Hatua kuu zinazoonyesha penzi limepoteza uelekeo ni hizi hapa:-
1. MAWASILIANO KUWA DUNI
2. USO KUONESHA KUWA HAPENDI KUONGEA
3. HASIRA ZA MARA KWA MARA
4. MANENO YASIYOFAA HUANZA KUZUNGUMZWA
5. KUDAI KUTENGANA
1. MAWASILIANO KUWA DUNI
Mapenzi na sawa na jani la mti. Huendelea kuwa na mawasiliano na shina
kwa kusaidiana na matawi. Ila siku ikifika jani linadondoka. Hii utokea
pale jani linapochoka na maisha ya kujishikiza. Haya ndiyo sawa yalio
kwetu binadamu. Mwanzo uanza kwa kasi zaidi na mwisho hufifia kwa
mawasiliano. Mtu anaweza kukata mawasiliano kwa sababu zake binafsi
zikiwemo hizo za hapo juu.
Kama mawasiliano yalikuwa ni mara tano kwa siku (kwa wale walio mbali,
mfano masomoni.), basi mawasiliano yanaaza kushuka hadi mara mbili hadi
mwisho wa siku mawasiliano kukaka kabisa. Hapa kila mmoja akiulizwa
swali kwanini husema nilibanwa na kazi ndio maana sikuweza kukutafuta.
Kwa walio kwenye ndoa mawasiliano pia yanakuwa nyuma kidogo. Kama
alikuwa anakusalimia kwa kukumbatiana, hapa hali hua tofauti kabisa.
Muda mwingine kila mtu na kazi yake. Kila mtu shuka yake, na kukicha
kila mtu kivyake.
Hii hua na athari sana pale mmoja wa wapenzi anapokuwa na mpenzi
mwingine. Yule ambaye ulidhani umemchagua anakuja kuwa sumu kwako.
Unapenda umwone yeye ataki. Unapenda umpe zawadi yeye ataki, unapenda
kutoka naye out yeye ataki, na pale anaposema uwasiliane naye basi roho
huweka pembeni. Utagundua kuwa kama analazimishwa aongee.
Ikifikia sehemu hii na kama ulimpenda kweli basi utaongeza jitihada za
kutaka kuwa naye, wasio na imani hufikia mahali wanasema nitaendelea
kukaa bila kuoa. Kauli hii ni udanganyifu tu. Akisahau yale
yaliyomtokea, anaamua kusaka mke au mume mwingine. Unapoona hali hii
imeanza jalibu kuwajilazimisha kuwa karibu yake sana. Na pale unavyoona
hali ni mbaya zaidi basi mweleze rafiki yake wa karibu ambaye humwamini
kwa kila jambo.
Au unaweza kumweleza mtu anayeheshimika ili asikilize kilio chako na
mwisho wa siku utaona mafanikio. Hii ni kwa wachumba na hata kwa
wanandoa itapotakiwa kufanya hili.
Kwa wanandoa ni muhimu wawaone pia wezee wa busara ambao wanaaminika na
kukubalika na jamii. Ikishindikana basi waende katika ofisi ya kata au
ustawi wa jamii kwa msaada zaidi.
2. USO HUONYESHA KUWA HAPENDI KUONGEA
Ni hali ya kawaida kuona mke au mme kuonyesha kuwa apendi kuongea na
wewe. Sababu kubwa anayo moyoni na hataki kuisema. Uso mara nyingi
unakuwa na asili ya mkunjo kwa wanawake. Na kwa wanaume sura inakuwa na
asili na makunyanzi. Hapo ujue kuwa hali ni mbaya sana. Hapo hata
ukimsesha anaona kama unajisumbua tuu. Na kama ataamua kusema ni kidogo
tu na mwisho inaedelea kukaa kimwa.
Pia hata majibu yake uteyaelewa tu. Ni ya unyonge hivi, na sauti ya
chini isiyo na mvuto au ushawishi kwa mwenzake. Pakifikia mahali kama
hapa jalibu kumnunulia zawadi mzuri, kumkisi, kumwambia oooo mpenzi
wangu….nakupenda sana…….leo umependeza namna hii….. Kweli mimi
nimechagua mke mzuri au mme mzuri sana……kwani najivunia sana kukuona na
kuwa na wewe muda wote.
Wakati mwingine unaweza kwenda kumsaidia kupika, kuosha vyombo na hata
kumwambia mkaoge pamoja. Utaona jinsi anavyoanza kubadilika mpenzi wako.
Hapa hakuna mchawi bali ni namna tabia yako ulivyomwonyesha. Hali hii
haiwezi kwisha ghafla kama kimbunga bali huenda taratibu na mwisho wa
siki hali inajirudia. Kwa hali ya kawaida uchukua kuanzia siku 21-22.
Uendelea kumwambia maneno yenye baraka na busara bila ya kukata tama.
Uwe na imanii ya hali ya juu kwani majibu utayokutana nayo si ya
kawaida, lakini mwisho wa siku hali itarudi kuwa ya kawaida kabisa.
3. HASIRA ZAMARA KWA MARA.
Hatua hii mpenzi wako huanza kuchukia kila jambo. Utende mema yeye kwake
ni baya. Utajiongelesha ni kama unamuongezea hasira. Hapa ndipo watu
huwa wanafikia kuchukua hatua ya kujiua wenyewe kisa mpenzi wake
amamsaliti. Mfano wa majibu utayokutana nayo ni kama haya:-
- mbona hivi mpenzi?
- mimi nifanyaje?
Wewe yanakuhusu nini?
Umepata hasara gani mimi kufanya hivi?
Fanya utakavyo?
Mimi ndo kila kitu?
- kwa nini yamefikia hapo?
- we ujui?
Hizi ni baadhi ya changamoto utazokutana nazo wakati wa maojiano yako na
mpenzi wako. Usimpige kisa majibu ya mkato. Kama mwanaume hali ikizidi
kuwa ni kelele tu, basi kaa kimya au ondoka na kwenda kufanya shughuli
zingine. Utavyorudi atashindwa anzie wapi.
Kama ni upande wa mwanamke yanamtokea haya basi fanya hivi:- kaa kimya
kwa muda, atakaa kimya mpenzi wako. Kasha usisite kumwandalia mmeo
chakula cha kutosha na kizuri. Hata kama hali usichoke kuandaa. Mpe
maneno matamu mkiwa kitandani na kujaribu kumgusagusa sehemu mbalimbali
za mwili. Hapa mwanaume ujanja unaisha hapo.
Kama hizo njia zinachukuwa muda mrefu basi anza kwa kumuomba msamaha.
Hata kumpigia magoti usione aibu. Piga huku ukionyeshwa kuwa hali hile
upendezwi nayo. Ni ya bahati mbaya. Hakirudi katika hali ya kawaida na
siku nyingi kupita anza kushusha makombola kwa njia ya utani kuwa pale
mme wangu kosa lilikuwa lako. Kama muelewa ataweza kijirekebisha
ipasavyo na mwisho wa siku mukarudi kama siku ya kwanza kuanza penzi
lenu.
4. MANENO YASIYOFAA HUANZA KUZUNGUMZWA
Hii ni hatua ya nne ambayo inahitaji uvumilivu wa hali ya juu. Mpenzi
wako hutamuona mchungu kupita kiasi. Hutaona kama kuna watu
wanamfundisha kuongea maneno haya. Ukweli ni kwamba ukishaona mke wako
mara nyingi yeye na wenzake, hana muda wa kukaa akuandalie chakula (kwa
mwanamke aliye kwenye ndoa) basi ujue kwamba rafiki zake wamemfundisha
na ujue kuna jambo linaendelea ambolo mwisho wake ni kutengana.
Kwa mchumba basi utaona maneno ya ovyo ovyo ili mradi umwambie sasa mimi
na wewe basi. Atafanya kila aina awezavyo utengane. Hii huweza kuwa
mwanaumme ndio kisa au mke mwenyewe ndio kisa. Akishindwa hapa anaamua
kuchukuwa maamuzi magumu sana ambayo hutasahau tena maishani. Kama vile
kumpigia mpenzi wake mpya na kuanza kuongea naye.
Hiyo atakuwa amekuheshimu, anamkumbatia na kumkiss ili mradi uhuzunike
kwa hili kasha mtenge ili awe huru. Hali hii huwa ni mbaya zaidi kama
mtu umependa. Hhiki ni sawa na wanavyofanya wanaume walio wengi katika
uchumba na doa. Ukimuuliza namba hii uliyosevu Juma mbona inaonyesha ni
hile ya Asha atakuambia ni rafiki yangu.
Ukiendelea kumbana atakuambia ni ya mke wangu. Sasa wewe unasemaje au
unataka nini? Haya utokea kwa wote wenye ndoa zao na wale walio kwenye
uchumba bila kujali mme au mke au mchumba.Haya ndiyo yanayojili sehemu
hii iwapo utashindwa kutatua hizo hatua tatu za mwanzo.
Namna ya kutatua sehemu hii ni kutumia zile njia elekezi ya hatua ya
kwanza. Kubwa zaidi hapa ni kuomba msamaha kwa kile kinachovumilika, na
kile ambacho akivumiliki ni kwenda kwa washauri nasaha kama vile maafisa
ustawi wa jamii kwa manufaa ya wote. Wao watakusaidia vizuri hata kama
uko peke yako na mwenza wako alikataa kwenda huko. Utamsahau na kuiona
dunia ni tamu zaidi y asana na utasema mwenyewe ulichelewa wapi kipindi
yanatokea haya.
5. KUDAI KUTENGANA
Kama mnavyojua, mti uota, ukua, utengeneza majani, huishi na hatimae
mwisho kufa. Hapa mpenzi wako utaona ni balaa tupu. Yaani hafai hata
kidogo. Kama una imani ndogo utatamani uondoke uende mbali ambako
hutamwona tena. Hapa hakuna jinsi, hata mahakama huamua kutenganisha
ndoa kama walioana. Hapa usipofanya kama atakavyo mpenzi wako unaweza
kuishia hata gerezani au kuchukua uamuzi wa kumpiga.
Kweli inauma sana kumwona mke/mme au mchumba unaempendaanataka
mutengane. Wengine huamua kujinyonga, wengine kunywa sumu, wengine
wanaamia baa na kuweka makazi yao. Mmoja hakikataa hakuna jinsi, mwache
aende kwa usalama.
Jinsi ya kutatua hili ni kwamba unapaswa kwenda kukubali tatizo
lililotokea. Kwani kinachotokea kwa wenzako hata wewe ipo siku
yatatokea. Katika maisha ya binadamu kuna kupenda na kutendwa, hivyo
kutengana ni moja ya sehemu ya maisha. Jaribu kutembelea sehemu zenye
mkusanyiko wa watu. Lakini usinywe pombe, na kama ulikuwa unakunya
unaweza kuacha kabisa hatakwa miezi kadha na usitembelee sehemu za
pombe.
Unaweza kwenda disco na sehemu nyinginezo mzuri kama vile kwenye mpira,
kucheza puru, drafti, bao na hata karata. Hali yako itarudi kama zamani.
Utajiona wa kawaida (hii ni kama kwa mwanaume). Ukikutana naye usimwone
kama ni adui ako mkubwa, kwani yaliyotokea ni majaribu ya dunia. Na
pale mkaapo kwa muda mrefu na kuona kuna umuhimu wa kurudiana basi
murudiane kwa moya mmoja.
Kwa wanawake huchukua muda mrefu kama tendo lilifanywa na mwanaume. Na
tatizo lenyewe kama kumfumania mme au mchumba wake wakiwa katika chumba
kile kile anacholala yeye. Huwa anaona ni unyama. Kwa hili, mke huyu
kurudiana naye itachukua muda mwingi kwani lile swala humrudia mara kwa
mara. Na kama alimpenda sana bwana wake huamua usikuone kamwe.
Lakini hakuna jambo lisilo na mwisho. Mme unapaswa kwenda kuomba msamaha
kwa yule mke wako uliyemwacha. Kukataliwa kwa mara ya kwanza ni jambo
la kawaida, kwani ile icha itaendelea kumrudia. Jifanye kama usikii,
fanya hivi zaidi ya mara tano hadi kumi. Mke wako au mme wako ataanza
kukuonea huruma na hatimae kuwa naye pamoja.
NB: ieleweke kwamba si kila unayemfanyia tukio baya ataweza kukusamehe.
Ni wachache wenye nyoyo kama hizo. Bora ubadilike na kutunza utu na
uthamani wako mapema. Kwa kufanya hili maisha utayaona kama maji ya
kunywa.