Home » , » Cannavaro: Yanga hii ni ‘non stop’

Cannavaro: Yanga hii ni ‘non stop’

BEKI wa kati na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,  amewaambia mashabiki wa klabu hiyo watulize moyo, kwani sasa kikosi chao ni ushindi mwanzo mwisho hakuna kusimama.
Ameenda mbali na kuwatambia wapinzani wao Simba akiwaeleza wasubiri kipigo Oktoba 20 kwani kikosi cha Jangwani sasa hakikamatiki.
Cannavaro “Sasa tumeanza, kasi hii ni ushindi mwanzo mwisho hakuna kusimama. Tumeanza kusogea na sasa tunawakaribia watani wetu (Simba) kwa karibu kabisa, tunataka tukae wenyewe kileleni.
“Hao Simba wasubiri kipigo tu kwa sababu hawawezi kutufunga hata kidogo, kama unavyoona kikosi chetu kimekamilika kila idara kuanzia beki, kiungo hadi ushambuliaji.”
Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 12, tatu nyuma ya Simba inayoongoza ligi hiyo. Azam FC inashika nafasi ya tatu, nayo ina pointi 12 pia, lakini imepungukiwa mabao.
Awali Yanga haikuwa na matokeo mazuri katika mechi zake za nyuma baada ya kufungwa 3-2 na Azam FC na kutoa sare tatu za bao 1-1 dhidi ya Coastal Union, Mbeya City na Prisons.
Hata hivyo, imeshinda michezo mitatu dhidi ya Mtibwa Sugar (2-0), Ashanti United (5-1) na Ruvu Shooting (1-0).
Kocha Mkuu wa Yanga, Ernest Brandts, kwa upande wake alisema: “Tunajipanga na kufanya mazoezi kwa bidii kuhakikisha tunafanya vizuri katika kila mechi iliyopo mbele yetu, nia ni kutetea ubingwa wetu.”
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger