Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwanafunzi Peter Robert Kilave wa
kidato cha tatu Shule ya Sekondari ya Kata Tushikamane ya mjini
Morogoro baada kuibuka mshindi wa kwanza katika shindano la Insha kuhusu
Ujenzi wa Miundombinu Afrika Mashariki.Mwanafunzi Peter amechukua
ushindi wa kwanza kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari wan chi tano
za jumuiya ya Afrika Mashariki .
Peter
alipokea tuzo hiyo wakati wa Mkutano wa wa kuu wan chi za jumuiya ya
Afrika Mashariki uliofanyika katika hoteli ya Speke’s Bay
Resort,Munyonyo, Kampala Uganda juzi.Kutokana na ushindi huo Mwanafunzi
huyo amepewa tuzo ya dola za Marekani 1500, na cheti na alikabidhiwa
zawadi hizo na mwenyekiti mpya wa jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais
Uhuru Kenyatta wa Kenya.