Oktoba 16, 
mwaka huu, majira ya saa saa nne na nusu usiku, huko katika Kijiji cha 
Mahenje Kata ya Myovizi, Tarafa ya Iyula wilayani Mbozi mkoani hapa, mtu
 mmoja asiyefahamika jina wala makazi, jinsi ya kiume, umri kati ya 
miaka 20-25, alikutwa ameuawa na watu wasiojulikana na mwili wake 
kutupwa shambani.
Wakati mwili 
huo umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Mbozi, polisi wameanza 
uchunguzi wao ili kubaini chanzo cha mauaji hayo ambayo marehemu 
alikutwa na jeraha upande wa kulia wa ubavu wake.
Kamanda wa 
Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Diwani Athuman alithibitisha 
kutokea kwa tukio hilo huku akitoa wito kwa ye yote mwenye taarifa juu 
ya mtu au watu waliohusika katika tukio hilo kuzitoa katika mamlaka 
husika ili wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake.
Katika tukio 
lingine, siku hiyo hiyo, katika Kijiji cha Isalalo, Kata ya Msia, Tarafa
 ya Igamba wilayani Mbozi, Tusamale Wilega (70) ambaye ni mkulima, 
alifariki dunia akiwa amelala ndani ya nyumba yake baada ya mtu au watu 
wasiofahamika kuchoma moto nyumba yake.
Ilielezwa kuwa marehemu alikuwa anaishi peke yake katika nyumba hiyo iliyojengwa kwa matofali mabichi na kuezekwa kwa nyasi.
Bado polisi wanaendelea kuchunguza chanzo cha moto huo.
Bado polisi wanaendelea kuchunguza chanzo cha moto huo.
Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu kwa mazishi.
Kamanda Athumani alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akitoa wito kwa mtu au watu wenye taarifa kutoa ushirikiano kwa polisi.
Kamanda Athumani alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akitoa wito kwa mtu au watu wenye taarifa kutoa ushirikiano kwa polisi.
-GPL
 
 
 
 
 
 
 
