Mwanamuziki
huyo akiwa kwenye viunga vya Club ya usiku ya Kibo iliyopo Tegeta
Jijini Dar pamoja masista du wakila bata ghafra kundi la watu watano
lilimvamia na kumkamta msobe msobe hadi nje ya ukumbi pamoja na
kumrukisha kichurachura huku wakina dada waliokuwa wamendamana nao
wakilia kwa uchungu kwa kumuonea huruma.
Habari
zaidi toka kwa chanzo chetu kilichoshuhudia timbwiri hilo kilisema kuwa
chanzo cha tukio hilo ni kudaiwa kwa Matonya na mtoto wa mjini
aliyefahamika kwa jina la Evance" Huyu
Evance ni mtoto wa mjini na huwa anawakopesha pesa wanamuziki mbalimbali
pamoja na wasanii wa bongo movie hivyo miezi ya hivi karibuni
alimkopesha shilingi laki nne msanii huyo kwa madai kuwa hakuwa na pesa
ya kula bata wikiendi ambapo baada ya kumkopesha msanii alianza
kuzungusha kurudisha hali iliyomfanya Evance kuchukua hatua za kumfanyia
unyambilisi huo" Kilisema chanzo chetu
Hata
hivyo baada ya kumkamata msanii huyo Evance alimpelekwa Oysterbay
ambapo aliiacha gari na simu kwa makubaliano atakapoleta pesa hiyo
atapewa gari yake.