Wema Sepetu ‘Madam’
STAA wa sinema za Kibongo, Simon Mwakipagata ‘Rado’ amefunguka kuwa Wema Sepetu ‘Madam’ aliponea chupuchupu kwani ilibaki kidogo amng’oe meno.
Akizungumza
na Stori, hivi karibu baada ya kukumbushiwa tukio hilo lililotokea hivi
karibuni katika ofisi za Wema zilizopo Mwananyamala jijini Dar kupitia
kipindi cha mlimbwende huyo cha In My Shoes,
Rado alifafanua:-
“Nilimlipa Wema afanye filamu yangu na kabla haijaisha yeye akaenda kutoa nywele na kila kitu bila kuniambia jambo ambalo halitakiwi kwenye filamu ndiyo maana nilifanya vile na siku ile ningemtoa meno,” alisema Rado