Home » » Mabeki wampangia mikakati Kiiza...!

Mabeki wampangia mikakati Kiiza...!


Straika wa Yanga mganda Hamis Kiiza ambaye amekuwa gomzo kwa mabeki wa Simba.Picha na Maktaba 

BEKI wa Simba, Joseph Owino amekiri ameifuatilia Yanga na kugundua kwamba mastraika wake wana kasi ambayo inahitaji nguvu na akili kukabiliana nao lakini amesisitiza kuwa wamekaa chini na Gilbert Kaze na kupata dawa yao.
Yanga na Simba zinacheza Oktoba 20 kwenye Uwanja wa Taifa lakini Owino amekuwa akifuatilia timu zote kabla ya kucheza nazo na sasa ameshamaliza kuwachunguza Mrisho Ngassa, Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza wa Yanga na anajua jinsi ya kuwatuliza .
“Kwa kweli Yanga inaonekana ipo vizuri, tena siku hadi siku wanaimarika, hivyo inatulazimu na sisi kujipanga zaidi ili kuwasimamisha wachezaji wao wajanja wajanja.
“Ngassa ninayemjua tangu wakati huo ni hatari na mjanja sana, tena ana kasi kubwa, lakini cha kushangaza nimemwona kwa kipindi kirefu akiwa na uwezo ule ule,”alisema Owino.
“Tutakuwa makini sana siku tukicheza na Yanga kwani ukitazama michezo ya Yanga mingi, wamekuwa wakitafuta mabao ya mapema ambayo kwa kiasi kikubwa yamewapa ari, nilishacheza ligi ya Tanzania muda mrefu, ninawajua wachezaji wengi, nafikiri nitakaa na wenzangu wa nafasi ya ulinzi hasa mgeni kama Gilbert Kaze kupanga jinsi tutakavyowapa wakati mgumu Ngassa na Kiiza,”alisisitiza mchezaji huyo msomi kuliko wote kwenye kikosi cha kwanza cha Simba.
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger