MABADILIKO makubwa ya Baraza la mawaziri yanayotarajiwa kufanywa wakati wowote kuanzia sasa na Rais Jakaya Kikwete yameanza kuonyesha kila dalili za kuibua sura mpya na ambazo hazitarajiwi na wengi sambamba na kupanda kwa baadhi ya manaibu waziri...
Dodoso zilizofanywa na RAI kutoka kwa watu wa kada na rika mbalimbali kuhusu muundo mpya wa Baraza la Mawaziri zimeonyesha kuwa iwapo rais Kikwete atakuwa amefikishiwa taarifa sahihi na wasaidizi wake kuhusu matakwa ya wananchi kuhusu aina ya viongozi wanaowataka, atalazimika kuwaingiza ndani ya baraza wanasiasa ambao watamudu kukabiliana na upepo wa mabadiliko unaovuma hapa nchini.
Hoja hiyo inajengwa katika msingi kwamba mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa yamelazimishwa kutokea.