Home » , » Wema Sepetu na Diamond wajirekodi wakifanya yao kitandani

Wema Sepetu na Diamond wajirekodi wakifanya yao kitandani



Penzi lenye historia ya kushamiri, kumwagana na kurudiana limezidi kuchukua sura mpya, safari hii, Wema Sepetu  amenaswa akimrekodi video baby wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Chanzo cha  kuvuja kwa scene hiyo mpya ilitokea Ijumaa iliyopita ambapo bila hiyana, bibie Wema aliamua kuitupia video katika Mtandao wa Instagram ambayo alimrekodi Diamond aliyekuwa akiandika mashairi kitandani, akamsumbua kwa kumrekodi huko na kusindikiza kwa ujumbe uliosomeka:
 
“In da middle of his writing session…just had to disturb him a little”(Katikati ya muda wake wa kurekodi...nikamsumbua kidogo).
 
Diamond aliyekuwa akiandika mashairi, alisumbuliwa na Wema kwa kumrekodi huku akimtaka aweke mapozi tofautitofauti hali iliyomfanya ‘boyfriend’ wake huyo waliyerudiana siku chache zilizopita, apoteze umakini wa kuendelea kuandika mashairi.
 
Baada ya muda mfupi, ‘posti’ hiyo ya Wema ilipata maoni kibao huku kila mmoja akiweka mtazamo wake. Kuna ambao walimpongeza kwa kufurahi kuona uhusiano wao huku wengine wakiponda kuwa wamechoka ‘drama’ zao za kila siku.

VIDEO IKO HAPO CHINI 
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger