Mama mzazi wa marehemu ‘Seven Kanumba’ Frola Mtegoa. |
MAMA
wa msanii nguli wa filamu nchini marehemu ‘Steven Kanumba’ Frola Mtegoa
amesema yuko katika mkakati wa kuandaa filamu inayohusu maisha ya
mwanaye kiasi cha kufikia hatua ya kuomba msaada ‘kutembeza bakuli’. Akizungumza
na paparazi wetu mama huyo alisema kwamba, anapata wakati mgumu
kukamilisha jambo hilo kutokana na kukwama na kutaka asaidiwe ili
kufanikisha jambo hilo.
“Nimekwama na nawaomba wadau wajitokeze kunisaidia nikamilishe hili, nahitaji msaada wa kifedha na hata ushauri,”alisema.
Mama huyo alisema lengo la kuandaa kazi hiyo ni kutaka kufikisha ujumbe katika jamii kwa kuamini kwamba wengi watajifunza kupitia maisha ya mwanawe.
Marehemu Steven Kanumba. |
Amemtaka yeyote ambaye atakayeguswa na jambo hilo asisite kuwasaliana naye na kumsaidia.