Home » » BIBI AJITOLEA KUWAOKOA WATOTO WALIOTELEKEZWA NA BABA YAO HUKO MBEYA...

BIBI AJITOLEA KUWAOKOA WATOTO WALIOTELEKEZWA NA BABA YAO HUKO MBEYA...

BIBI Mariam Mponzi (80) amepambana kwa hali na mali kuwatetea wajukuu zake waliotelekezwa na baba yao Emmanuel Yuta.
Emmanuel alidaiwa kuuza nyumba waliyokuwa wakiishi katika Kijiji cha  Hatwelo, Kata ya Ijombe, Mbeya Vijijini na kutokomea kusikojulikana huku akiwaacha watoto wake wawili wenye umri wa miaka 9 na 11 wakikosa pa kuishi.
Kikongwe huyo alichukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa kitendo kilichofanywa na mwanaye kwa kushirikiana na serikali ya kijiji si cha kiungwana.
Bibi huyo alilazimika kukopa shilingi laki nne kutoka kwa mtu ambaye hakumtaja jina kwa lengo la kuzirejesha kwa mtu aliyenunua nyumba hiyo aitwaye Dati Nsagaje ambaye alisema akirudishiwa fedha zake angeiachia nyumba hiyo.
Akizungumza baada ya kurejeshewa nyumba hiyo, kikongwe huyo alisema kwa sasa makazi hayo ni mali ya wajukuu zake hivyo mwanae akishindwa kuendelea na maisha huko alikokimbilia na kuamua kurejea akatafute sehemu nyingine ya kuishi.
Baadhi ya majirani wa eneo hilo walisema kitendo alichokifanya baba wa watoto hao hakipaswi kufumbiwa macho na mlalamikiwa akikamatwa achukuliwe hatua kali za kisheria
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger