Ayubu Mnazi Alphonce(24) ni kijana ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete akipatiwa matibabu baada ya kuamua kuukata uume wake kwa kutumia wembe mpya ili kuepukana na usumbufu anaoupata kutoka kwa wanawake ambao amekuwa nao kimapenzi...
Imeelezwa
kuwa baada ya kutokea mfarakano baina yake na mwanamke mmoja ambaye
jina lake halijafahamika,Ayoub aliamua kuingia ndani na kuukata uume
wake kwa kutumia wembe mkali na kisha kuutupa nje..
Taarifa
kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa baba mzazi wa Ayubu baada ya
kubaini kuwa mtoto wake alikuwa amejifungia chumbani kwa muda mrefu,
aliamua kumgongea mlango na alipopata fursa ya kuingia ndani ndipo
alipogundua ukweli juu ya jambo hilo na hivyo kumpeleka Ayubu Kituo
kikubwa cha Polisi Tabora ambapo jalada la kesi ya kujidhuru
lilifunguliwa.
Hata
hivyo hali ya Ayubu kwasasa inaendelea vizuri licha ya kuwa amejikata
na kubakisha kipande cha sentimeta 5 huku akisubiriwa kufikishwa
mahakamani kwa kutenda kosa hilo la kujidhuru mwenyewe pasipo sababu za
msingi.