Watu wawili wameuawa katika tukio la utata lililotokea jana asubuhi majira ya saa 3 na dakika kadhaa, katika eneo la barabara ya msikiti wa Ijumaa jijini Mwanza.
Chanzo
cha mauaji hayo kinadaiwa kusababishwa na kijana mmoja maarufu kwa jina
la Mkandarasi kumchoma kisu kijana mwenzake ambaye alikuwa mgeni
akifanya kazi za usaidizi kwa mamantilie wanaopika chakula katika moja
ya viunga vya ndani eneo la vichochoro vya mtaa wa Msikiti wa Ijumaa
kufuatia majibizano ambayo yalisababisha kijana Maarufu kwa jina la
'Mkandarasi' amchome mwenzake kisu cha shingoni na sehemu nyingine za
mwili.
Kijana
huyo alipoona amezidiwa alitafuta upenyo na kukimbia huku damu
zikimchirizika, hata hivyo hakufika mbali kwani alizidiwa na hatua
chache baadaye alianguka chini nakuaga dunia.
Wananchi
wenye hasira walimzingira muuaji ambaye naye alikuwa akijihami kwa kisu
alichokuwa nacho mkononi na ndipo walipofanikiwa kumbwaga chini na
kumshambulia kwa mawe hadi umauti.
Maafisa polisi na wananchi wakiwa wameuzingira mwili wa marehemu Mkandarasi.
Umati wa watu mtaa wa Msikiti wa Ijumaa.
Mashuhuda wakiutizama mwili wa kijana aliyeuwa kwa kuchomwa kisu.
Mwili wa kijana aliyekuwa akifanya kazi kwa mamalishe mtaa wa Msikiti wa Ijumaa ukiwa umelowa damu mara baada ya kuchomwa kisu kufuatia majibizano na jamaa (maarufu kwa jina la 'Mkandarasi') ambaye naye aliuawa na wananchi wenye hasira waliojichukulia sheria mkononi.
Mashuhuda.
Polisi walifika eneo la tukio na kisha wakaondoka na miili ya marehemu hao nao wengine wakibakia eneo la tukio kubaini nini chanzo.
Mwananchi akifukia damu zilizotapakaa kwenye barabara.
-Habari kwa hisani ya G.Sengo