BARAZA
la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki iliyopita lilikabidhi kibali
kwa ajili ya uendeshaji wa Tamasha la Krismasi litakaloendeshwa na
kampuni ya Msama Promotions. Tamasha
hilo ni muendelezo wa tamasha la Pasaka lililoasisiwa tangu mwaka 2000
likiwa na lengo la kumtukuza na kumtumikia Mungu kupitia nyimbo
mbalimbali za waimbaji wa Tanzania na nje ya nchi.
Kabla
ya tamasha la Krisimass, Msama alipewa mawazo mengi kutoka kwa wadau
mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari wa kutoka vyombo mbalimbali vya
habari. Sababu za kumtaka Msama kuandaa Tamasha la Krisimass ni
kupanua wigo wa kuhubiri Neno la Mungu na kuwapa waamini na wadau wa
muziki wa Injili fursa ya kupata burudani kupitia nyimbo za watumishi
mbalimbali.
Kampuni
ya Msama inayoandaa matamasha hayo mawili yenye mlengo unaofanana,
imedhamiria kuandaa matamasha hayo mawili ni kufikisha neno la mungu
kupitia nyimbo sambamba na mapato yatakayopatikana yatasaidia yatima,
walemavu, wajane, waathirika wa Ukimwi na wanaoishi katika mazingira
hatarishi.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni hizo, Alex Msama tamasha la Krisimas
litafanyika mikoa mbalimbali ili kuwafikia waumini wengi zaidi lengo
likiwa ni kumtukuza na kumuabudu mungu. “Waumini baada ya kuguswa na
neno la mungu katika tamasha la Pasaka, wamenishauri niandae tamasha la
Krismass lengo likiwa ni ibada,” alisema Msama.
Ili
kunogesha tamasha hilo lenye hadhi ya kimataifa,kupitia waimbaji wa
Tanzania pia litashirikisha waimbaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika
kama ilivyo kwenye tamasha la Pasaka siku hiyo waimbaji wote wataimba
‘live’ na hakutakuwa na matumizi ya Play back CD ama mshindo
nyuma. Lengo la Tamasha la Krismasi kumuabudu Mungu kwa njia ya sifa
lakini pia mapato yatakayopatikana yatasaidia wenye uhitaji maalum kama
wajane,walemavu, yatima, waathirika wa Ukimwi na wanaoishi katika
mazingira hatarishi.
Anasema
lengo lingine ni kusherehekea sikukuu ya Krismass na mashabiki na wadau
wa muziki wa injili hapa nchini na kufikisha ujumbe wa neno la mungu
wenye lengo la kudumisha amani na utulivu hapa nchini.
Anasema
pia tamasha hili litashirikisha watumishi wa Mungu kutoka huduma na
makanisa mbalimbali kwa ajili ya kuiombea Baraka na amani Taifa
laTanzania pamoja na viongozi wao. Aidha Msama alitumia fursa hiyo
kuwataka mashibiki na wadau wa muziki wa injil waendelee kufuatilia
ratiba kamili ya tamasha hilo kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Aidha
Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa wa Basata, Nsao Shalua anashauri, tamasha
la krismass mwaka 2013,lianzie mikoani na siku ya kilele ambayo ndio
sikukuu yenyewe tukio lifanyike Dar es Salaam.
Anasema
kuwe na vitu vya ziada kama akina mama wajasiriamali kutoka
makanisani na vikundi vingine vitumie fursa hiyo ili kuleta hamasa ya
tamasha husika. Mkuu wa Matukio wa Basata, Kurwijira Maregesi alisema
waimbaji watakaopanda jukwaani mbali ya kuimba nyimbo zilizozoeleka
waimbe pia tungo zenye ujumbe wa Krisimass ili kudhihirisha uhalisia wa
siku yenyewe. Anasema kabla ya tamasha hilo, Basata itatoa semina kwa
waimbaji ili kuwaweka sawa kabla ya matamasha hayo kuanza.
Maregesi
alitumia fursa hiyo kuwaasa waandaaji wa tamasha hilo kulitumia tamasha
hilo kama sehemu ya kuwaasa vijana kuachana na mavazi yasiyo ya heshima
na matendo mengine yanayomchukiza mungu na kudumisha maadili ya
muziki wa injili. “Ifike mahali Tamasha kama la Krismass kufikisha
ujumbe kwa jamii kuhusu mienendo mibovu kama mavazi na mengineyo
yanayomchukiza mungu.