Najua
Watanzania wameshuhudia foleni kubwa sana ya Bongo star search 2013
kupitia TV, Magazeti na hata kusikia kwenye Radio kuhusu waliojitokeza
kushiriki ila mshindi ni mmoja na atajulikana Jumamosi November 30 2013
kwenye fainali ambazo nimeambiwa zinafanyika ufukweni, sehemu inayovutia
na salama kabisa kwa kila mtu.
Nimeambiwa
pia Mshindi anajichukulia milioni 50 ambapo waliofanikiwa kuingia
fainali ni Amina Chibaba (MBEYA), Melisa John (DSM), Elizabeth
Mwakijambile (DSM), Emmanuel Msuya (MWANZA) na Maina Thadei (DSM) ambapo
kabla ya mshindi kutangazwa, Snura, Barnaba, Young Killer, Shaa,
Walter Chilambo, Peter Msechu na Makomandoo watapewa nafasi ya kumiliki stage.
VIP unaimiliki kwa 50,000/ na huku kwingine ni 20,000/=ambapo tiketi za siku ya Fainali zinapatikana Shear illusion, Biggy Respect (Kariakoo) Steers Mjini, Zizzou Fashion (Victoria na Sinza) Photo Point (Mayfair) Robby One Fashion (Kinondoni) Best Bite, Engen Mbezi, Escape One (Mikocheni), Benchmark Office Mikocheni, American Nails (Kinondoni).