid walikuwa wakimzomea Blatter aliyemkandia Ronaldo hivi karibuni na kumfagilia Lionel Messi wa Barcelona.
Na wakawa wanamuimba Ronaldo Ballon d' Or, maana yake anastahli kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia.  Ronaldo alifunga dakika ya 12, 26 kwa penalti na 76, wakati mabao mengine ya Real yalifungwa na Benzema dakika ya 18 na Khedira dakika ya 36. Bao la kufutia chozi la wapinzani wao lilifungwa na Griezmann dakika ya 61.
Ronaldo sasa amefunga mabao tisa katika mechi nne zilizopita na anaongoza kwa mabao La Liga. Amefunga mabao 62 mwaka huu na sasa amefikisha hat-tricks 19 katika Ligi ya Hispania.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: López, Carvajal, Arbeloa, Alonso/Illarramendi dk70, Varane, Pepe, Khedira/Isco dk77, Modric, Benzema/Morata dk83, Bale na Ronaldo.
Real Sociedad: Bravo, Martínez/Ansotegi dk59, José Ángel, Elustondo/Zurutuza dk45, González,  Iñigo Martínez, Vela, Bergara, Seferovic/De la Bella dk45, Xabi Prieto na Griezmann.
Kiwango tofauti: Cristiano Ronaldo amefunga hat-trick ya 19 La Liga jana akiiongoza Real Madrid kuirarua 5-1 Real Sociedad
Different level: Cristiano Ronaldo scored a hat-trick as Real Madrid comfortable saw off Real Sociedad
Celebration: Gareth Bale congratulates the No 7, though he perhaps should have got on the scoresheet himself
Celebration: Gareth Bale congratulates the No 7, though he perhaps should have got on the scoresheet himself
Celebration: Gareth Bale congratulates the No 7, though he perhaps should have got on the scoresheet himselfPANDE ZA MUNICH

KLABU ya Bayern Munich imepaa kileleni mwa Bundesliga kwa pointi nne zaidi na sasa imeweka rekodi mpya ya kucheza mechi 37 bila kufungwa, kufuatia ushindi wa 3-0 dhidi ya Augsburg jana.
Jerome Boateng, Franck Ribery na Thomas Muller ndio walifunga mabao hayo.
Ushindi huo unaifanya Bayern - ambayo mara ya mwisho ilifungwa katika ligi Oktoba 2012 - iipiku rekodi ya Hamburg kucheza mechi 36 bila kufungwa kati ya Januari 1982 na Januari 1983.
37 games unbeaten: Thomas Mueller blows a kiss to his fans after coring a penalty
Unstoppable: Bayern Munich players celebrate after securing victory
Unstoppable: Bayern Munich players celebrate after securing victory

Borussia Dortmund ilifungwa 2-1 na Wolfsburg. Dortmund walitangulia kupata bao dakika za majeruhi kipindi cha kwanza kupitia kwa Marco Reus, lakini Ricardo Rodriguez akasawazisha dakika ya 56 na Ivica Olic akafunga la ushindi dakika ya 69.
Rare goal from defence: Jerome Boateng got Bayern off to the perfect start
Rare goal from defence: Jerome Boateng got Bayern off to the perfect start
Surprise: Wolfsburg's Ivan Olicscored as his side beat Borussia Dortmund 2-1
Surprise: Wolfsburg's Ivan Olicscored as his side beat Borussia Dortmund 2-1
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger